Status
Not open for further replies.
Awali ya yote nawapa pole watanzania na wapenzi wote wa amani na demokrasia Tanzania. Chadema na wananchi wote waliogubujikwa na kushtushwa na shambulio lililompata Mh Tundu Lissu.

Mimi nataka kutoa maoni na sina shaka yatamfkia bwana mkubwa Raisi Dr.Magufuli.

Raisi,mimi sina chama,ila ni mkerketwa na mshabiki namba moja kwako kutokana na ari mpya na uzalendo ulionao juu ya Tanzania.

Kusema ukweli,Tanzania imechezewa na kuibiw a sana. Nakusapoti kile unachofanya na usirudi nyuma.
Lakini pia,katika tendo jema unalofanya mengine unarudi nyuma. Sitaki kukuhukumu kwa jambo lolote lakin junanmanbo yako wazi.

Suala la upinzani Tanzania limekuwa kama uadui. Upinzani sio sawa mchezo wa miguu au kuonekana wewe ni bora zaid ya yule. Tafsiri niijuavyo ya upinzani ni kusaidiana na kuelekezana pale mmoja anapokuwa anakosea kwa hoja za msingi na zenye maslahi chanya kwa Tanzania.

Upinzani sio mangumi,matusi na kejeli kaka watanzania wengi wanavyofanya.Lazima tutangulize maslahi mbele ya nchi bila kupepesa macho au kuangalia pembeni.

Kumekuwa na siasa katika mashule na kazini nk. Vikundi cya chama mashuleni,huku tunatafuta nini? tumeenda kusoma au kufanya siasa. Pamoja hii sio hoja yangu ya msingi sana naona ni wakati kutenganisha siasa na weledi na pia kutoa siasa makazini na mashuleni.

Mh Raisi Magufuli nikufahamishe tu kuwa mkuu,upo katika vita kali sana ya uchumi. Wazungu na wachina na waarabu huko wanakuangalia sana kwa macho mabaya.Hizi ghasia zinazotokea hapa na pale unaweza ukawapa mwanya mkubwa sana wa kuharibu amani iliyopo.
Pia wapo watanzania wengi ambao hawakutaki na wengine wanaona umeleta kauzibe. Nguvu yake unaweza kudharau lakini itapeleka nchi kubaya.
Tanzania ni nchi ambayo imekuwa tulivu na kipekee sana kwa muda mrefu. Kwasbabu hatukuwa tumejitambua. Huko mbele tutarajie misukosuko kwa mfano kibiti ni mfano halisi wa watu wa nje wanaotaka kuharibu amani yetu. Hawa watu wapo wazungu na middle eastern countries na ndio wafadhili wakuu.

Mh Raisi huu ni mchezo wa akili na tumia akili kuwazidi na ujue utapita wapi kabla ya matukio na baada. Wapo hawatakuelewa lakni naamini ipo siku.
Nakushauri kuongea na upinzani na kuwaweka mbele katika vita hii. Usifanye vita hii pekee yako. Hata ukifa leo,Tanzania itarudi kulekule kutokana na kwamba hujatuonyesha njia na haujatufumbua macho au kutusaidia.Ni wewe tu ndio unashika tochi na kusonga mbele.

Nafahamu nia yako ni njema. Najaribu kufikiri kuwa huna wasaidizi wanaona mbali zaidi ya matumbo yao.
Magufuli hakuna analofanya kwa ajiri ya nchi yetu,anachofanya ni kiki kwa ajiri ya maslahi yake binafsi 2020.watz mtandanganywa kwa siasa nyepesi hadi lini? Kama haoni kuwa nchi yetu inakatiba mbovu,kama haoni kuwa sheria zetu ni mbovu ndo maana akaamua kuendesha nchi kwa matamko sasa uzalendo wake uko wapi? Hiyo ni mroho wa madaraka kama waroho wengine ila hata chembe ya uzalendo hana
 
Unakaaje na wapinzani ambao wanachotwa na haohao maaduizetu wa kiuchumi, wanaomba taarifa kutoka kwa wanyonyaji ili wazitumie kukwamisha mikakati ya taifa kujinasua katika hii mitego tuliyonasa? Kuondoa hili la wanasiasa kuzuiwa kuitisha mikutano, Magufuli yuko sahihi 100%. Upinzani wamethibitisha kuwa hawana hata chembe ya uzalendo. Sad!

Sent using Jamii Forums mobile app

Unaanzaje kujiita mpambanaji wa vita ya kiuchumi wakati hutaki kuwagusa watangulizi wako waliounajisi uchumi wa nchi?Leo tunashangilia kukamatwa kwa almasi yenye thamani ya bilioni 64,wakati tumekabidhiwa ripoti ikimtaja mstaafu wa ikulu aliyehongwa almasi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 400!

Hatuwezi kushinda vita kwa njia za maigizo,hivi 64bn na 400bn ni zipi zilipaswa zirejeshwe kwa nguvu?Mzigo huo wa 400bn si ungetosha kulipia bombadia yetu iliyokamatwa huko kanada na bado tungebakiwa na chenji ya zaidi ya 313bn?
 
Awali ya yote nawapa pole watanzania na wapenzi wote wa amani na demokrasia Tanzania. Chadema na wananchi wote waliogubujikwa na kushtushwa na shambulio lililompata Mh Tundu Lissu.

Mimi nataka kutoa maoni na sina shaka yatamfkia bwana mkubwa Raisi Dr.Magufuli.

Raisi,mimi sina chama,ila ni mkerketwa na mshabiki namba moja kwako kutokana na ari mpya na uzalendo ulionao juu ya Tanzania.

Kusema ukweli,Tanzania imechezewa na kuibiw a sana. Nakusapoti kile unachofanya na usirudi nyuma.
Lakini pia,katika tendo jema unalofanya mengine unarudi nyuma. Sitaki kukuhukumu kwa jambo lolote lakin junanmanbo yako wazi.

Suala la upinzani Tanzania limekuwa kama uadui. Upinzani sio sawa mchezo wa miguu au kuonekana wewe ni bora zaid ya yule. Tafsiri niijuavyo ya upinzani ni kusaidiana na kuelekezana pale mmoja anapokuwa anakosea kwa hoja za msingi na zenye maslahi chanya kwa Tanzania.

Upinzani sio mangumi,matusi na kejeli kaka watanzania wengi wanavyofanya.Lazima tutangulize maslahi mbele ya nchi bila kupepesa macho au kuangalia pembeni.

Kumekuwa na siasa katika mashule na kazini nk. Vikundi cya chama mashuleni,huku tunatafuta nini? tumeenda kusoma au kufanya siasa. Pamoja hii sio hoja yangu ya msingi sana naona ni wakati kutenganisha siasa na weledi na pia kutoa siasa makazini na mashuleni.

Mh Raisi Magufuli nikufahamishe tu kuwa mkuu,upo katika vita kali sana ya uchumi. Wazungu na wachina na waarabu huko wanakuangalia sana kwa macho mabaya.Hizi ghasia zinazotokea hapa na pale unaweza ukawapa mwanya mkubwa sana wa kuharibu amani iliyopo.
Pia wapo watanzania wengi ambao hawakutaki na wengine wanaona umeleta kauzibe. Nguvu yake unaweza kudharau lakini itapeleka nchi kubaya.
Tanzania ni nchi ambayo imekuwa tulivu na kipekee sana kwa muda mrefu. Kwasbabu hatukuwa tumejitambua. Huko mbele tutarajie misukosuko kwa mfano kibiti ni mfano halisi wa watu wa nje wanaotaka kuharibu amani yetu. Hawa watu wapo wazungu na middle eastern countries na ndio wafadhili wakuu.

Mh Raisi huu ni mchezo wa akili na tumia akili kuwazidi na ujue utapita wapi kabla ya matukio na baada. Wapo hawatakuelewa lakni naamini ipo siku.
Nakushauri kuongea na upinzani na kuwaweka mbele katika vita hii. Usifanye vita hii pekee yako. Hata ukifa leo,Tanzania itarudi kulekule kutokana na kwamba hujatuonyesha njia na haujatufumbua macho au kutusaidia.Ni wewe tu ndio unashika tochi na kusonga mbele.

Nafahamu nia yako ni njema. Najaribu kufikiri kuwa huna wasaidizi wanaona mbali zaidi ya matumbo yao.

unashauri mtu ambaye hashauriki mtu mwenye kiburi mtu anayejiona yeye ndio mkubwa baada ya mungu, yeye ndio mbabe wa kila kitu, yeye ndio sahihi kwa kila kitu, pole sana uyu mtu dawa yake ni kuandamana kushinikiza utawala wa sheria kwa kila mtu hadi yeye ikishindikana tunapiga chini 2020 basi, mana tunaambiwa analeta maendelo wakati watu ata kula inakuashida
 
Scotland Yard wako vizuri kwenye upelelezi kuliko hata FBI, tutumaini kuwa raisi wetu atatumia ukuu wake kuwaleta hawa wafanye upelelezi tukio la Lissu

Nilikuwa sijui kwamba kumbe Scotland Yard ya Uingereza wako vizuri Kiupelelezi / Kijasusi kuliko MOSSAD ya Israel.
 
Mtoa mada hujitambui, Nani amekwambia anashida ya kushauliwa, hicho ulicho kishauri Rais anakijua kabra yako na ndio maana baadhi ya wapinzani anawateuwa kwenye baadhi ya idara.
Onyo
Ucrudie tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Good to have you back here Kiranga.

The sacking of Mafuru was quite unfortunate - the same goes for Mwele Malecela. What I am surprised by the leadership style of the top man is that that has not ruffled the wrong way people like Mahiga or other technically abled personnel in the administration. It seems non possess both the intestinal and testicular fortitude to resign.

Thanks Epigenetics.

It is good to have thoroughly reasoned input here. Whenever I see your input, I am in equal parts delighted and inclined to pay attention and ponder seriously.

The question of how to deal with a mad emperor (and let's face it, this, in all earnest, is the question here) has puzzled political analysts since before the times of Tiberius, Caligula and Nero. It is not an easy one to solve.

What does an aide with integrity do? Does one resign in protest and to expose the madness in the hope that doing so will hasten the demise of the regime and stop the bleeding before too much blood is shed and the body politic dies?

Or does one stay onboard to serve despite all the chicanery, in the hope that doing so has the chance of at least minimizing the damage?

Is the known present state of chaos and confusion better than or worse than (for the country, that is) a half of the scenarios that would probably play out after a resignation?

The answer, by some not so uninformed estimation, depends on a very well calibrated set of scenarios.

I remember reading on The Wall Street Journal a few months ago on this very question. The article was centred on why the clearly failing Maduro administration is not deserted by some very sane Venezuelan politicians. The conclusion was, there is a critical mass point where deserting is meaningful. Resign before reaching that point, only to have the regime pass through some doldrums successfully, and you become an impotent has been, even an enemy of a powerful cabal in the deep state. Stay on too long past this point only to fall later with an unpopular government, you become a pariah that fell on the wrong side of history.

I will try to look for a paywall free version of that article and post it here.

The biggest reason I can think of that keeps people like Dr. Mahiga going is an impenetrable sense of patriotism and optimism, in fact let's take Dr. Mahiga as an example here. I can speak from personal knowledge of Dr. Mahiga, his working philosophy and history going back to the Nyerere era, so this is not just a generalization or speculation. I know Dr. Mahiga personally.

Dr. Mahiga, is a diplomat, he is a natural optimist. To a fault. Going to Somalia to mediate for the UN requires such a person. I suspect he realizes the unenviable position he is in but justifies his staying on by rationalizing that the country needs people like him now than ever, lest an inexperienced person -or even an experienced one who is a sinister opportunist- comes on board and the country faces some major embarassment without having an able diplomat at the top who can do some serious fire fighting.

This is the biggest reason I think Dr. Mahiga stays on. Otherwise he would have resigned to enjoy his sizable (by Tanzanian standards) UN pension.

Of course you have the element of personal ego of "I am not a quitter" and "I have to finish whatever I started" on his part and many of his counterparts. Of course some characters are motivated more by being in power than anything else. These elements are not to be ignored.

I feel that in Tanzania, the Machiavellian adage "tumikia kafiri upate mtaji wako" is taken very seriously. People in power are respected tremendously regardless of what their ability is. Magufuli himself served for almost two decades under Mkapa and Kikwete, watching all this business about dubious mining contracts, and even passing the minutes at the cabinet level with neither a public protest nor a resignation. All along, we have to assume -if at all the current mining contracts overhaul is serious- he was irked and reserved his ire until he clinched the throne. People who justify his former silence on the matter argue that, had he resigned in protest, he wouldn't be in his current position that gives him the power to overhaul everything with presidential powers.

I am big on nuance and equivocating to get the other side's point of view. This argument is hard to dismiss, especially from a realpolitik Tanzanian experience that is devoid of a highminded morality that sometimes is seldom realistic. We are often accused of analyzing the Tanzanian political landscape with ivory tower theories that are far removed frim realpolitik.

I would like to see people resigning in protest, public protest at that. But apart from the fact that that could turn really dangerous really fast (one can easily say to hell with that and stand for principle), the thinking goes, there is no guarantee that the next person filling the position will be any better. In fact chances are a stooge will be in place.

In fact, we are seeing the exact opposite. Instead of people like Dr. Mahiga resigning, we are seeing elements of the opposition, people like Dr. Kitila Mkumbo - a walking contradiction and an embarassment to the opposition if there ever was one- and Anna Mghwira are recruited into Magufuli's administration, lending it credence in the process.

The sad reality is that, without protest resignations and even expose books like Kenya's Miguna Miguna "Peeling Back The Mask: A Quest for Justice in Kenya" -this book helped me understand Raila Odinga so well- we will be shortchanging our democracy severely.

An even bigger reality is that most of people in power will not resign.Whether by a quaint sense of patriotism and sense of duty that borders denial, like Dr. Mahiga, or out of sheer sense of severe power hunger, culture of collective oversurbodination and an unhealthy respect for authority like so many of the gang.

There is a need to raise the voice that creates a criticall mass to call them out to either do the needful and resign, or be counted with the pariah team that is sinking the ship.

This includes abled people who are almost in denial with their quaint sense of duty, patriotism, optimism and a collective unhealthy respect for authority that only serves to enable and normalize our current Caligula.

Unfortunately, we do not yet have the requisite political awareness to see past certain machinations and propaganda from the current ruler and his enablers.

But this has hardly stoped a determined movement.

Bill Ayers said a revolution looks impossible before it happens and inevitable after it happens.
 
Natumia nafasi hii kama ilivyoelezwa kwenye katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kifungu cha 18, kipengele cha kwanza ambayo inasomeka hivi nanukuu:
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Mwisho wa kunukuu.

Natumia haki yangu ya kikatiba kama inavyoeleza hapo juu kumshauri rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ni ndugu John Magufuli, kuendelea kudumisha, kuimarisha na kujenga umoja wa kitaifa katika taifa ambalo watanzania sote tulizoea kuishi kwa upendo kama ndugu kwa kuvumiliana na kusikilizana hivyo kushiriki katika umoja wetu huo ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere katika ujenzi wa taifa letu pendwa vizuri.

Siku zinavyozidi kwenda mbele inedhihirika wazi ule umoja wa kitaifa unasambaratika kwa spidi kali sana na kupotea.
Natoa mfano kwa visa nilivyoshuhudia nikiwa hapa Tanzania, mie ni mkazi wa kijijini sasa kuna sehemu ambako wazee kwa vijana, walikuwa wanakutana kupata supu hapa kijijini kabla wewe rais hujaingia madarakani lakini ulipochukua tu madaraka pametokea mgawanyiko mkubwa sana uliosababishwa na chuki zinazohubiriwa na watawala wa awamu hii na wewe ukiwemo.

Sasa kile kibanda cha supu kimechomwa moto na watu wasojulikana na watu hawachangamani tena kwa pamoja ila wanakaa kusikojulikana kutegemea na mlengo wao wa kisiasa yani mwanachama wa chama A, atakaa na wa chama A wenzake na yule wa chama B atakaa na wa chama B wenzake. Mambo hayakuwahi kufikia hatua hii hapo awali kabla yako madarakani hakika kama taifa tunaelekea kusikojulikana ndugu rais.

Siyo hivyo tu nachosikitika zaidi ni huku kijijini tulikuwa na utamaduni wa kusaidiana kwa hali na mali bila kujali itikadi zetu za aina yoyote ile, lakini ulipoingia madarakani hali imekuwa tofauti sasa watu wanasaidiana kwa itikadi zao za kisiasa tu.
Nimeshuhudia babu yangu akikataa kumuazimisha kitu jirani yake tena kwa kumkaripia kwa maneno makali kuwa jirani yake ni mwanachama wa chama cha kisiasa tofauti na chake hawezi kumsaidia na asimsumbue tena siku nyingine aende kwa wenzake wa chama chake. Hii ni hatari sana watanzania tumefika pabaya.

Nakushauri rais nusuru hii hali kwa kunusuru umoja wetu wa kitaifa, unda kamati ya maridhiano ikijumuisha wakuu wa vyama vya siasa nchini, viongozi wa kidini yani wachungaji, mashehe na maaskofu, watu kutoka asasi za kiraia nk ili kujadili kwa pamoja ili turudishe umoja wetu wa kitaifa tuliozoea kuwa nao hapo awali.

Tanzania ni nchi yetu sote na machafuko yakitokea tutakaoumia ni sisi watanzania siyo watu wa Rwanda au Burundi.
Tutaumia sisi watanzania.

Mungu ibariki Tanzania ,
Mungu ibariki Afrika.

NB:
Natumaini ushauri wangu utakufikia na utachukua hatua.
Lakini naomba univumilie kama nitakuwa nimekukwaza ndugu rais.
 
Japo kuwa mimi si MLENGWA wa hoja yako, nitasema ushauri wako ni mzuri tu kama raia mwema wa nchi yetu hii..

ISIPOKUWA umenishangaza kidogo kusikia kuwa watu vijijini WANANYIMANA hata chumvi ama MISAADA kama jirani kwa sababu ya ITIKADI za kisiasa.
Ningependa kuuliza yafuatayo:

1.Je mkuu huu unaweza kuwa ni UKWELI kabisa ama ni kuongeza chumvi katika hoja yako?
Ama mimi naishi nchi nyingine?

2. Mbona mimi SIJASIKIA?
3. Je Hicho kijiji unachotoka kwani HAMNA serikali?
Hata ya Wenyeviti wa VITONGOJI ili kutatua matatizo kama hayo?. Kwangu Hii haingii akilini.

Ila NAKUBALIANA nawe kwa jambo moja kuwa,
WANASIASA wote wanahitajika kuhubiri AMANI na UMOJA bila kubaguana kwa misingi ya itikadi za KISIASA KIDINI ama VYAMA.
Nchi ni MUHIMU sana kuliko CHAMA chochote kile wala MWANASIASA yeyote yule!.
 
MKUU

Alichoandika mtoa hoja ni ukweli kabisaa....tembea vijiji mbalimbali utaona kwa uhakika badala ya kusimuliwa.
 
Hata Kwenye misiba hawazikani.Mwenzetu ameumizwa vibaya alichoamvulia toka Chama A ni matusi na masimango
 
Japo kuwa mimi si MLENGWA wa hoja yako, nitasema ushauri wako ni mzuri tu kama raia mwema wa nchi yetu hii..

ISIPOKUWA umenishangaza kidogo kusikia kuwa watu vijijini WANANYIMANA hata chumvi ama MISAADA kama jirani kwa sababu ya ITIKADI za kisiasa.
Ningependa kuuliza yafuatayo:

1.Je mkuu huu unaweza kuwa ni UKWELI kabisa ama ni kuongeza chumvi katika hoja yako?
Ama mimi naishi nchi nyingine?

2. Mbona mimi SIJASIKIA?
3. Je Hicho kijiji unachotoka kwani HAMNA serikali?
Hata ya Wenyeviti wa VITONGOJI ili kutatua matatizo kama hayo?. Kwangu Hii haingii akilini.

Ila NAKUBALIANA nawe kwa jambo moja kuwa,
WANASIASA wote wanahitajika kuhubiri AMANI na UMOJA bila kubaguana kwa misingi ya itikadi za KISIASA KIDINI ama VYAMA.
Nchi ni MUHIMU sana kuliko CHAMA chochote kile wala MWANASIASA yeyote yule!.
chuki imekuwa kwa kiwango cha juu sana yani we fahamu hapa sasa wanakijiji wamefikia hatua ya jino kwa jino na we ukienda kuazima kitu kwa wa itikadi tofauti na yako utafukuzwa kama mbwa mwizi.

Viongozi kila uchao wanahubiri chuki
 
Hili swala kuna Mtu anaitwa Jicho la Bundi nilimwambia hali ilivyo nikamwambia hivi vyama ambavyo kila mmoja ana wafuasi wake kutokea la kutokea japo hathatuombei nini wakuwaita wayamalize wakati mmoja ni kiburi Je mwenye kiburi atakubali na asiyependa.

Nchi ilikuwa ni moja sio mbili.
Ee Mwenyezi Mungu naomba uzidishe amani ktk hii nchi
 
Simpangii namshauri tu bado maamuzi yanabaki kwake.
Hashauriki. Yeye ndiye anashauri washauri wake.

I am serious. Kunamtu anaitwa Lawrence Mafuru alimshauri kwamba kuingilia mzunguko wa fedha kiholela ni kitu kitakachoharibu uchumi.

Hakusikia. Kamtoa kazini Hazina.

Leo kafanya anavyoona yeye bila kufuata ushaur, alichoonya Lawrence Mafuru kimetokea, mzunguko wa fedha umeharibika,uchumiunadidimia.

Lawrence Mafuru ni banker anayeheshimika anajulikana mpaka City of London. Youko Registered kwenye charted yao ya bankers huko.

Hakumsikiliza.

Atakusikiliza wewe hapa JF?
 
MKUU

Alichoandika mtoa hoja ni ukweli kabisaa....tembea vijiji mbalimbali utaona kwa uhakika badala ya kusimuliwa.

Ok bila kupapasa matako wala mdomo. Nani unahisi sababu ya mambo haya ya kunyimana chumvi. Viongozi wa Upinzani. Usidhani wako radhi JPM aseme wakutane. Ruhusa hiyo ni matusi yatafuata. Wanasiasa kukiwa na amani watashindwa uchaguzi. Usidhani haya matangazo na Mikutano na waandishi wa habari ni ya kusimamia amani bali ni kujenga chuki. Kubali KaZaA siasa ni uchafu mkubwa sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom