Akilinjema
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 11,433
- 11,747
Kuna watu hawaoni aibu jamani!
Nape ni mtu sahihiNape na Makonda nani yuko jirani na Rais?!
mmhKwanini asikuteue wewe?
Nape amekuzidi nini hadi umbebe mgongoni?!
Hao machizi wa chato washughulikiwe wameharibu nchi kama wanavyoharibu misitu ya nchi hii.Nape anafaa sana,atapambana na ili kundi la Sukuma Gang linaloongozwa na Makonda nasikia, wapo bize kumkosoa nakumtusi Mh. Rais
Watu wapi unawasemea, binafsiii nina imani nae kubwa tu, na siko peke yanguu#Mama ongeza umakini, minong'ono imekuwa ni mingi sana sio bara sio visiwani Watu wanaanza kupoteza imani na wewe...mpaka ndani ya bunge lako majadiliano ya pembeni yamekuwa ni mengi. Sikukosoi lakin kuna mambo ingefaa sana uyatafakari sana kabla ya maamuzi.
Wapo pia umewatia moyo kwamba kwao mambo yanaenda kukaa sawa sasa Hao ni wale, wanaoamini kuwa umasikin wao na njaa zao ni makosa yanayotokana na serikali tu Not their faults...hao ni wale people of full of excuses, in the same time some of them are making money as well.
Binafsi nakuunga mkono Lakin usiturudishe Misiri utumwani kufanya vibarua. Hapa wale waliopitapita vyuoni hawatanielewa maana baadhi yao wanaishi kizamani yaan #Education is a key of success by being employed ..!! right! but..Dunia inabadilika sana sio bongo tu ni kote ulimwenguni, if you expect for employment sometimes is so complicated. Ukimwambia kijana ajiajiri atasema ummpe mtaji, but mtaji ni maarifa..any way mimi sio Nanauka
Back to the point; Maneno yanazidi kuwa mengi na imani ya watanzania kwa sasa wanaamini baadhi ya maamuz unayoyatoa si yako bali unatumika na watu flan kwa maslahi yao na mikakati yao. Mimi ni mmbeya tu nimeona nikuletee habari hii. Najua hujachaguliwa na wananchi Lakin uliaminiwa na yule aliyechaguliwa na wananchi kuwa unafaa kuwa mshauri wake ndio maana kwenye kikaratasi cha kura picha yako pia iliwekwa kwa pembeni, Kumbuka ushindi wa 80% ulikuwa wa Mgombea urais naye alikuamini na wewe, Usipoamini haya ngoja Uchaguzi 2025 ndipo utasadiki haya niyasemayo.
Asante...!
Boss Asante Sana! Huyu mama ni Jembe ila aende kwa tahadhari! JPM hakupendwa tu hivi hivi bali kwa sababu ya uzalendo wake. Hakuwa malaika kwa hiyo kuna umuhimu wa mabadiliko lakini sio kwa mambo ya 'pride' yetu kama watanzania.Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.
Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:
Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.
Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.
Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.
Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.
Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Usipende kurejea ushindi wa uchaguzi kila mtu anajua huo ulikuwa mchezo wa kuigiza, ila mama ni afadhali mara 200 kulinganisha na yule bwana.#Mama ongeza umakini, minong'ono imekuwa ni mingi sana sio bara sio visiwani Watu wanaanza kupoteza imani na wewe. Mpaka ndani ya bunge lako majadiliano ya pembeni yamekuwa ni mengi. Sikukosoi lakini kuna mambo ingefaa sana uyatafakari sana kabla ya maamuzi.
Wapo pia umewatia moyo kwamba kwao mambo yanaenda kukaa sawa sasa Hao ni wale, wanaoamini kuwa umasikin wao na njaa zao ni makosa yanayotokana na serikali tu Not their faults. Hao ni wale people of full of excuses, in the same time some of them are making money as well.
Binafsi nakuunga mkono Lakini usiturudishe Misiri utumwani kufanya vibarua. Hapa wale waliopitapita vyuoni hawatanielewa maana baadhi yao wanaishi kizamani yaan #Education is a key of success by being employed! right! but..Dunia inabadilika sana sio bongo tu ni kote ulimwenguni, if you expect for employment sometimes is so complicated. Ukimwambia kijana ajiajiri atasema ummpe mtaji, but mtaji ni maarifa..any way mimi sio Nanauka
Back to the point; Maneno yanazidi kuwa mengi na imani ya Watanzania kwa sasa wanaamini baadhi ya maamuz unayoyatoa si yako bali unatumika na watu flan kwa maslahi yao na mikakati yao. Mimi ni mmbeya tu nimeona nikuletee habari hii. Najua hujachaguliwa na wananchi Lakin uliaminiwa na yule aliyechaguliwa na wananchi kuwa unafaa kuwa mshauri wake ndio maana kwenye kikaratasi cha kura picha yako pia iliwekwa kwa pembeni.
Kumbuka ushindi wa 80% ulikuwa wa Mgombea urais naye alikuamini na wewe, Usipoamini haya ngoja Uchaguzi 2025 ndipo utasadiki haya niyasemayo.
Asante!
Nashukuru ndugu yangu. Upo sahihi sana, hakuna yeyote asiyependa mabadiliko chanya, lakini kama ulivyosema JPM alitengeneza pride ya kitanzania iliyokwishapotezwa na tawala kadha wa kadha nyuma yake. Mama ajitahidi "kuboost" morale na pride ya watanzania kupitia speech zake na matendo yake. Body language kwenye uongozi ni kitu cha msingi sana, na mtangulizi wake alifanikiwa sana kuambukiza confidence miongoni mwa raia.Boss Asante Sana! Huyu mama ni Jembe ila aende kwa tahadhari! JPM hakupendwa tu hivi hivi bali kwa sababu ya uzalendo wake. Hakuwa malaika kwa hiyo kuna umuhimu wa mabadiliko lakini sio kwa mambo ya 'pride' yetu kama watanzania.