OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,210
103,795
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

---
Taarifa kutoka ukurasa rasmi wa CHADEMA mtandao wa X

Leo tarehe 07 Februari 2024 Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. Tundu Lissu alipata mwaliko wa kufanya mahojiano maalum na kituo cha Luninga cha Wasafi Tv katika kupindi cha Good Morning kinachoanza saa 11 alfajiri mpaka saa mbili asubuhi. Jana usiku moja ya watangazaji wa kipindi hicho alimpigia Mhe. Lissu na kumjuza kuwa mahojiano hayo yameahirishwa kutokana na maelekezo kutoka juu.

Aidha, asubuhi ya leo Mhe. Tundu Lissu amefika Wasafi Tv kujua sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo. Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea muda huu katika ofisi za Wasafi Tv.

Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi.

lissu1.jpg

Picha: Tundu Lissu akiwa ofisi za Wasafi

=============For English Audience Only============​
Tundu Lissu's scheduled interview at Wasafi FM was abruptly canceled, leading to some tension as Lissu insisted on understanding the reasons for the cancellation. Initially, it was announced that Lissu would participate in an interview on Wasafi TV's "Good Morning" show. However, the interview was postponed following directives from unspecified high-ranking officials.

On February 7, 2024, Lissu received an invitation to the special interview segment on Wasafi TV. Last night, one of the show's presenters informed Lissu that the interview had been postponed due to directives from above. This morning, Lissu visited Wasafi TV to seek clarity on the reasons behind the cancellation. The management of Wasafi apologized without providing specific reasons for the cancellation.

Despite being informed about the cancellation over the phone, Lissu was unsatisfied and decided to personally visit Wasafi FM to seek genuine reasons. The management, while apologizing, did not disclose the underlying reasons behind the abrupt cancellation.

Pia soma: Nape Nnauye: Hatujazuia mahojiano ya Tundu Lissu, Wasafi FM
 
Kasema juzi mujahid twendeni kwa wananchi na marufuku hizo media zote zimekatazwa kurusha mikutano ya wapinzani.Jana nilijiuliza hando alifukuzwa efm,huenda na wasafi akafukuzwa.KAMA MKURUGENZI WA VIPINDI ZINAKUTOSHA jiuzulu.
 
Ndio muone sasa umuhimu wa kuwa na VYOMBO vyenu vya HABARI...mnaweza kusema ohoo havitosajiliwa, sawa ILA mlishajaribu kuomba kwa kufuata TARATIBU zote?..

Ombeni kwa kufuata taratibu zote,wakikataa ,NJOONI kwa Wananchi
Kwani wasafi ni ya CCM? Halafu kwanini Tundu wanamwogopaga sana? Watakubali mahojiano na watu wote lakini sio Tundu, why? Si wanasema demokrasia na utawala bora ikiwa pamoja na ukweli na uwazi vimetamalaki mbona wanaogopa watu kuexpresi feelings zao, si for the people by the people? Au nasema uwongo ndugu zangu?
 
Diamond atakujibu
Wasafi, nao Wana mumunya mumunya tu.

Hatahivyo, tabia ya kukurupuka na kwenda kuvamia kituo cha redio, eti kwasababu hakuridhika na taarifa ya kufutwa au kubadilishiwa Mahojiano yake-Kina uashiria wa Udikteta. Ubabe Ubabe.

Sidhani kama Diamond ana wajibu. Labda kama makubaliano hayakuwekewa kipengele cha "Kusitisha mahojiano bila ya sababu yeyote ile"

....anywho
 
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wameingia cha kike, hawamjui Lissu. Saafi kabisa
 
Kwani wasafi ni ya ccm ? Alafu kwanini Tundu wanamwogopaga sana ? Watakubali mahojiano na watu wote lakini sio Tundu, why ? Si wanasema demokrasia na utawala bora ikiwa pamoja na ukweli na uwazi vimetamalaki mbona wanaogopa watu kuexpresi filings zao, si for the people by the people ? Au nasema uwongo ndugu zangu ?
Lissu Akiongeza anasililizwa sana na watu kwa sababu Mara nyingi haongei SIASA anaongea Fact na sheria..
Sheria Mara nyingi inachoma kuliko Hata Siasa
 
Back
Top Bottom