Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,495
113,591
Wanabodi,

Hili ni bandiko la pongezi kwa ITV kuwa ndio the first mainstream TV Station kumhoji Tundu Lissu. Huu ni mwanzo mzuri, TV nyingine zifuate.

Pia nampongeza Mhe. Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu, ametumia lugha za staha, amemwaga sera.

Kati ya freedom zote, freedom ambayo ni absolute freedom is the freedom to think, uhuru wa kufikiri ndio uhuru pekee ambao hauna mipaka, mtu unaruhusiwa kufikiri lolote, lakini sio uhuru wa kuongea lolote.

Nimemsikiliza Tundu Lissu katika mahojiano haya, amezungumzia sera nzuri za Chadema, generally kipindi hiki ni kizuri, kimeijenga ITV na kimemjenga Tundu Lissu, but...

Naomba hapo kwenye but nisiseme kitu kwasababu siku hizi, mimi ni kada.

Kitu pekee Lissu alichoharibu, ni kutaja majina ya watu, anaowahisi wanafanya mambo fulani ndivyo sivyo. Nimesema kuhisi ni sawa lakini usitaje hadharani majina ya hao unawahisi, ukiambiwa thibitisha, ukashindwa utahesabika ni muongo!

Kumhisi mtu yoyote au kumshuku mtu yoyote is your right, lakini kumtaja hadharani kwa majina huyo unayemhisi, is not right unless una ushahidi usiotia shaka, na ukiitwa kuthibitisha, utathibitisha pasipo kubabaika wala kujiuma umma.

Katika kipindi cha leo, kuna jina la mtu, Tundu Lissu amemtaja, na kumsingizia kuwa kabla hajafanya maamuzi yoyote ni lazima kwanza amuulize aliyemteua.

This is not right, ofisi ile ni independent, kumsingizia yule aliyemsingizia, tena kwa kumtaja jina kuwa hawezi kufanya maamuzi yoyote hadi amuulize aliye mteua kama uamuzi huo utamfurahisha, is not right.

Kwa mujibu wa katiba yetu, wakuu wa Taasisi zote za umma wanateuliwa na rais. Kati ya taarifa hizo, kuna Taasisi ni independent, rais anaweza kukuteu tuu lakini hawezi kukutengua, Taasisi hizo ni pamoja na Mahakama, Ofisi ya CAG, Gavana wa Benki Kuu, Tume ya Haki za Binaadam na Utawala Bora, na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, nafasi zao zinalindwa na kitu kinaitwa security of tenure. Rais anaweza kumteua tuu mtu kama Jaji Mkuu, CAG, Msajili wa Vyama, lakini hawezi kumtengua. Hivyo kitendo cha Tundu Lissu kumsema mteule fulani hawezi kufanya maamuzi mpaka amuulize aliyemteua, sio kumtendea haki mteule huyo.

Alichosema Lissu is as if, kwa vile wakuu fulani wameteuliwa na rais, hivyo kazi yao ni kufanya maamuzi ya kumfurahisha rais, kitu ambacho sii kweli.

Mfano ni mimi mwenyewe, baada ya Mkuu fulani kusema hadharani kuwa fulani alimpigia simu kumuuliza aumteue nani kwenye issue fulani. Mimi nikauliza, kitu fulani, niliitwa Dodoma kuhojiwa na Kamati fulani kwa swali langu hilo!. Sasa leo Tundu Lissu amesema mtu fulani hawezi kufanya maamuzi hadi amuulize aliyemteua!, jee akiitwa kuthibitisha, ataweza?

Kingine ambacho Tundu Lissu ameharibu kwenye mahojiano haya ni alipoulizwa kama atagombea urais 2025, Tundu Lissu amejibu "ndio, nitagombea!". This is not right kwasababu it's as if Chadema imeisha mteua yeye kugombea. Alipaswa ajibu kuwa nina nia ya kugombea tena urais na nitaomba ridhaa ya chama changu, nikipitishwa, nitagombea!. Jibu la Lissu its as if kwa vile yeye ndie mgombea urais Chadema uchaguzi wa 2020, sasa amejimilikisha ugombea wa 2025, kama Dr. Slaa alivyojimilikisha ugombea urais wa Chadema 2015 hivyo Chadema ilipopata mgombea bora kuliko Dr. Slaa, Dr. Alisusa akazira na kutimka zake mamtoni!. Hivyo Chadema ikipata mgombea bora kuliko Tundu Lissu, mtu atasusa kuzira na kutimkia zake Ubelgiji!.

My Take:
Natoa wito kwa wanasiasa, japo kwenye kampeni uongo unaruhusiwa na propaganda za kisiasa rukhsa katika kutafuta kura, mnapo nadi sera zenu, epukeni kutaja majina ya watu katika vitu ambavyo ni hisia tuu!.

Namalizia kwa kutoa hongera kwa ITV, hongereni sana, mmetusaidia kumsikia Tundu Lissu na kumsililiza bila kukereka.
Pia nampongeza Tundu Lissu kuzungumza kwa utulivu katika mahojiano hayo, bila kusahau kumpongeza Mtangazaji Farhia Middle, kwa maswali mazuri kwa Tundu Lissu, hiki ni kipaji kingine kizuri katika utangazaji, ITV imekiibua, na hongera kwa menejimenti ya ITV, kumwalika Tundu Lissu na kumpatia Airtime ya kutosha, katika zama hizi za Tanzania ya sasa, it's a bold decision! mimi niliulizaga tu swali mahali, kilichofuata..., only God knows, hadi ilibidi...

Pia nasisitiza the freedom to expression, ruksa kuhisi lolote, rukhsa kumhisi yoyote, lakini sio fair kutaja majina ya watu kwa jambo la hisia tuu kwa kumhisi. Niliwahi kushauri humu kuwa sio lazima mtu kuusema kila ukweli unaoisikia au kuujua!. Kwa mfano kuna member mwenzetu humu, anamjua kiongozi fulani kuwa sio, akanitajia, na mimi nikajiridhisha kuwa alichokisema ni kweli lakini ukweli huo hauhitaji kusemwa!

Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

I wish him, Tundu Lissu, all the best katika ugombea wake, maana mimi ni miongoni mwa watu tuliomchagiza Lissu kugombea ili kuuchangamsha uchaguzi wa urais.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Paskali
 
Pascal acha kuanza kupoteza mjadala wa leo wa Lissu kuwafunika vibaya sana CCM na mgombea wenu. Hoja kuu ya leo ni Lissu alivyoonesha uwezo wake mkubwa kwenye upeo na maono ya kuipeleka hii nchi mbali.

Huu mjadala unaoanzisha hapa kuhamisha hoja kuu ya leo, napenda kukwambia umeshafeli kabla hujaanza. Hakuna hata moja ambalo Lissu amekosea kwenye kujibu kwenye kipindi cha dk 45.
 
Mkuu kada mtiifu mgombea yeyote ana haki yakuweka mbinu chafu azionazo zitamharibia kura zake, hakuna sababu ya kunyamaza, na kwa mtu mzima kama yeye na dhamana aliyonayo kwa sasa akitoa tahalifa jua anamanisha nini anaongea , na kama mgombea lazima anavyo vyanzo vyake vya kumfikishia taharifa muhimu bila chenga.
 
Back
Top Bottom