[QUOTE="Molemo,
Mimi nilijiuliza swali moja kubwa la msingi sana, kwamba: "TUMEFARAKANA LINI HADI KUFIKIA HATUA KUBWA HIVI YA KUHITAJI MARIDHIANO YA KITAIFA?"

Kauli ya Mh.Freeman Mbowe: "....Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari....." ni nzito na pengine anaweza kuwa aliitoa pasipo kuwa anaelewa uzito wa kile alichoongea. Kwa mtizamo wangu mimi, tuna tofauti za msingi tu za ki-itikadi ambazo zipo kila mahali popote duniani, ambazo huwa hazikosekani katika mazingira yoyote yale ambapo Siasa ipo, na kwa sababu hakuna mahali ambapo Siasa haipo.

Basi kinachoendelea ndani ya Nchi yetu ni maisha tu yale ya kawaida, na harakati za kawaida za binadamu waliomo kwenye Siasa na wasiokuwemo. Sasa hili la kusema Rais alete maridhiano, lini tumefarakana kiasi cha kufikia stage ya kuhitaji kitu kama hiki? Mimi siyo Political Scientist lakini ninachokiona hapa Mh. Mbowe ni kama alimaanisha maridhiano yanayohusiana na situtaion kama iliyowahi kutokea Kenya mwaka 2007 halafu Rais Mstaafu JK akaenda kuokoa jahazi!
 
CalvinKimaro, Swali moja? Why Mbowe? Mbowe? Mbowe? Why? Kuna wenyeviti wengi but why Mbowe? Anawafanya Nini huyu MTU? Mbaya zaidi hajawahi hata siku moja kujibu chochote kile! Juzi Mwanza kila chombo cha habari kilimtaja Mbowe like Mbowe ndio alikua mgeni pekee! Mfano ni hizi media mbili...
 
Sikupata fursa kutazama maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika.
Lakini mitandaoni pamechafuka,watu wanamshambulia Mbowe kwa kuwapeleka Chadema kujisalimisha kwa mtesi wao.

Wengine wanampongeza kwa kwenda kuungana na serikali kutaka maridhiano.

Swali langu,kwenu wana jamvi,dola ilisemaje kuhusu ombi la Mbowe?

Au mpaka wakae vikao watatoa tamko kuhusu ombi la Maridhiano?

Wananchi tutatumia kipimo gani kutofautisha hali kabla ya Mbowe kuomba maridhiano na baada ya Mbowe kuomba ?

Mikutano itaruhusiwa?

Wapinzania hawatanyanyaswa tena?

Waliojitoa serikali za mitaa baada ya maelekezo ya vyama vyao watarudishwa na uchaguzi kuanza upya?

Kama hayo hayatotokea ni maridhiano gani yanaombwa na Mbowe mbele ya Rais.

Waliogomea kwenda kwenye sherehe za uhuru ,kwa madai ya Uhuru wetu kugubikwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za raia,vitisho uhuru wa habari kuporwa,mauaji yasiyofanyiwa uchunguzi,silaha kutumika hadharani kunyamanzisha wabunge(Nape Nauye).

kunajisiwa kwa misingi ya uhuru vilivyo wafanya ACT-Wazalendo wagomee ikiwa ni sehemu ya kuonesha hisia zao,ACT walistahili kuonesha hisia zao kwa kutohudhuria kilele cha siku ya uhuru?

Kipi sahihi kuomba maridhiano au kugomea kwenda?

Tujadiliane



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawazo yako yote ktk uzi huu yanamezwa ktk nyuzi nyingine nyingi zilizofunguliwa kabla yako. Jaribu kuzipitia utapata majibu ya maswali yako
 
Tupo kwenye mgogoro wa nini hadi waombe maridhiano?

God first
Mkuu

Siku ambayo waliovunjiwa kimara huku kukiwa na stop order ya mahakama watakapo amua kuonyesha machungu waliyo nayo ndipo utakapo elewa

Au wale watoto wa masikini walioshindwa kwenda shule huku baba zao na mama zao wakiwa hawajalipwa hela zao za korosho watakapo amua kuonyesha machungu yao ndipo ambapo utaelewa ladha hiyo elfu 7 unayopata kwa kusifu na kuabudu ..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kuna tatizo gani mpaka Mbowe aombe maridhiano. Sijaona vyama vinavyopigana mpaka kuwe na maridhiano.
Au ni ile kesi ndio inawaendea vibaya sasa kisiri siri wanaomba msamahaa??????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We can't negotiate with terrorist USA slogan


State agent

Sent using Jamii Forums mobile app
Walikuwa wakiitukana serikali na kutetea wauaji wa mkuranga,kibiti na Rufiji.Chadena is a terrorist group.Hawajawahi toa pole kwa Askari waliouawa na magaidi Wala kutoa pole kwa serikali wait kutwa walikuwa Wawe bungeni kauli zao Ni kuilaani tu serikali na kutetea ile migaidi.
Namuunga mkono Trump to hell with chadema or AcT wazalendo hatuwezi jadiliana na terrorists
 
Molemo,
Nimeshindwa kupata picha halisi ya anachomaanisha Mh. Mbowe katika maneno yake ya KAMA TAIFA INABIDI TUWE NA MARIDHIANO NA CHADEMA IKO TAYARI KWA MARIDHIANO.

sasa maridhiano hayo ni ya kisiasa km yaliyofanyika Kenya au? Na kwanini yawepo hayo maridhiano? Kuna nini hasa hata yawepo maridhiano ambayo CHADEMA ipo tayari kuyafanya?

Kwa picha ya upande wa pili wa shilingi inamaanisha ni kukiri kushindwa ktk namna moja au nyingine na chama tawala kisiasa jambo ambalo linatia na litatia mashaka wa Tanzania wengi ambao wanasapot & kupenda upinzani kuendelea kuwa na nguvu za kushawishi wananchi ktk nyanja nzima ya demokrasia ktk taifa letu. Kumbuka Upinzani TZ ikiwemo CDM hawajawahi kumtambua Raisi aliyepo km Raisi wa Taifa la TZ toka uchaguzi mkuu mwaka 2015 ulipokamilika na kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi ule, sasa 9 Dec 2019 ndio kusema wameanza kumtambua & kumkiri km Raisi wa TZ? Hii inatia mashaka na ni doa kwa upinzan kwa ujumla.
 
Kuomba maridhiano ni sawa na kuunga mkono juhudi. Mbowe anaomba kurudi nyumbani, kama Lowassa na Sumaye.
 
Maridhiano ni muhimu sana!! Wananchi kukaa kwao kimya usizani wanafurahia yanayofanyika. We need to be free in all aspects.
 
Walikuwa wakiitukana serikali na kutetea wauaji wa mkuranga,kibiti na Rufiji.Chadena is a terrorist group.Hawajawahi toa pole kwa Askari waliouawa na magaidi Wala kutoa pole kwa serikali wait kutwa walikuwa Wawe bungeni kauli zao Ni kuilaani tu serikali na kutetea ile migaidi.
Namuunga mkono Trump to hell with chadema or AcT wazalendo hatuwezi jadiliana na terrorists
Mbinu zote zimewaishia chombo chazama hicho
Kila mwanaccm anatakiwa asikilize santuri hii

😁 ✌
 
Mbowe anatapa tapa tu
Bada ya watu kugoma kuwabembeleza wanataka maridhiano,watu tupo bize nyakati hizi yeye aendelee na kususa tu
 
Back
Top Bottom