Mbowe: Hatutajitoa kwenye Maridhiano na CCM licha ya Changamoto za hapa na pale zinazojitokeza!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,988
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amesema chama chake hakitajitoa kwenye Maridhiano na CCM licha ya Changamoto za hapa na pale zinazojitokeza

Mbowe Alikuwa anaongea na Diaspora huko Uingereza
===

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesisitiza kuwa hawatajitoa katika mchakato wa maridhiano na Chama Cha Mapinduzi (CCM), licha ya changamoto za hapa na pale zinazojitokeza.

Mbowe alitoa msimamo huo juzi wakati wa mkutano wake na Watanzania waishio nchini Uingereza na nchi nyingine za Ulaya (diaspora) uliofanyika jijini London na wengine walifuatilia mkutano huo kwa mtandao.

Kiongozi huyo yupo Uingereza kwa ziara ya siku saba iliyoanza Juni 19, mwaka huu ikiwa imepita wiki mbili tangu alipofanya ziara kama hiyo katika nchi za Italia na Ujerumani. Katika mkutano na Daispora uliofanyika AFC Wimbledon, Mbowe aligusia masuala ya siasa, kijamii na uchumi.

Msingi wa Mbowe kutoa msimamo huo, ulikuja baada wanadaispora kuumuliza mwenendo wa mazungumzo kati ya Chadema, CCM na Serikali, wakitaka kujua yanamalizika lini.

Katika majibu yake Mbowe alisema maridhiano ni mchakato unaohitaji muda mrefu huku akitaja faida zake.

Alisema miongoni mwa faida hizo ni kurudishwa kwa mchakato wa Katiba mpya uliotengewa takribani Sh9 bilioni katika bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ya mwaka 2023/2024, kurejeshwa kwa mikutano ya hadhara, kesi za kisiasa kushughulikiwa na viongozi wa Chadema waliokuwa wakiishia uhamishoni kurejea nchini.

Mchakato wa Katiba mpya ulikwama mwaka 2014 kwa Katiba inayopendekezwa iliyotungwa na Bunge Maalumu la Katiba kusubiri kupigiwa kura ya maoni.

Tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha nia ya kuuendeleza.
“Chadema hakitoki katika mchakato wa mazungumzo, tutaendelea kupambana katika mazungumzo haijalishi tunapata mkanganyiko wa kiasi gani huku tukiendelea kujenga chama chetu.

“Kwa sababu wakati tunaendelea maridhiano ya upanga huu, upanga mwingine unakwenda Kagera, Kigoma, Mwanza na Shinyanga. Tutakwenda kijiji kwa kijiji ili kujenga mizizi ambayo ipo siku itasimama na kuleta mabadiliko,” alisema Mbowe ambaye ni mbunge wa zamani wa Hai.

Majadiliano kati ya Chadema na viongozi wa Serikali na CCM yalianza Mei 20, 2022 Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma, kwa Rais Samia akiambatana na viongozi waandamizi waliokutana na ujumbe wa viongozi wa Chadema, ulioongozwa na Mbowe.

Hata hivyo, baadhi ya Wanachadema kwa nyakati tofauti wamekuwa wakisikika na kuandika katika mitandao ya kijamii wakidai hawaridhishwi na mwenendo wa majadiliano na kutaka wajiondoe.

“Ni kweli kuna wengine wanasema tujitoe… sawa tujitoe halafu nini kitafuata? Tambueni tulijitoa mwaka 2014 katika Bunge Maalumu la Katiba, baada ya hapo tukaa miaka tisa ndugu zangu hadi 2022 tukarudi katika mchakato huu,” alisema Mbowe.

Mchakato wa Katiba

Mbowe aligusia suala la Katiba akisema itakayopatikana haitakuwa Chadema wala CCM, bali kwa masilahi ya Taifa, ingawa mchakato wake ni mrefu unaojumuisha hata yule usiyempenda lakini lazima wote waketi pamoja ili kupata mwafaka.

“Katiba ni mchakato unaojumuisha unayempenda na usiwe mpenda, lazima ukubali hutapata 100 ya unachokitaka, lakini ukubali adui yake hatapata 100 ya anachokihitaji. Hii ndio kazi ngumu ya makubaliano ya Katiba.

Alidai kuwa mchakato wa Katiba uliokwama mwaka 2014, ulisababishwa na utashi wa kiongozi aliyekuwa madarakani. Hata hivyo, Chadema inaamini katika mchakato usiokuwa na upendeleo na utakaoshirikisha makundi yote ili kupata Katiba bora.

“Ndio maana msimamo wetu Chadema, badala ya Rais kusimamia mchakato wa Katiba, iundwe tume ya kitaifa itakayokuwa na uwakilisha wa vyama vyote, asasi za kiraia, diaspora na watu wote ambao ni wadau watakaokaa pamoja na kusimamia suala hili,” alisema.

Mbowe alifafanua katika mazungumzo yao na CCM kuna maeneo wanakubaliana na mengine wanavutana, akisema lazima mazingira hayo yajitokeza kwa sababu ni mchakato wenye maumivu lakini anaamini penye nia pana njia.


Sakata la bandari

Katika hatua nyingine, Mbowe alisema chama hicho hakina chuki wala hila katika msimamo wao wa kutokubaliana na hatua ya Serikali kuingia makubaliano na Serikali ya Dubai kuhusu uwekezaji wa bandari.

“Hatupingi jambo kwa sababu tuna chuki, hila au wivu bali tunataka Taifa letu liwe mahali salama, bora zaidi kwa kuishi,” alisema.


Source Mwananchi
 
Ktk hili sikubaliani na Mkt.

Mmewauliza wananchi ikiwa wanaridhia muendelee na maridhiano na watu wanaouza Nchi mkiwa mnajadiliana nao mezani?

Katika hili, picha inaanza niijia kuwa ninyi ndio mlipenyezewa mkataba Ule muuvujishe na kutengeneza safari ya nje ya mchongo.
 
Back
Top Bottom