CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,760
6,294
Habari wasomaji na wananchi wote.

Je, tumekuwa Taifa la ovyo hivi.

Je, hili ni suluhisho la mjadala katika mambo ya Kitaifa?

Akiuawa, tunatuna ujumbe gani.

Pia soma
-
Kwa mujibu wa ibara ya 14 ya katiba ya nchi yetu kila mtu ana haki ya kuishi na kwamba anapaswa kupata hifadhi ya maisha yake kutoka kwenye jamii hiyo.

Maneno yaliyosemwa dhidi yake na watu wengine waliojiita masheikh yalikuwa yanasikitisha kwa mtu ambaye anamfahamu Profesa Issa Shivji kwa uzalendo wake na utumishi wake uliotukuka na kujitoa kwake kwa nchi yetu, wale watu walikuwa wanaongea kana kwamba ni maneno yao bali kulikuwa na watu ambao walikuwa nyuma yao.

Damu yangu kama itamwagika basi ikapalilie mapambano ya kulinda rasilimali za nchi yangu Tanzania.

Mtu hawezi kuishi katika nchi ambayo ni Jamhuri na watu wengine wakawa na leseni ya kuondoa uhai wao. Mwenye leseni, ruhusa na mamlaka pekee ya kuondoa uhai wa mtu hapa duniani ni Mwenyezi Mungu pekee.

Kiukweli kuua watu kupo na watu wamefariki, watu wamejeruhiwa na kupata matatizo makubwa. Kufuatia hilo nimeamua kuja mbele ya umma wa Watanzania kuwaambia kwamba mimi Rugemeleza Nshala maisha yangu yako hatarini. Kuna maagizo kutoka ndani kwamba nitakapopatikana niteketezwe, niangamizwe na kuitwa marehemu.

Mkataba huu wa bandari umesainiwa au umepewa kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kibali hiko kinaonekana katika kiambatanisho kimojawapo katika mkataba huo ambacho kina saini ya Rais Dkt. Samia

===
Wakili wa kujitegemea Dkt.Rugemeleza Nshala amesema amepokea taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya mifumo kuwa anatakiwa kuuwawa kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na msimamo wake dhidi ya watu waliojitokeza kumshambulia kwa maneno ya kejeli na kuudhi Prof.Issa Shivji baada ya msomi huyo wa sheria kutoa maoni yake dhidi ya sakata la uwekezaji wa Bandari linaloendelea sasa hapa nchini

Akizungumza na Wanahabari kwenye ukumbi wa Mesuma Hotel, Makumbusho Jijini Dar es Salaam, Dkt.Nshala ambaye pia amewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ameeleza kuwa hivi karibuni kupitia jukwaa la 'club house' alitoa maneno makali ambayo kiuhalisia amedai kuwa ndio msimamo wake dhidi ya watu hao ambao anaamini kuwa walichokizungumza si maneno yao bali wanatumiwa na watu wenye mamlaka nchini kutoa lugha za kashfa na kuudhi dhidi ya mtu mwenye umri mkubwa na anayestahiki heshma kubwa dhidi yao kwenye jamii

Dkt.Nshala aliyefika kwenye Kikao hicho akiwa amebeba Vitabu viwili alivyoeleza kuwa anavyoviamini zaidi (Biblia na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) amesema anawaeleza wenye mamlaka walio nyuma ya mpango huo kuwa yuko tayari kufa kwaajili ya nchi yake

Ikumbukwe kuwa kupitia jukwaa hilo ambalo lilijadili mjadala wa kina kuhusiana na uwekezaji wa Kampuni ya DP World ya Dubai kwenye Bandari, Dkt.Nshala alitoa kauli zolizoonekana kuwashambulia zaidi viongozi waandamizi serikalini akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa nk
---

Ndugu Watanzania!
Dkt. Rugemeleza Nshala ametujulisha kuwa maisha yake yako hatarini. Wakili Dkt. Nshala anasema kuwa ametaarifiwa juu ya mipango ya kutaka kumuua (assassination) inayopangwa dhidi yake! Vitisho dhidi ya maisha ya Wakili Dkt. Nshala vinakuja muda mfupi tu baada ya yeye kutoa maoni yake kwa hisia kali akipinga Mkataba wa Bandari kati Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Dubai.

Dkt. Rugemeleza Nshala, ambaye alikuwa Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) ni wakili na mwanasheria mbobevu anayejua vema mipaka yake kikatiba na kwa nafasi yake anao wajibu wa kutoa ushauri na maoni kwa Watanzania katika masuala ya sheria na katiba ya nchi.

Sisi Askofu tumepata muda wa kuomba na Dkt. Nshala na kumtia moyo kuwa asiogope kwani alitoa maoni yake kama raia anayeipenda nchi yake na hakuvunja sheria ye yote ya nchi. Kwa maoni yetu, watu wanaomtisha Dkt. Nshala au wanaotaka kuondoa uhai wake ni watu waoga ambao wanataka kumchafua Rais Dkt. Samia ili dunia ifikiri ameanza kuwaua wakosoaji wake.

Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao wanapanga kutoa uhai wa Dkt. Nshala pamoja na wanaharakati wengine wanaotoa maoni yao au hata kuikosoa Serikali kuhusiana na suala la Mkataba wa Bandari waache mara moja. Kama wao wanafikiri kuwa Dkt. Nshala na wenzake wamefanya kosa lo lote kisheria, wawapeleke mahakamani badala ya kuanza kuwatisha.

Kutisha watu na kutaka kuwaondoa au kuwaua watu nje ya mfumo wa kisheria ni uhaini, uuaji, unyama na ujambazi bila kujali mtu anayefanya matendo hayo. Sisi Askofu tunatoa tahadhari hii kama kukinga mapema ili watu hao wajue kuwa wanachokipanga kufanya hakikubariki. Kama Dkt. Nshala na wenzake watadhulika kwa lolote, watu waliowahi kutoa kauli zao kwa lengo la kuwatisha, hao watawajibika. Kukinga ni bora kuliko kutibu! Tumetimiza wajibu wetu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 6 Julai 2023; 09:39 am.

06 Julai 2023​

🅻🅸🆅🅴 DKT NSHALA ADAI KUTISHIWA MAISHA '' MAISHA YANGU YAKO HATARINI

Mkutano na waandishi wa habari Dr. Nshala athibitisha kupata taarifa kutoka vyanzo vinavyothibitika kuna njama za kuondoa uhai wake Ikiwemo uhai wa wakili Boniface Mwabukusi Prof. Issa Shivji hivyo siwezi kukaa kimya kwani imewahi kutokea kwa Mwangosi, Azori, Ben Saanane kupigwa risasi Tundu Lissu.

Dr. Nshala anasema inasikitisha kuona kuna watu wamejipatia leseni ya kuondoa uhai wa watu kwa kuwa tu kuna wametoa maoni yanayokinzana na wale waliopo madarakani .

Dr. Nshala amesisitiza kuwa mkataba wa bandari unamuhusu rais kutokana na kibali cha rais na mara nyingi mikataba huwa haina muongozo wa rais.

Kulinda maliasilia ya nchi yetu ni haki ya kila raia iliyotamkwa ndani ya katiba ya Tanzania. Hivyo tunavyopiga kelele tunatimiza haki yetu ya msingi ibara ya 26.1 ya katiba inasema .

Ibara ya 9 (c) ya katiba inaitaka serikali kuwajipika pia kutunza mali za taifa.

Huu mkataba unamilikisha mali zote kwa mtu binafsi yaani kampuni ya DP World ya Dubai.

Juzi kumevuja marekebisho yaani Miscellaneous amendments laws ili kuondoa bandari za maziwa na katika mito ya maji ili DP World waweze kufaidi Mali ya asili ya bandari.

DP World anaendelea kupewa ukiritimba wa kumiliki mali zetu kwa aina ya ajabu kupitia muswaada huu mpya utakaopelekwa bungeni kinyume na sheria ya rasilimali iliyotungwa mwaka 2017 ya kulinda mali kwa vizazi vyetu na vizazi vijavyo.

Dr. Nshala nimepata utaalamu mkubwa katika vyuo vikuu tajwa vya Yale na Harvard vyote vya nchini Marekani kwa miaka 10 1/2 kuelewa mikataba na sheria za wawekezaji vizuri. Hivyo elimu niliyopata siwezi kuacha kuitumia kutetea mali ya nchi yetu Tanzania ambayo imenisomesha.

Ningeweza kubaki Marekani kuajiriwa wakati ule kwa mshahara wa dola za kimarekani 22,000.00 kwa mwezi na bonasi kubwa kila mwaka.

Dr. Nshala amesema sitaweza kutishika kukimbia nchi yangu nitabaki hapa hapa Tanzania na wale waovu wanaotaka kuondoa uhai wangu wakifanikiwa basi wao na vizazi vyao laana hii itawaandama milele na kuwasumbua sana.

Mwandishi John Marwa wa Jambo TV anauliza swali kwa Dr. Nshala kuwa kauli za wakili Dr. Nshala zilikuwa kali kwa maoni ya baadhi ya Tanzania.

Vibaraka wa ndani ya nchi wanajidanganya kupindisha maana ya kauli na maneno utetezi wa mali ya umma. Anasisitiza Dr. Nshala kujibu swali la mwandishi, Lugha ni ya uchungu na siyo kali bali kuwaamsha rais, makamu wa rais, mawaziri, bunge kuwa wanapaswa kukubali makosa yao kwa kuwaambia ukweli ....

F0VtOqVWwAAWAur.jpeg
 
TOKA MAKTABA:

03 Julai 2017​

Dodoma, Tanzania

Bunge lapitisha Miswada ya sheria za ulinzi wa Maliasili za Taifa​

HOTUBA YA WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA MH. PROF. PALAMAGAMBA KABUDI

Hansard :
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
1
BUNGE LA TANZANIA
____________
MAJADILIANO YA BUNGE
___________
MKUTANO WA SABA
Kikao cha Hamsini na Nane – Tarehe 3 Julai, 2017
(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)
D U A
Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua
MWENYEKITI: Tukae, Katibu!
NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:
HATI ZA KUWASILISHA MEZANI:
Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:-
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA:
Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu
Muswada wa Sheria ya Mamlaka na Nchi kuhusiana na Umiliki
wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and
Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017]
Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu
Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu
masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka
2017 (The Natural Wealth and Resources Contracts (Review
and Re-negotiation of Unconscionable Terms) Bill, 2017] ...

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:
MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na
Umiliki wa Maliasili, 2017 (The Natural Wealth and
Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017)
na
Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu
Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi, 2017
(The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and
Re-negotiation of Unconscionable Terms) Bill, 2017)
(Kusomwa Mara ya Pili)
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu
Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 86 ya Kanuni za Kudumu za
Bunge, Toleo la Mwaka 2016, naomba kutoa hoja kwamba
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki
wa Maliasili wa 2017 (The Natural Wealth and Resources
(Permanent Sovereignty) Bill, 2017) na Muswada wa Sheria ya
Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba
inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 (The Natural Wealth and
Resources Contracts (Review and Re-negotiation of
Unconscionable Terms) Bill, 2017) sasa usomwe kwa mara ya
pili na Bunge lako Tukufu lijadili na hatimaye lipitishe Miswada
hii na kuwa sehemu ya sheria za nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kuwasilisha
maudhui ya Miswada hii, naomba nianze kwa kumshukuru
Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuturuzuku uhai,
kutujalia afya na kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hii pia
kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani kubwa
aliyoonesha kwangu kwa kuniteua kuwa Mbunge na Waziri
wa Katiba na Sheria. (Makofi)...

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo
ya utangulizi, naomba sasa kutoa maelezo kuhusu Muswada
wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa
Maliasili wa Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources
(Permanent Sovereignty) Bill, 2017) na Muswada wa Sheria ya
Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba
inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 (The Natural Wealth and
Resources Contracts (Review and Re-negotiation of
Unconscionable Terms) Bill, 2017).
Mheshimiwa Naibu Spika, misingi ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania; Muswada wa Sheria ya Mamlaka
ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa 2017
unapendekeza kuweka masharti yanayohusianisha misingi
iliyomo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
1977, mikataba na misingi ya sheria mbalimbali za Kimataifa
ambazo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazitambua
na ama imesaini au kuridhia.
Mheshimiwa Naibu Spika, sheria inayopendekezwa
kupitia Muswada huu ina msingi wake katika Ibara ya 8(1) ya
Katiba ambayo inaweka masharti kuwa Tanzania ni nchi
inayozingatia msingi wa demokrasia na haki ya kijamii na
kwa msingi huo, wananchi wake ndio msingi wa mamlaka
yote ya nchi na Serikali inawajibika kwa wananchi wake.
Ibara hiyo inaeleza kama ifuatavyo:-
“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi
inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii na kwa
hiyo: –
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na
Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa
wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) Wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali
yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.” Mwisho wa
kunukuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla, Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ikiwa ni nchi yenye uhuru kamili ina
haki na mamlaka ya kusimamia maliasili na utajiri wake. Kwa
msingi huo, Serikali inayo wajibu wa kulinda maslahi ya
wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
mikataba inayoingia kuhusiana na maliasili na utajiri huo
kama inavyoelekezwa katika Ibara ya 27 ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania. Ibara hiyo inaeleza kama
ifuatavyo:-
“(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya
Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali
yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia
kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali
ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za
uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa Taifa kwa
makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye
ya Taifa lao.”
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia misingi hiyo
iliyowekwa na Katiba, Ibara ya 9(1)(c) ya Katiba inaelekeza
kuwa shughuli za Serikali zitekelezwe kwa njia ambazo
zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa,
unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi
wote kwa ujumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu
mwingine.
Mheshimiwa Naibu Spika, misingi ya maazimio ya
Umoja wa Mataifa; Muswada huu unazingatia uwepo wa
Sheria ya Kimataifa inayotambua haki ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuhusiana na umiliki wa maliasili.
Aidha, Muswada umezingatia kwamba Tanzania imesaini na
kuridhia mikataba mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo Azimio
la Umoja wa Mataifa Namba 523(vi) la tarehe 12 Januari, ..
 
Wasiojulikana bado wapo, kama walifanya kazi huyu msaliti akiwa msaidizi na hakuwahi kuwakemea, sitashangaa msaliti nae akiamua kuwaacha wasiojulikana wamsaidie kuwafunga watanganyika midomo wanaolilia ardhi yao iliyopewa mwarabu.

Anawaacha wasiojulikana wamsaidie kwasababu ameshaona maji yamezidi unga, watanganyika wanachachamaa, japo alijidai kuziba masikio lakini sasa anaona kelele zinazidi, huku majibu ya maswali ya watanganyika akiwa hana, Samia anaelekea kuchanganyikiwa.

Huyu mtu anayeelekea kuchanganyikiwa anaweza kuja kuwa dikteta mbaya zaidi ya wote, kwasababu anajua anaongoza watu wasiomuamini, hivyo hata akijitahidi vipi itakuwa ngumu kwake kurudisha imani kwao, lakini pia, mamlaka makubwa aliyopewa kikatiba, anaweza kuyatumia kuwaumiza anaowaongoza, hasa kwa tabia zake za kukomoana kama alivyomfanya Job.
 
Huyu Mwamakula ni askofu wa CHADEMA hivyo apuuzwe. Achague kuwa askofu au mwanasiasa. Anachofanya hakikubaliki kwa Mungu wala kwa shetani. NI MNAFIKI
Watanganyika wanalalamika uhuru wao ndani ya mipaka ya nchi yao uko hatarini. Hiyo kadi ya Chadema ulimpa wewe? Kwa akili zako fupi hujui iko siku hata wewe hali yako inaweza kuwa mbaya, Askofu Mwamakula atageuka mtetezi wako.

Tambua tu, aliyezoea kula nyama za watu huwa haachi, akiwamaliza wa mbali, atawageukia ndugu zake.
 
Back
Top Bottom