Mawakili wa DKT. Rugemeleza Nshala wadai Askari wamepekua maktaba ya mteja wao kinyume cha Sheria

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987


Siku chache baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumpa wito Wakili Rugemeleza Nshala aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kufika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam, kuna mambo kadhaa yameibuka.

Ikumbukwe kuwa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar ilidai kuwa inafanya Uchunguzi kuhusu kauli zilizotolewa na Dkt. Nshala Julai 3, 2023 na kusambazwa katika Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii, hivyo wito huo unalenga kukamilisha Uchunguzi.

Julai 3, 2023, Dkt. Nshala alitoa maoni ya kupinga Makubaliano yanayohusu Uwekezaji, Uendelezaji na Uendeshaji wa Bandari uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na DP World akieleza baadhi ya Vifungu vinapingana na Katiba ya Nchi.

Tamko la leo Ijumaa Julai 14, 2023
Mawakili wa Dkt. Nshala, Nyaronyo Mwita Kicheere na Jebra Kambole wametoa tamko juu ya kinachoendelea kwa mteja wao.

Wakili wa Nyaronyo Kicheere amesema kuwa mnamo Julai 11, 2023, Polisi watatu waliwasilisha wito wa Kipolisi katika ofisi ya Dkt. Nshala wakimkata kufika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar (ZCO) saa tisa asubuhi ambayo ni usiku wa manane, na kuwa hadi wito ulipofika tayari ulikuwa upo nje ya muda.

Anasema Wanausalama hao mmoja alivaa kiraia huku wawili walivaa sare na kuwa walipofika katika ofisi ya Dkt. Nshila, askari mmoja aliingia kwenye maktaba ya mteja wao bila ruhusa wala kuwa na mtu mwingine aliyemsindikiza.

Ameeleza Askari mwingine aliingia upande wa pili wa ofisi na kufungua makabati mawili, moja likiwa ni la vitabu na majalada ya wateja wake na kabati lingine la nguo za Mahakama.

Amesema vitendo hivyo ni kinyume na Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara ikitoa haki ya faragha.

“Ofisi ya Wakili na nyaraka zake ni siri kati ya Wakili na wateja wake na kwa namna yoyote ile hatakiwi kutoa usiri huo kwa mtu yeyote.

“Askari kuingia kwenye ofisi ya wakili na kuanza kupekua nyaraka hizo ni kinyume ch Sheria na kanuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kanuni ya 30 ya Kanuni za Maadili ya Kitaaluma ua mawakili,” amesema.

Ameongeza kuwa Dkt. Nshala hajakataa wito wa Polisi bali akirejea Nchini ataitikia wito.

Ameongeza kuwa akirejea atatoa ufafanuzi wa kutoaminika kwa Rais na Waziri Mkuu, ni jukumu la kila raia kulinda Katiba ya Nchi, Arshi na umoja wa kitafa pamoja na kutoa ufafanuzi juu ya Ibara tata zinazokiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Naye, Jebra Kambole amesisitiza “Askari walivyofika ofisini kwa Dkt. Nshala, walifanya upekuzi bila mhusika kuwepo ndio maana tunasema ni kinyume cha Sheria, pia ulifika nje ya muda.

Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatoa haki ya faragha, mawakili tunawasiliana kwa njia ya nyaraka, kuna mikataba mbalimbali ya wateja.

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kuzingatia haki kwa kila mtu na haya mambo yanafanyika kwa mujibu wa Sheria.

Kama wakili anayejua Sheria anafanyiwa mambo kama hayo, vipi kuhusu raia wa kawaida ambaye hana ufahamu wa masuala ya Sheria! Tutawaeleza Polisi wamekiuka Katiba.

Nchi hii ni ya kwetu sote, Nchi ni ya Wananchi na ndio maana Serikali inapata mamlaka kupitia kwa Wananchi.
 
Sasa hao askari wameenda kupekua huko maktaba kutafuta nini?

Au wanataka kuvikamata vitabu vilivyompa Dr. Nshalla maarifa ya kuhoji ubovu wa ule mkataba wa hovyo wa bandari?

Hivi vitisho vya kijinga vimepitwa na wakati, acheni watu wahoji kazi yenu iwe kutoa majibu ya maswali yao, lakini huu mchezo wa vitisho hauna maana, hauwezi kuishinda nguvu ya dhamira zilizopo ndani ya watu.

Haya yote yanafanyika huku Samia akiwa kimya mpaka leo, kiongozi mkuu wa nchi aliyeamua kunyamaza kimya wakati ambao anaona kabisa kuna sintofahamu kwa wale anaowaongoza..

Huyu kiongozi ana nia mbaya kabisa na Tanganyika yetu, hatufai, ni dhaifu sana.
 
Hawamfanyi lolote,mwakabusi akimaliza mahojiano na tume anaenda Zambia kwa wajomba zake kupumzika🙏
 
Back
Top Bottom