uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Mjanja M1

    JamiiForums Tanzania Kinana: Wasimamizi wa Uchaguzi watakuwa Waadilifu na Waaminifu mnataka nini tena?

    Abdulrahman Kinana amesema Uchaguzi ujao utakuwa wa haki kwani wasimamizi watakuwa Waadilifu na Waaminifu. "Bunge limekubali (Bunge la Tanzania) limesema wasimamizi wa uchaguzi watakuwa watumishi wa umma waandamizi. Mtu atateuliwa kwa sifa; sifa za uadilifu, uhodari wa kazi na uaminifu...
  2. K

    JamiiForums Tanzania Mjadala bungeni kuhusu sheria ya uchaguzi

    Nimefuatilia mijadala Bungeni kuhusu Sheria za Uchaguzi. Nilitegemea kusikia ushauri, maoni yaliyotolewa na wadau wote yakijadiliwa moja baada ya moja lakini cha kushangaza Wabunge wengi wamejikita kujadili tu marekebisho kuhusu Wakurugenzi na Jinsia. Kuna ushauri uliotolewa na wadau kama...
  3. Msanii

    JamiiForums Tanzania Mene Mene Tekeli na Peresi... Kitanga kinaandika kwenye kuta za utawala wa nchi hii. mbele siyo kuzuri

    Tusidanganywe na lugha zenye hadaa nyingi za wabunge wetu wanaojadili miswada ya sheria za Uchaguzi. Hawana nia njema kwa nchi Hawana maono mema kwa nchi Hawana huruma kwa nchi. Kinachojulikana sasa ni kwamba, Serikali na Chama cha Mapinduzi ni wamoja dhidi ya uhalali, haki na wajibu kwa...
  4. Mystery

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Ni kwanini wabunge wa CCM waendelee kung'ang'ania wakurugenzi wa miji wawe wasimamizi wa uchaguzi, licha ya hao wakurugenzi kukosa sifa?

    Moja ya malalamiko makubwa kabisa ya chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na wananchi walio wengi nchini, ni kukosoa suala la wakurugenzi wa miji kuwa wasimamizi wa uchaguzi Mkuu. Ni jambo lililo wazi kuwa katika suala zito sana la uchaguzi Mkuu, ni lazima wanaopangwa kusimamia uchaguzi...
  5. chiembe

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 CHADEMA hawawatambui Halima Mdee na wenzake, lakini wanawataka wawapitishie sheria nzuri za uchaguzi, na wakaenda kuwapelekea maoni yao

    Mbombo ngafu, hii imekaaje? CHADEMA hawawatambui Halima Mdee na wenzake, lakini wanaenda kwenye kamati ya Bunge la akina Mdee kutoa maoni yao kuhusu sheria za uchaguzi, na wanatarajia hao hao wawapitishie sheria tamu na nzuri ambazo zitawafanya waanze kula, na wanaokula sasa wakubali kwa hiyari...
  6. Suley2019

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Mbunge Edward Olelekaita: Hakuna tatizo kubadili jina la Tume ya Uchaguzi

    Mbunge wa jimbo la Kiteto ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Edward Olelekaita amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikubainisha Tume ya Uchaguzi iitwe jina gani, hivyo hakuna tatizo katika kubadili jina la sasa ambalo ni Tume ya Taifa...
  7. Nehemia Kilave

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Nadhani Maandamano ya kudai Katiba MPYA yana tija zaidi kuliko kudai Tume Huru ya Uchaguzi

    Habari JF , kwa kifupi kabisa kwa katiba tuliyo nayo ni katiba ambayo ina upendeleo mkubwa kwa watawala na kuwapa nguvu kubwa kutawala . Kwa maana nyingine sio katiba ya kizalendo sababu haiwapi nguvu sana wananchi na hailindi sana mali za Nchi yetu . Chama chochote kikisha ingia madarakani...
  8. P

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Kampeni za Uchaguzi 2025 zimeanza?

    Wakuu, Msikilize kiongozi huyu aliye ambiwa amkaribishe Makonda, yaani ni kampeni kabisa zimeanza. "Wilaya ya Hai sasa imepata maendeleo makubwa, ninachotaka kuwaomba msifanye makosa, kina mama na akina baba twendeni na Dr. Samia Suluhu Hassan. "Tunakwenda kwenye uchaguzi mwaka kesho...
  9. P

    JamiiForums Tanzania Huwa unazingatia nini kabla hujaenda kuangalia mkutano wa kisiasa?

    Wakuu, Huwa unazingatia nini kabla hujaamua kwenda kwenye mkutano wa siasa, iwe mkutano wa hadhara au kampeni? Ni mada inayoenda kuzungumzwa, mzungumzaji mwenyewe, nguvu ya chama au nini? Nini huwa na umuhimu zaidi kwako ambapo kisipokuwepo huwezi kwenda kwenye mkutano huo au hata kuufatilia...
  10. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Dkt. Mhagama: Sheria za Uchaguzi zinazotungwa hazitazingatia maandamano yanayoendelea

    Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Dkt. Joseph Mhagama amesema maandamano sio suluhu ya kupata muafaka wa maoni ya Muswada wa Sheria ya Uchaguzi na kuongeza kuwa tayari maoni hayo yameshapokelewa na kupelekwa Bungeni na kamati yake inaendelea kuyachakata...
  11. P

    JamiiForums Tanzania Kauli gani kutoka kwa mwanasiasa ilikuvunja moyo kufatilia mambo ya siasa?

    Wakuu kwema? Kama kichwa kinavyosema hapo juu, kauli gani imewahi kutolewa na mwanasiasa iwe kwenye kampeni, mkutano wa hadhara, au kiongozi akiwa anatimiza majukumu yake ikakufanya uchukie siasa ama uache kabisa kufatilia mambo yanayohusu siasa? "Haiwezekani Mkurugenzi nikuteue mimi...
  12. TZ-1

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 LGE2024 Rais Samia: Jeshi na vikosi vyote vya Ulinzi vikae tayari kwa lolote wakati wa uchaguzi

    Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba mwaka huu na mwakani tunaelekea kwenye chaguzi za nchi yetu na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii, mwaka huu tunaanza...
  13. R

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Kutofautiana kauli na mtizamo wa Katibu Mkuu na Mwenezi CCM kunaashiria nini kuelekea Uchaguzi?

    Salaam, Shalom!! Katibu MKUU wa CCM ameanza ziara yake kivyake na anasema yake, wakati huo huo Mwenezi naye ameendelea na uelekeo wake. KM anasema, viongozi wa CCM wasiwakaripie hadharani watendaji wa Serikali, wakati huo huo Mwenezi Yeye ameendelea kupiga simu akiwahoji na Kutoa maelekezo...
  14. Heparin

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Dkt. Nchimbi: Makundi baada ya uchaguzi hayatavumiliwa ndani ya CCM

    Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amekemea na kuonya tabia ya baadhi ya Wana CCM wanaovunja taratibu za Chama kwa kuendekeza makundi baada ya uchaguzi, akisema haikubaliki na haitavumiliwa ndani ya CCM. Amesema kuwa ni muhimu Kiongpzi anayeshinda awe...
  15. Heparin

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Makonda: Yetote mwenye sifa atasimamia uchaguzi

    “Wanasema wakurugenzi wasisimamie uchaguzi. Sisi tunasema Mtanzania mwenye sifa Tume itampa nafasi ya kusimamia uchaguzi.” – Paul Makonda, Katibu wa Halmashauri Kuu CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo PIA, SOMA: Matamko mengine ya Makonda Makonda: 2024 na 2025 tutakupima kwa kazi; sio kwa...
  16. Msanii

    JamiiForums Tanzania Mfumuko wa bei upo juu, Viongozi wapo bize na uchaguzi na kununua makasri Dubai

    Ndugu zangu, Bidhaa ghafi kama sukari inakimbilia TZS 5,000+ halafu Waziri wa Kilimo anatuambia mashamba ya miwa yamejaa maji... ina maana mipango na mikakati ya serikali ni namna wanavyosurvive leo na hawana 10+ years plan. Serikali haina akiba ya chakula ndiyo maana soon watakimbilia...
  17. The Sheriff

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Makonda: 2024 na 2025 tutakupima kwa kazi; sio kwa maneno, sio kwa kugawa kanga kipindi cha uchaguzi

    Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda, leo January 19,2024 ameanza ziara yake kwa kuongea na Wakazi wa Tegeta Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema Wabunge, Wawakilishi na Madiwani watapimwa kwa kazi wanazofanya na sio kwa maneno au kujipendekeza kwa...
  18. K

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Kama itapendeza uchaguzi usogezwe mbele na Rais apewe muda ili tupate Katiba Mpya

    Kama itapendeza Chaguzi zote zisogezwe mbele kwa muda wa miaka miwili na Rais aendelee kutawala na kumpa muda wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ili uchaguzi uwe huru na wa haki. Mambo yote yanayobishaniwa mfano Rais kumchagua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Rais kumteua Mkurugenzi wa Uchaguzi...
  19. P

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Askofu Mwamakula: Naona huu sio muda sahihi wa kuwahukumu wabunge kuhusu miswada ya sheria za uchaguzi

    Wakuu kwema? Askofu Mwamakula akiwa anahojiwa na mwandishi wa habari kutoka Jambo TV amesema anaona sasa sio muda sahihi wadau na vyama vya siasa kuanza kuwahukumu wabunge juu ya miswada ya sheria ya sheria za uchaguzi inayotarajiwa kurudi bungeni kusomwa tena baada ya kupokea maoni kutoka kwa...
  20. Ritz

    JamiiForums Tanzania Msajili: Vyama vya Siasa vinatakiwa kufanya uchaguzi wa viongozi kama Sheria inavyowataka na kuepuka kukaa muda mrefu bila uchaguzi

    Wanaukumbi. Vyama vya siasa ambavyo muda wa ongozi wa viongozi wake unakaribia kuisha, vinakumbushwa kufanya uchaguzi wa viongozi wake kabla ya muda huo kuisha..
Back
Top Bottom