Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,047
Moja ya malalamiko makubwa kabisa ya chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na wananchi walio wengi nchini, ni kukosoa suala la wakurugenzi wa miji kuwa wasimamizi wa uchaguzi Mkuu.
Ni jambo lililo wazi kuwa katika suala zito sana la uchaguzi Mkuu, ni lazima wanaopangwa kusimamia uchaguzi huo wawe watu waaminifu sana na watambulike kwa jamii kuwa watatekeleza "fairness" katika chaguzi hizo.
Lakini hoja hiyo inapingwa vikali na wabunge wa CCM na wanaendelea kuunga mikono kuwa hao makada wa CCM ndiyo wanaostahili kusimamia chaguzi hizo, katika mjadala wa miswada hiyo 3 iliyowasilishwa bungeni, ili hatimaye ipitishwe na kuwa sheria.
Tunatambua wazi kuwa hao wakurugenzi ni makada kindakindaki wa CCM, ambao wengi wao wameteuliwa kushika madaraka hayo, baada ya kushindwa kwenye kura za maoni ya kugombea ubunge kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Hivi itakuwaje hao wakurugenzi wasiwe "biased" katika chaguzi hizo?
Niwaulize saali dogo tu hao wabunge wa CCM, hivi kweli inaingia akilini, kwa pambano la mpira la Simba na Yanga, ukute amepangwa refa ambaye ni mshabiki kindakindaki wa timu mojawapo?
Hivi hiyo timu nyingine pinzani inaweza kukubali kuingia kwenye mechi hiyo??
Kama hao wabunge wa CCM wanajua wazi kuwa HAIWEZEKANI kabisa kwa hiyo timu pinzani kuingiza timu yao, je ni kwanini wao waamini vyama vya upinzani vinaweza kuingia kwenye uchaguzi, wakati wasimamizi (marefa) ni hao makada kindakindaki wa CCM??