Makonda: 2024 na 2025 tutakupima kwa kazi; sio kwa maneno, sio kwa kugawa kanga kipindi cha uchaguzi

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda, leo January 19,2024 ameanza ziara yake kwa kuongea na Wakazi wa Tegeta Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema Wabunge, Wawakilishi na Madiwani watapimwa kwa kazi wanazofanya na sio kwa maneno au kujipendekeza kwa Viongozi ambapo amesemaa wasiofanya kazi taarifa zao zitapelekwa kwa Mwenyekiti wa CCM (Rais Dkt. Samia), kwamba hawafai kupewa nafasi ya kugombea tena mwaka 2025.

Makonda amenukuliwa akisema “Duniani kote hawajawahi kumaliza matatizo hata Mataifa makubwa tunayokimbilia kuyaomba bado yana changamoto, nilikuwa namsikia Rais wa Marekani anajadili jinsi gani wanataka kujenga barabara na madaraja kwenye Nchi yao Marekani nao wapo kwenye ujenzi wa barabara, tafsiri yake ni kwamba changamoto haziwezi kuisha siku moja, zinaendelea kuwepo kutokana na idadi ya Watu, mabadiliko ya tabianchi na hali ya kiuchumi, vinginevyo tungeweza kujenga lami kote

“Mwaka huu 2024 na 2025 tutawapima Wabunge na Wawakilishi na Madiwani namna gani wanatatua changamoto za Wananchi wao na jinsi gani wapo mstari wa mbele kukijenga Chama chao, awamu hii CCM hii ya Dkt. Samia na Mimi nikiwa Msemaji na nimeshasema tangu nakabidhiwa ofisi sitobeba mzigo kila Mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kama hamfanyi kazi ya utekelezaji wa Ilani na kutatua changamoto za Watu, kwa kauli moja tutakupima kwa kazi, sio kwa maneno, sio kwa kugawa kanga kipindi cha uchaguzi na kuwarubuni Wajumbe, sio kwa kujipendekeza kwa Viongozi bali tukienda kwa Wananchi wakasema naam Mbunge wetu ndiye alipambania hii Shulea au Kituo cha Afya kikajengwa kauli hizo ndio zitafanya uteuliwe tena kupeperusha bendera ya CCM”

“Na kwenye ziara kote nitakakopita kama wewe Mbunge haufanyi kazi na hauonekani tunayo Timu ya kutosha kuchukua taarifa tutampelekea taarifa Mwenyekiti, kwamba Mwenyekiti tukienda na huyu tunapigwaa”

========For English Audience Only==========

NEC Secretary Paul Makonda Launches Accountability Tour, Pledges Performance Evaluation for CCM Representatives

On January 19, 2024, the Secretary of the National Executive Committee for Ideology, Publicity, and Training, Paul Makonda, embarked on a tour starting in Tegeta, Dar es Salaam. During his interaction with residents, Makonda announced a robust accountability initiative, stating that Members of Parliament, Representatives, and Ward Councilors would be assessed based on their actions and achievements rather than unfulfilled promises and Favours from other leaders.

Makonda emphasized that the upcoming evaluation would focus on how well elected officials addressed the challenges faced by their constituents and contributed to the growth of the ruling party, CCM. He was quoted saying, "In 2024 and 2025, we will assess Members of Parliament, Representatives, and Ward Councilors on how they solve the people's challenges and how actively they contribute to building their party. In this term under President Samia and myself as the spokesperson, I have made it clear that I will not carry anyone's burden. If you are not actively implementing the party's manifesto and solving people's issues, we will assess you based on your actions, not words."

Makonda further stressed that the focus of this evaluation would be on tangible accomplishments rather than pre-election promises or attempts to influence party leaders. He affirmed that representatives failing to deliver on their responsibilities would be reported to the CCM Chairman, President Samia Suluhu Hassan.

During his tour, Makonda assured the public that a comprehensive team would gather information on the performance of elected officials. He warned that those found lacking in their duties would face repercussions, including the possibility of not being selected to run for office in the 2025 elections. However, the public is questioning if all these efforts are done because we about to elect new leaders.

PIA, SOMA:


Uteuzi Katibu Mwenezi​
Matamko mengine
 
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda, leo January 19,2024 ameanza ziara yake kwa kuongea na Wakazi wa Tegeta Jijini Dar es salaam ambapo pamoj na mambo mengine amesema Wabunge, Wawakilishi na Madiwani watapimwa kwa kazi wanazofanya na sio kwa maneno au kujipendekeza kwa Viongozi ambapo amesemaa wasiofanya kazi taarifa zao zitapelekwa kwa Mwenyekiti wa CCM (Rais Dkt. Samia), kwamba hawafai kupewa nafasi ya kugombea tena mwaka 2025.

Makonda amenukuliwa akisema "Duniani kote hawajawahi kumaliza matatizo hata Mataifa makubwa tunayokimbilia kuyaomba bado yana changamoto, nilikuwa namsikia Rais wa Marekani anajadili jinsi gani wanataka kujenga barabara na madaraja kwenye Nchi yao Marekani nao wapo kwenye ujenzi wa barabara, tafsiri yake ni kwamba changamoto haziwezi kuisha siku moja, zinaendelea kuwepo kutokana na idadi ya Watu, mabadiliko ya tabianchi na hali ya kiuchumi, vinginevyo tungeweza kujenga lami kote"

"Mwaka huu 2024 na 2025 tutawapima Wabunge na Wawakilishi na Madiwani namna gani wanatatua changamoto za Wananchi wao na jinsi gani wapo mstari wa mbele kukijenga Chama chao, awamu hii CCM hii ya Dkt.

Samia na Mimi nikiwa Msemaji na nimeshasema tangu nakabidhiwa ofisi sitobeba mzigo kila Mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kama hamfanyi kazi ya utekelezaji wa llani na kutatua changamoto za Watu, kwa kauli moja tutakupima kwa kazi, sio kwa maneno, sio kwa kugawa kanga kipindi cha uchaguzi na kuwarubuni Wajumbe, sio kwa kujipendekeza kwa Viongozi bali tukienda kwa Wananchi wakasema naam Mbunge wetu ndiye alipambania hii Shulea au Kituo cha Afya kikajengwa kauli hizo ndio zitafanya uteuliwe tena kupeperusha bendera ya CCM"

"Na kwenye ziara kote nitakakopita kama wewe Mbunge haufanyi kazi na hauonekani tunayo Timu ya kutosha kuchukua taarifa tutampelekea taarifa Mwenyekiti, kwamba Mwenyekiti tukienda na huyu tunapigwaa"

Millard Ayo
 
Back
Top Bottom