Dkt. Nchimbi: Makundi baada ya uchaguzi hayatavumiliwa ndani ya CCM

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amekemea na kuonya tabia ya baadhi ya Wana CCM wanaovunja taratibu za Chama kwa kuendekeza makundi baada ya uchaguzi, akisema haikubaliki na haitavumiliwa ndani ya CCM.

Amesema kuwa ni muhimu Kiongpzi anayeshinda awe Mnyenyekevu kutumikia nafasi yake aliyochaguliwa na yule anayeshindwa anapaswa kuvumilia hadi mwaka mwingine, huku akisisitiza kwamba mambo yote mawili, kushinda na kushindwa katika uchaguzi, huenda sambamba na mipango ya Mungu.

Dkt. Nchimbi amesema hayo wakati akiwahutubia Wanachama wa CCM na Wananchi wa Zanzibar, waliojitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya kumpokea Kiongozi huyo, yaliyofanyika leo Ijumaa, January 19,2024 Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, iliyoko eneo la Kisiwandui, Unguja.

Dkt. Nchimbi amesema Chama Cha Mapinduzi kimedhamiria kwa dhati kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuhakikisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, inadumishwa ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuwaenzi waasisi wa Mapinduzi hayo, ambao walikusudia kuhakikisha Wazanzibar wote wanakuwa wamoja katika kutafuta ustawi na maendeleo ya Zanzibar, bila kujali tofauti za kisiasa, kidini, rangi, kabila, wala hali zao za maisha.

“Wana CCM wote tunapokwenda kwenye uchaguzi tutaanza kumnong’ononeza Mtu mmoja unataka kugombea anakwambia anakuunga mkono anakuwa wa kwanza, unamnong’oneza wa pili, wa tatu, wa nne wakati mwingine wanafika 20,30,40 wakishafika hapo wanaitwa kundi kwa hiyo unakuwa na kundi lako wewe na wenzako, hivyo hivyo na mwingine na mwingine hivyo, tukimaliza uchaguzi makundi lazima yafe, unapotoka kupika ndio unawasha moto, ukiipua unauzima moto wako, ni Mjinga peke yake anayekoleza moto wakati keshapakua”

==========For English Audience Only=============
CCM Secretary General Warns Against Factionalism Post-Elections

The Secretary General of the ruling party Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr. Emmanuel John Nchimbi has recently address members of CCM and strongly condemned and warned them against breaking regulations of the party and the formation of factions amongst themselves after elections, asserting that such behavior is unacceptable within CCM. He emphasized that unity is key, and divisive actions undermine the core values of the party and the nation.

Dr. Nchimbi emphasized the importance of humility in both winning and losing, urging elected leaders to serve their positions with humility and those who face defeat to patiently wait for the next opportunity. He emphasized that both success and failure in elections are part of a greater plan.

Addressing a crowd at the CCM headquarters in Zanzibar, Dr. Nchimbi stated that the party is dedicated to honoring the Revolutionary ideals of Zanzibar and ensuring the continuity of the National Unity Government in Zanzibar. This unity, he stressed, is crucial in upholding the principles laid out by the founders of the Revolution, aiming for the collective well-being and development of Zanzibar, irrespective of political, religious, ethnic, or socio-economic differences.

As the CCM Secretary General concluded his address, he urged party members to foster unity and discouraged the formation of divisive factions, stating, "It is foolish to stoke the fire after cooking. If you don't need the fire, put it out. Only a fool keeps fueling the fire when it's already burning."

The Secretary General's stern warning against post-election factionalism underscores the party's commitment to internal cohesion and adherence to the ideals of the Zanzibar Revolution.​
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amekemea na kuonya tabia ya baadhi ya Wana CCM wanaovunja taratibu za Chama kwa kuendekeza makundi baada ya uchaguzi, akisema haikubaliki na haitavumiliwa ndani ya CCM...
Binadamu wanabadilika kwani Nchimbi huyu ni tofauti na yule wa timu lowassa?
 
Back
Top Bottom