Mfumuko wa bei upo juu, Viongozi wapo bize na uchaguzi na kununua makasri Dubai

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,626
29,786
Ndugu zangu,
Bidhaa ghafi kama sukari inakimbilia TZS 5,000+ halafu Waziri wa Kilimo anatuambia mashamba ya miwa yamejaa maji... ina maana mipango na mikakati ya serikali ni namna wanavyosurvive leo na hawana 10+ years plan.

Serikali haina akiba ya chakula ndiyo maana soon watakimbilia kuagiza sukari kutoka nje.


Tumemsikia mkosa tonge mmoja juzi hapa akimwaga siri za mtungi kwamba viongozi wengi wananunua majumba Dubai tena kwa cash.

Tunawaona CCM wakihaha huku na kule kwa uchaguzi mkuu ujao na agenda kuu ya nchi sasa ni mitano mingine kwa mama. Na wataanza kuchomoana uhai soonest.

Serikali hasa mama (ambaye ndiye kila kitu) wamefeli pabaya mno. Ameteua wasaidizi wanaofanana naye yaani lazy affair hawajigusi wala kustushwa na kuanguka kwa nchi upande wa mfumuko na uhaba.

Hakuna umeme na maji, hakuna anayesema lolote kiasi kwamba tunaona kabisa, kumbe wanatengeneza matatizo ili wayatumie kwenye kampeni za uchaguzi.

Tunakwama wapi.....
 
Umeenda mbali sana, Dubai?

mbowe-jpeg.2812967

...wengine wanasema ukiwa na mjumba, huwezi kufisadi.
 
Mkuu
Yes wapo watawala. Walijitwalia mamlaka kwa kupora chaguzi na kutengeneza katiba za kubumba
Jibu zuri, hii nchi hatuna viongozi tuna watawala, bado hatujapata viongozi, siku tukipata hizi kero zitapungua.
 
Nataka majina ya hao Wanaoshindana kununua makasri kwa kodi zetu huko Dubai yawekwe hapa tuwalaani.
 
Back
Top Bottom