Rais Samia: Jeshi na vikosi vyote vya Ulinzi vikae tayari kwa lolote wakati wa uchaguzi

TZ-1

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
3,208
5,441

Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba mwaka huu na mwakani tunaelekea kwenye chaguzi za nchi yetu na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii, mwaka huu tunaanza na chaguzi za serikali za mitaa kwa sababu tuko wengi, ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa kwahiyo ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitogeza.

Hatusemi tukafanye chaguzi za kutumia nguvu hapana, taratibu, sheria na miongozo ya uchaguzi itafuatwa lakini Jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vikae tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza, mwakani tunaenda kwenye uchaguzi mkuu na ule ndiyo wenye vishindo vikubwa basi ikabidi nitoe tu taarifa na kuwaweka 'alert' kwamba hayo mambo yanakwenda kutokea na jeshi hatuna budi kujiweka tayari.

========For English Audience Only===========

President Samia: Military and Defense Forces Should Be Ready for Any Situation During Elections
President Samia Suluhu has addressed the need of heightened security in the country because of the upcoming local and general elections in our country this and next year. She has requested the Tanzania People's Defense Force to get prepared due to the vast population in the country and the involvement of multiple political parties with diverse agendas. This action is for the purpose of making sure everything goes according to plan and to be ready to face any unforeseen challenges.

She added "Let me emphasize that we are not advocating the use of force in elections. The electoral processes will strictly adhere to procedures, laws, and guidelines. However, the military and all security forces must be prepared to address any situations that may arise. Next year, we will be heading into the general elections, which are known for their significant dynamics. Therefore, I felt it necessary to provide this alert, urging the military to be ready for potential developments."

Furthermore, she added that it is not about using force but rather about being proactive and ready to ensure safety and stability of our nation during these critical times. Let us be vigilant and steadfast, adhering to the rule of law while maintaining a readiness to address any challenges that may emerge.
 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT amevitaka vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na hasa Jeshi kukaa tayari Kwa Lolote Ili kulinda amani ya Nchi wakati Taifa linajitayarisha na uchaguzi Mkuu kuanzia mwaka huu.

Sio Kwa Nia mbaya ni Kwa Nia njema tuu maana Machadema hayakawii kuogopa 😆😆

===

Watani zangu CHADEMA wataanza kulialia kama kawaida yao.maana wamezoea malalamiko na kulialia kama vifaranga vya kuku vilivyotelekezwa
 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT amevitaka vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na hasa Jeshi kukaa tayari Kwa Lolote Ili kulinda amani ya Nchi wakati Taifa linajitayarisha na uchaguzi Mkuu kuanzia mwaka huu.

Sio Kwa Nia mbaya ni Kwa Nia njema tuu maana Machadema hayakawii kuogopa 😆😆

View: https://twitter.com/eastafricatv/status/1749370818486747229?t=UXieFH56JudV5tJ7GtRzyg&s=19

Amri nyinginw inayoenda kuvuruga zoezi la uchaguzi.

Circumstantial ameongea neno la kitisho kwa wapigakura.

Rais ambaye anawaambia wanajeshi na wanausalama wajiandae kwa lolote, maana yake yeye na chama chake wamejipanga kuyokabidhi madaraka wakianguankwenye uchaguzi hivyo jeshi lisimamie hilo.

Mark my words, uchaguzi ujao tutawaona mabaka mabaka kwenye vituo vya kura. Hii ni kinyume na Katiba.

Wapenda DEMOKRASIA tunapinga na kulaani kauli ya rais kuwaalika wanajeshi kwenye michakato ya chaguzi. Wanajeshi wasihusishwe na siasa. Inatosha sasa
 
Baki kwenye reli acha porojo wewe zisizo na msingi.

Acheni msishiriki si mumesema mtagoma muone
 
Mimi ni CCM hai, nalipia mpaka ada za jumuiya ya Wazazi niliyomo. Lakini kuta yangu ya urais na mbunge napigia ipinzani na hauna la kunifanya.
Sasa kama umeamua kupoteza kura Yako itakusaidia nini?

Hakuna Rais wa upinzani Tzn hii na wewe unalijua Hili vizuri
 
Back
Top Bottom