Askofu Mwamakula: Naona huu sio muda sahihi wa kuwahukumu wabunge kuhusu miswada ya sheria za uchaguzi

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu kwema?

Askofu Mwamakula akiwa anahojiwa na mwandishi wa habari kutoka Jambo TV amesema anaona sasa sio muda sahihi wadau na vyama vya siasa kuanza kuwahukumu wabunge juu ya miswada ya sheria ya sheria za uchaguzi inayotarajiwa kurudi bungeni kusomwa tena baada ya kupokea maoni kutoka kwa wadau.

Mwamakula amesema kwa sasa baadaya ya wadau kutoa maoni Kamati, serikali na wabunge wana nafasi ya kurekebisha na kuboresha miswada hiyo, na kwamba kuwahukumu wabunge sasahivi wanaweza kusema muswada bado haujafika kwao, Kamati ikianza kunyooshewa mikono inaweza kusema bado wanapokea maoni na hawajatoa muhtasari, vipi kama maono yao yamefanyiwa kazi?

Serikali nayo ikianza kunyooshewa mikono sasa hivi wanaweza kusema wanasubiri maoni yakikusanywa ikienda pale bungeni wanaweza kuinyofoa miswada hiyo, na kwamba anaona kwa sasa bado sio muda sahihi wa kuwahukumu.

Akiongeza kuwa hapingi wanaokataa miswada hiyo isifike kabisa bungeni sasa hivi sababu ni maoni yao, wanatakiwa wasikilizwe na wasipuuzwe, lakini yeye anaona sio muda sahihi.
 
Huyu askofu wa mchongo ni wakati gani anafanya kazi yake? Km anataka siasa si ajitose?
Na huyu shehe ubwabwa hapa anafanya nini? Wacheni chuki zenu za kipumbavu
JamiiForums-903871903.jpg
 
Askofu machachari, Mwamakula ameeleza kwamba chadema hawana sababu za msingi kuandamana kwa kuwa maoni waliyotoa bado yanafanyiwa kazi, na bado wanasubiri mrejesho.

Mwamakula ni mmoja kati ya watu wengi ambao wamewapuuza chadema kwa kufanya maamuzi ya hovyo.

Wengine no jumuiya ya wafanyabiashara nchi nzima, vyama vya siasa na wananchi wa kawaida.
---

Mwamakula.jpg

Askofu Mwamakula

Ili miswada kuwa sheria inapitia katika hatua mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa maoni, kupelekwa bungeni hatua ambazo zinakuwa na muda maalumu. Hayo yamesemwa na Askofu Emmaus Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Morovian amesema, mchakato kwenye mahojiano na Jambo TV ofisini kwake ambapo amesisitiza kuwa, kwa hatua ya sasa ni kukusanya maoni kwa ajili ya kuboresha miswada hiyo.

Ameendelea kwa kusema kuwa, serikali inayo nafasi ya kuifanyia marekebisho miswada kabla haijafikishwa bungeni lakini pia inayo nafasi ya kuiondoa miswada hiyo kwa ajili ya kwenda kuirekebisha. Askofu Mwamakula ameongeza kuwa, kwa sasa haipaswi kuilaumu serikali, bunge au wabunge kwani bado muda wa kufikishwa huko bado na suala hilo lipo kwenye kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Kuhusu wakati gani wa kuinyooshea serikali, Askofu Mwamakula amesema "Tunataka kuiangalia serikali kama imeyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wananchi na kama haijayafanyia kazi hapo ndipo tutaanza kusema.

Kama wananchi wametoa maoni na hayajafanyiwa kazi na Bunge pamoja na kamati ya Bunge, nawakati huo serikali imeona hayo mapungufu na haijachukua hatua yoyote kurekebisha, hapo tutainyooshea kidole serikali" Alisisitiza Askofu Mwamakula Vilevile amesema, kazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ni kukusanya maoni na kwa uelewa wake inayo pia nafasi ya kuboresha miswada na baada ya hapo wataipeleka bungeni kwa wabunge ambapo watapata nafasi ya kuijadili, kuiboresha au kuikataa ile miswada."

Tukiinyooshea kidole serikali, Serikali itasema tunasubiri hayo maoni yakikusanywa kisha yakienda pale bungeni tunaweza tukinyofoa hiyo miswada.Tukiwahukumu wabunge hivi sasa watasema hiyo miswada iko wapi? Au tukiinyooshea kidole Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria watasema ndio kwanza tunakusanya maoni, na hatujatoa hata muhtasari, mmejuaje hayo maoni kuwa tumeyakataa?"

Wakati hayo yakiendelea, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chini ya mwenyekiti wake Freeman Mbowe alitangaza kufanyika kwa maandamano mnamo tarehe 24 Januari, mwaka huu kwa walichodai ni katika kuishinikiza serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau wa uchaguzi nchini.

Kauli ya Mbowe imekuja wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ikikamilisha zoezi la ukusanyaji wa maoni kuhusu miswada mitatu iliyosomwa bungeni jijini Dodoma mwezi Novemba, 2023.

Miswada hiyo ni muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sheria wa mwaka 2023, muswada wa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi wa mwaka 2023 na Muswada w Sheria ya Marekebisho wa Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2023.Kufuatia hayo, Askofu Mwamakula ametoa maoni yake kwa kusema kwamba"Nimesoma ile miswada, yale yote ambayo wanayalalamikia (CHADEMA) yapo kwenye public domain (yapo hadharani) na kila mtu anajua.

Ilipotoka nafasi ya serikali kupeleka miswada bungeni ilipeleka miswada, sasa imekuja nafasi ya Kamati ya Kudumu ha Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuchukua maoni ya wananchi pamoja na wadau, mimi Askofu (Mwamakula) na wadau wengine tuliiambia serikali sikilizeni ya wananchi na pia tuliwaambia wananchi pelekeni maoni yenu.

Tunataka kuiangalia serikali kama imeyafanyia kazi Maoni na kama haijayafanyia kazi ndipo tutaanza kusema, lakini sio sasa" alihitimisha Askofu Mwamakula
 
Askofu machachari, Mwamakula ameeleza kwamba chadema hawana sababu za msingi kuandamana kwa kuwa maoni waliyotoa bado yanafanyiwa kazi, na bado wanasubiri mrejesho...
Kwa hiyo sisi tunaoyakubali haya maandamano tunatoka nchi gani?
 
Askofu machachari, Mwamakula ameeleza kwamba chadema hawana sababu za msingi kuandamana kwa kuwa maoni waliyotoa bado yanafanyiwa kazi, na bado wanasubiri mrejesho.

Mwamakula ni mmoja kati ya watu wengi ambao wamewapuuza chadema kwa kufanya maamuzi ya hovyo.

Wengine no jumuiya ya wafanyabiashara nchi nzima, vyama vya siasa na wananchi wa kawaida.
---

View attachment 2877568
Askofu Mwamakula

Ili miswada kuwa sheria inapitia katika hatua mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa maoni, kupelekwa bungeni hatua ambazo zinakuwa na muda maalumu. Hayo yamesemwa na Askofu Emmaus Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Morovian amesema, mchakato kwenye mahojiano na Jambo TV ofisini kwake ambapo amesisitiza kuwa, kwa hatua ya sasa ni kukusanya maoni kwa ajili ya kuboresha miswada hiyo.

Ameendelea kwa kusema kuwa, serikali inayo nafasi ya kuifanyia marekebisho miswada kabla haijafikishwa bungeni lakini pia inayo nafasi ya kuiondoa miswada hiyo kwa ajili ya kwenda kuirekebisha. Askofu Mwamakula ameongeza kuwa, kwa sasa haipaswi kuilaumu serikali, bunge au wabunge kwani bado muda wa kufikishwa huko bado na suala hilo lipo kwenye kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Kuhusu wakati gani wa kuinyooshea serikali, Askofu Mwamakula amesema "Tunataka kuiangalia serikali kama imeyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wananchi na kama haijayafanyia kazi hapo ndipo tutaanza kusema.

Kama wananchi wametoa maoni na hayajafanyiwa kazi na Bunge pamoja na kamati ya Bunge, nawakati huo serikali imeona hayo mapungufu na haijachukua hatua yoyote kurekebisha, hapo tutainyooshea kidole serikali" Alisisitiza Askofu Mwamakula Vilevile amesema, kazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ni kukusanya maoni na kwa uelewa wake inayo pia nafasi ya kuboresha miswada na baada ya hapo wataipeleka bungeni kwa wabunge ambapo watapata nafasi ya kuijadili, kuiboresha au kuikataa ile miswada."

Tukiinyooshea kidole serikali, Serikali itasema tunasubiri hayo maoni yakikusanywa kisha yakienda pale bungeni tunaweza tukinyofoa hiyo miswada.Tukiwahukumu wabunge hivi sasa watasema hiyo miswada iko wapi? Au tukiinyooshea kidole Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria watasema ndio kwanza tunakusanya maoni, na hatujatoa hata muhtasari, mmejuaje hayo maoni kuwa tumeyakataa?"

Wakati hayo yakiendelea, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chini ya mwenyekiti wake Freeman Mbowe alitangaza kufanyika kwa maandamano mnamo tarehe 24 Januari, mwaka huu kwa walichodai ni katika kuishinikiza serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau wa uchaguzi nchini.

Kauli ya Mbowe imekuja wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ikikamilisha zoezi la ukusanyaji wa maoni kuhusu miswada mitatu iliyosomwa bungeni jijini Dodoma mwezi Novemba, 2023.

Miswada hiyo ni muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sheria wa mwaka 2023, muswada wa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi wa mwaka 2023 na Muswada w Sheria ya Marekebisho wa Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2023.Kufuatia hayo, Askofu Mwamakula ametoa maoni yake kwa kusema kwamba"Nimesoma ile miswada, yale yote ambayo wanayalalamikia (CHADEMA) yapo kwenye public domain (yapo hadharani) na kila mtu anajua.

Ilipotoka nafasi ya serikali kupeleka miswada bungeni ilipeleka miswada, sasa imekuja nafasi ya Kamati ya Kudumu ha Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuchukua maoni ya wananchi pamoja na wadau, mimi Askofu (Mwamakula) na wadau wengine tuliiambia serikali sikilizeni ya wananchi na pia tuliwaambia wananchi pelekeni maoni yenu.

Tunataka kuiangalia serikali kama imeyafanyia kazi Maoni na kama haijayafanyia kazi ndipo tutaanza kusema, lakini sio sasa" alihitimisha Askofu Mwamakula
Nadhani ugomvi mkubwa unaanzia pale hoja na dhana ya minimum Reform ya ibara muhimu za katiba inapokataliwa na kamati ya Bunge. Shida iliyopo ni kuhusu methodology na approach inayofaa kuhusu maboresho ya miswada. Ifanyikeje kuleta tija. Hili ndilo limetikisa nchi,Askofu alione hilo ambalo ndilo limeleta mgongano. Arejee hoja za Zitto Kabwe na mapendekezo ya Kamati ya Rais.
 
Back
Top Bottom