Msajili: Vyama vya Siasa vinatakiwa kufanya uchaguzi wa viongozi kama Sheria inavyowataka na kuepuka kukaa muda mrefu bila uchaguzi

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,580
17,685
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini imevikumbusha Vyama ambavyo muda wa Uongozi wa Viongozi wake unakaribia kuisha, kufanya Uchaguzi wa Viongozi hao kabla ya muda huo haujaisha

Barua iliyotumwa kwa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye Usajili kamili leo, Alhamisi Januari 18.2024 imefafanua kuwa Kifungu cha 9(2)(e) kikisomwa pamoja na Kifungu cha 8D(1) cha Sheria 'The Political Parties Act, CAP 258' kinaelekeza kuwa kila Chama cha Siasa kinapaswa kufanya Uchaguzi wa Kidemokrasia wa Viongozi wake kwa Vipindi ambavyo vimewekwa katika Katiba yake

Aidha, Barua hiyo ambayo imesainiwa na Sisty Nyahoza ambaye ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi imeendelea kufafanua kuwa Kanuni ya 16 ya Kanuni 'The Political Parties (Registration and Monitoring) Regulations, 2019 (TS. 953/2019)' inaeleza kuwa Uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Siasa unapaswa kufanyika siyo zaidi ya miaka Mitano (5) tangu Uchaguzi uliopita kufanyika na kwamba Chama husika kitaomba ruhusa ya Msajili wa Vyama vya Siasa endapo kinataka kufanya Uchaguzi zaidi ya kipindi hicho.
20240118_161947.jpg
 
Msajili mbona yakiongelewa ya CCM haongei kitu huyu ni msajiliCCM.

Huyu ni kada uchwara na inabidi tumkumbushe na tuanzie hapo kwenye mapendekezo yaliyotolewa kwenye hiyo barua ina miaka 3 ikielekea 4 alifanyia kazi?
images (1).png
 
Mbona msajili ana haraka sana, anaogopa kitu gani?

Kawakumbusha wafanye maana yake anajua huwa wanasahau, au inakuwaje?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Just a remainder kama ambavyo TRA inavyokumbusha walipa Kodi.
Na sio kwamba eti wamesahau ndio maana akasema watoe taarifa za either kusogeza mbele au kucomply na Sheria inavyosema.
 
Mbowe si amuweke hata shemeji yake yoyote kuwa mwenyekiti!?.....ama basi hata babamkwe wake!....

Kuepuka hii kadhia ya chama cha kifamilia na kikanda!.... Ama anataka afie hapo!?
Na kwa nini asiwe Lissu?, anyway hayo ni maoni yako .
 
Back
Top Bottom