Wazee wenzangu wa kuweka mzigo (Kubet) - karibuni tubashiri mechi za leo!

Rockcity native

Rockcity native

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2012
Messages
2,094
Points
1,500
Rockcity native

Rockcity native

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2012
2,094 1,500
Karibuni tuinvest katika soko letu la hisa iwe meridian, iplay8 casino, m-bet, premier betting, skybet, landbrokerz, bet365... n.k
GG (maana yake tim zote zifungane).. GGGG ( tim zote zifungane kila kipindi)

2+ (katika mechi yote yapatikane magoli kuanzia mawili)...

I 2+ (kipindi cha kwanza yapatikane magoli kuanzia mawli)...

II2+ (kipindi cha pili yapatikane magoli kuanzia mawili)....

H2+ (tim ya nyumbani ipate magoli kuanzia mawili)...

A2+ (timu ya ugenini ipate magoli kuanzia mawili)...
Watu wengi katika ulimwengu wa GAMBLING wanajikuta wakipoteza kiasi kikubwa cha pesa bila hata ya kujitambua.Ni kutokana na kutokujua au kutambua misingi kadhaa ya kushiriki katika Mchezo huu

LEO NAOMBA NIWAJULISHE WADAU WA MCHEZO JINSI AU NAMNA YA
KUSHIRIKI KIKAMILIFU NA KUFANIKIWA KUSHINDA KWA KIASI KIKUBWA.
KWA KUZINGATIA MAMBO HAYA #8 ,UTAWEZA KUFANIKIWA KUTENGENEZA FAIDA KUBWA KATIKA MCHEZO HUU.


#1 . UFANYE UWE MCHEZO,KISIWE CHANZO CHA MAPATO.


Watu wengi hufanya mchezo wa football betting kama ni kituo cha kujipatia mapato kwa ajili ya kukidhi haya mbalimbali za kimaisha kama vile
1.kulipa kodi ya nyumba,
2.Kupata ada ya watoto,
3.Kupata fedha ya kununua mali fulani i.e Pikipiki, Simu.
4. Kupata fedha ya kulipa Deni. ...na mengineyo!
Hili ni kosa kubwa sana. Unapofanya huu mchezo kama ni chanzo cha pesa kwa ajili ya suala fulani, linakupotezea nafasi ya kuweza kufanya machaguzi ya Odds
yaliyo sahihi.Watu wenye utaratibu huu ,huwa wanachagua Odds ambazo zitawaletea zao kubwa la pesa na kusahau kuwa si michezo yote katika orodha inayoweza kukupa tokeo chanya.
(Kumbuka, Mahesabu ya kina hufanywa na wenye hizi Betting Companies kuhakikisha hakuna mtu anaweza kupata kiasi kikubwa cha pesa kama matokeo ya betting(Mkeka) wake).

#2 . ZITAMBUE LIGI VIZURI.

Watu wengi hujihisisha katika huu mchezo hata bila ya kutambia mienendo (Trend) ya ligi kuu mbalimbali barani Ulaya.Kutokana na Betting Companies kuwa na aina mbali mbali za "kubet", Pia kuna baadhi ya ligi zina "facilatate successful betting" kutokana na aina ya betting.

Kwa mfano:- Ligi ya Uingereza(EPL) , inafaa sana kutumika katika kubeti katika category ya "NORMAL" kwa asilimia 80%.Hii ni kutokana na ligi kuwa na wababe wanaotabirika , Baadhi ya timu kuwa out-of-form kwa muda mrefu, Mjeruhi ya mara kwa mara.
Ligi ya Spain(LA LIGA), inafaa sana kutumika katika "NORMAL" kwa silimia 70% na "HANDCAP" kwa silimia 30%( timu za R.madrid,Barca,A.madrid)

Ligi ya Ufaransa(LIGUE 1).Kutokana na hii ligi kuto kuwa na wababe wa kueleweka , hapa ni mahali salama sana kuitumia "HANDCAP" 80% na.Pia ni ligi iliyo na idadi ndogo sana ya magoli hivyo basi "FOURTYFIVE" prediction inafaa.Hii ni kutokana na matokeo mengi ya ligi hii kuwa na tofauti ya goli moja.
Ligi kuu ya Itali (Serie A), hii ligi haina tofauti sana na ligi kuu ya Ufaransa.Baadhi ya mechi huwa na tofauti ya goli moja, na mara nyingi huwa na matokeo ya suluhu katika dakika 45 za kwanza. Hivyo "HANDCAP" ina asilimia 60% na "FOURTYFIVE" ina asilimia 40%.(Tahadhari: Hii ligi inahitaji uchambuzi wa kina katika mechi zake kabla ya kuweka bet,)

#3 . BOBEA KWENYE LIGI CHACHE TU.

Si mbaya sana ukichagua baadhi ya timu zenye nguvu kutoka ligi nyingine, bali umuhimu wa kubobea katika ligi chache ni veyma zaidi.Hii itakufanya uwe mwenye uelewa na utambuzi wa kutosha na mwenendo wa hizo ligi chache. Pia hii itakuwezesha kuweza kufanya maamuzi sahihi yaliyo na ufahamu na uelewa yakinifu.,

#4 . MARA NYINGI NI VYEMA KUFUATA HISIA.

Umeshawahi kutazama orodha ya michezo/mechi za siku husika kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho, na katika akili yako kuna hisia/vochochezi ambavyo vina kuambia kwamba "huyu anashinda" au "huyu anafungwa" au "hii mechi suluhu"?
Basi kwa taarifa yako, hizo hisia-za-mwazo(PRESCIENCE) husadikika kuwa sahihi kwa asilimia 80%.
Hii ni kwa upande wa wale wanao-Bet katika category ya "NORMAL".

#5 . EPUKA USHABIKI.

Kuna nyakati ambazo inakuhitaji uchague mechi ambayo timu uipendayo inacheza.Hiki kimekuwa kipindi kigumu sana kwa watu wengi.Hupenda kuchagua timu zao kuwa zitashinda hata kama ukweli ni kwamba zinauwezekano mkubwa sana wa kupoteza mchezo.
Au kuwekea timu fulani ishindwe kwa mategemeo timu yake(anayoishabikia) iendelee kuongoza ligi.
Ukiona umejawa na hisia za ushabiki na huwezi shindana nazo, basi ni bora kuacha kabisa kuchagua mechi hizo.

#6 . FANYA UCHAMBUZI YAKINIFU.

Hili ni pamoja na kuzingatia aina ya mchezo unaocheza. Mfano
-NORMAL; katika hii category unashauriwa kuchagua mechi zenye timu dhaifu na imara.Hii inaleta uwezekano wa kutokea kwa matokeo yaliyo-tabiriwa.
-HANDCAP; hapa unashauriwa kuchagua mechi zenye timu ambazo zenye uwezo unaokaribia na kulingana,kwa kuwa timu moja hupewa goli la kufikirika ambayo mara nyingi huwa ni ile dhaifu basi ni vyema kuchagua matokeo ya Suluhu huku ukiamini kuwa ile timu yenye nguvu zaidi huenda ikashinda kwa tofauti isiyozidi goli 1.Yaani 2-1 au 1-0 au hata 3-2.
-FOURTYFIVE(45); hapa sasa ni mahala ambapo mechi za machaguo ya suluhu kuzingatiwa.Kutokana na mechi kuanza kwa suluhu ya bila kufungana,kuna uwezekano wa asilimia 80% ya hizo mechi kumaliza dakika 45 za kwanza bila kufungana ili uweze kuchagua suluhi ya dakika 45, inashauriwa kuchagua mechi ambazo zina upinzani mkubwa sana baina yao au mechi zenye timu zilizodhaifu sana.

#7 . JIWEKEE KIASI KATIKA KU-BET.

Huu mchezo unaathiri sana tabia-ya binadamu (Addictive).Kuna kipindi unasikia hamu ya kubet kila mara hata pale unapoona mkeka(Betting Form) umeharibika, ili tu uweze kurudisha kile kiasi cha pesa ulicholiwa.Hii hutokea kwa sababu ya kutojiwekea "kikomo".
Weka kikomo ,mfano Tsh 5000/= tu itumike ndani ya saa 72.Itakufanya uwe na kikomo katika mchezo na kukusaidia kutopoteza kiasi kikubwa cha pesa kutoka mfukoni mwako.

#8 . FUATILIA UTABIRI WA MITANDAONI.

Ni vyema kufuatilia utabili wa mitandaoni kwa sababu huwa na takwimu sinazoonyesha historia, Perfomance, na matarajio ya mechi husika.
Hakikisha una-zingatia mechi tano(5) zilizopita.
-Head-to-head ya timu hizo.
-Perfomance ya timu katika dakika 45 za kwanza
-Majeruhi walio n'je ya kikosi kikuu.
-Usajili waliofanya
-zingatia idadi ya magoli ambayo timu hizo zinafunga(score) na kufungwa(concede).
-zingatia idadi ya mechi ambazo timu imeshinda na kupoteza.
-zingatia msimamo/stance ya timu katika mechi za nyumbani na ugenini.
Kuna baadhi ya mitandao maarufu ambayo hutumika kutoa tabiri za mechi mbalimbali.
(1)windrawin.com
(2)predictZ.com

(3)soccervista.com na
(4)livescore.com tu kwa matokeo yaliyo "live" na ya mechi zilizopita.

Nakaribisha maswali na Maoni kwenye eneo lolote lisilo eleweka...!

DemiGod,
Top Handcapper in Tanzania
 
Rashford Lingard

Rashford Lingard

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2018
Messages
819
Points
1,000
Rashford Lingard

Rashford Lingard

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2018
819 1,000
Nataka kutake risk wadau kwenye jackpot ya sport pesa over 800,000,000 . Naitaji.mawazo yenu wadau kwani humu kuna watalamu na wabobezi katika hii fani. Kiasi nilichokiandaa ni 800,000 hii pesa niko willing kuipoteza .

Nacho hitaji kufanya kila wiki nataka nitumie 100,000 nitengeneze mikeka 50 mfululizo kwa wiki 8 nione kama naweza angukia bahati yangu. Najua mikeka 50 nimichache kupata matokeo halisi ndio maan a nimekuja kuomba ushauri katika uchambuzi wa timu kwani nikichambua mwenyewe nitakuwa buyers .

Najua kuna alternative nyingi za kumpiga muhindi ila betting/gambling ni ileile mwenye mawazo na ushauri naombeni tafadhaliView attachment 1181023
Ninawazo hilo pia. Ila nataka Weekend hii nianze na ticket 5 tu
 
BASIASI

BASIASI

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Messages
4,907
Points
2,000
BASIASI

BASIASI

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2010
4,907 2,000
STAKEWIFE
⚽⚽⚽⚽⚽⚽
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖

14 – August – 2019

⏰ 5:00pm

🌎EUROPE: Europa League – Qualification

⚽Guimaraes (Por) – Ventspils (Lat)

✍ Tip: 1/1 HT/FT Odds: 1.80
 
Rooney

Rooney

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2015
Messages
3,232
Points
2,000
Rooney

Rooney

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2015
3,232 2,000
Nataka kutake risk wadau kwenye jackpot ya sport pesa over 800,000,000 . Naitaji.mawazo yenu wadau kwani humu kuna watalamu na wabobezi katika hii fani. Kiasi nilichokiandaa ni 800,000 hii pesa niko willing kuipoteza .

Nacho hitaji kufanya kila wiki nataka nitumie 100,000 nitengeneze mikeka 50 mfululizo kwa wiki 8 nione kama naweza angukia bahati yangu. Najua mikeka 50 nimichache kupata matokeo halisi ndio maan a nimekuja kuomba ushauri katika uchambuzi wa timu kwani nikichambua mwenyewe nitakuwa buyers .

Najua kuna alternative nyingi za kumpiga muhindi ila betting/gambling ni ileile mwenye mawazo na ushauri naombeni tafadhaliView attachment 1181023
Cheza double chance tu
 
Cash Money Forever

Cash Money Forever

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2019
Messages
542
Points
1,000
Cash Money Forever

Cash Money Forever

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2019
542 1,000
Mwaka 2017 nilikuwa nashida ya MILIONI 15 ya kufanya jambo flani. Rafiki yangu akanishauri niingie kucheza betting nitakula hela nje nje kwa kuwa ninacho kismart cha kubashiri matokeo kwa mdomo.

Akanifundisha jinsi ya kubet online nikaanza kubet zile ligi kubwa nachagua win au draw kulingana na jinsi navyoiona match itakuwaje. Nakumbuka mkeka wa kwanza nilistake 5000 na siku hiyo kulikuwa na match kubwa Madrid na Athletico nikaweka draw na match nyingine win win win.

Nikala ule mkeka nikasema haya ndio maisha nitakuwa tajiri. Kwa kweli elfu 60, laki laki zilikuwa hazinipigi chenga.

Nilivyoanza tamaa ya kujifunza kucheza kucheza market nyingine GG, OV, UN nk nikaanza kuharibu sasa kula kwa shida, nikaanza kufollow wanaotoa tips nikazidi kujichanganya.

Mwisho Nikapiga hesabu nilicheza bet za laki 6 nikawin laki 9, faida laki 3, nikatoa mtaji nikaendeleza laki 3 ikayeyuka yote hahahaha nikajisemea kupata ile milioni 15 ninayotaka nitaishia kufilisika nikaingia mitini.

Now Nimekuwa nikicheza bet kwa kujifurahisha tuu kwasababu ni mpenzi wa mpira lakini sijaweka akili zote na mtaji wa maana. Nile au niliwe ila nisiathirike kiuchumi. Nina miezi zaidi ya 4 sijaplace bet lakini kila siku naingia hapa kucheki mnavyompiga muhindi

Hongereni sana wakina Void, Mayu, soka255 mko vizuri.
 
mjr95

mjr95

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
6,061
Points
2,000
mjr95

mjr95

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
6,061 2,000
Hapna mkuu Monflis amekuwa na majeraha yanayo msumbua sana kama ni mfuatiliaji wa tennis bila shaka unalifaham hilo. Hali hiyo ilipelekea ashindwe kucheza katika nusu fainali juzi kati katika mashindano ya Rogers ilikuwa apambane na mnyama Nadal lakini kutokana na majeraha alijitoa. Ndio maana uliona katika game ya kuamkia leo alipewa odd nyingi sana asinge weza kuhimili mpaka mwisho.

Hahaha, ila anayecheza nae ni nyanya zaidi. Let's see how they come out today. Shida ya Tennis ni "one man army" ... akizingua siku hiyo basi ndo uhesabu kuliwa. Tofauti na Football wachezaji 11, mmoja akizingua anaweza kupigwa sub chap

Lakini hizo mbili ni 90% possible.
 

Forum statistics

Threads 1,326,600
Members 509,543
Posts 32,227,906
Top