Howard Webb: Lulu ya Soka katika Dunia

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
Kwa nadharia, mpira wa miguu ni mchezo rahisi sana. Ila kiuhalisia, sio kweli ni mcheo mgumu na mchezo wa kikatili sana. Mchezo una sheria 17 pekee, lakini ni sheria ambazo utafsiri wake huwa ni mgumu sana endapo mwamuzi sio makini. Waamuzi wa Ligi kuu za mataifa mbalimba wanapaswa kufanya maamuzi zaidi ya 50 kwa kila mchezo.
1709626715547.png

Maamuzi mengi hayazingatiwi, kwa sababu mwamuzi anaamua kutosimamisha mchezo ipasavyo Baadhi ya maamuzi yanahusu mambo ya wazi, kama vile kukosea kurusha mpira uliotoka nje na kadhalika. ndani mpira unapotoka nje ya mchezo. Lakini maamuzi mengi ni tafsiri ya kukutana kimwili, na asilimia ndogo na mengine yana ukubwa wake katika uwezo wa kutengeneza matokeo ya mechi husika. Kandanda ni mchezo mrahisi sana ila mgumu, ikiwa na maana jukumu la mwamuzi ni muhimu sana; kosa moja la mwamuzi linaweza kubadilisha kabsa mchezo.
GettyImages-73755940-scaled.jpg

Waamuzi sasa wanatakiwa kufuata mpango maalumu wa mazoezi ya utimamu wa mwili na kuhudhuria vipindi vya mafunzo kwa vitendo, ambapo hutumia nafasi hiyo kutazama na kuchambua sehemu za matukio na kupokea mawazo ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa michezo, wanasaikolojia na wataalamu wa lishe, asikudanganye mtu, mwamuzi lazma uwe na mbio tena uwe na kasi ya kutosha, kuna waamuzi Ulaya katika mataifa ya Uingereza na Uhispania wanatembea mpaka kwa mwendo wa mita 20 kwa saa.
DuPD6eqXcAIFcdZ.jpg

Ile tukio linatokea tu jamaa ameshafika muda mrefu sana, huku akipewa usaidizi na waamuzi wasaidizi. Ingawa katika kipindi fulani, aliyekuwa Mwalimu wa timu ya Arsenal, bwana mkubwa Arsène Wenger aliwahi kulalamika kuwa waamuzi wa ligi kuu ya Uingereza ni wabovu kila msimu, huku pia aliyekuwa mwalimu wa Cardiff, Neil Warnock akionesha wasiwasi wake kwa waamuzi wa ligi kuu ya Uingereza.
Getty-Wenger.jpg

Uingereza imepata kuwa na mtu mmoja ambaye anaonekana ni miongoni mwa waamuzi wanaoheshimika zaidi wakati wote, na pengine mwamuzi bora zaidi wa Kiingereza. Wasifu wake ulidumu kwa miaka mingi na alihusika katika michezo mikubwa zaidi katika kandanda ya ulimwengu katika kiwango cha kitaifa na kimataifa. Kwa sasa amepata kuteuliwa kuwa Afisa Mkuu wa Waamuzi wa PGMOL, huyu mwamba amepata kusifiwa sana kwa falsafa yake, ambayo imekuwa katika kiwango kipya cha ajabu sana.

Alianza kuwa mwamuzi wa soka toka akiwa na umri wa miaka 18 na akapanda daraja haraka. Baada ya miaka mingi ya mapambano na harakati za utafutaji, aliteuliwa kuwa mwamuzi wa kwa Ligi Kuu Uingereza mwaka 2003 na kuwa mwamuzi wa kimataifa wa FIFA miaka miwili baadaye yaani 2005. Wengi wanamfahamu kwa mwili wake mkubwa, pande la mtu, huku akijulikana kwa mtindo wake wa utulivu na upekee wake katika kutoa maamuzi. Pia alikuwa mtu mwenye nidhamu na hakuogopa kuonyesha kadi nyekundu kwa mchezaji au kocha pale inapobidi.
_65116261_webb.jpg

Asubuhi alhamis ya tarehe 24 mwezi wa Agosti mwaka 2017 kampuni ya uchapishaji wa vitabu ya Simon & Schuster UK iliipatia dunia zawadi ya kitabu mahususi kinachoelezea Maisha ya mtu moja ambaye amepata kutoa mchango mkubwa katika soka dunia. Kitabu cha nomino ya The Man in the Middle: The Autobiography of the World Cup Final Referee, ni kitabu kinachoungumia Maisha yaH Howard Melton Webb, Afisa wa Polisi ambaye alituburudisha sana kwa namna yake ya pekee ya kusimamia sheria 17 za soka uwanjani.
1692288003542_9e9d441c-420a-4fb9-9276-2081546f431e.jpg

Mechi inaanza kwa kasi sana na taratibu unaona kabsa kuwa hii shughuli sio ya kitoto hata kidogo, hapa ni Brazili Watoto wa Samba wamekutana na wajomba wa kazi Chile, mbungi inawakutanisha wataalamu wa soka kwenye michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2014 pale kwenye dimba la Estadio Mineirao, Brazili ambayo ndani yake ilikuwa na vichwa haswa, watu kama Julio Cesar huku Chile wao wakiwa na jembe Claudio Bravo, walinda milango ambao walikuwa kwenye viwango bora na vya juu sana. Msimamizi wa sheria 17 alikuwa ni mwamba Howard Webb, mmoja ya waamuzi bora kuwahi kutokea, mwamuzi ambaye alitoa maamuzi ambayo hata kama hutaki basi utataka tu.
1709623485182.png

Katika orodha ya waamuzi bora, basi binafsi nitawaweka watu kama Pierluigi Collina aka Omni-Man, Fran De Bleeckere mbeligiji pamoja na Jorde Larrionda. Ila leo natamani nimzungumzie kwa uchache ila kwa ukamilifu Howard Webb, mwamuzi ambaye kwa umbo lake tu, ilikuwa unatakiwa ujitazame vizuri kabla ya kwenda kuzungumza naye upuuzi.
1709624126507.png

Howard Webb mtoto wa Bwana Billy Webb na mkewe Slyvia na mzaliwa wa Rotherham, kitu cha ajabu ni kuwa Mzee Billy Webb pia alikuwa ni mwamuzi wa soka kwa kipindi cha zaidi ya miaka 35 (Kama Baba kama Mtoto). Webb alianza purukushani zake za kuisakua ndoto yake katika ligi za chini kabsa hapo ni miaka ya 1989, na alihitaji miaka minne tu kabla ya kupata nafasi ya kuwa mwamuzi msaidi maarufu kama lineman (mshika kibendera) katika ligi ya Northern Counties East League, nafasi hii aliitumia vyema ukizingatia kuwa alihitaji kuelewa vyema sheria za mpira pamoja na saikolojia za wachezaji kabla, wakati na hata baada ya mchezo.
webbbb.jpg

Webb ana maajabu yake bwana, huyu ndo mwamuzi wa kwanza na nadhani mwamuzi pekee kuchezesha Fainali mbili ndani ya mwaka mmoja, yaani Fainali ya Mabingwa Ulaya UEFA pamoja na Kombe la Dunia la FIFA zote ndani ya mwaka 2010. Michezo 534 uliyosimamia inatosha sana kukufanya uwe wa kipekee sana.

Ile mechi uliyosimamia kati ya Ireland Kaskazini didhi ya Ureno ndo ilifungua njia yako kimataifa, mbungi ilipigwa katika uwanja wa Windsor Park mwaka 2005, mechi iliisha kwa sare ya goli moja kwa moja huku Webb ukitoa kadi tatu tu, watu walikusifia sana kwa namna ambavyo ulikuwa mwepesi kufika kwenye matukio kama faulo pamoja na kutoa suluhu. Webb unaacha sifa kubwa sana kwa waamuzi dunia katika kuelewa mchezo kabla, wakati na baada ya mchezo. Katika mchezo huo Ireland Kaskazini walianza kwa kujifunga kupitia Stephen Craigan, ila kipindi cha pili, Bwana mkubwa Warren Feeney alisawazisha bao hilo na kufanya ngoma iishe kwa sare.
Feeney_2906935.jpg

Webb katika moja ya mahojiano na BBC aliwahi kusema kuwa kabla ya kuchezesha mchezo wowote alifanya utafiti mfupi kujua tabia na msisimko wa kila mchezaji ili tu akiwa uwanjani ajue kuwa fulani huwa anacheza kwa mtindo upi na mazoea yake katika upande wa nidhamu. Fainali ya Kombe la FA mwaka 2009 uliwaacha hoi mashabiki kwa kuchezesha moja ya mechi ngumu sana, Webb ulitoa kadi tano kwa makosa ya kinidhamu, ilikuwa ni kati ya Watoto wa Stamford Bridge na Everton, ngoma ikaisha mbili kwa moja huku Chelsea akibeba ndoo.
chelsea.jpg

Mwaka 2006 mwezi Mei ulichezesha mechi baina ya Grays Athletic dhidi ya Woking ambapo Grays Athletic walishinda kwa jumla ya magoli mawili kwa sifuri,magoli ya Dennis Oli pamoja na fundi wa mpira, Glenn Poole. Ila upekee wa mech hii ni kwamba hakuna ambaye ulimpa kadi, ni wazi kuwa watu walipeana mitama ya kutosha na ugomvi wa hapa na pale ila Bwana mkubwa ulijua saikolojia zao kuwa hii mbungi ni fainali hivyo acha wacheze mpira.
gettyimages-57609148-612x612.jpg

Mwaka 2007 ulichezesha fainali ya Kombe la Ligi baina ya wanyawezi wawili mahasimu kupita maelezo, ni Chelsea dhidi ya Arsenal, katika mechi hiyo kulizuka ugomvi watu wakatamani kuzichapa, ilibidi mpaka walimu Arsene Wenger pamoja na Jose Mourinho kuingia uwanja kuwatulia vijana kuwa mpira sio ndondi, na katika kutoa adhabu kwa sababu ya utovu wa nidhamu, ilimbidi Webb atoe kadi nyekundu kwa Mikel John Obi wa Chelsea pamoja na kadi mbili nyekundu kwa Kolo Toure pamoja na Emmanuel Adebayor kwa upande wa Arsenal.
skysports-arsenal-chelsea-carling-cup_3962033.jpg

Lakini pia alitoa onyo kwa kuwapatia kadi za njano Frank Lampard pamoja na Cesc Fabregas. Hii ikawa ni mara ya kwanza katika fainali ya kombe la ligi kutoka kwa kadi tatu nyekundu, ajabu ni kuwa kabla ya fainali hii, rekodi zinaonesha kuwa kulikuwa na kadi nyekundu tat utu katika fainali zote zilizopita.
internazionale_corpo.jpg

2010 Diego Milito, Master of Goals akawapatia Inter Milan taji la Ligi ya Mabingwa UEFA akiwafumua Bayern Munich mabao mawili katika dimba la Santiago Bernabeu, Webb ulichezesha vyema sana ile game kiasi kwamba mpaka mashabiki wakavutiwa na namna ulivyokuwa ukiwasiliana na wachezaji, game iliisha huku ukitoa kadi za njano mbili tu kwa Martin Demichelis pamoja na Mark Van Bommel. Kwenye ile mechi kumtazama Diego ilikuwa ni kama kutazama filamu ya The Walking Dead enzi hizo, ilikuwa ni hatari sana kuona unyama wa Andrew Lincoln akicheza uhusika wa Rick Grimes.

gettyimages-107948633-612x612.jpg

Mwaka 2011 kwenye mchezo baina ya Manchester United dhidi ya Liverpool, ulionekana kama umelalia upande mmoja, upande wa Mashetani wekundu kwani walizidiwa sana na Majogoo ambao walionesha wazi kuwa mechi ilikuwa ni yao kwa zaidi ya 70% ila Webb bhana ukawazawadia mkwaju wa penalty Manchester United huku ukimtoa Steven Gerrard kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi Carick, Mashetani wakachukua game kwa bao moja kwa sifuri, ,mashabiki wana kila la kusema kuwa ile mechi ulipokea bahasha mzee wangu, siku hiyo mashabiki wa Liverpool walikaa kwa huzuni wakisikiliza wimbo wa Cry me a river wa Justin Timberlake. Ila kama hiyo ni ngumu kukumbuka basi turudi nyuma kidogo zaidi.
ronaldo.jpg

Miaka miwili nyuma, 2009 kwenye mchezo wa ligi baina ya Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspur ambapo Mashetani walishinda kwa magoli 5 kwa 2, mashabiki wana nadharia kuwa Webb ni mpenzi wa Manchester United kindakindaki, kwani Spurs walianza kwa kuongoza kwa magoli mawili kwa sifuri, ila Webb ukawapatia nafasi Mashetani kurudi kwenye mchezo kwa kuwapatia mkwaju wa penalty ambao uliwapata matumaini, Ronaldo na wenzake wakaamka kuoka usingizini kwa mbeleko ya Webb na kuwamaliza Spurs magoli matano kwa mawili, siku hiyo mashabiki wa Spurs walilala na viatu huku kwa mbali ala za wimbo wa “The Myth of Trust” kutoka kwa Billy Bragg ukiwaliwaza mdogo mdogo.
wozal3iarcr4up4wpkyk.jpg

Binafsi sina shaka kuwa wewe ni mmoja ya waamuzi ambao hukuwahi kuhitaji msaada wa VAR ili kutoa maamuzi, kwa sababu ulikuwa unawafahamu kabsa wachezaji karma zao hata kabla hujaruhusu mchezo kuanza. Michezo 296 ndani ya ligi kuu ya Uingereza, michezo 43 ya Kombe la FA, michezo 36 ya ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA, michezo 6 ya kombe la Dunia, na michezo 5 ya Mabingwa wa Ulaya, hii yote inaonesha kuwa wewe ulikuwa na talanta ya uamuzi na kiongozi. Hauna deni kwangu kwa kile ambacho umekionesha ndani ya mchezo wa soka, mchango wako hata Kayoko anaufahamu, waamuzi machipukizi wana mengi ya kujifunza kutoka kwa watu kama wewe.
kayoko.jpg

Afisa wa polisi ambaye ulikuwa ni jitu lenye miraba minne, mchezaji alikuwa anakufuata kwa nidhamu maana lolote linaweza kutokea. Asante kwa kusimamia nidhamu ndani ya uwanja! Ishi sana Mwamba! Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Webb huku tukijifunza pia kupitia wazawa wa hapa hapa nyumbani, kina Bamlak Tessema Weyesa, Bakary Papa Gassama pamoja na Gehad Zaglol Grisha.
Bakary-Gassama-750x375-1-1280x720.jpg

Waamuzi wengi wanmeona kuwa kuna haja ya kufichua ukweli kwamba wanahangaika na afya ya akili katika soka na maisha yao kiujumla. Unyanyapaa na kejeli nyingi unaleta athari nyingi katika afya ya akili au saikolojia. Sehemu ya tatizo ni kwamba wengitunahisi kuwa waamuzi wa soka ni watu wasiohisi hisia au ni mifano wa maroboti ila sio kweli. Waamuzi mara nyingi hununua katika hali ya kutoweza kushindwa ambapo hawawezi kufanya vibaya.
202202100528-main.cropped_1644445722.jpg

Hakuna mtu anayeelewa jinsi ilivyo ngumu kuwa mwamuzi katika soka. Sote tunaelewa mara moja, kwenye mchezo wetu wa kwanza. Mwamuzi Ovidiu Hategan alichezesha mcheo baina ya Uholanzi dhidi ya Ujerumani huku akiwa ametoka kumpoteza mama yake mzazi. waamuzi nao ni wanadamu hivyo wakikosea tusiwalaumu kana kwamba hawapaswi kukosea.
1709626549280.png

Howard Webb usisahau kupita kwenye mgawaha wa The Brecks Beefeater upate zako cocktail ya Martini uchambe koo! Kazi nzuri sana Bwana Mkubwa!
 
Usijekurudia kuandika Makalla ndefu za hivi!

Nimeona nikukope! Uzi upate japo hata mchangiaji mmoja!.... Unapaswa kunilipa kwa hili!
 
Hii takataka ilipewa promo ikachezesha fainali ya kombe la dunia Afrika Kusini kilichotokea ni aibu mtu anarukiwa kifuani anashindwa kutoa kadi
 
Hii takataka ilipewa promo ikachezesha fainali ya kombe la dunia Afrika Kusini kilichotokea ni aibu mtu anarukiwa kifuani anashindwa kutoa kadi
Mechi mbichi kama ile ulitaka atoe kadi nyekundu ngapi Alonso mwenye ile Mechi ilibidi alabwe umeme aliku anachapa sana kiatu Na Ndio maana De jong akaja kumtia meno tumboni Heitinga naye alistaili kadi Nyekundu tu sio kwa mirafu aliyekua anacheza ile ile mechi Refa angeamua kutembeza umeme kuna wachezaji kama wanne walikua wanaenda nje
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom