Wakuu wapi ntapata chimbo la kununua simu ndogo za jumla kwa Bei rahisi MKOANI MBEYA.

Battery orijino,USB og na vichwa orijino.

Na machimbo yaliyopo Dar es Salaam pia yanapatikana wapi na Bei zake zikoje.
 
Nauza friji ,ni jipya tu maisha magumu nichek wasap 0742537423
IMG_20210318_230654_9.jpg
 
Maeneo ya gerezani sekondari au wapi mami.?

Opposite dear
Au kwa kifupi, daladala za gerezani temeke za kijani mkolezo zile zinakopaki, sasa ile barabara unakuja nayo moja kwa moja Kama unataka kwenda mnazi, utaona tu nje maturubai vitambaa mazulia

au ukifika gerezani tu uliza utaelekezwa
 
Asante sana Mamy🙏
 
Mkuu kuhusu nguo za ndani nilienda ile mitaa yake pale Kariakoo ila bei ilikuwa kubwa kuliko bei ya Mbeya ambako ndio nilitaka nitume baadhi ya mzigo. Nilikata tamaa maana nilienda kama mara tatu kutafuta bei nafuu ila wote bei zilezile
Ukitaka bidhaa bei nafuu sa hv jilipue Tu uagize nje Mzee....kariakoo pale pamebadilika Sana, wezi wengi alaf bei wanauza juu kweli ....dunia ya sa hv watu wanajitahd kumkwepa mtu wa Kati (dalali) kadiri inavyowezekana, sa hv kama Una hela unachukua mzigo kiwandani we unakuja uza reja reja unamkwepa mtu wa kati
 
Mkuu hela za za boom kuagiza mzigo China nitakula sana mihogo. Its too dangerous
 
Baadhi ya mahitaji ya wadau:
Naombeni kupewa orodha ya maduka ya suti za kiume (za kisasa) yaliyopo Kariakoo. Nahitaji kuyazungukia. Kwasababu ya muda siwezi ku-design kwa fundi ndo maana nataka kuitungua dukani. Shukrani.

Kariakoo au Dar ni wapi tutapata pochi, vitenge na viatu vya kike bei za jumla? Maana wenyeji wengi hawapendi kutupeleka kwenye machimbo.

Baadhi ya majibu/maelekezo ya wadau:
Fanya Biashara ya kununua na kuuza nguo za ndani za, na hasa zile za bei za kawaida za kike na kiume wakubwa na watoto kutoka Dar kariakoo.
Biashara hii Ina faida ya kuanzia 50% hadi 100% na kuendelea.
Dukani kwetu Tunauza bidhaa hizo kwa Jumla Kwa kuanzia Nusu Dozen.
Na tuna saidia kutuma mzigo wako Popote tanzania.
Wasiliana nasi kwa ushauri zaidi kwa whatsapp/simu #0743207176
View attachment 1736463
 
Sawaa mkuu...Ila leo nmetoka Kkoo, vijora vingi Bei yake ya jumla ni-:
Vya mtandio elf 11 hadi 12 inategemea
Visivyo na mtandio elf 6.

Ila kuna sehemu nimeona maeneo ya shimoni kuna cherehani nyingi watu wapo kazini, sasa sijajua ndio watu wanaoshona hivyo vijora au mafundi tu... Maana nilisikia vijora wanaagiza kutoka Mombasa.

Madira bado nafatilia.
Vp kaka ulishapata hilo chimbo la vijola?
 
Vp kaka ulishapata hilo chimbo la vijola?

Kuna jamaa aliniambia vijora vingi vya kkoo ni vya kushonesha so unaenda tandika unachagua kitambaa chako unamtafuta fundi mzuri anakushonea kwa maelewano tu... pia chimbo za bei nafuu zama ndani ndani yaaduka au panda maduka ya juu ukichukua mzigo mkubwa wanakupunguzia tu.
 
Wakuu
Naomba kufahamu machimbo wanayouza vitu vya dukani vya jumla kama soksi, vitambaa, miswaki, rula, pen, toothpick, super glue, aina za pipi zote...nk

Natanguliza shukrani
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom