Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,762
4,576
kariaakoo.jpg

Baadhi ya mahitaji ya wadau:
Naombeni kupewa orodha ya maduka ya suti za kiume (za kisasa) yaliyopo Kariakoo. Nahitaji kuyazungukia. Kwasababu ya muda siwezi ku-design kwa fundi ndo maana nataka kuitungua dukani. Shukrani.

Kariakoo au Dar ni wapi tutapata pochi, vitenge na viatu vya kike bei za jumla? Maana wenyeji wengi hawapendi kutupeleka kwenye machimbo.

Baadhi ya majibu/maelekezo ya wadau:
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!

Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo Kariakoo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa.Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale. Ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF.

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000, 8000, 12000 lipo maeneo ya Nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee Msimbazi Kota, karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa Congo na Aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka Aongo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k, 25k, 28k, 30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k.

Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo Mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh, pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy

Jengo la benki ya posta walifahamu? Basi ukimaliza lile jengo kama unakuja msimbazi police mtaa wa kwanza kata Kulia majengo yote matatu mkono wa kushoto ndio wauzaji wa viatu vya kike, usinunue kwa wale waliomwaga nje mi wauzaji wa rejareja. Usiogope ingia ndani mkono wa kushoto zunguka vya kutosha fanya window shopping mjomba, by the way zipo sehemu nyingine ila anza na hapo ukifeli nitag nije kukuelekeza.

Usiwe na papara mjini mawinga/madalali wengi

Ukifika msimbazi kwenye jengo la police pale kuna road ya mkono wa kushoto na kulia. Hii ya mkono wa kulia ukinyoosha, moja kwa moja mbele huko utakutana na maduka meengi tuu yanayouza nguo na vitu vingi vinavyowahusu watoto. Ila mtaa huu bei zao kidogo huwa zimechangamka.

Nyingine ni ukiwa umesimama pale kituo cha gari za Mwananyamala au Police kwa nyuma, nyooka na hiyo njia, utakutana na T-joint ya kwanza kisha songa mbele then utakutana nayo ya pili; baada ya hiyo ya pili sasa ingia maduka ya mkono wa kulia japo huko wanauza zaidi vitenge na khanga. Ukikosa huko ingia maduka ya mkono wa kushoto huko ndo kuna nyingi zaidi za watoto.
 
Ukifika msimbazi kwenye jengo la police pale kuna road ya mkono wa kushoto na kulia. Hii ya mkono wa kulia ukinyoosha, moja kwa moja mbele huko utakutana na maduka meengi tuu yanayouza nguo na vitu vingi vinavyowahusu watoto. Ila mtaa huu bei zao kidogo huwa zimechangamka.

Nyingine ni ukiwa umesimama pale kituo cha gari za Mwananyamala au Police kwa nyuma, nyooka na hiyo njia, utakutana na T-joint ya kwanza kisha songa mbele then utakutana nayo ya pili; baada ya hiyo ya pili sasa ingia maduka ya mkono wa kulia japo huko wanauza zaidi vitenge na khanga. Ukikosa huko ingia maduka ya mkono wa kushoto huko ndo kuna nyingi zaidi za watoto.
 
Ukifika msimbazi kwenye jengo la police pale...Kuna road ya mkono wa kushoto na kulia. Hii ya mkono wa kulia ukinyoosha ,moja kwa moja mbele huko utakutana na maduka meengi tuu yanayouza nguo na vitu vingi vinavyowahusu watoto. Ila mtaa huu bei zao kidogo huwa zimechangamka.

Nyingine ni ukiwa umesimama pale kituo cha gari za mwananyamala au police kwa nyuma,nyooka na hiyo njia, Utakutana na T-joit ya kwanza kisha songa mbele then utakutana nayo ya pili baada ya hiyo ya pili sasa ingia maduka ya mkono wa kulia japo huko wanauza zaidi vitenge na khanga. ukikosa huko ingia maduka ya mkono wa kushoto huko ndo kuna nyingi zaidi za watoto

Hayo.maduka hapo mbona huwa hawauzi jumla
 
Hayo maduka hapo mbona huwa hawauzi jumla
Hapo wapi sasa maana hapo me nimetaja ya sehemu mbili mkuu. Ila kimsingi kwa maduka ya kariakoo huwa ni rejareaja na jumla sasa ww unapofika mwambie muuzaji unataka kwa bei ya jumla na wengi huuza kuanzia p3.
 
hapo wapi sasa maana hapo me nimetaja ya sehemu mbili mkuu.
Ila kimsingi kwa maduka ya kariakoo huwa ni rejareaja na jumla sasa ww unapofika mwambie muuzaji unataka kwa bei ya jumla na wengi huuza kuanzia p3
Hapo maeneo ya kituo cha polisi msimbazi.

Hayo maduka yooote kuanzia kwa halima toto hadi ule.mtaa wa pili narung'ombe sijawahi pata duka la.nguo kwa jumla hasa hasa ukizunguka sana utapata tu.yenye bei nafuu
 
hapo maeneo ya kituo cha polisi msimbazi....
hayo maduka yooote kuanzia kwa halima toto hadi ule.mtaa wa pili narung'ombe sijawahi pata duka la.nguo kwa jumla hasa hasa ukizunguka sana utapata tu.yenye bei nafuu
Wauzaji wa k'koo karibia woote ujanja mwingi sasa na ww unatakiwa uwe shap. Nikija me nitakupeleka mkuu
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom