Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, tarehe 27 Mei, 2023 wamepata nafasi ya kujifunza kuhusu nishati safi ya kupikia pamoja na kupitishwa kwenye Rasimu ya Dira ya Taifa ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia pamoja na Mpango Mkakati wa Utekelezaji kupitia semina maalum iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA); Semina iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa ndani ya majengo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma.

Semina hiyo iliongozwa na Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato pamoja na Naibu Katibu Mkuu Bwana Athuman Mbuttuka sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bwana Maharage Chande pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi, Hassan Saidy.

Awali wakati akifungua semina hiyo Waziri wa Nishati, Mhe. Makamba alisema takriban asilimia 85 ya Watanzania wanatumia nishati ya tungamotaka ambayo inatokana na kuni, mikaa, magogo, mabaki ya mazao na vinyesi vya wanyama ambapo asilimia 72 ya nishati yote inayozalishwa na kutumika uwa inatumika majumbani kwa kupikia, ukilinganisha na nishati nyengine zinazotumika kwenye usafirishaji, viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.

“Asilimia kubwa ya nishati inayotumiwa na Watanzania ni ya tungamotaka na inatumika majumbani kwa kupikia kwa hiyo kuzungumzia tu mitambo ya kuzalisha na kusafirisha umeme, gesi au mafuta haitoshi, kwani Watanzania wengi wanatumia nishati ya kupikia ambayo ni ya tungamotaka hivyo ili kuitendea haki kazi tulizopewa, tumeona lazima tuingilie kati kwenye nishati safi ya kupikia na hilo ndiyo chimbuko la kulipa nguvu suala hili.” amesema Waziri Makamba.

Waziri Makamba amesema ni muhimu kuitazama nishati ya kupikia kwa kuwa inatumika kwenye kila nyumba iwe ya tajiri au maskini, utofauti upo kwenye aina ya nishati inayotumika na kuongeza kuwa nyumba ya tajiri itatumika nishati safi na nyumba ya maskini inatumika nishati chafu.

------
Waziri wa Nishati, Januari Makamba anatuhumiwa kuhonga wabunge wote milioni 10 kila mbunge pamoja na kuwapa rushwa ya majiko 300 ya gesi kwa kila mbunge kama shinikizo la kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati wiki wiki hii.

Rushwa hizo anadaiwa kuzitoa Waziri Makamba kwa mfumo wa semina za wabunge kama sehemu ya kuwaziba mdomo wasizungumzie madudu na ubadhirifu mkubwa unaoikabili wizara ya nishati na madudu mengine ikiwemo mgogoro wa umeme ulivyoharibu uchumi wa wananchi na kupanda kwa gharama za gesi.

Taarifa za ndani ni kuwa kwenye semina hizo za wabunge zimeanza wiki iliyopita na zinaendelea ambapo ametangaza kugawa majiko 100 kwa kila mbunge lakini ukweli uliopo anadaiwa kuwapa majiko 300 ambayo wabunge wenyewe wataamua kwenda kuyagawa kwa baadhi ya wananchi au kwenda kuyauza ili yasije yakawaletea mgogoro wa kisiasa majimboni mwao kwani idadi ya wananchi majimboni ni kubwa kulinganisha na majiko hayo ambayo wananchi wengi watakosa na kutengeneza fitna kubwa za kisiasa majimboni.

Rushwa hizi zinatolewa wazi mchana kweupe mbele ya kamera za waandishi wa habari lakini wabunge wengi wamejiuliza hivi TAKUKURU iko wapi kwanini isimuhoji Waziri Makamba kwamba fedha hizo anazohonga wabunge na majiko hayo anayogawa amezipata wapi, wengine wakaenda mbali zaidi kuhoji kwanini ayatoe majiko na semina mfululizo wiki hii ambayo ndio ratiba ya bajeti yake na kama huo ni mpango wa Serikali kwa nini haukutolewa siku zote usibiri bajeti.
 
Story za Carbon emissions kutokana na Kuni na eti mosh wa kupika ni sumu .. ni story za kupambana kuuza alternatives, 70% ya mama zetu wangekuwa washakufa.

Hayo ya Rushwa kwa wabunge wetu hii ni kama kawaida, kwa jina la semina, posho nk.

Hapo January anatengenezewa agenda.
 
Waziri wa Nishati, Januari Makamba anatuhumiwa kuhonga wabunge wote milioni 10 kila mbunge pamoja na kuwapa rushwa ya majiko 300 ya gesi kwa kila mbunge kama shinikizo la kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati wiki wiki hii.

Rushwa hizo anadaiwa kuzitoa Waziri Makamba kwa mfumo wa semina za wabunge kama sehemu ya kuwaziba mdomo wasizungumzie madudu na ubadhirifu mkubwa unaoikabili wizara ya nishati na madudu mengine ikiwemo mgogoro wa umeme ulivyoharibu uchumi wa wananchi na kupanda kwa gharama za gesi.

Taarifa za ndani ni kuwa kwenye semina hizo za wabunge zimeanza wiki iliyopita na zinaendelea ambapo ametangaza kugawa majiko 100 kwa kila mbunge lakini ukweli uliopo anadaiwa kuwapa majiko 300 ambayo wabunge wenyewe wataamua kwenda kuyagawa kwa baadhi ya wananchi au kwenda kuyauza ili yasije yakawaletea mgogoro wa kisiasa majimboni mwao kwani idadi ya wananchi majimboni ni kubwa kulinganisha na majiko hayo ambayo wananchi wengi watakosa na kutengeneza fitna kubwa za kisiasa majimboni.

Rushwa hizi zinatolewa wazi mchana kweupe mbele ya kamera za waandishi wa habari lakini wabunge wengi wamejiuliza hivi TAKUKURU iko wapi kwanini isimuhoji Waziri Makamba kwamba fedha hizo anazohonga wabunge na majiko hayo anayogawa amezipata wapi, wengine wakaenda mbali zaidi kuhoji kwanini ayatoe majiko na semina mfululizo wiki hii ambayo ndio ratiba ya bajeti yake na kama huo ni mpango wa Serikali kwa nini haukutolewa siku zote usibiri bajeti.

Ushaidi?
 
Stuka Hivi unatumia makalio kufikiri ama!?

Milioni 10 ni hongo kwa mbunge!? Hivyo ni vijihela tu vya kuendea sokoni kwao....Hivi unajua pesa wanoipata hawa wabunge lakini!?

Laiti ungejua fedha wanazopata usingeandika thread....ndio washoboke na hivyo vihela vya nyanya kwao!?....Nonsense!
 
Kama anaweza kufanya yote hayo alafu tunasema tuna mifumo basi bora afanye kwa bidii zaidi hadi siku moja tuwe na akili.

Tupe shule hadi tu graduate mzee wa nishati, tupo pamoja.
 
Ndio Tanzania hii kama huijui tulia tu baba wizi kila kona hao Wabunge ukuwoana wameshupalia jambo ujue kuna hela yaani wanatia aibu sana hao watu wanakera mnoo..
 
Back
Top Bottom