Mbunge Amina Mzee Akabidhi Mitungi 200 ya Gesi, Aungana Kushiriki Iftar na Waumini wa Dini ya Kiislam

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946
Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa (Mkoa wa Mjini Unguja, Zanzibar), Mhe. Amina Ali Mzee ameongoza semina ya mafunzo ya kutumia gesi kupikia na amewataka wajasiriamali kutumia nishati safi ya kupikia (gesi) ili kurahisisha shughuli zao za kujikomboa kiuchumi.​

"Tunaelewa lengo kuu na Dira ya Serikali juu ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia. Tumekabudhi mitungi ya gesi 200 kwaajili ya wajasiriamali wa Vijana walioamua wenyewe kujiajiri. Matumizi sahihi ya gesi ndiyo yanapelekea mazingira mazuri ya uhifadhi" - Mhe. Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

Vilevile, Mhe. Amina Ali Mzee ameungana na Waumini wa dini ya Kiislam na wanachama wa CCM katika Iftar ya pamoja iliyoandaliwa na Tawi la CCM Kikwajuni Bondeni Mkoa wa Mjini Unguja huku akiwasisitiza Waumini kufanya ibada, kutoa sadaka na kuombeana mema.

Aidha, katika hatua nyingine, Mhe. Amina Ali Mzee amewashukuru Kampuni na Watendaji wa ORXY ENERGY kwa kuwapatia elimu ya mafunzo ya namna bora ya kutumia majiko ya gesi wajasiriamali ili kuwaepusha na ajali zinazoweza kutoa nyumbani wakatili wa kutumia jiko la gesi

Baadhi ya wajasiriamali wamemshukuru Mbunge Amina Mzee kwa juhudi ya kushirikiana na jamii na kuahidi kutumia msaada wa gesi kwa malengo yaliyokusudiwa kwani walikuwa hawajui kutumia jiko la gesi na kuahidi kwenda kuwaelimisha wengine.

WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.53.06.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.53.07(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.57.20.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.57.20(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 10.59.31.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.56.43.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.56.44.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.56.44(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.56.45.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.57.33.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-09 at 11.56.46(1).jpeg
 
Back
Top Bottom