Mkuu hii ishu ni tata kidogo,Kuna Mmarekani ambaye kitaaluma ni endocrinologist(mtaalamu wa homoni na glands) kutoka chuo cha Cornell nchini Marekani ambaye ndiye aliyeenda huko Dominica mwaka 1970 kufanya utafiti anasema hali hio inatokana na "mutation"( kubadilika mfumo wa mwili) ambapo imesababisha kuzuia/ ukuaji wa Uume mpaka pale mtu anapobalehe.

Kwahio hawa watoto huzaliwa na uke na sura na kike kisha anapobalehe kuanzia miaka 13 hadi 15 ndipo uume,korodani na vingine ambavyo hupaswa kuwanavyo mwanaume hujitokeza,na huko kwao watoto wa namna hii huitwa "Guevedoces' au Machihembras.

Kifupi hawa hata huko Dominican republic sio kwamba wanazaliwa kila mahali ila ni kijiji kimoja tu kinaitwa Salinas lakini badae imekuja kugundulika watu wa namna hii huzaliwa pia nchini Uturuki na New Guinea.
Kwenye picha niliyoweka hapo chini, huyo ni mtu mmoja tangu alipokuwa mtoto wa 'kike' na kisha mvulana na mwisho akiwa mwanaume kamili .

Na wanapobadilika kuwa wanaume wanakuwa na uwezo wote wa 'kiume' japo huwa inawaletea shida kidogo sababu umekuzwa kama mtoto wa kike kuanzia jina, mavazi midoli na hata kukaa na wasichana then ghafla unatakiwa kuaanza kuvaa mavazi ya kiume,kuambatana na wavulana wenzio na hata kuwa na demu wakati huohuo wewe ulikuwa 'demu' mwenzao.

Ya Mungu mengi,unaweza kutafuta google ukiandika Guevedoces au Machihembras kuna makala BBC walienda kutafiti huko.

View attachment 1878933
Asante sana mkuu
 
IMG-20210803-WA0172.jpg
 
Back
Top Bottom