Constantine Oswald Millinga: Mmoja wa waasisi 17 wa TANU mwaka 1954

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200

MAKALA: MZEE MILLINGA MUASISI WA TANU TUTAMKUMBUKA DAIMA​

1709594011072.png
Mzee Constantine Oswald Millinga mmoja wa waasisi wa TANU akiwa na rais Jakaya Kikwete

Na Kassian Nyandindi,
SIKU zote binadamu anapozungumzia jambo la kimaendeleo kuelekea Uhuru wa Tanganyika, amekuwa akitoa taswira au picha ya mchango wa watu mbalimbali ambao wamefanya kazi hiyo, hadi kufikia kilele cha mafanikio ambapo ndani yake wapo wanasiasa na jamii ya kawaida ambao walivuma na wengine wasiovuma.

Aidha katika kundi hilo wapo wake kwa waume, wametangulia mbele ya haki ambao ni wengi na wachache ndiyo waliobaki ambapo kwa maana hiyo, wapo Waasisi wa siasa ya nchi hususan katika chama chetu cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho ndicho kimebeba chimbuko la Uhuru na maendeleo ya Tanganyika na baadaye tukaipata Tanzania.

Katika makala haya mmoja wa hao yupo Mzee Costantine Oswald Millinga (96) huyu ni Mwanasiasa mkongwe na Mtanzania, mwenye historia ndefu katika kuasisi vyama vya Tanganyika African Association (TAA) na Tanganyika African National Union (TANU) akiwa mkazi wa baadhi ya miji iliyokuwa nguzo za vyama hivyo hapa nchini.

Mvuto huo ndiyo uliomfanya Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa madarakani, kumualika Mzee Millinga kuwa mmoja wa watu katika uzinduzi wa sherehe ya miaka 50 ya Uhuru zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es salaam mwezi Julai mwaka 2011 na akawa kivutio kikubwa.

Mzee Millinga alionesha kuwa na uwezo mkubwa na kumbukumbu ya kusimulia kwa ufasaha historia ya TAA na TANU licha ya umri wake kuwa mkubwa, huku akiibua mambo ambayo wengi wao hawakuyajua au hayapo katika maandishi ya historia.

Katika vyama vyote vya TAA na TANU Mzee huyo anayo “mikono yake” ambapo safari hiyo ilianza katika simulizi ya mwaka 1952 akiwa mjini Ngudu Wilayani Kwimba, Mwanza kwa baba yake mdogo aliyekuwa Inspekta wa Polisi ambaye alikuwa akifanya mipango ajiunge na Shirika la Posta.

Hapo walitembelewa na rafiki wa baba yake mdogo alitokea mjini Masasi, Mtwara aliyemtambua kwa jina la Frederick Mchauru ambapo mgeni huyu alikuja na mawazo ya kumshawishi aachane na kazi za Posta na badala yake ajiunge na ajira ya Ofisi ya Maendeleo ya Jamii huko Masasi.

Pamoja na mambo mengine, baadaye kulikuwepo mawazo mbadala ambapo alipata ajira hiyo mjini Tabora wakati huo kukiwa na vuguvugu kubwa la mchakato wa kuanzishwa kwa TAA, kikiwa ndiyo chama kilichojumuisha Wakulima na Wafanyakazi wazalendo.

Pia Mzee Costantine Oswald Millinga anamkumbuka kiongozi wake wa kazi kwa wakati huo aliyemtaja kwa jina la Leonard Kunambi, ambaye huyu alimshawishi kujiunga na TAA lakini ndani ya kipindi kifupi mchango wake uliwavutia wanachama wengine hata akachaguliwa kuwa Katibu.

Hapo ndipo mwanzo wa ushiriki wake kikamilifu wa Mzee huyu katika siasa ulipoanza wakati huo akiwa kijana mwenye umri wa miaka 26 tu, katika zama hizo kasi ya kujijenga na TAA ilipamba moto mjini Dar es Salaam, Tabora na maeneo mengine hapa nchini.

Joto la siasa kwa Watanganyika kutaka haki ya kujitawala wakati huo lilikuwa juu, wakati TAA ikilenga kudai usawa kati ya jamii ya Waasia, Wazungu na Waafrika.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida jambo hili liliwakera Serikali ya Kikoloni ya Mwingereza chini ya Gavana Edward Twining huku Wakoloni hao wakikerwa na msukumo huo wa Waafrika na kusababisha kupiga marufuku wafanyakazi wa Serikali kushiriki siasa za chama cha TAA.

Mzee Costantine Oswald Millinga akiwa Tabora waliandika barua kwa Serikali ya kikoloni wakitaka watumishi wa Serikali waendelee kushiriki katika siasa za chama hicho na kwamba ombi hilo lilikubaliwa kwa kupewa miezi sita ikiwa ni kipindi cha angalizo.

Kufikia mwaka 1953 alifahamishwa na Mwenyekiti wake aliyemtaja kwa jina la Mwalimu Said Haroub, kwamba wangetembelewa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni kiongozi mkubwa wa TAA kutoka Dar es Salaam ikiwa ni muda mfupi tu tangu aliporejea kutoka masomoni, Chuo kikuu cha Edinburgh Uingereza.

Mwalimu Said Haroub alikuwa akifundisha katika Sekondari ya Tabora na huko nyuma alikwisha mfundisha Mwalimu Nyerere katika shule hiyo.

Mzee huyo anataja wajumbe wengine wa Kamati ya TAA huko Tabora kuwa ni pamoja na Walimu wa shule hiyo ya Tabora ambao ni Stephen Mhando na Erasto Mangenya.

Wengine ni mshairi maarufu Abdul Saadan Kandoro, Sheikh Amri Abeid Kaluta anayetajwa na Mzee Millinga kwamba “alikuwa maarufu sana” na Sheikh Abdallah Kivuruga ambaye anamtaja alikuwa “alwatani wa mjini”.
Mwingine katika safu hiyo ni Germanus Pacha aliyekuwa mtendaji mkuu wa Baraza la Machifu Tabora na mwanasiasa aliyejulikana baadaye, Balozi Andrew K. Tibandebage.
1709677905441.png

Picha : Balozi Andrew K. Tibandebage (kulia)

Wakati huo kwamba Mwalimu Nyerere alifika na kuwahutubia, hata hivyo katika kufunga kikao Mwenyekiti wa TAA Tabora alitamka kwamba “ndicho kikao cha mwisho cha Katibu” yaani Mzee Millinga anahama.

Mwalimu Nyerere akauliza anakwenda wapi?, ambapo Mzee Millinga katika tukio hilo ambalo ilikuwa mara ya kwanza kwake kuonana ana kwa ana na Nyerere, ambapo Nyerere alijibiwa kwamba Katibu (Millinga) anahamishiwa Dar es Salaam.

Mzee Millinga alipoingia Dar es Salaam
Mzee huyu wakati anasoma Januari mwaka 1954, tayari alikwisha ripoti jijini Dar es Salaam, kituo chake cha kazi kikiwa katika idara ya Maendeleo ya Jamii jengo la Arnatoglu, eneo maarufu la Mnazi Mmoja akiwajibika chini ya kiongozi wake aliyemtaja kwa jina la Dennis Phombeah.

Anasema Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na kawaida ya kufika mjini Dara es Salaam mara kwa mara akitokea Pugu nje kidogo ya Dar es Salaam hasa kwa siku za Jumamosi na kwamba walipokutana na Nyerere jirani na jengo hilo Dar es Salaam alimtamkia kwamba; “Millinga umekuja, nilivutiwa sana na maneno aliyoyasema Mwenyekiti wa (TAA-Tabora) juu yako”. Hapo Mzee Millinga alimjibu akisema; “na mimi nasema chama ni hicho hicho”.

Jambo hilo walikubaliana na Mwalimu Nyerere aliyemuahidi kwamba atawashawishi wenzake wamuingize katika Kamati ya TAA Dar es Salaam na hatimaye walikubali, katika hali ambayo Mzee huyu anasema ndivyo alivyoingia katika Kamati hiyo.

Katika vikao vyao vya TAA mkoa wa Dar es Salaam, walianza kujenga hoja ya kuibadili ili iwe na sura ya kisiasa kwa kuwa iliyokuwapo TAA haikuwa na nguvu na waliafikiana kufanya hivyo.

Vilevile mjadala ulikuwa mkali na walitaka kuondoa neno “Association” katika jina la chama hicho TAA - Tanganyika African Association , hiyo 'Association' ilimaanisha Ushirika jambo ambalo waliona waachane nalo na kukipatia jina la “Union” ikimaanisha “Umoja” wakiamini lina ushirikishaji wa wengi.

Kwa maana hiyo walipata pendekezo katika kikao chao cha TAA kwamba chama kiitwe Tanganyika African Union (TANU) na hasa neno Union liliwekwa kwa nia ya kujumuisha watu wote, lakini hilo wakalitafakari na waliona kwamba kwa kuwa nchi ya Kenya kuna Kenya African Union (KAU) chini ya Jomo Kenyatta, iliyopingwa marufuku na Uganda ambapo kulikuwepo Uganda African Congress (UAC) ikizingatiwa kwamba maeneo hayo kulikuwa na makoloni ya Mwingereza.

Hatua hiyo ilifanya Wajumbe wa TAA wagawanyike kwa makundi ya kanda, ambapo kila kundi walikuwa wakitafakari ni jina gani linafaa kwa ajili ya kuanzisha chama kipya cha siasa.

Kanda hizo ni Mashariki yaani Dar es Salaam, Pwani na Morogoro na kwamba Magharibi kulikuwa na Kigoma, Tabora na Mpanda huku kukiwa na kanda ya Mwanza na Bukoba pamoja na ya Kaskazini yaani Arusha na Moshi.

Wakati huo waliokuja na wazo la TANU ni wenzetu wa kutoka Mwanza ambao ni akina Saddan Kandoro, Lameck Makaranga na Walter Bugoke au kwa jina lingine maarufu alikuwa anaitwa “Kenyatta wa Tanganyika”.

Mnamo mwaka 1954 hapo ndipo Chama cha TANU kilizaliwa na kuandikishwa rasmi ikiwa ni chama kipya cha kisiasa kuchukua nafasi ya TAA.

Wakati huo, Serikali ya Kikoloni ilipiga marufuku watumishi wa Serikali (Umma) kushiriki kwenye masuala ya siasa, jambo ambalo lililomfanya aendelee kushiriki katika mikutano ya siasa za TANU kwa siri bila kuwa na kadi ya chama ili kuweza kulinda ajira yake, tofauti na wana – TANU wengine waliokuwa katika ajira ya Serikali kama vile Mwalimu Nyerere wao waliamua kujitosa kikamilifu na kuwa huru katika shughuli za chama.

Lakini maisha ya Mzee Millinga binafsi nimebaini yana mengi katika siasa za nchi na utumishi wa umma kwa ujumla, ikiwemo kujenga urafiki mkubwa na wanasiasa waandamizi nchini kama vile Hayati Rashid Kawawa.

Mzee Millinga alifikia hatua ya kujikita katika masuala ya siasa na utumishi baada ya kupitia uzoefu muda mrefu wa kusaka maisha hadi Ughaibuni yenye simulizi na vitimbi vingi baada ya kukerwa na mfumo wa uongozi wa kikoloni nchini.

Mbali na kushiriki siasa hasa katika harakati za kuanzisha TAA na TANU pia ni kinara katika utumishi wa umma ambapo baada ya Uhuru amekuwa katika idara ya Maendeleo ya Jamii hadi alipostaafu akiwa mzoefu hasa.

Baada ya Uhuru 1961 alikuwa daima mkimya kuhusiana na masuala ya siasa huku akijikita zaidi katika utumishi wa umma ingawa mapenzi yake makubwa kwa TANU hakuweza kuyaweka pembeni, aliyaweka rasmi alipojiunga na chama hicho kwa kukata kadi baada ya Uhuru ambapo huko nyuma alihofia angeachishwa kazi na Serikali ya kikoloni ambayo ilipiga marufuku watumishi wote wa umma kushiriki siasa.

Tangu zama hizo alikuwa pia ni rafiki wa karibu wa baba wa Taifa la Tanganyika Julius Nyerere , Kleist Sykes na vilevile ni rafiki wa karibu wa hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Tunamkumbuka Rashid Kawawa alivyoshiriki katika harakati za Uhuru wa Tanganyika kwa namna mbalimbali.

Wasifu kama huo na mengi umemfanya Mzee Millinga awe mtu anayeheshimika miongoni mwa wanaomfahamu, hasa kwa hulka yake ni vigumu kujikweza na ndilo jambo linalomfanya asifahamike.

Miongoni mwa wanaomtambua na kumheshimu kwa hadhi anayostahili ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa ambaye amekuwa akimtambua kwa staili ya kipekee kwenye shughuli muhimu za kitaifa ambapo huwa hakosi kufanya hivyo.

Hilo ndilo lililotokea wakati Rais Jakaya Kikwete alipozuru wilayani Mbinga mwezi June tarehe 4 mwaka 2011 katika sherehe ya kumtawaza Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Mbinga mhashamu askofu John Ndimbo ambapo alikuwa miongoni mwa wazee waalikwa wakibadilishana mawazo na Rais Jakaya Kikwete.

Mazungumzo hayo yaliweza kumuongezea elimu ya ziada Rais Jakaya Kikwete juu ya mengi kuhusu maisha binafsi ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, tangu zama hizo akiishi Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Kumbe kumtambua ni muasisi wa TANU, suala hilo lilimgusa Rais Jakaya Kikwete na hata kuagiza uongozi wa chama kufanya utaratibu wa kuhakikisha kwamba anakuwa miongoni mwa wageni rasmi wa kuzindua sherehe za miaka 50 ya Uhuru iliyofanyika Julai 7 mwaka 2011, na kwamba bila kujua kinachoendelea alipewa taarifa na uongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na wa Mkoa wa Ruvuma walimsafirisha hadi Dar es Salaam.

Kuhusu mchakato wa Uhuru
Mzee Millinga ana mengi kuhusu kipindi hicho, wakati huo Rashid Kawawa akiwa tayari ni Katibu Mkuu na mwanaharakati mwandamizi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TFL).

Wakati huo vuguvugu la TANU iliyoshirikiana kwa karibu na TFL mwaka 1958 katika uchaguzi mkuu ulitokea mgogoro mkubwa, juu ya ama TANU ikubali kushiriki au wakati huo Serikali ya kikoloni ilikuja na hoja kwamba uchaguzi utafanyika kwa utaratibu wa kura tatu ambazo ni za Mzungu, Mhindi na Mwafrika.

Mwalimu Julius Nyerere alifanya jitihada ya kuwashawishi wana – TANU wakubali hoja hii kwa kutumia mkutano uliofanyika Tabora ulioongozwa na Sheikh Kihore, lakini wanachama wengine kama Bwana Zuberi Mtemvu hakukubaliana na hoja hiyo na wakati wa uchaguzi alijitoa TANU na kuanzisha chama kilichoitwa UTP.

Wakati huohuo wapo watu wengine waliosimama kama wagombea binafsi bila vyama vya siasa na walifanikiwa kama vile Chifu Amri Dodo wa Mbulu na Chifu Herman Sarawati wa Babati.


Walikuwepo pia wahindi walioshiriki uchaguzi wa kuiunga mkono TANU kama vile Bwana Karimjee Jivanjee na Amir Jamal, mzungu Dereck Bryceson aliiunga mkono TANU na kwamba katika uchaguzi huo TANU iling’ara kwa kuwa hata wale waliosimama kama wagombea binafsi walikiunga mkono.

Licha ya upoinzani uliojitokeza hoja ya mwalimu Nyerere ilionekana ni ya msingi, kwani TANU iliibuka kinara na kuwa na hadhi ya kupewa haki ya kuongoza nchi.

Itakumbukwa kuwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Tanganyika ilikabidhiwa kwa wakoloni wa Kiingereza kutoka kwa Wajerumani kwa udhamini hadi itakapopata uwezo wa kujitawala.

Katika harakati hizi Mzee Millinga na wadau wengine muhimu wa Uhuru wa Tanganyika, John Rupia ambaye aliweza kutoa mchango wake wa shilingi 14,000 katika kumfahamisha safari hiyo ya Mwalimu Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa.

Ambapo wakati huo wakoloni waliweza kuwakatisha tamaa jamii ya Wamisionari na walitumia nafasi zao kuwakejeli Watanganyika kuwa bado hawakuwa na uwezo wa kujitawala, lakini ndoto ya Watanganyika ilitekelezwa Disemba 9 mwaka 1961.

Maisha ya Mzee Millinga
Mzee Constantine Oswald Millinga alizaliwa Novemba 22 mwaka 1921 akiwa mtoto wa kwanza wa Mzee Oswald Millinga na mama yake Victoria katika kijiji cha Nkaya, Kata ya Lituhi Wilaya ya Nyasa (Zamani Mbinga) Mkoani Ruvuma.
Yeye ni mzaliwa wa kwanza katika uzao wa watoto watatu, baba yake alikuwa fundi cherehani na mdogo wake mmoja alifariki dunia angali mdogo. Dada ya Mzee Millinga ana umri wa miaka 93.

Mzee Millinga alianza masomo mwaka 1926 katika shule ya msingi Nkaya kuanzia ya awali na baadae shule ya msingi hadi darasa la nne, alisoma palepale kijijini kwao Nkaya.

Baadae aliendelea na masomo ya darasa maalum la Kiingereza kwa miaka miwili katika shule ya Mision Peramiho. Mwaka 1936 hadi mwaka 1938 alipata mafunzo ya ualimu hapo hapo Mision ya Peramiho ilivyokuwa chini ya Wajerumani.

Alipohitimu, alianza kazi ya kufundisha katika shule ya maalum iliyokuwepo pale Mision Peramiho katika Seminari ya Kikatoliki ya Peramiho, akiwa hapo aliingia katika mgogoro na Mkuu wa shule ambaye alimtuhumu kuwa hafuati amri ya uongozi ya kukata nywele kila baada ya wiki mbili, ambapo Mzee huyu wakati wote alikuwa mtanashati na wakati huo alipenda kuchana nywele kwa mtindo wa “Way”.

Mgogoro huu ulisababishwa asimamishwe kazi kwa muda na kisha akahamishiwa kufundisha katika shule ya Nkaya alikosomea, aliweza kufundisha katika shule hiyo mpaka yalipotokea manyanyaso mengine ya kikoloni, ambapo Mwalimu Mkuu alimkera baada ya kumtukana mbele ya Wanafunzi na kumchapa makofi.
Sakata hilo liliamuliwa na Mkaguzi wa elimu kutoka Peramiho ambaye katika uamuzi wake alimhamishia katika kata ya Lituhi, jirani na Ziwa Nyasa ambako kulikuwa ni maili mbili kutoka alikokuwa huko alifanya kazi kwa mwaka mmoja na akaamua kuacha.

Mwaka 1942 Mzee Millinga aliibuka na uamuzi mwingine wa kuachana na kazi ya ualimu na akaamua kufanya safari ya kwenda South Africa kutafuta kazi, wakati huo nchi hiyo ilikuwa chini ya utawala wa Makaburu.
As far back as the 1940s, the Gold Mines of South Africa had set up what they called the Witwatersrand Native Labour Association (WNLA) later and more popularly known as Wenela. It was such a vast labour recruitment organisation that it spread its wings right across Southern Africa to Basutoland (Lesotho), Swaziland, South West Africa (Namibia), Bechuanaland (Botswana), Northern Rhodesia (Zambia), Southern Rhodesia (Zimbabwe), Nyasaland (Malawi), Angola and Mozambique. Labourers even went to the gold mines from as far as the Belgian Congo (DRC) and Tanganyika (Mainland Tanzania)! With time the acronyms Wenela and Soweto (South Western Townships) became words...https://www.herald.co.zw/purezha-the-germ-that-glitters-like-a-gem/
Alivyoianza safari ya kwenda huko akiwa na wenzake watatu, alikusanya nguo zake akizitaja kuwa ni Kaptura ya ziada (Mtindo wa vijana wakati huo ilikuwa kuvaa Kaptura) shati na shuka.
Wakati huo walipanda Mtumbwi, kutoka ukingoni mwa Ziwa Nyasa na waliweza kusafiri hadi Kyela na kisha wakaenda mji wa Karonga walikopanda meli ya MV Mpasa kwa nauli ya shilingi 30 wakati huo, mpaka Nkhata Bay na baadae walipanda gari Moshi hadi mji mkuu wa Blantyre Nyasaland (Malawi).

Baada ya hapo safari iliendelea kwa gari Moshi kupitia Mozambique na kuendelea hadi Rhodesia (Zimbabwe), walipofika katika mji wa Salisbury (Harare) wakiwa katika gari Moshi walikamatwa na askari waliowahoji kuhusu vibali vyao vya kusafiria.

Pamoja na mambo mengine, wakati huo walisafiria kwa kutumia nyaraka walizozitayarisha kwa maarifa yao zilizofanana na hati za kusafiria za wakati huo, lakini askari wale hawakuwaamini hivyo waliwekwa mahabusu na kuwafungulia mashitaka.

Wakiwa mahabusu walikutana na baadhi ya askari waliotokea Tanganyika ambao waliwasaidia kwa kuwaelekeza kwamba, ili wajinasue wajifanye hawajui Kiingereza wala Kiswahili bali wazungumze lugha ya Kimanda tu.

Mbinu hiyo ilileta utata mkubwa walipopelekwa Mahakamani, ilibidi Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi yao atafute mwendesha mashitaka anayejua Kiswahili ambapo pia iligundulika kuwa hawakijui Kiswahili.

Hivyo Mahakama iliwapa kibali cha kuwepo Zimbabwe kwa siku 14, waliishi huko wakihifadhiwa na Watanganyika wenzao na baadae waliendelea na safari ya kwenda Afrika Kusini, safari iliyowachukua siku tano huku wakivuka mbuga ya Transvaal kwa mguu wakiwa kundi la watu wapatao 10 walikabiliana na wanyama wakali na ukosefu wa maji ya kunywa, kuna wakati hawakulala huku baadhi ya maeneo walipofika walikuwa wakipeana zamu pale walipotaka kulala wengine wanakuwa macho wakijilinda na kukoka moto, kitu cha kustaajabisha ni kwamba baadhi ya wanyama wakali kama vile Faru waliuzunguka moto huo.

Walilazimika kuingia kwenye mashimo yaliyochimbwa na wanyama kutafuta maji, wakati mwingine walikuwa wakifukua mabonde ya mito ili kuweza kupata maji hatimaye safari yao ilifika katika mgodi wa Transvaal, ambako alienda kuomba kazi na akabahatika kupangwa katika stoo ya vyombo vya kuchimbia mgodi wa madini.

Constantine Oswald Millinga alipewa kazi hiyo kutokana na kuwa na mwandiko mzuri na wenzake walipata kazi katika vitengo vingine vya uchimbaji.
Mzee Millinga na wenzake walipofika pale mgodini waliweza kuonana na Watanganyika wengine, waliokuwepo huko na hao ndiyo waliowapa mbinu za kuwaingia Makaburu na kufanikiwa kupata kazi mgodini.

Hata hivyo hakuridhika na kazi hiyo, hivyo baada ya miezi miwili aliamua kuondoka pale na kuelekea mjini Johannesburg na kisha Cape Town ambako alipata ajira, kazi hii ya sasa ilikuwa ngumu kwa kuwa alipata kazi ya kubeba vifaa vya wachimba migodi, alikuwa anaingia mgodini asubuhi na kutoka jioni wakati huo malazi yalikuwa katika hema.

Baada ya mwezi mmoja wafanyakazi wenzake kutoka Tanganyika walimnong’oneza kuwa kuna nafasi ya kazi ya kitengo cha Ofisini, wakamsihi aandike barua ya maombi ambapo aliandika barua kuomba kazi hiyo na katika usaili alifanya vizuri na hapo alifanikiwa kupanda cheo na kuongezewa marupurupu na kuna wakati alilipwa posho ya ziada kwa kufanya kazi ya watu wawili.

Mwanzoni mwa mwaka 1950 alirejea nyumbani Tanganyika baadae alipata habari kuwa baba yake mzazi alikuwa mjini Dodoma, aliamua kumfuata ili aweze kumshawishi arudi nyumbani Lituhi ambapo alikubali na akarejea nyumbani, lakini Mzee Millinga hakurudi nyumbani bali aliendelea na safari hadi Wilayani Ngudu kwa baba yake mdogo aliyekuwa Inspekta wa Polisi ambapo ilikuwa sasa ni chimbuko la kupata ajira katika Idara ya Maendeleo ya Jamii, kwa msaada wa rafiki wa Inspekta huyo aliyekuwa anafahamika kwa jina la Fredrick Mchauro.

Mzee Millinga alijiunga na chama cha TAA mkoani Tabora, akiwa mtumishi wa Idara hiyo huko alipandishwa cheo kuwa katibu wa TAA Tabora katika kipindi hicho, Bwana Fredrick Mchauro alikuwa amehama Tabora kabla ya hapo alikuwa Mwenyekiti wa TAA Tabora.

Baada ya safari ndefu ya utumishi wa Serikali na harakati za TAA na TANU, baada ya Uhuru Mzee huyo akiwa mkaazi wa mtaa wa Lindi na baadae Temeke Wailesi Kota, Dar es Salaam na hapo baada ya Uhuru alijikita zaidi katika ajira yake ya Serikali.

Utumishi wake ulipitia katika sehemu tofauti, kuanzia Kilindi alikokuwa amehamia baada ya kutoka Dar es Salaam mara tu baada ya Uhuru na baadaye alihamia Morogoro na baada ya mizunguko ya muda mrefu, aliomba ahamishiwe kwao Mbinga ambako aliondoka miaka mingi na kustaafu utumishi rasmi mwaka 1976.

Mzee Millinga, ambaye ni kati ya Waasisi 17 wa TANU mwaka 1954 hapa nchini, amefariki dunia usiku wa kuamkia Machi 5 mwaka 2018 saa 7:40 Mbinga mjini akiwa nyumbani kwake amezungukwa na familia yake.
maeneo ya nyumbani kwake mtaa wa Mhekela Mbinga mjini.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ndugu Rodrick Mpogolo akiweka shada la maua katika kaburi la Muasisi wa TANU, Marehemu Costantine Millinga mara baada ya mazishi yake kufanyika leo Mbinga mjini
Source : Kwa hisani kubwa ya : nyandindi2006.blogspot.com/2018/03/makala-mzee-millinga-muasisi-wa-tanu.html?
 
Ndugu zanguni,
Mwandishi wa historia ya Mzee Millinga haijui historia ya African Association.

Halikadhalika historia ya Mzee Millinga haiko sawa kwa kukosa rejea zenye ithibati.

Yametajwa majina mfano wq Denis Phombeah na Erasto Mang'enya hawa walikuwapo wakati harakati za uhuru zinaanza lakini kama alivyokuwa Millinga mwenyewe hawa si msingi wa kuijua historia ya TANU.

Nakuwekeeni kipande hapo chini kutoka kitabu cha Abdul Sykes:

Historia ya TAA Jimbo la Magharibi, 1955

Tabora ilianza kushiriki katika siasa mwaka 1945 wakati African Association ilipoingizwa mjini Tabora kutoka Dodoma kutokana na juhudi za Edward Mwangosi.

Tabora kwenyewe msukumo wa katika kuanzisha chama cha Waafrika zilitoka kutoka Combine Dancing Club, kilabu kilichoanzishwa na vijana wa pale mjini kwa ajili ya kujifurahisha.

Wanachama mashuhuri wa kilabu hiyo walikuwa ndugu wawili Wamanyema - Maulid na Abdallah Kivuruga, Chamng’anda Usingizi, Ramadhani Nasibu, Rashid Mussa, Issa Kibira, Hamis Wabeba, Mwinyi Khatib Hemed, Swedi Juma, Issa Hamis Pama na Rajab Kanyama.

Wanachama wengi wa kilabu hii walikuwa Wamanyema, kizazi cha pili baba zao wakiwa wametokea ile iliyokuwa wakati huo Belgian Congo, wakafanya maskani Kigoma, Ujiji na Tabora mwishoni mwa karne ya 19.

Wamanyema likiwa kabila la Waislam watupu ilikuwa rahisi kuungana kama kikundi cha kabila moja na kuanzisha chama cha siasa.

Kwa hiyo Combine Dancing Club kidogo kidogo ilijigeuza kutoka chama cha starehe na kuwa chama cha siasa.

Kumbukumbu za kikoloni zinaonyesha kwamba kamati ndogo ndani ya kilabu iliundwa katika mwaka 1945, Mwinyi Khatibu Hemed, Mzigua kutoka Bweni, Pangani, akiwa katibu.

Hemed aliandika barua makao makuu yaAfrican Association mjini Dar es Salaam kuujulisha uongozi ju ya dhamira ya kufungua tawi mjini Tabora.

Tarehe 3 Machi, 1945 African Association mjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais), M. K. Hemed (katibu), Chamngíanda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).

African Association, kama ilivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema.

Hivi ndivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika.

Julius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Maryís School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa African Association.

Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu ya historia kazi yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake.

Mwaka 1946 wasomi wa Makerere walianza kujishughulisha na African Association pale Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walipochaguliwa Katibu na Katibu Msaidizi na nafasi nyingine za uongozi zikishikwa na Wamanyema.

Baada ya uhamisho wa Mwapachu kutoka Tabora, Nyerere akashika nafasi yake na kuwa katibu wa chama. Mwaka huo huo Nyerere alisafiri kwenda Dar es Salaam kama mjumbe wa Tabora kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa African Association.

Katika mkutano huu ndiyo kwa mara ya kwanza Dossa Aziz alimtia Nyerere machoni. Lakini urafiki baina ya Dossa na Nyerere haukushamiri hadi mwaka 1952, Nyerere alipokuja Dar es Salaam na kuungana na wazalendo wengine.

Mwaka uliofuata, African Association Tabora ilikuwa imejiimarisha vizuri kiasi cha kuwa na uwezo wa kushiriki katika mgomo wa mwaka 1947 ambao ulianza katika bandari ya Dar es Salaam.

Kuwako kwa Waislam wengi sana katika ajira ya bandarini kwa kiasi kikubwa kulichangia kuwasha moto wa mshikamano uliolipua mgomo.

Wakati wa mgomo Tabora, Mwalimu Pinda, aliyekuwa miongoni mwa walimu wa St. Maryís School na mwanachama wa African Association, alichukua jukumu la kuwa mtu wa kati baina ya wawakilishi wa wafanyakazi waliogoma na African Association.

Siku ya mgomo wafanyakazi wengi wao kutoka karakana ya magari moshi ya wakiongozwa na Salum Abdallalh, walikusanyika katika viwanja vya Tabora Town School chini ya miembe.

Tabora ni maarufu kwa wingi wa miembe. Kuanzia siku hiyo viwanja hivyo vikawa ndiyo mahali pa mikutano yote ya African Association.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Nyerere hakujihusisha na hizi harakati za tabaka la wafanyakazi zilizokuwa zikiibuka.

Mwaka 1950 Tanganyika African Association (TAA) kama sasa ilivyokuwa ikijulikana ilikuwa chini ya uongozi wa George Magembe, mwalimu wa St. Maryís School. Magembe, Mbondei kutoka Muheza, alikuwa akiandikiana barua nyingi na Stephen Mhando, Mbondei mwenzake aliyekuwa mjumbe wa kamati ndogo ya siasa ya TAA mjini Dar es Salaam.

Wakati ule kamati ndogo ya siasa katika TAA ndiyo kwanza ilikuwa imeundwa. Kupitia uhusiano huu baina ya Magembe na Mhando, TAA Tabora iliweza kuimarisha mawasiliano kati yake na makao makuu na kupeana taarifa za siri.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

Huyu Salum Abdallah anetajwa kuwa alikuwa anaongoza mgomo wa wafanyakazi wa Relwe mwaka wa 1947 ni babu yangu na ndiyo mwaka alihamishwa Dar es Salaam kuja Tabora.

Hao wazalendo wengine anaowataja ukoo wa Kivuruga mimi ni baba zangu: Abdalla na Maulid Kivuruga mtu na nduguye.

Said Mussa na Germano Pacha wote nikiwafahamu.

Harub Said akijuana na wazee wangu toka udogoni hadi wamekuw watu wazima.

Ninachotaka kusema ni kuwa mimi ni sehemu ya historia hii na naijua vyema.

1709617148071.jpeg

Salum Abdallah (President)na kushoto kwake ni Kassanga Tumbo (Secretary) Tanganyika Railways African Union (TRAU) na viongozi wengine

1709617315692.png

Abdallah Kivuruga
1709617358566.png

Maulidi Kivuruga​
 
Mzee huyo anataja wajumbe wengine wa Kamati ya TAA huko Tabora kuwa ni pamoja na Walimu wa shule hiyo ya Tabora ambao ni Stephen Mhando na Erasto Mangenya.
Chifu wa wabondei Erasto Mangenya
1709635422125.png

balozi Erasto Andrew Mbwana Mang'enya - Alizaliwa Aprili 17, 1915 (umri wa miaka 104), Kijiji cha Mkuzi Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga, Tanzania. Yeye ndiye mtoto wa kwanza wa Canon Henry na Mary Eleanor Mang'enya

Elimu

Kuanzia 1919 hadi 1933 alipitia shule kadhaa za Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na Tanga. Shule alizosoma ni Mkuzi, Magila, Kiwanda, na hatimaye Shule ya Mafunzo ya Ualimu Minaki.

Mnamo 1934 alijiunga na Chuo cha King's College Budo katika taasisi nyingine ya Anglikana, ambapo alifanyia Mtihani wa Kuingia Chuo cha Makerere.

Kuanzia 1935 hadi 1937 alikuwa katika Chuo cha Makerere.
Erasto Andrew Mbwana Mang'enya ( 17 Aprili 1915 – ) alikuwa mwanadiplomasia wa Tanganyika/Tanzania na mwanasiasa.

Alikuwa chifu wa Wabondei, kutoka Milima ya Usambara kaskazini - mashariki mwa Tanzania. Kabla ya kuwa chifu wa Wabondei, Mang’enya alikuwa mwalimu mkuu katika Shule ya Sekondari Old Moshi.

Alikuwa mmoja wa Watanganika wa mwanzo kupata shahada ya chuo kikuu, alijihusisha sana na utambulisho wa kisiasa wa Bondei mwishoni mwa miaka ya hamsini, lakini alifanikiwa kuandika historia ya maisha yake na kujihusisha na utaifa mkubwa wa Tanganyika, na baadaye kuacha kuweka ukabila kwa kupendelea jukumu lake katika utumishi wa umma.


Mwaka 1938 aliingia katika Idara ya Elimu ya Tanganyika, mtangulizi wa Wizara ya Elimu ya Tanzania, na kufanya kazi katika Shule za Sekondari zifuatazo:
1938 - 1943 Malangali,;
1943 - 1947 Moshi,;
1947 - 1952 Tanga,;
1953 - 1957 Tabora,.
Mwaka 1958 alifundisha Shule ya Sekondari Songea.

Mwishoni mwa mwaka 1958, Mang’enya alichaguliwa kuwa Mtema (Mkuu) wa Wabondei wa Wilaya ya Muheza.

Mwaka 1960 aliingia Bungeni kwa tiketi ya Tanganyika African National Union Party na kuchaguliwa kuwa Naibu Spika.

Mwaka 1962 aliteuliwa kuwa Waziri Mdogo katika Wizara ya Mawasiliano, Nguvu na Ujenzi wa Serikali ya Tanganyika mpya.
Mwaka 1963 alihamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na kupelekwa New York kama Mjumbe Mkuu wa Tanganyika katika Umoja wa Mataifa.

Kuanzia Aprili 17, 1963 hadi 1964 alikuwa mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa.
Kuanzia 1964 hadi 1965 alikuwa waziri wa maendeleo ya jamii na utamaduni wa kitaifa.

Mwaka 1965 alikua Mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi ya Tanzania (Ombudsman).

Mnamo 1970 aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mahakama iliyosikiliza rufaa kuhusu Majengo Yanayopatikana.

Mnamo 1972 alikua tena Mwenyekiti wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi.

Akiwa Mwenyekiti, alitembelea Australia, New Zealand na Israel.
Mnamo 1967 alisafiri kwenda nchi za Skandinavia, Ujerumani Mashariki na kutembelea Umoja wa Kisovieti.

Alikuwa Spika wa Bunge kuanzia Novemba 1973 hadi Novemba 1975.
 
Mzee huyo anataja wajumbe wengine wa Kamati ya TAA huko Tabora kuwa ni pamoja na Walimu wa shule hiyo ya Tabora ambao ni Stephen Mhando

WAZEE WAWILI MAARUFU WA TANU MKUTANO WA BOMBAY (MUMBAI)

Wanasiasa wawili wa TANU waliohudhuria mkutano wa Bombay: Stephen Mhando na Ali Mwinyi Tambwe.

1709644997718.png

Picha maktaba : Stephen Mhando (kuzaliwa mwaka 1918) : waziri wa mashirikiano 1968 - 1969.

Si Mhando wala Tambwe waliochapisha hadithi ya maisha yao, kwa hivyo makala haya yanageukia ripoti za kijasusi za wakoloni
iliyo ndani ya faili za 'kumbukumbu zilizohamishwa' zilizohifadhiwa kwenye
Kumbukumbu za Kitaifa huko London.

Uwepo wa faili hizi ilikuja kujulikana kupitia kesi ya kisheria dhidi ya Waingereza serikali iliyoletwa na manusura wa unyanyasaji wa kikoloni dhidi ya Mau Mau inashukiwa nchini Kenya.9 Faili hizi, pamoja na marejeleo ‘FCO 141/…’ inajumuisha wingi wa polisi ambao hawakujulikana hapo awali
kuripoti harakati za kupinga ukoloni.10 Licha ya kuendelea.


kampeni za kurejesha faili hizi zenye taarifa za ukoloni wa zamani nchi za Afrika ya Mashariki, hubakia tu kwa watafiti huko London.

Yaliyomo ndani ya faili hizi zilizokusanywa na kitengo cha polisi wa kikoloni yanapaswa kutibiwa kwa uangalifu. Mara nyingi nyingi ripoti hizo lengo linaonyesha zaidi kuhusu mahangaiko ya maafisa wa kikoloni kuzijua harakati za kisiasa za wakoloni kuliko nia ya Waafrika wanasiasa wa mwanzo kabisa ambazo ni somo kwao.

Walakini, ripoti hizi zikitumiwa kwa umakini, kina cha kuripoti huturuhusu kuchunguza siasa za TANU kwa undani usio na kifani.

Kabla ya kuanza, ni lazima ieleweke kwamba kulikuwa na
mwanachama wa tatu wa TANU huko Bombay: Lawi Sijaona. Ingawa wasifu unabaki bado kuandikwa, hadithi ya Lawi N. Sijaona ni mwanaharakati bora zaidi
anayejulikana kama mwanasiasa huko Mtwara, Tanganyika kiongozi wa Umoja wa Vijana wa TANU
, na aliyepewa nyadhifa nyingi katika baraza la mawaziri baada ya uhuru.11 Safari za Lawi Sijaona mwenyewe huko Asia Kusini zilikuwa chache na pana kuliko za Stephen Mhando au Ali Tambwe; kwa kweli, kama sisi
utaona, taarifa za Lawi Sijaona kuhusu tabia zao ziliporipotiwa Dar es Salaam ilichangia kutengwa kwao kwa muda
ndani ya TANU.


Ripoti za special branch ya polisi wa kikoloni kuhusu mwanasiasa Stephen Mhando
Njia za kuingia TANU

Stephen Mhando alizaliwa Moshi mwaka 1918. 12 alihudhuria
Tabora Boys School na kisha kuendelea na masomo kupitia a
stashahada ya kufundisha huko Makerere - njia ile ile iliyochukuliwa baadaye na Nyerere, mdogo wake kwa miaka minne.

Imeundwa kuzalisha a
tabaka la watumishi wa umma wa kikoloni mkoa, Tabora na
Makerere yalikuwa maeneo muhimu katika uundaji wa tabaka la Mwafrika mpya lililo na wasomi wa kisiasa.

Mhando alihitimu kutoka Makerere mwaka 1939 na alirudi Tanganyika, ambako alifanya kazi kama mwalimu wa shule. .13 Kurudi kwa Stephen Mhando, Tanganyika kulilingana na kujiimarisha katika maisha ya kisiasa kupitia kuzindua upya Jumuiya ya Waafrika, AA ambayo alijiunga nayo miaka ya 1940.

Mnamo 1951, aliteuliwa kwa muda mfupi kama rais wa baraza la viongozi waafrika lililoitwa Tanganyika African Association TAA. Pia alichukua majukumu ya kulea ofisi nyingi za matawi ya TAA katika maeneo yaliyochipuka Tanganyika
: mnamo 1952 alikuwa katibu wa Jumuiya ya Watumishi wa Serikali walio waafrika (African Government Servants’ Association) na Chama cha Walimu walio Waafrika (African Teachers’ Association).


Ali Mwinyi Tambwe alichukua mkondo tofauti katika siasa. Kwanza, hakuwa na asili ya Tanganyika, bali Mgazija wa Comoro. Baada ya kuwa
alizaliwa kati ya 1916 na 1918 katika Visiwa vya Comoro, ambavyo vilikuwa koloni la Ufaransa.18 Familia yake iliondoka Comoro kwenda Zanzibar alipokuwa mtoto.

Familia ya Tambwe walijiunga katika jumuiya ndogo ya wangazija waliowakuta Zanzibar lakini ilizidi kukua kama
jumuiya ya diaspora iliyopo Zanzibar, ambao wengi wao walishawishiwa na biashara na
fursa za ajira zinazopatikana katika Visiwa vya Zanzibar iliyokuwa chini ya Usultani.

Jumuiya wa wangazija walichukua mrengo wa tabaka la watu usiyoeleweka na yenye ushindani ndani ya tawala za kikoloni za Zanzibar. Ingawa
kimuonekano sawa na Waafrika, Comorians alichota zaidi desturi za Kiarabu.

Ali Tambwe asili aliyotokea na elimu yake ilimpa uwezo wa lugha za Kiingereza, Kifaransa, na Kiswahili. Baada ya kumaliza shule ya sekondari, Tambwe alihamia Tanganyika, ambako alianza kazi katika utumishi wa umma katika wilaya, ambayo
hatimaye kumleta Dar es Salaam.

Katika mji mkuu, Ali Tambwe alianza kujishughulisha na maisha mahiri lakini mara kwa mara tukio lenye mkanganyiko wa maisha ya ushirika wa Kiislamu. Mnamo 1933,
Waislamu mashuhuri wa Kiafrika jijini Dar es Salaam waliunda
Jamiatul al-Islamiyya (Jumuiya ya Waislamu Tanganyika).

Wao waislamu watanganyika 'wenyeji' wakidai kuwa taasisi za Kiislamu za jiji hilo zilitawaliwa
na Waasia wasomi , ambao walishindwa kutoa elimu ya kutosha kwa Waafrika.20 Wakati fulani mwishoni mwa miaka ya 1930, Tambwe alikua kiongozi
katibu wa shirika Jumuiya ya Waislamu Tanganyika . Alifanya hivyo kwa wakati usiofaa, kama
shule ya msingi ya jamii ilikuwa imefungwa na wakoloni
utawala huku kukiwa na mivutano kati ya Jamiatul
wanachama, hasa kuhusu jukumu lake kama rais, liwali wa Dar es Salaam.21 Liwali, ambaye
alisimamia haki kwa wakazi wa jiji 'wenyeji'.

Zogo kubwa liendelea baina ya waislamu Dar es Salaam.
Wakimtuhumu Ali Tambwe kuwa ni mtu mwenye utata katika maisha ya kisiasa ya mijini.

Baada yake kuanzishwa mwaka 1921, ofisi ya liwali iliongozwa
pekee na Waarabu, hili lilipelekea ukosoaji wa waislamu waKiafrika. Baadhi ya wasomi wa mjini, wengi wao wakiwa Waarabu na wazee wa mijini wa Kiafrika (wenye mji),
kuendelea kumuunga mkono liwali. Lakini baadaye , zaidi
kundi la wahamiaji wa Kiafrika waliowasili hivi karibuni
(watu wa kuja), akiwemo Tambwe, walipinga vikali
dhuluma ya rangi katika mpangilio wa uongozi wa waislamu .22

Harakati za Ali Tambwe kutetea 'waafrika wenzake' pia zilizua machafuko kati ya Wacomoria wa Dar es Salaam ambao
jamii yao iliyo wahafidhina zaidi walijihusisha zaidi kuwa wao wangazija ni ‘Waarabu’.

Mwaka 1946, Ali Tambwe alishikiliwa kuwajibika kwa mgawanyiko ndani ya jamii ya Comorian ya Dar es Salaam
. Katika mabishano haya yanayoingiliana kwenye
Jamiatul na miongoni mwa Wacomoria wenzake, Ali Tambwe ilikubali wazo lililozungukwa zaidi la rangi ya Waafrika kama
utambulisho wao kuliko uarabu ulizidi kuwa msingi wa kisiasa
Ushirika mjini Dar es Salaam.

Hii ilikuwa tofauti kabisa
kutoka kwa chaguo lililofanywa na watu wengi wa Comoro, haswa katika Zanzibar, waliojifungamanisha na maslahi ya Waarabu. Haya
matukio pia yanaonyesha jinsi Ali Tambwe alikuwa tayari
kama mhusika mkuu wa mgawanyiko, anayeweza
kujenga madaraja katika jamii ya mijini wakati huo huo
kuwachoma wengine.


Ali Tambwe anaibuka tena katika rekodi ya kumbukumbu tena mapema Miaka ya 1950, maisha ya kisiasa ya Kiafrika yaliposhika kasi. Akawa
hai katika Jumuiya ya wafrika TAA jijini Mwanza, akikutana na
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayehusika na masuala ya kikoloni katika ziara yake Tanganyika mwaka 1950.23


Ali Tambwe alirejea Dar es Salaam mnamo 1952, ambapo alifanya kazi kwa muda mfupi idara ya serikali ya ujenzi . Alianza tena kujihusisha na Jamiatul Islamiyya, ambapo aliteuliwa tena kuwa katibu mkuu.24 Ali Tambwe pia alihusika katika uundaji wa Kituo Kikuu Jumuiya ya Waislamu wa Tanganyika mwaka 1954. Shirika hili liliwaleta waislamu chini ya mwamvuli mmoja ikijumuisha Waafrika, Waarabu, na Waasia katika jaribio la kuweka viraka kutokana na tofauti zilizokuwepo mwanzo za kimadhehebu na rangi nchini Jumuiya ya Kiislamu.25

Mpango huu ulimletea tena mgongano na liwali ambaye alikuwa hana raha katika jukumu lililochezwa ndani ya Jumuiya ya Mrengo wa Kati iliyoongozw na mwafrika kijana , mwenye msimamo mkali zaidi
Waislamu kama Tambwe.26

Ali Tambwe alianzisha tena vita vyake na Jumuiya ya Comorian, ambayo ilikuza uhusiano mzuri
pamoja na liwali ambaye siku zote ni mwarabu .27

Rais wa chama alitoa wito kwa
Mkuu wa Wilaya kumfukuza Ali Tambwe Dar es Salaam.
Tambwe alichukua mtaji wa kisiasa na kijamii aliokuwa nao
ambao Uliopatikana kupitia ushiriki wake katika Jumuiya ya Waafrika AA / TAA na maisha ya kisiasa ya Waislamu kuyaingiza katika shughuli za TANU jijini Dar es Salaam. Baada ya kuingizwa TANU na Zuberi
Mtemvu, katibu mkuu wa kwanza wa shirika hilo mwezi
Januari, Tambwe alichaguliwa kuingia katika
Kamati Kuu ya TANU mwaka 1955.28

Umahiri wake katika uongozi wa ushirika wa waafrika wa TAA pia jumuiya ya waislamu na
ujuzi wa lugha ulithibitisha awe rasilimali muhimu kwa TANU. Mwezi wa sita,Tambwe aliwahi kuwa mfasiri na aliwekwa katika msafara wa John Hatch,
afisa kutoka Chama cha Labour cha Uingereza, aliyeondoka Tanganyika pamoja na ofisa mpendwa wa TANU kwenda Nairobi.29
John Hatch alikuja kutembelea Tanganyika kama mgeni wa TANU mara Juni 1955. TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Mnazi Mmoja na Hatch akawahutubia wananchi. Inakisiwa takriban wanachama wa TANU na mashabiki wake jumla yao kiasi watu elfu ishirini walijitokeza kwenye mkutano huo. Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mkalimani wa Hatch. Denis Phombeah pamoja na katibu mkuu wa TANU, Oscar Kambona vilevile walihutubia halaiki ile. Hatch akiwa anaunga mkono ukombozi wa watu weusi aligundua kuwa TANU haikuwa na tawi la akina mama. Katika dhifa ya chai iliyoandaliwa na TANU kwa heshima yake, Hatch alilieleza tatizo hili kwa Schneider Plantan na John Rupia. Hatch alimwambia Schneider kwamba ili kuwa na chama chenye nguvu TANU isiwaache akina mama nyuma. Hatch alimwambia Schneider kwamba huko Uingereza Labour Party kilikuwa kimejikita kwa wanawake kama moja ya nguzo yake kuu.
Mwezi Desemba, Tambwe
alifuatana na Nyerere katika ziara za kikanda zilizofanikiwa kuongeza idadi ya
Wanachama wa TANU kote Tanganyika.30 Akiwa TANU
alitumika kujenga uungwaji mkono miongoni mwa jamii ya Tanganyika iliyoathiriwa na ubaguzi wa rangi
mgawanyiko, Tambwe aliibuka kuwa dalali muhimu katika Dar es Salaam kuwaleta pamoja
Jumuiya za Waafrika na Waasia za Salaam, ikizingatiwa
uzoefu wake katika vikundi kama Jumuiya ya Mrengo wa Kati. Alikusanya fedha kwa niaba ya TANU kutoka kwa jumuiya ya Waasia wa Dar es Salaam
, kwa muda mfupi mapema 1956, aliwahi kuwa mtoa habari wa siri aliyelipwa wa ubalozi wa India huko Nairobi kuhusu vuguvugu la maendeleo ya kisiasa Tanganyika kudai uhuru.

Hata hivyo Tambwe naye aliendelea mabishano mahakamani. Nafasi yake katika siasa za Kiislamu ilisababisha
wasiwasi miongoni mwa baadhi ya wanachama wa TANU, kutokana na
kuhusika katika Jumuiya ya Kati ya Waasia kadhaa ambao
walikuwa wanashaka kama Tanganyika ipo tayari kwa uhuru chini ya waafrika 31

Kama kwa Stephen Mhando, Ali Tambwe pia alituhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za chama.
Mhando na Tambwe walichukua njia tofauti kuelekea TANU
lakini walionyesha uwezo wao wa kutengeneza miunganisho katika mazingira ya kisiasa yenye alama ya kuenea kwa
utamaduni wa ushirika. Mwenendo wa Mhando ulikuwa ni wa mzalendo wa kiafrika zaidi. Ya Tambwe ilikuwa zaidi
isiyo ya kawaida na ya kimataifa, kama inavyofichuliwa na mitandao ya mahusiano aliyoyaanzisha jijini Dar es Salaam, ambayo
wakati huo huo mgawanyiko wa rangi wakati wa kuchochea
makabiliano kati ya Waislamu na Wakomoro wa jiji hilo la mchanganyiko.

3.0 Tikiti za kwenda Bombay
Kampeni ya TANU ya uhuru ilipozidi kupamba moto, wao
wakiwa pamoja huko Asia walijadili jinsi ya kutafsiri siasa
za uhuru katika maendeleo ya kiuchumi. Indonesia
Ilitangaza uhuru mwaka 1945. Utawala wa kikoloni uliishia
Burma, India, na Pakistani mwaka wa 1947. Ilisukuma kwenye siasa za kusaka uhuru .

Watanganyika watatu Stephen Mhando, Ali Mwinyi Tambwe na Lawi N. Sijaona walifika Bombay tarehe 5 Novemba.
Mara moja walijihusisha katika mkutano huo, ambao
Ulihudhuriwa na idadi ndogo ya Waafrika wengine, wakiwemo
Mkenya Joseph Murumbi. Kama waangalizi, Watanganyika hawakuwa na haki ya kupiga kura lakini waliruhusiwa
kuhutubia mkutano huo. Stephen Mhando na Lawi Sijaona walishiriki
kamati ndogo ya ukombozi wa Afrika. Waliondoka zao wakiacha alama kwenye mkutano huo, ambao ulitoa azimio lililoitisha
kwa Uingereza kutamka kuwa Tanganyika itaendelezwa
'kimsingi kama taifa la Afrika', kwa kuanzishwa kwa
uchaguzi wa kidemokrasia bila uwakilishi wa jumuiya
zimetengwa kwa ajili ya makundi mbalimbali ya rangi.

Pia ilizua wasiwasi kuhusu kutengwa kwa ardhi ya Tanganyika na walowezi wa kigeni, hasa kutoka Afrika Kusini, ili ‘hadithi ya Kenya Isirudiwe tena’ – rejeleo la mzozo wa Mau Mau.43

Nje ya ukumbi wa mikutano, Stephen Mhando alihutubia mkutano wa hadhara
kuadhimisha Siku ya Watu tegemezi tarehe 11 Novemba. Aliwaambia umati wa watu unaokadiriwa kuwa watu 20,000 kwamba mkutano huo ulikuwa ‘Unaonesha Picha Halisi ya Ukoloni Mbaya '

Ukumbusho kwamba mamilioni ya watu walibaki chini ya ukoloni
kandamizaji. Mhando alisema kuwa nia njema aliyokuwa nayo
uzoefu katika mkutano huo utawatia moyo Waafrika katika
kupigania uhuru wao.44

Yote kwa yote, basi, Mtanganyika
mchango kwa mkutano wa ASC Bombay India ulikuwa mdogo. Kwa ujumla zaidi,
ripoti kuhusu mkutano huko Bombay zilizimwa na
migogoro ya iliyochipuka mahali pengine: uvamizi wa Soviet
Hungaria na udhalilishaji wa Franco-Uingereza-Israeli juu ya
Suez Canal mikononi mwa Misri ya Nasser. Lakini, kama ripoti ya Mhando na karatasi za Tambwe zilivyofichua, wakati wao huko Bombay ulikuwa wa manufaa kwa ukombozi za nchi zilizokuwa chini ya ukoloni.

4.0 Ripoti ya 'Yule mhuni dhidi ya mkoloni?' ndiyo alivyoonekana Mhando baada ya Bombay.
Baada ya mkutano huo, wajumbe wa Bombay wa Tanganyika walikwenda
njia zao tofauti. Stephen Mhando alipewa jukumu la kuhakikisha
msaada wa kisiasa na hasa wa mali kwa TANU. Yeye
alianza safari iliyompeleka kuzunguka Asia ya Kusini,
kupitia Mashariki ya Kati, na kurudi Afrika. Hata hivyo
Mhando alisafiri kama mwakilishi wa TANU, nyaraka
maofisa wa kikoloni walinakili aliporudi kuonyesha kwamba alifanya hivyowakati huo huo akifuatilia miradi yake ya kisiasa.
Katika safari zake, Mhando alifanya kazi kwa karibu na
Munukayumbwa Sipalo, ambaye pia alikuwa amehudhuria mkutano wa ASC. Sipalo alikuwa mwanafunzi wa sheria kutoka Kaskazini Rhodesia (Zambia), ambaye alikuja India kwa ufadhili wa masomo mwaka wa 1954.
Source : Declassified Colonial
intelligence reports
TANU’s Bombay Delegates: Stephen Mhando, Ali
Mwinyi Tambwe, and the Global Itineraries of
Tanganyikan Decolonisation
George Roberts
University of Sheffield and European University Institute,
Florence
AbstractDespite the recent move to understand African decolonisation in more global and transnational terms, the history of TANU’s
struggle for independence remains understood primarily through a
nationalist paradigm. Tanganyikans remain largely overlooked in the new historiography of ‘Afro-Asian’ connections in the 1950s.
This article addresses this lacuna by sketching out the dual
biographies of two less prominent TANU leaders, Stephen Mhando
and Ali Mwinyi Tambwe. Using recently declassified colonial
intelligence reports, it follows their journeys to the meeting of the
Asian Socialist Conference in India in 1956 and subsequent travels
around the Indian Ocean coastline. Through these life-stories, the
article argues that activism under the auspices of African
nationalism provided a platform for aspiring politicians to pursue
their own projects in a decolonising world. These included the
organisation of pan-African conferences, creating transoceanic solidarities between Muslim organisations, securing patronage from Cold War powers, and advancing anticolonial causes in Africa’s Indian Ocean basin
 
mwanasiasa aliyejulikana baadaye, Balozi Andrew K. Tibandebage.

1709678140795.png

Katika Picha : (kulia Balozi) Andrew Kajungu Tibandebage

Balozi Andrew K. TIbandebage alizaliwa mwaka wa 1921 katika kijiji cha Kasheshe Karagwe Bukoba na kubatizwa kwenye Kanisa la Katoliki mwaka 1932. Alijiunga na Shule ya Msingi Bugene mnamo mwaka 1933 na mwaka uliofuatia alihamia shule ya Kajunguti – Rubya – Bukoba.

Elimu ya sekondari aliipata kwenye shule ya St Mary’s Tabora kati ya mwaka 1939 na 1941. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere – Uganda mnamo mwaka 1942.

Baada ya masomo yake, alifundisha kwenye shule yake ya St Mary’s Tabora. Akiwa mwalimu wa Kiingereza na Hisabati. Mwaka 1955 aliteuliwa kuwa mkuu wa Shule ya Kati ya Bugene Karagwe. Mwaka 1956 alihamishiwa sekondari ya Mtakatifu Thomas (Ihungo) Bukoba, kufundisha Kiingereza na kuwa mkuu wa Idara ya Hisabati.

Kati ya mwaka 1956 na 1957 alikuwa mhadhiri mshiriki katika Chuo Kikuu cha London. Aliporudi Tanganyika, aliendelea kufundisha Ihungo – Bukoba mpaka 1961 alipojiunga na utumishi wa umma serikalini.

Agosti 1961 alirudi London, Uingereza Kuhudhuria semina ya utumishi wa kidiplomasia. Na Septemba 1961 alifanya kazi katika Ubalozi wa Uingereza huko Ankara, Uturuki. Januari 1962 alifanya kazi katika Ubalozi wa Tanganyika huko London, Uingereza.

Ni mtu wa kwanza kufungua ubalozi wa Tanganyika nchini Ujerumani mnamo mwaka 1962. Februari 1963 aliteuliwa kuwa balozi wa kwanza wa Tanganyika nchini Ujerumani.

Balozi Tibandebage alikuwa pia mtu wa kwanza kufungua ubalozi wa Tanganyika kule Congo-Kinshasa na kuwa balozi kule hadi mwaka 1967 aliporudishwa nyumbani kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari na Utalii. Mwaka 1968 aliteuliwa tena kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, na mwaka 1970 alirudishwa tena nyumbani kuwa Msaidizi wa Rais (Mambo ya Nje). Mwaka 1972 alirudishwa Kinshasa kuwa Balozi wa Tanzania kwa nchi za Congo, Rwanda na Burundi. Desemba 21, 1975 aliacha kufanya kazi za kidiplomasia na Mei 31, 1976 akastaafu utumishi wa umma.

Aliporudi nyumbani kwao Karagwe aliendelea kushirikiana na wananchi kuiendeleza wilaya yao. Kazi hizi alizifanya kwa kujitolea bila kutafuta namna yoyote ile ya kujitajirisha. Aliwasaidia vijana wengi kwenda shule bila kujali uhusiano wa karibu.

Julai 1976 aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uanzishwaji wa Shule ya Sekondari Karagwe. Leo hii, sekondari hiyo ni kati ya shule bora kwenye mkoa wa Kagera. Shule hiyo ilipofunguliwa mwaka 1977, Balozi Tibandebage ndiye alikuwa mwalimu mkuu wa kwanza. Baadaye aliteuliwa kuwa meneja wa shule hiyo na baadaye kabisa mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo. Kwa vile alikuwa na moyo wa kujitolea, Juni 1977 aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Karagwe (KARADECO).

Mwaka 1984 Balozi Tibandebage aliteuliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe ambayo alitumikia nafasi hiyo kwa muhula mmoja; wakati huo huo aliteuliwa pia kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Leseni za Usafirishaji, nafasi aliyoitumikia kwa kipindi cha miaka minne.
 
Masasi, Mtwara aliyemtambua kwa jina la Frederick Mchauru

1709679575087.png

Picha: Frederick Jones Mchauru

MCHAURU alizaliwa siku ya Jumapili ya tarehe 25.4.1920 huko Newala, Mtwara, Tanganyika.

3. MASOMO

MCHAURU alisoma St. Joseph's college, Chidya na alikuwa ni kijana hodari sana darasani. Hiyo ilipelekea afaulu mitihani yake kwa kiwango cha juu hadi kuchaguliwa kujiunga na St. Andrew's college, Minaki.

4. MCHAURU APATA "SCHOLARSHIP"

JMwaka 1944, MCHAURU na Mangi Mkuu wa Wachaga Bw. THOMAS MAREALLE walipata scholarship toka serikali ya Ukoloni ya Uingereza kwa ajili ya kwenda kusoma London School of Economics, LSE UK. Wawili hawa ndio walikuwa Watanganyika wa kwanza kupata Scholarship hapa nchini. Walisoma UK hadi 1946 waliporejea nchini baada ya kuhitimu mafunzo yao.

5. MCHAURU AAJIRIWA OFISA MAENDELEO TABORA

Baada ya kurejea, MCHAURU aliajiriwa kama Afisa Maendeleo wa Jamii Tabora. Kati ya 1947 na 1952, alikuwa Bwana maendeleo wa nusu ya Tanganyika nzima ie mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, Ziwa Magharibi, Kusini na Nyanda za Juu Kusini. Licha ya barabara mbovu na changamoto lukuki, MCHAURU aliifanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu.

Mwenzake MAREALLE akapewa Dodoma kupanda juu kuelekea Morogoro, Pwani, Dsm na Kaskazini kote.

6. MCHAURU AANZISHA ELIMU YA WATU WAZIMA NCHINI

MCHAURU ni mtu wa maendeleo sana na alipenda kuwainua Watanganyika wenzake. Hivyo, MCHAURU akawa Mtaganyika wa kwanza kuanzisha Elimu ya Watu Wazima nchini mwaka 1959 huko Singida
 
Ndugu zanguni,
Mwandishi wa historia ya Mzee Millinga haijui historia ya African Association.

Halikadhalika historia ya Mzee Millinga haiko sawa kwa kukosa rejea zenye ithibati.

Yametajwa majina mfano wq Denis Phombeah na Erasto Mang'enya hawa walikuwapo wakati harakati za uhuru zinaanza lakini kama alivyokuwa Millinga mwenyewe hawa si msingi wa kuijua historia ya TANU.

Nakuwekeeni kipande hapo chini kutoka kitabu cha Abdul Sykes:

Historia ya TAA Jimbo la Magharibi, 1955

Tabora ilianza kushiriki katika siasa mwaka 1945 wakati African Association ilipoingizwa mjini Tabora kutoka Dodoma kutokana na juhudi za Edward Mwangosi.

Tabora kwenyewe msukumo wa katika kuanzisha chama cha Waafrika zilitoka kutoka Combine Dancing Club, kilabu kilichoanzishwa na vijana wa pale mjini kwa ajili ya kujifurahisha.

Wanachama mashuhuri wa kilabu hiyo walikuwa ndugu wawili Wamanyema - Maulid na Abdallah Kivuruga, Chamng’anda Usingizi, Ramadhani Nasibu, Rashid Mussa, Issa Kibira, Hamis Wabeba, Mwinyi Khatib Hemed, Swedi Juma, Issa Hamis Pama na Rajab Kanyama.

Wanachama wengi wa kilabu hii walikuwa Wamanyema, kizazi cha pili baba zao wakiwa wametokea ile iliyokuwa wakati huo Belgian Congo, wakafanya maskani Kigoma, Ujiji na Tabora mwishoni mwa karne ya 19.

Wamanyema likiwa kabila la Waislam watupu ilikuwa rahisi kuungana kama kikundi cha kabila moja na kuanzisha chama cha siasa.

Kwa hiyo Combine Dancing Club kidogo kidogo ilijigeuza kutoka chama cha starehe na kuwa chama cha siasa.

Kumbukumbu za kikoloni zinaonyesha kwamba kamati ndogo ndani ya kilabu iliundwa katika mwaka 1945, Mwinyi Khatibu Hemed, Mzigua kutoka Bweni, Pangani, akiwa katibu.

Hemed aliandika barua makao makuu yaAfrican Association mjini Dar es Salaam kuujulisha uongozi ju ya dhamira ya kufungua tawi mjini Tabora.

Tarehe 3 Machi, 1945 African Association mjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais), M. K. Hemed (katibu), Chamngíanda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).

African Association, kama ilivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema.

Hivi ndivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika.

Julius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Maryís School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa African Association.

Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu ya historia kazi yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake.

Mwaka 1946 wasomi wa Makerere walianza kujishughulisha na African Association pale Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walipochaguliwa Katibu na Katibu Msaidizi na nafasi nyingine za uongozi zikishikwa na Wamanyema.

Baada ya uhamisho wa Mwapachu kutoka Tabora, Nyerere akashika nafasi yake na kuwa katibu wa chama. Mwaka huo huo Nyerere alisafiri kwenda Dar es Salaam kama mjumbe wa Tabora kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa African Association.

Katika mkutano huu ndiyo kwa mara ya kwanza Dossa Aziz alimtia Nyerere machoni. Lakini urafiki baina ya Dossa na Nyerere haukushamiri hadi mwaka 1952, Nyerere alipokuja Dar es Salaam na kuungana na wazalendo wengine.

Mwaka uliofuata, African Association Tabora ilikuwa imejiimarisha vizuri kiasi cha kuwa na uwezo wa kushiriki katika mgomo wa mwaka 1947 ambao ulianza katika bandari ya Dar es Salaam.

Kuwako kwa Waislam wengi sana katika ajira ya bandarini kwa kiasi kikubwa kulichangia kuwasha moto wa mshikamano uliolipua mgomo.

Wakati wa mgomo Tabora, Mwalimu Pinda, aliyekuwa miongoni mwa walimu wa St. Maryís School na mwanachama wa African Association, alichukua jukumu la kuwa mtu wa kati baina ya wawakilishi wa wafanyakazi waliogoma na African Association.

Siku ya mgomo wafanyakazi wengi wao kutoka karakana ya magari moshi ya wakiongozwa na Salum Abdallalh, walikusanyika katika viwanja vya Tabora Town School chini ya miembe.

Tabora ni maarufu kwa wingi wa miembe. Kuanzia siku hiyo viwanja hivyo vikawa ndiyo mahali pa mikutano yote ya African Association.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Nyerere hakujihusisha na hizi harakati za tabaka la wafanyakazi zilizokuwa zikiibuka.

Mwaka 1950 Tanganyika African Association (TAA) kama sasa ilivyokuwa ikijulikana ilikuwa chini ya uongozi wa George Magembe, mwalimu wa St. Maryís School. Magembe, Mbondei kutoka Muheza, alikuwa akiandikiana barua nyingi na Stephen Mhando, Mbondei mwenzake aliyekuwa mjumbe wa kamati ndogo ya siasa ya TAA mjini Dar es Salaam.

Wakati ule kamati ndogo ya siasa katika TAA ndiyo kwanza ilikuwa imeundwa. Kupitia uhusiano huu baina ya Magembe na Mhando, TAA Tabora iliweza kuimarisha mawasiliano kati yake na makao makuu na kupeana taarifa za siri.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

Huyu Salum Abdallah anetajwa kuwa alikuwa anaongoza mgomo wa wafanyakazi wa Relwe mwaka wa 1947 ni babu yangu na ndiyo mwaka alihamishwa Dar es Salaam kuja Tabora.

Hao wazalendo wengine anaowataja ukoo wa Kivuruga mimi ni baba zangu: Abdalla na Maulid Kivuruga mtu na nduguye.

Said Mussa na Germano Pacha wote nikiwafahamu.

Harub Said akijuana na wazee wangu toka udogoni hadi wamekuw watu wazima.

Ninachotaka kusema ni kuwa mimi ni sehemu ya historia hii na naijua vyema.

View attachment 2924876
Salum Abdallah (President)na kushoto kwake ni Kassanga Tumbo (Secretary) Tanganyika Railways African Union (TRAU) na viongozi wengine

View attachment 2924878
Abdallah Kivuruga
View attachment 2924879
Maulidi Kivuruga​
Yaani meshampoteza historia ya huyo mzee !
 
Historia ya Tanganyika inatakiwa kufanyiwa utafiti wa kina .


Simulizi za Mzee Ahmad Ibrahim Bakundukize : Vuguvugu la kisiasa 1950 - 1960 nchi za Maziwa Mkuu za Tanganyika, Burundi, Ruanda na Congo Zaire



Waswahili wa nchi hizi 4 wamefanya makubwa bila kujali mipaka ya nchi zao, waliunganishwa na lugha ya kiSwahili na u-mjini wao kuwa popote ni kambi hivyo palipo na "waswahili" yaani panapoongewa lugha ya kiSwahili ni nyumbani na Panafaa kuongoza harakati.

Parti politique ya kwanza kupigania uhuru wa Ruanda-Urundi ilianzishwa na mnyamwezi wa Tabora Tanganyika ambaye alizaliwa Buyenzi Bujumbura Urundi . .

Chama cha biashara cha commercial corporatif (Corporative Commercial) walimtumia Rajabu Kaminambeyo kupeleka barua ilivyoshonwa kwa kificho ndani ya suti iliyonunuliwa hapa Bujumbura kuipeleka Tabora kisha Mzee Selemani Takadiri akaichukua hadi Dar es Salaam Tanganyika

TAA ya Tanganyika walikorogana ikakatika vipande viwili ikatoka party mbili moja UTP na nyingine TANU .... hivyo ndivyo politique ya Tanganyika ilivyo evolved Mzee Ahmad Ibrahimu Bakundukize akielezea jinsi siasa za Rwanda-Urundi na Tanganyika zilivyofanywa kwa pamoja baina ya waswahili wa Bujumbura, Kigoma,,Tabora na Dar es Salaam ...

Source : Mashariki TV
 
Duh mbona tuliaminishwa TAA & TANU ilikuwa ya Waislam ?.Sasa huyu Mgalatia katokea wapi tena au yule Ustadhi Mohamed Said alimsilimisha maana hata katika kitabu chake cha hustoria ya Kariakoo hajamtia Bwana Millinga kabisa.

Ndugu zanguni,
Mwandishi wa historia ya Mzee Millinga haijui historia ya African Association.

Halikadhalika historia ya Mzee Millinga haiko sawa kwa kukosa rejea zenye ithibati.

Yametajwa majina mfano wq Denis Phombeah na Erasto Mang'enya hawa walikuwapo wakati harakati za uhuru zinaanza lakini kama alivyokuwa Millinga mwenyewe hawa si msingi wa kuijua historia ya TANU.

Nakuwekeeni kipande hapo chini kutoka kitabu cha Abdul Sykes:

Historia ya TAA Jimbo la Magharibi, 1955

Tabora ilianza kushiriki katika siasa mwaka 1945 wakati African Association ilipoingizwa mjini Tabora kutoka Dodoma kutokana na juhudi za Edward Mwangosi.

Tabora kwenyewe msukumo wa katika kuanzisha chama cha Waafrika zilitoka kutoka Combine Dancing Club, kilabu kilichoanzishwa na vijana wa pale mjini kwa ajili ya kujifurahisha.
Huyo hapo
 
Mzee Ahmad Ibrahimu Bakundukize akielezea jinsi siasa za Rwanda-Urundi na Tanganyika

MUINGILIANO WA FREE CONGO STATE, RUANDA-URUNDI NA TANGANYIKA

MBELGIJI KUKALIA MAENEO YA UJIJI, KIGOMA, TABORA HADI MOROGORO



Source : Tanganyika TV

VITA VYA DUNIA HISTORIA YA MBAVU MOYA​

SHUJAA TOKA TARAFANI FIZI Wakati huu wa kumbukumbu la Vita vya Kwanza vya Dunia (Première Guerre mondiale ) vya 1914-1918 ambavyo huitwa pia "Vita vikuu" (Grande guerre),tumkumbuke afisa (officier) shujaa toka Fizi wa Force Publique ya Congo-Belge,1er Sergent Major Mbavu Ndogo Michel (wengine wanamwita Mbavu Moya).

Kwa mwaka wa 1916, Ubeljiji (Belgique) iliamua kufukuza Wajerumani katika nchi zao za ukoloni hasa Urundi (Burundi, kwa leo) na Tanganyika (Tanzania, kwa leo).Kamanda Mkuu wa Force Publique aliitwa Jemadari Charles Henri Marie Ernest Tombeur.

Sergent Mbavu Ndogo alikuwa kamanda wa kikosi kilichoitwa "Brigade du sud ". Le 6 juin 1916, alivamia Usumbura (Bujumbura, kwa leo) na kufukuza wa Allemands (Wajerumani) , chini ya uongozi wa afisa mbeleji Lieutenant-Colonel Frédérick Olsen.Tarehe 27 juillet 1916, Sergent Mbavu Ndogo kazibiti Kigoma.

Hapo Le 28 juillet 1916, akakamata Ujiji. Le 19 septembre 1916 akazibiti Tabora chini ya uongozi wa Général Tombeur. Le 9 octobre 1916, akadhibiti Mahenge chini ya uongozi wa Afisa mwengine wa kibeleji Lieutenant-Colonel Armand Huyghe. Sergent Mbavu Ndogo aliwafukuza wa Allemands (wajerumani) Burundi na Tanzania. Général Tombeur alipewa tunzo kama "Baron Charles Tombeur de Tabora".

Lieutenant Colonel kapewa tunzo kama "Chevalier Armand de Mahenge". 1er Sergent Major Mbavu Ndogo kakumbukwa kwa mwaka wa 1958 baada ya Vita vya pili vya dunia (Deuxième Guerre mondiale 1940-1945) ambako huyo afisa shujaa wa RDC alipigana mara tena zidi ya Wajermani.

Kama tunzo : 1) Alipewa pete ya 1er Sergent Major wa Force Publique na akatumwa Bukavu. 2) Picha yake ilitiwa kwenye noti ya franka kumi (10 Fr) ya Banque Centrale du Congo-Belge et du Ruanda-Urundi. Benki kuu hiyo ilichapisha picha ya 1er Sergent Major Mbavu Ndogo Michel le 01 décembre 1958. 3) Wengine wanasema kwamba pale Bukavu/Kadutu Carrefour palikuwa monumenti yake.

Kwa leo, hakuna trace hata moja ya monument zaidi ya mitaa ya Kinshasa na Lumbumbashi nchini Free Congo State wakati wa Ukoloni wa mBelgiji kupewa majina ya “Avenue Kigoma”, “Avenue Tabora”, “Avenue Mahenge” na mji wa Boma kuwa na kambi ya kijeshi ya “Camp Tabora”. Mobutu Sese Seko pia alipata kuwa Mcongomani wa kwanza kupewa cheo cha Sajenti pengine ndiyo maana akaamua kumuenzi Master Sajenti Mbavu Ndogo Moya kwa ujasiri kupambana na dola uliyokuwa na nguvu ya Ujerumani chino ya Kaiser.

Source: VITA VYA DUNIA HISTORIA YA MBAVU MOYA

Noti ya kutambua utumishi wa kutukuka iliyotolewa na Mfalme wa Ubelgiji kwa Sajenti-Major Mbavu Ndogo Moya

43879615_182126672664801_2217129751045210112_n.jpg
Congratulations to 1st Sergent Major Mbavu
 
Mzee Said hawezi kuwataja sana watu kama hawa, kisa kivuli cha dini.
Yaani kwa akili za mzee Said, Uhuru wa Tanganyika ni matokeo ya juhudi za waislamu wa Pwani (watu ambao kielimu na kivita) walikuwa nyuma sana, anasahau kabisa juhudi kamili za kupigania Uhuru zilipiganwa zaidi na wapagani wengi na wagalatia wa Tanganyika.
 
Chifu wa wabondei Erasto Mangenya
View attachment 2925155
balozi Erasto Andrew Mbwana Mang'enya - Alizaliwa Aprili 17, 1915 (umri wa miaka 104), Kijiji cha Mkuzi Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga, Tanzania. Yeye ndiye mtoto wa kwanza wa Canon Henry na Mary Eleanor Mang'enya

Elimu

Kuanzia 1919 hadi 1933 alipitia shule kadhaa za Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na Tanga. Shule alizosoma ni Mkuzi, Magila, Kiwanda, na hatimaye Shule ya Mafunzo ya Ualimu Minaki.

Mnamo 1934 alijiunga na Chuo cha King's College Budo katika taasisi nyingine ya Anglikana, ambapo alifanyia Mtihani wa Kuingia Chuo cha Makerere.

Kuanzia 1935 hadi 1937 alikuwa katika Chuo cha Makerere.
Erasto Andrew Mbwana Mang'enya ( 17 Aprili 1915 – ) alikuwa mwanadiplomasia wa Tanganyika/Tanzania na mwanasiasa.

Alikuwa chifu wa Wabondei, kutoka Milima ya Usambara kaskazini - mashariki mwa Tanzania. Kabla ya kuwa chifu wa Wabondei, Mang’enya alikuwa mwalimu mkuu katika Shule ya Sekondari Old Moshi.

Alikuwa mmoja wa Watanganika wa mwanzo kupata shahada ya chuo kikuu, alijihusisha sana na utambulisho wa kisiasa wa Bondei mwishoni mwa miaka ya hamsini, lakini alifanikiwa kuandika historia ya maisha yake na kujihusisha na utaifa mkubwa wa Tanganyika, na baadaye kuacha kuweka ukabila kwa kupendelea jukumu lake katika utumishi wa umma.


Mwaka 1938 aliingia katika Idara ya Elimu ya Tanganyika, mtangulizi wa Wizara ya Elimu ya Tanzania, na kufanya kazi katika Shule za Sekondari zifuatazo:
1938 - 1943 Malangali,;
1943 - 1947 Moshi,;
1947 - 1952 Tanga,;
1953 - 1957 Tabora,.
Mwaka 1958 alifundisha Shule ya Sekondari Songea.

Mwishoni mwa mwaka 1958, Mang’enya alichaguliwa kuwa Mtema (Mkuu) wa Wabondei wa Wilaya ya Muheza.

Mwaka 1960 aliingia Bungeni kwa tiketi ya Tanganyika African National Union Party na kuchaguliwa kuwa Naibu Spika.

Mwaka 1962 aliteuliwa kuwa Waziri Mdogo katika Wizara ya Mawasiliano, Nguvu na Ujenzi wa Serikali ya Tanganyika mpya.
Mwaka 1963 alihamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na kupelekwa New York kama Mjumbe Mkuu wa Tanganyika katika Umoja wa Mataifa.

Kuanzia Aprili 17, 1963 hadi 1964 alikuwa mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa.
Kuanzia 1964 hadi 1965 alikuwa waziri wa maendeleo ya jamii na utamaduni wa kitaifa.

Mwaka 1965 alikua Mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi ya Tanzania (Ombudsman).

Mnamo 1970 aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mahakama iliyosikiliza rufaa kuhusu Majengo Yanayopatikana.

Mnamo 1972 alikua tena Mwenyekiti wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi.

Akiwa Mwenyekiti, alitembelea Australia, New Zealand na Israel.
Mnamo 1967 alisafiri kwenda nchi za Skandinavia, Ujerumani Mashariki na kutembelea Umoja wa Kisovieti.

Alikuwa Spika wa Bunge kuanzia Novemba 1973 hadi Novemba 1975.
Ahsante sana,kuna Ustadhi kila siku anataka kuwaaminisha watanzania kwamba historia ya Kariakoo ndio historia ya watanganyika.

Kwamba watanganyika wa dini tofauti na uislam hawakushiriki katika harakati za kupigania uhuru.

Kwamba uhuru wa Tanganyika ni Kariakoo.
Kwamba uhuru wa Tanganyika ni Babu zake.
Kwamba uhuru wa Tanganyika ni uislamu.
Kwamba kitabu chake ndicho kitabu sahihi kuhusiana na historia ya Tanganyika.
 
Muarabu aje Tanganyika na kukupa elimu dunia ili iweje?
Elimu ambayo yeye muarabu mwenyewe kiasili alikuwa hana, haitaki, haipendi, halafu akugawie?
Mzee Said anapenda kuwaaminisha watu njozi zake za kidini.

Narudia tena, Uhuru wa Tanganyika haukupiganiwa misikitini bali mtaani, ofisini na msituni. Hizi dini za kisasa hazikuwa na malengo ya kuwaletea watu uhuru bali kuwafanya watumwa wa fikra kwa mgongo wa Imani.
 
Ahsante sana,kuna Ustadhi kila siku anataka kuwaaminisha watanzania kwamba historia ya Kariakoo ndio historia ya watanganyika.

Kwamba watanganyika wa dini tofauti na uislam hawakushiriki katika harakati za kupigania uhuru.

Kwamba uhuru wa Tanganyika ni Kariakoo.
Kwamba uhuru wa Tanganyika ni Babu zake.
Kwamba uhuru wa Tanganyika ni uislamu.
Kwamba kitabu chake ndicho kitabu sahihi kuhusiana na historia ya Tanganyika.
Yaani wale waswahili waliokuwa wanashinda kariakoo wakinywa Kahawa, kucheza bao, kupiga story za umbeya halafu wakisikia adhana wanakimbilia kuswali ndio wapiganie Uhuru wa Tanganyika?

Mzee Said aende akajitafakari upya kabla ya kuja na story zake za kimchongo wa kidini.
 
Mzee Said hawezi kuwataja sana watu kama hawa, kisa kivuli cha dini.
Yaani kwa akili za mzee Said, Uhuru wa Tanganyika ni matokeo ya juhudi za waislamu wa Pwani (watu ambao kielimu na kivita) walikuwa nyuma sana, anasahau kabisa juhudi kamili za kupigania Uhuru zilipiganwa zaidi na wapagani wengi na wagalatia wa Tanganyika.
Zanzibar...
Mimi napenda kupata elimu mpya kila kuchao.
Naomba unipe historia za viongozi na wanachama wa TANU Wapagani.

Nakuwekea hapo chini wanawake waliopigania uhuru lakini hawafahamiki:

1709956625400.png

Tatu bint Mzee
1709956707438.jpeg

Nyange bint Chande
1709956943171.png

Shariffa bint Mzee



 
Mzee Millinga alikuwa muoga kuacha kazi ili ajitose kwenye siasa moja kwa moja.Angeacha kazi na kuwa kwenye siasa moja kwa moja angekuwa mmojawapo wa viongozi wakubwa sana nchini.Tatizo alifanya siasa kama part time. Angejitosa moja kwa moja akajiunga na akina Nyerere kawawa nk walioacha kazi angekuwa mbali.mno
 
Back
Top Bottom