Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa mwaka 2024/25

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,994
12,346
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imewasilisha Bungeni Bajeti ya Tsh. 67,905,259,000 inayotarajiwa kutumiwa na Wizara hiyo katika kipindi cha mwaka 2024/25

Katika wasilisho lake Bungeni, Waziri Dkt. Doroth Gwajima amesema Tsh. 47,487,079,000 kati ya Fedha hizo zitakuwa ni Matumizi ya Kawaida yakiwemo malipa ya Mishahara Tsh. 21,650,426,000 na Matumizi Mengineyo Tsh. 25,836,653,000

Pia, Wizara itatekeleza shughuli mbalimbali za Maendeleo kupitia Miradi yake ambapo Tsh. 20,418,180,000 zimetengwa. Tsh. 18,025,673,000 kati ya Fedha hizo ni Fedha za Ndani na Tsh. 2,392,507,000 ni Fedha za Nje.

=====

HOTUBA YA BAJETI
HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAM I I , JI NSI A, W ANAW AKE NA MAKUNDI MAALUM, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (MB), KUHUSU MAKADIRIO
YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2024/25.


HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAM I I , JI NSI A, W ANAW AKE NA MAKUNDI MAALUM, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (MB), KUHUSU MAKADIRIO
YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2024/25.
  • UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ndani ya Bunge lako Tukufu, ambayo imechambua Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, ninaomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum (Fungu 53) kwa mwaka 2023/24 na Vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2024/25. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida pamoja na Miradi ya Maendeleo ya Wizara kwa mwaka 2024/25.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu leo ili kuwasilisha hotuba yangu. Pia, nitumie fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuendelea kutuongoza

vyema kwa mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali kwa kipindi hiki cha miaka mitatu ya uongozi wake. Kipekee niendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuniamini kuiongoza Wizara hii. Natambua kuwa Mheshimiwa Rais ana matarajio makubwa ya kuona hali ya usawa wa kijinsia hapa nchini inaimarika na utoaji wa huduma za maendeleo na ustawi wa jamii unafanyika kwa kasi kubwa na ufanisi. Ninamuahidi kwamba nitaendelea kutimiza majukumu yangu kwa weledi mkubwa ili kuhakikisha kwamba matarajio yake yanafikiwa kikamilifu.
Mheshimiwa Spika, pia, napenda kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika jitihada za kuboresha huduma za maendeleo na ustawi wa jamii, kuhimiza usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake kiuchumi pamoja na kuzingatia haki za wazee, wanawake, wanaume na watoto katika jamii. Hivyo, Wizara yangu itaendelea kutekeleza kikamilifu maelekezo anayoyatoa.
Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake mahiri uliowezesha kuleta tija na ufanisi katika utendaji na kuimarisha huduma zinazotolewa katika Sekta ya Maendeleo na Ustawi ya Jamii. Aidha, ninampongeza kwa hotuba yake

aliyoiwasilisha kwenye Bunge lako Tukufu tarehe
15 Aprili, 2024 ambayo imetoa mwelekeo wa majukumu yatakayotekelezwa na Serikali katika mwaka 2024/25.
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee naomba nimpongeze Mheshimiwa Dotto Mashaka Biteko (Mb), Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu. Aidha, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mheshimiwa Spika, ninapenda kukupongeza wewe binafsi kwa uongozi wako mahiri na weledi wa kuendelea kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, ninampongeza Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uchapakazi wake uliotukuka. Mwenyezi Mungu awajalie utashi, weledi na ufanisi mkubwa katika kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, vilevile, nawapongeza Mheshimiwa Dkt. Joseph Mhagama (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Mheshimiwa Deo Mwanyika (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo

na Mifugo kwa kuchaguliwa kuwa Wenyeviti wa Bunge. Nawatakia majukumu mema katika kuliongoza Bunge.
Mheshimiwa Spika, kipekee namshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Mwanaidi Ali Khamis (Mb), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa ushirikiano mkubwa anaonipa katika kutekeleza majukumu yangu ya kila siku.
Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii, kumshukuru Mheshimiwa Angellah Kairuki (Mb), Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Utekelezaji wa Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa kwa jitihada zake katika kufikia kizazi chenye usawa nchini. Chini ya uenyekiti wake, Kamati imeweza kusimamia utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa (Tanzania Generation Equality Programme - TGEP, 2021- 2026) inayoainisha afua muhimu zitakazo tekelezwa na Wizara za Kisekta na kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeachwa nyuma katika maendeleo na ujenzi wa Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, ninapenda kuwashukuru Mawaziri wenzangu kwa ushirikiano wanaonipatia ambao unaiwezesha Wizara yangu kuendelea kuimarisha na kuboresha utoaji wa huduma za maendeleo na ustawi wa jamii. Wizara itaendelea kushirikiana nao na kuhakikisha tunatimiza dhamira ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya

kuhakikisha mafanikio katika Nyanja za Maendeleo na Ustawi wa Jamii yanafikiwa.​
Mheshimiwa Spika, kipekee ninapenda kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, chini ya Mwenyekiti Mheshimiwa Fatma Hassan Toufiq (Mb) na Makamu wake, Mheshimiwa Riziki Said Lulida (Mb) kwa ushauri na maelekezo waliyoyatoa wakati wa maandalizi ya Bajeti hii. Vilevile, ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa ushirikiano mzuri wanaotupatia wenye lengo la kuboresha huduma za ustawi na maendeleo ya jamii.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa pole kwa Serikali na Chama cha Mapinduzi kufuatia kifo cha Ndugu, Ally Hassan Mwinyi aliyekuwa Rais wa awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ndugu Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, nitoa pole kwako, Spika na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge lako Tukufu kwa kuondokewa na wapendwa wetu Mheshimiwa Francis Leonard Mtega aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali na Mheshimiwa Ahmed Yahaya Abdul-wakil aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar.
Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa pole kwa wakazi wa Wilaya ya Hanang’ pamoja na wananchi wa Mkoa wa Manyara kwa ujumla kufuatia maporomoko ya matope yaliyotokea

Desemba 3, 2023 kutokana na mvua kubwa na kusababisha vifo, majeruhi, upotevu wa mali na makazi. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi. Amina.
Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezo ya awali, ninapenda sasa kutoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2023/24, Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi pamoja na Maombi ya Fedha kwa ajili ya kutekeleza Vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2024/25.
  • MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2023/24
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sera, Mpango Mkakati pamoja na Makubaliano ya Kimataifa na Kitaifa yenye lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za maendeleo na ustawi wa jamii nchini. Sera hizo ni pamoja na Sera ya Maendeleo ya Jamii (1996); Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (2001); Sera ya Taifa ya Wazee (2003), Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008) na Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake (2023). Vilevile, katika kuandaa mpango na bajeti, Wizara imezingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020, Dira ya Taifa ya Maendeleo (2025), Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 - 2025/26), Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals, 2030);

na Agenda ya Afrika Tuitakayo (2063). Aidha, Wizara inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Ahadi za Nchi katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum – GEF, 2021 – 2026).
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, Wizara ilipanga kutekeleza vipaumbele mbalimbali vyenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma za maendeleo na ustawi wa jamii katika maeneo yafuatayo: -
Kuratibu afua za kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi (Generation Equality Forum - GEF);
Kuratibu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA);
Kutekeleza Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na Kusimamia Maendeleo Ngazi ya Msingi wa mwaka 2022/23 - 2025/26 (Bottom Up);
Kukuza ari ya jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo;
Kutambua na kuratibu Makundi Maalum wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo ili kuboresha mazingira ya biashara zao;
Kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii;

Kuratibu utoaji wa huduma za msingi kwa watu wenye mahitaji maalum ikiwemo huduma za msaada wa kisaikolojia kwa manusura wa majanga mbalimbali na makundi mengine yenye uhitaji katika jamii;
Kuratibu na kuwezesha upatikanaji wa haki za watoto na huduma za ustawi wa jamii kwa wazee;
Kuimarisha mifumo ya malezi, ulinzi na maendeleo ya watoto na familia; na
Kuimarisha utendaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili mchango na ushiriki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika maendeleo ya taifa uweze kutambulika na kuwa na tija kwa Jamii.
Mapato na Matumizi ya Fedha za Wizara (Fungu 53)
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, Wizara ilipanga kukusanya kiasi cha Shilingi 8,500,000,000.00 kutoka kwenye ada za wanafunzi, uuzaji wa Mitaala ya kufundishia fani za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii pamoja na malipo ya hosteli katika vyuo nane (8). Vyanzo vingine ni mapato ya ada ya usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, ada za mwaka na faini kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Sura ya 56 pamoja na marekebisho yake na mapato mengineyo (Fedha za mwaka uliopita

zinazorejeshwa). Hadi kufikia mwezi Aprili 2024, Wizara imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi 3,184,370,155.50 sawa na asilimia 37.46 ya makadirio ya mapato kama inavyoonesha katika Jedwali Na. 1.
Jedwali Na. 1:
Ukusanyaji Mapato ya Ndani kwa Kipindi cha Julai, 2023 – Aprili, 2024
Chanzo cha Mapato
Mapato Yaliyoidhinishw
a​
Makusanyo Halisi​
Ufanisi (Asilimia
)​
Ada ya Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii

6,204,497,000

2,355,091,240.50​
37.96
Uuzaji mtaala wa maendeleo
ya jamii

40,000,000

51,500,000​
128.75
Ada ya Malazi kwa wanafunzi wa Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii

600,000,000

167,231,239​
27.87
Ada ya usajili wa
wafanyabiashar a ndogondogo

1,000,000,000

64,284,000​
6.43
Usajili na Ada za mwaka za NGOs638,500,000
534,013,676​
83.64
Uuzaji wa Mitaala ya Vyuo
vya Ustawi

15,000,000

10,500,000​
70.00
Mapato
Mengineyo
2,003,000
1,750,000​
87.37
Jumla8,500,000,000
3,184,370,155.5
0
37.46

Mheshimiwa Spika, kutofikiwa kwa lengo la Makusanyo ya Mapato kunatokana na sababu zifuatazo; wanafunzi kutoripoti wote kama ilivyokadiriwa; Kumekuwa na upungufu wa wanafunzi 1,691 ambao hawajaripoti kutoka katika makadirio ya 7,190; Kutokukamilika kwa malipo ya Ada ya Malazi kwa wanafunzi vyuoni, Kuchelewa kuanza kwa utaratibu wa usajili na utambuzi wa wafanyabiashara ndogondogo ambao ulianza mwezi Machi, 2024 na hadi sasa tumeweza kukusanya kiasi cha shilingi 64,284,000 kati ya Shillingi Billioni moja. Aidha, ufutaji wa usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 14 kutokana na ukiukwaji wa Sheria na Kanuni na Miongozo inayosimamia shughuli za Mashirika hayo, imechangia kupunguza mapato.
Mheshimiwa Spika, Wizara inafanya jitihada kuhakikisha makusanyo yote yaliyobaki yanakusanywa katika kipindi kilichobakia ili kuweza kuongeza makadirio ya makusanyo yaliyokadiriwa kwa mwaka 2023/2024.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, Wizara iliidhinishiwa na Bunge lako Tukufu kiasi cha Shilingi 74,223,193,000.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 43,664,963,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Shilingi 26,577,510,000.00 ni fedha za Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 17,087,453,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara. Aidha, kiasi cha Shilingi 30,558,230,000.00 kilikuwa ni kwa ajili ya Miradi

ya Maendeleo ambapo Shilingi 26,800,000,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi 3,758,230,000.00 ni fedha za nje.
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2024, Wizara imepokea jumla ya Shilingi 30,114,668,978.89 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida sawa na asilimia 68.97. Kati ya Fedha zilizopokelewa, Shilingi 15,640,771,358.89 ni Matumizi Mengineyo na Shilingi Shilingi 14,473,897,620.00 ni Mishahara. Aidha, hadi kufikia Aprili, 2024, Wizara imepokea Fedha za Maendeleo Shilingi 4,949,880,000.00 sawa na asilimia 16.20. Shilingi 4,883,800,000.00 ni Fedha za Ndani na Shilingi 66,080,000.00 ni Fedha za Nje, kama inavyoonesha katika Jedwali Na. 2.
Jedwali 2:
Fedha za Matumizi ya Kawaida na Maendeleo Zilizopokelewa Julai 2023 hadi Aprili 2024.
Eneo
Fedha
zilizoidhinishwa
Fedha
zilizotolewa
Asilimia
Fedha za Matumizi ya Kawaida
Mishahara
17,087,453,000​
14,473,897,620
84.70​
Matumizi
Mengineyo
26,577,510,000​
15,640,771,359
58.85​
Jumla Ndogo
(a)
43,664,963,00030,114,668,979
68.97
Fedha za Miradi ya Maendeleo
Fedha za
Ndani
26,800,000,000​
4,883,800,000​
18.22​
Fedha za Nje
3,758,230,000​
66,080,000​
1.76​
Jumla Ndogo
(b)
30,558,230,0004,949,880,000
16.20
JUMLA KUU
74,223,193,000
35,064,548,979
47.24

  • UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA (FUNGU 53)
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, utekelezaji wa majukumu ya Wizara ulilenga kuimarisha ushiriki wa jamii katika shughuli za maendeleo, utambuzi na uratibu wa Makundi maalumu, kuimarisha upatikanaji wa haki na maendeleo ya mtoto, kuboresha huduma za ustawi wa jamii, kuleta usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, kuratibu utekelezaji wenye ufanisi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuratibu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). Uratibu wa utekelezaji wa majukumu haya ulifanywa na Wizara kwa kushirikiana na Taasisi zake pamoja na wadau mbalimbali.
ENEO LA 1: MAENDELEO YA JAMII
Mheshimiwa Spika, dhana ya maendeleo ya jamii ni kuwashirikisha wananchi kujiletea maendeleo yao wenyewe kwa kutumia rasilimali zilizopo na kwa kuzingatia mahitaji na vipaumbele vyao, ambapo maafisa maendeleo ya jamii hushirikiana nao kwa kuwapatia utaalamu wa namna ya kufanikisha shughuli za maendeleo yao. Kupitia dhana hii, Wizara imeendelea kutekeleza programu ya Amsha Ari ya Jamii na Mpango wa Taifa wa kuhamasisha na Kusimamia Maendeleo Ngazi ya Msingi ulioanza 2022/23 kwa ushirikiana wa jamii na Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka

katika Halmashauri zote nchini. Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii wameendelea kutoa mchango wao katika kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Jamii kwa kupitia Programu ya Kuamsha Ari ya Jamii ambayo inalenga kukuza moyo wa uzalendo, kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo ikiwemo kampeni ya kitaifa ya ujenzi wa Makazi Bora.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta, imeendelea kutekeleza Kampeni endelevu ya Ujenzi wa Nyumba Bora zenye gharama nafuu katika maeneo yenye makazi duni inayotumia mifumo ya asili ya kusaidiana miongoni mwa jamii. Mafanikio ya zoezi hili yanategemea ari ya wananchi, uongozi bora na juhudi za Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii. Kupitia kampeni hiyo, idadi ya nyumba bora imeongezeka kutoka 5,732 kwa 2022/23 hadi 11,883 kufikia Aprili, 2024, sawa na ongezeko la nyumba 6,151.
Nitumie fursa hii kuzishukuru Wizara za kisekta ikiwemo Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na OR-TAMISEMI kwa ushirikiano kwenye kampeni hii.
Mheshimiwa Spika
, miradi mingine iliyotekelezwa kupitia kampeni hii ya Amsha Ari katika Mikoa yote ni pamoja na iliyo kwenye sekta mbalimbali mfano Afya na Elimu ambapo ni jumla ya miradi 29,641 mathalani inayohusu ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya 6,761

(Zahanati 5,887 na Vituo vya afya 874), ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na madarasa ya awali 17,986 na madarasa ya shule za sekondari 4,894 kama ilivyotajwa na Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa (Mb), Waziri wa OR TAMISEMI wakati akiwasilisha Bungeni makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2024/25. Ni dhahiri, uwepo wa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kutosha utaongeza kasi na ari ya wananchi kushiriki na kumiliki shughuli za maendeleo ikiwemo kubuni miradi mbalimbali. Shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kuongeza ajira 762 za Maafisa Maendeleo ya Jamii mwaka 2023/24 hivyo, kuwezesha kufikia idadi ya maafisa 3,675 (69.4%) kati ya 5,296 wanaohitajika jambo litakalochochea zaidi uwajibikaji ngazi ya msingi.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza Mpango wa Taifa wa kuhamasisha na Kusimamia Maendeleo Ngazi ya Msingi ambao ulianza 2022/23 na unaolenga kuchochea hamasa na utayari wa wananchi kushiriki kwenye maendeleo. Wizara kwa kushirikiana na OR- TAMISEMI inatekeleza mpango huu kwa lengo la kuwezesha wananchi kuwa kitovu cha maendeleo ngazi ya jamii na Taifa kwa kutumia rasilimali walizonazo katika kuibua changamoto, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Mheshimiwa Spika, kupitia mpango huu Wizara kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI imefanya mafunzo kwa wataalam 1,146

ikijumuisha watalaam kutoka Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na washiriki wengine, ambapo hadi kufikia Aprili, 2024 jumla ya viongozi na wataalam 1,979 wameweza kupatiwa mafunzo kuhusu mpango huo. Mafunzo hayo yalilenga kuchochea na kufanya mageuzi ya kifikra, mtazamo na utendaji wa wataalam ngazi ya Kata ili kuwezesha jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao na kujiletea maendeleo yao wenyewe. Miongoni wa wataalam waliopatiwa mafunzo ni Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Kilimo, Maafisa Mifugo na Maafisa Afya. Mpango huo umeendelea kutekelezwa na Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI na Wizara za Kisekta zikiwemo Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Elimu na Afya kwa kusudi la kuimarisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa jamii katika ngazi za msingi.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru pamoja na Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (Community Development Professional Association of Tanzania
- CODEPATA) ilifanya kongamano la wataalam wa Maendeleo ya Jamii katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (Arusha International Conference Center - AICC) tarehe 20 – 22 Novemba, 2023. Kongamano lililenga kufanya tathimini ya mchango wa maendeleo ya jamii

katika kuchochea na kukuza ari ya jamii kujiletea maendeleo endelevu pamoja na kubadilishana uzoefu na mbinu mpya zinazotumika katika kukabiliana na changamoto za jamii na kuwafanya wananchi kuwa kitovu cha maendeleo; kupokea na kujadili mifano mizuri ya kuwezesha wananchi na kujenga uwezo wa washiriki kupitia mada mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya jamii. Aidha, Kaulimbiu iliyoongoza kongamo hilo ni “Sekta ya Maendeleo ya Jamii: Msingi Imara wa Uwezeshaji wa Wananchi.”
Mheshimiwa Spika,
Kongamano lilihusisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu wa serikali wataalam wa maendeleo ya jamii kutoka katika taasisi za Serikali na binafsi pamoja na wadau wa maendeleo. Katika kongamano hilo ulifanyika Mkutano Mkuu wa wataalam wa Maendeleo ya Jamii na maadhimisho ya miaka 60 ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na jumla ya Wataalam 700 walishiriki. Vilevile, kupitia kongamano hilo mafunzo mbalimbali yalitolewa kuhusu umuhimu na mchango wa maendeleo ya jamii katika kuwezesha wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu pia ina jukumu la kuzalisha wataalamu wanaotekeleza afua za maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii. Katika kuhakikisha kuwa wataalam wanaozalishwa na Taasisi na Vyuo wanakuwa bora na mahiri na wenye weledi wa kutosha, Wizara imefanya mapitio ya Mitaala inayotumika kutoa mafunzo ya

taaluma kwa ngazi ya Astashahada hadi Stashahada. Mitaala hiyo imeandaliwa ikilenga kuwapa Wahitimu maarifa na ujuzi unaoakisi mahitaji ya soko la Ajira, Mahitaji ya Sekta na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia. Hadi kufikia Aprili 2024, mitaala hii iliyoboreshwa inatumika katika jumla ya Vyuo 67 (12 vya Serikali na 55 binafsi) vinavyotoa Mafunzo ya Programu ya Maendeleo ya Jamii nchini.
Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais, kwa kutupatia fedha za kuboresha miundombinu ya vyuo hivyo hali iliyotuwezesha kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 5,255 (Me 2,089 na Ke 3,166) mwaka 2022/23, hadi wanafunzi 5,499 (Me 1,966 na Ke 3,533) kwa mwaka 2023/24 sawa na ongezeko la wanafunzi
244 (4.6%). Aidha, mwaka 2022/23, wanafunzi
4,978 (Me 1,875 na Ke 3,103) walihitimu katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ikilinganishwa na wanafunzi 4,710 waliohitimu mwaka 2021/22 sawa na ongezeko la 5%.
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia vyuo vyake inatekeleza programu ya uanagenzi kwa wanafunzi waliohitimu mafunzo katika Vyuo vyetu. Wahitimu hawa huunganishwa na Makampuni, Mashirika na Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuwapa ujuzi na stadi mbalimbali zitakazowawezsha kukabiliana na changamoto za soko la ajira. Maeneo ya waliopatiwa ujuzi ni pamoja na ujenzi wa miradi ya maji, Material Testing, Road

Construction na Building Construction. Maeneo mengine ni utoaji wa elimu ya lishe, uandishi wa maandiko ya miradi na ujasiriamali, utatuzi wa changamoto za wananchi, kutatua migogoro ya ardhi, kusimamia mafunzo kwa vikundi vya kifedha, kutoa elimu ya kodi na ukusanyaji wa kodi za Serikali ngazi ya Kata na Halmashauri, kusaidia wananchi kujaza fomu za maombi ya vitambulisho vya Taifa na kushiriki vikao mbalimbali vya maamuzi kwa kushirikisha wananchi. Katika mwaka wa fedha 2023/24 jumla ya wanafunzi 2,200 walijiunga na program hiyo ambapo, kati yao wanafunzi 1,104 (50.2%) walifanikiwa kuhitimu. Aidha, wanafunzi 1,096 (49.8%) wanaendelea na mafunzo hayo. Kutokana na umuhimu wa program hii, Wizara inaendelea kuhimiza wanafunzi/wahitimu wa Vyuo Jamii kujiunga na progamu hii ili kupanua fursa ya kuajirika, kujiajiri na kuajiri wengine.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kupitia programu za ubunifu inatoa fursa kwa wanafunzi na jamii inayozunguka Vyuo kufanya kazi za ubunifu unaosaidia kutatua changamoto zilizopo na kuzalisha ajira kwa wabunifu na wahitimu. Programu hii inatolewa na vyuo 9 vyenye vituo vya ubunifu na maarifa katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Buhare, Monduli, Mlale, Rungemba, Uyole, Ruaha, Mabughai na Misungwi.
Mheshimiwa Spika katika mwaka wa fedha 2023/24 bunifu mbalimbali zinazolenga

kutatua changamoto za kijamii ziliibuliwa ikiwa ni pamoja na;​
Utengenezaji wa Oil kwa kutumia Malighafi zisizo za Viwandani pamoja na Sabuni kwa kutumia Jivu na malighafi zisizo za viwandani (Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare). Wazo hili liko katika hatua ya uatamizi (Incubation)
Utengenezaji wa Switches mbalimbali za Umeme na lift ya baiskeli ya Walemavu katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba. Wazo hili liko katika hatua ya Sampuli kifani (Prototype);
App ya dirisha la taarifa kwa Vijana katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli. Wazo hili liko katika hatua ya uatamizi (incubation);
Bidhaa lishe kwa ajili ya kutatua changamoto ya utapiamlo katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha. Wazo hili tayari ni bidhaa (Minimum Viable Product);
App kwa ajili ya wagonjwa kupata taarifa zao katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole. Wazo hili liko katika hatua ya wazo (Ideation);
Teknolojia ya kupata taarifa za masomo bila kuwa na simu janja (Elitek) katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Mabughai. Wazo hili liko katika hatua ya uatamizi (incubation); na

Teknolojia ya kugundua madini ardhini na kutumia pumba za mchele kutengeneza Simenti katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi Wazo hili liko katika hatua ya uatamizi (Incubation).
Mawazo haya ya ubunifu wa mifumo yaliyo katika hatua za uatamizi yanalenga kufikia hatua ya bidhaa kwa matumizi.
Mheshimiwa Spika, Wizara inatekeleza programu ya ushirikishwaji jamii zinazozunguka Taasisi na Vyuo nane (8) vya Maendeleo ya Jamii katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka. Katika mwaka 2023/24, jumla ya wananchi na wanafunzi 6,740 walipata mafunzo mbalimbali yakiwemo: elimu juu ya maadili mema katika shule za Msingi zilipo katika Kata ya Ruaha na Igumbiro Mkoani Iringa; elimu juu ya ukatili wa kijinsia katika Kata tano (5) za Ruaha, Mshindo, Kitanzini, Makolongoni na Mlandege na katika vijiji vya Kinko, Ndabwa, na Migambo katika Wilaya ya Lushoto, Mkoani Tanga, elimu ya uibuaji na uanzishaji wa Miradi ya kujiingizia kipato kwa vijana katika vijiji vya Magagula, Masangu na Lusonga Mkoani Ruvuma.
Nichukue nafasi hii kupongeza jitihada zinazofanywa na vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini kwa kutoa wataalamu katika fani hii. Pia, natoa rai kwa Wadau wa Maendeleo kutoa ajira kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii

hususan ngazi za msingi ambapo kuna upungufu mkubwa ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa afua za kutatua changamoto zinazoikabili jamii yetu. Aidha, Wizara inatoa wito kwa wahitimu kujiajiri kwa kutumia fursa za Mikopo bila riba, kujinunulia vifaa na mitaji.
ENEO LA 2: KUTAMBUA NA KURATIBU WA SHUGHULI ZA KIUCHUMI ZA MAKUNDI MAALUM
Mheshimiwa Spika,
Wizara imeendelea kutambua, kuratibu na kusimamia mipango mbalimbali ya kuwezesha na kuendeleza Makundi Maalum katika mambo mbalimbali zikiwemo shughuli za kiuchumi. Makundi yanayolengwa ni wafanyabiashara ndogondogo halali wote mfano wakiwemo Machinga, Mama/Baba Lishe, Waendesha Bodaboda na Bajaji, wasusi, wanaofanya biashara za kushona nguo na wengine mbalimbali. Makundi haya yanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kutofikia fursa za kiuchumi kama kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha, kupata maeneo wezeshi ya kufanyia biashara zao pamoja na kuwepo kwa ofisi zao rasmi kuwawezesha kukutana na kuratibu masuala yao wenyewe.
Mheshimiwa Spika, katika kuwaondolea changamoto hizo, Serikali imekamilisha Mpango wa kutoa mikopo kwa kundi hili kupitia taasisi za kifedha ambapo tarehe 06 Mei, 2024 Wizara

imeingia mkataba wa makubaliano na benki ya NMB. Benki hiyo itatoa mikopo kwa wafanyabiashara hawa kwa mujibu wa mwongozo ulioandaliwa na pande zote mbili. Kupitia makubaliano haya, katika mwaka 2023/2024 Serikali itaipatia benki ya NMB kiasi cha shilingi bilioni 18.5 kwa ajili ya kutoa mikopo yenye riba nafuu ya (7%).
Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha mikopo hii inaratibiwa vizuri na kuwanufaisha walengwa Wizara, imeshirikiana na OR – TAMISEMI, Wizara ya Viwanda na Biashara, Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC), Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) Tanzania na wadau wengine kukamilisha maboresho ya mfumo wa utambuzi, usajili na utoaji wa vitambulisho ujulikanao kama Wafanyabiashara Ndogondogo Management Information System (WBN-MIS).
Mheshimiwa Spika, mfumo huo kwa sasa umeunganishwa na Mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Mfumo wa Kieletroniki wa Malipo ya Serikali (GePG). Mpango wa baadaye ni kuunganisha na mifumo mingine ikiwemo Anwani za Makazi, Taasisi za Fedha, Bima ya Afya na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kunufaika na huduma mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, ili kuwezesha zoezi la utambuzi na usajili kutekelezwa kwa urahisi nchi nzima, Wizara imekamilisha mafunzo kwa wataalamu

wa maendeleo ya jamii, maafisa biashara na maafisa TEHAMA wapatao 660 kutoka ngazi za Mikoa, Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji yote. Aidha, tayari zoezi la utambuzi na usajili limeanza Machi, 2024 na linaendelea katika Halmashauri zote nchini na hadi kufikia Aprili 2024, wafanyabiashara ndogondogo 11,003 (Me 4,079 na Ke 6,924) wamesajiliwa kwenye mfumo huo wakisubiriwa kukamilisha hatua ya malipo ya shilingi elfu ishirini (20,000) na baada ya hapo kila mmoja atapatiwa kitambulisho kitakachomuwezesha kutambuliwa wakati wa kwenda kuomba mkopo.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI inafuatilia maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wafanyabiashara ndogondogo katika ngazi ya Mikoa yote. Hadi sasa Mikoa 9 imekamilisha ujenzi wa ofisi hizo na Mikoa
17 ujenzi upo katika hatua mbalimbali kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na.3. Ofisi hizo zitasaidia uratibu wa shughuli za wafanyabiashara hao nchini pamoja na kurahisisha mawasiliano kati yao, Wizara za Kisekta na wadau wengine wa maendeleo. Wizara kwa kushirikiana na OR- TAMISEMI inaendelea kuhimiza mikoa ambayo bado kukamilisha, wafanye hivyo kabla au ifikapo tarehe 30 Juni 2024.

Jedwali Na. 3: Hali ya ujenzi wa Ofisi za Wafanyabiashara
ndogondogo hadi kufikia mwezi Aprili, 2024.
NA.
MKOA
HALI YA UJENZI

1.
Arusha, Mbeya, Katavi, Manyara, Songwe, Pwani, Lindi, Rukwa na
Tanga.
Ujenzi wa ofisi umekamilika.

2.
Morogoro, Dar es Salaam na Geita.Ofisi zimepauliwa na
kazi za umaliziaji zinaendelea.

3.
Mtwara, Njombe, Kagera, Tabora, Dodoma, Shinyanga, Singida Kigoma, Mara
na Kilimanjaro.
Ofisi zipo hatua ya lenta na ujenzi unaendelea.
4.Ruvuma, Simiyu na
Iringa.
Ujenzi wa boma
unaendelea.
5.Mwanza.Hatua za awali za kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo Wizara imeliwekea mkazo ni la kutoa elimu kwa viongozi wao makundi haya maalum ili kuhakikisha wanakuwa na weledi ambapo, Wizara imefanya mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa ngazi ya Taifa na Mikoa kuhusu masuala ya utii wa sheria bila shuruti, uzalendo na umuhimu wa kuzingatia misingi ya utawala bora kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na mshikamano wakati wa kutatua changamoto zao. Mafunzo hayo yalifanyika mwezi Desemba 2023.
Mheshimiwa Spika, eneo lingine muhimu la kuwezesha kundi hili kiuchumi ni kuwapatia maeneo rasmi ya kufanyia biashara ili

kuwaondolea usumbufu na bughudha kwa kuweka mazingira wezeshi ya kupata wateja. Wizara kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI imeendelea kuboresha mazingira ya kufanyia ambapo, taarifa kutoka OR – TAMISEMI inaonesha kuwa, hadi kufikia Aprili, 2024 jumla ya masoko
367 yamejengwa na kuboreshwa katika maeneo mbalimbali nchini. Uwepo wa masoko hayo yamewezesha jumla ya wafanyabiashara ndogondogo 136,041 kuendesha biashara zao katika mazingira rafiki. Kati ya masoko hayo, 16 yamejengwa na kuboreshwa kwa fedha zilizotolewa na Mheshimiwa Rais, Shilingi Bilioni 5. Masoko hayo 16 (Jedwali Na.4) yamejengwa katika Mkoa ya Dar es Salaam (masoko 9) na soko moja moja katika Mikoa ya Mbeya, Songwe, Dodoma, Arusha, Mwanza, Morogoro na Tanga.

Jedwali Na. 4: Orodha ya Masoko ya Machinga yaliyojengwa kwa fedha zilizotolewa na Mheshimiwa Rais.
RI
ADI KWA AJILI YA
WAJASIRIAMALI
DSMDSM CCUjenzi wa soko la Kigogo Fresh (Mashedi mawili makubwa na
machinjio ya kuku).
Ubungo MCSoko la wajasiriamali simu 2000.
Mabibo Gamit (mabanda
matatu).
Soko la wajasiriamali Mbezi
Luis (Banda Moja).
Soko la wajasiriamali Mbezi Njia ya Goba (Mabanda
Mawili).
Temeke MCUjenzi wa Mabanda manne
katika soko la Buza.
Ujenzi wa Mabanda matatu
katika soko la TAZARA.
Ujenzi wa Karakana ya miundombinu ya soko la
Mbande, mabanda matatu katika soko la TAZARA.
Kinondoni MCUjenzi wa Soko la Bunju B.
MbeyaMbeya CCUjenzi wa Soko- la Old Airport.
SongweTundumaUjenzi wa Soko Tunduma.
Dodom
a
Dodoma CCUjenzi wa soko la wazi la
Machinga Complex.
ArushaArusha CCUjenzi wa soko – Engutoto.
MwanzaMwanza CCUjenzi wa soko la Mchafukoge.
Morogor
o
Morogoro MCUjenzi wa soko la Fire.
TangaTanga CCUjenzi wa jengo la soko la
Kange.
Chanzo: OR -TAMISEMI

Mheshimiwa Spika, katika kujenga uzoefu na kuongeza fursa za kibiashara, Wizara kwa kushirikiana na sekta nyingine hutoa nafasi za ushiriki katika maonesho ya biashara ya ndani na nje kwa wafanyabiashara ili kuweza kuonesha bidhaa zao, kuuza, kujifunza kwa wenzao na hatimae pia kujipatia uzoevu. Katika kipindi cha mwaka 2023, Wizara ilihamasisha wafanyabiashara ndogondogo kushiriki katika shughuli mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa zikiwemo Maonesho ya Kilimo ya Nanenane ambapo jumla ya wafanyabiashara ndogondogo 968 walishiriki Maonesho hayo yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya.
ENEO LA 3: HAKI NA MAENDELEO YA MTOTO
Mheshimiwa Spika, Wizara inalo jukumu la kusimamia na kuratibu maendeleo ya mtoto pamoja na upatikanaji wa haki za msingi kwa mtoto kama zilivyoainishwa katika Mikataba ya Kimataifa, Kikanda na Kitaifa, Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008 na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2019.
Mheshimiwa Spika, haki za mtoto ni pamoja na kuishi, kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili, kuendelezwa kupitia vipaji na elimu, kushiriki katika masuala yanayomhusu kulingana na umri wake na kutobaguliwa kwa namna yoyote ile. Aidha, mtoto anahitaji malezi bora yenye kuzingatia haki na mahitaji yake ya msingi hasa

katika kipindi cha umri wa miaka 0-8 ambapo ubongo hukua kwa 90%. Nguvu kubwa inahitajika hapa ili kuhakikisha mtoto anakua na kufikia utimilifu wake na hatimaye kuja kuwa nguvu kazi yenye tija kwa Taifa. Hata hivyo, baadhi ya watoto wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na malezi duni na vitendo vya ukatili kutoka kwa ndugu wa karibu, familia na jamii inayowazunguka.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wizara za kisekta imeendelea kuboresha mifumo ya kisheria ili kuimarisha ulinzi na usalama wa mtoto kwa kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Mtoto, Sura ya 13, Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 na Sheria ya Makosa ya Mtandao, Sura ya 443 kwa lengo la kumlinda mtoto nje na ndani ya Mtandao.
Mheshimiwa Spika, kupitia Bunge lako Tukufu, Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 imefanyiwa marekebisho katika kifungu cha 127(2) kupitia Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Sekta ya Sheria za mwaka 2023 (The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) ili kuhakikisha maslahi ya mtoto yanalindwa hasa pale anapotoa ushahidi wake mahakamani. Aidha, Wizara inaendelea kurekebisha Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za mwaka 2012, Kanuni za Makao ya Watoto za mwaka 2012, Kanuni za Uasili Watoto za mwaka 2012 na Kanuni za Malezi ya Kambo za mwaka

2012 ili kuhakikisha mazingira ya malezi ya mtoto wa kitanzania ni salama kwa makuzi stahiki.​
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais aliyoyatoa Mei Mosi, 2024 Mkoani Arusha, kuhusu waliojifungua watoto kabla ya siku zao kutimia (njiti) kwamba, kipindi cha uangalizi maalumu wa watoto hao hakitahesabiwa kama likizo ya uzazi; Wizara inashirikiana na Wizara nyingine za kisekta kwenye kuboresha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366. Lengo la marekebisho haya ni kuweka vifungu vya kumuongezea muda mama aliyejifungua mtoto njiti ili kuweza kupata muda wa kutosha wa kumhudumia mtoto vizuri tofauti na sheria ilivyo kwa sasa.
Mheshimiwa Spika, matokeo ya utafiti wa kujua kiwango cha ukatili dhidi ya Watoto kupitia mitandao (online child abuse) wa mwaka 2022, umebainisha asilimia 67 ya watoto wa umri wa miaka 12 hadi 17 wanatumia mitandao ambapo, kati yao 4% wamefanyiwa vitendo vya ukatili na uonevu bila ya ridhaa yao. Hii ni kwa kuwa Matumizi ya mitandao hayawezi kuepukwa kutokana na mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo mitandao ni sehemu ya maisha hasa kwa kizazi kilichopo sasa.
Mheshimiwa Spika, katika kuwalinda watoto dhidi ya ukatili mitandaoni, Wizara ilizindua Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Mtandaoni tarehe 10

Februari, 2024 Jijini Dodoma ambapo wadau zaidi ya 460 walishiriki. Lengo la kampeni hiyo ni kuelimisha watoto, wazazi, walezi, walimu, viongozi wa dini, viongozi wa Taasisi zisizo za Serikali, Wizara za kisekta, na jamii kuhusu kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili mitandaoni sambamba na ukatili wa aina nyingine. Aidha, uzinduzi uliambatana na kuwajengea uelewa wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari ili waweze kutoa kipaumbele katika utoaji wa taarifa kuhusu usalama wa watoto mtandaoni. Baada ya uzinduzi huo, Kampeni hii iliendelea kutekelezwa katika Mikoa yote kupitia majukwaa ya watoto, wazazi na walezi, viongozi wa dini na mikusanyiko mbalimbali katika Jamii. Aidha, Wizara imezindua Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni kwa lengo la kuishauri Serikali kuhusu usalama wa mtoto mtandaoni.
Mheshimiwa Spika, katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia aina nyingine ya ukatili wa watoto kupitia Sanaa mbalimbali ambapo watoto wanashirikishwa kwenye matamasha ya usiku wakihusishwa katika michezo na shughuli za maonesho ya mitindo, sherehe za harusi na shughuli nyingine za starehe mazingira ambayo katika maeneo mengi yamekuwa yakichangia mmomonyoko wa maadili na pia ni kinyume na Sheria ya Mtoto kifungu cha 158(1)(b).

Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, waandaji wa vipindi, filamu na wanaoonesha filamu kwenye majukwaa mbalimbali baadhi yao wamekuwa hawazingatii kuandaa maudhui yanayoendana na mila na desturi zetu ili kumlinda mtoto na jamii kwa ujumla. Kupitia bunge lako tukufu, napenda kutoa taarifa kuwa, Wizara haitavumilia jamii kuletewa maudhui ambayo ni kinyume na sheria za usajili wa huduma inayotolea kwenye maeneo haya na mengine yanayohusu kuzalisha maudhui yanayopokelewa na jamii. Hivyo, Wizara itakuwa mstari wa mbele kushirikiana na wizara za kisekta kuhakikisha sheria husika zinafanya kazi yake dhidi ya watu hao.
Mheshimiwa Spika,
katika kukabiliana na suala zima la mmomonyoko wa maadili, Serikali imeunda Kamati Maalum inayojumuisha Wizara yangu pamoja na Wizara nyingine za Kisekta, na Taasisi za Serikali zilizo chini ya Wizara hizi ambapo, lengo la kamati hii, ni kubaini vyanzo vya mmomomyoko wa maadili kwa ujumla ukiwemo ule wa watoto, kutambua ukubwa wa tatizo na kuandaa mpango kazi wa kutekeleza ili kuzuia na kumaliza tatizo hili. Aidha, mbinu mbalimbali zitatumika katika kukabiliana na tatizo hili na kuishirikisha jamii kuhusu taarifa ya utekelezaji ili kupata elimu na kuchukua hatua kwa nafasi yao.

Mheshimiwa Spika, suala la kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto ni jukumu la kila mmoja wetu, katika kutimiza azma hiyo, Wizara inashirikiana na vikundi mbalimbali vya kijamii kwa hiari vikiwemo SMAUJATA (Mashujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii), SAWATA (Sauti ya Watoto Tanzania), Malezi Bora Network, FAGDI (Foundation for Ambassodors Gender Development Initiatives) na vingine kadhaa. Kupitia Kampeni ya Wizara kwa ushirikiano na SMAUJATA yenye lengo la kuelimisha watoto na jamii kuhusu kukabiliana na vitendo vya ukatili, hadi kufikia Aprili, 2024 jumla ya wananchi 10,525 wamejiunga na mtandao huu wa mashujaa katika mikoa yote na matokeo mojawapo ni jumla ya matukio 799 ya ukatili dhidi ya watoto yameibuliwa na kuwasilishwa kwenye mamlaka za kusimamia sheria kwa hatua zaidi.
Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha Haki ya Watoto ya Kushiriki kwenye masuala yanayowahusu Wizara imeendelea kuratibu Uanzishwaji na uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto katika ngazi ya Kijiji/Mtaa, Kata, Halmashauri, Mikoa na Taifa. Mabaraza ya Watoto ni jukwaa maalum kwa watoto kutoa maoni, kujadiliana na kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu uongozi, uadilifu, uzalendo na masuala mengine mtambuka ikiwa pamoja na elimu ya jinsia, mazingira na UKIMWI. Aidha, Mabaraza ya Watoto yamewezesha watoto kuwa na uwezo mkubwa wa kujitambua, kujieleza na

kujiamini ambapo ni ishara nzuri kwa kizazi chenye tija katika Jamii kwa siku za usoni. Hadi kufikia Aprili, 2024 jumla ya Mabaraza ya Watoto 865 yameundwa nchini ikilinganishwa na Mabaraza ya watoto 592 yaliyokuwa yameundwa hadi Aprili, 2023 sawa na ongezeko la 46%.
Mheshimiwa Spika; katika kukabiliana na changamoto za Malezi na Makuzi duni ya watoto wenye umri kati ya miaka 0 – 8; Wizara imeendelea kuratibu na kusimamia Programu mbalimbali zikiwemo; Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ya mwaka 2021/22 - 2025/26 inayojulikana kama MMMAM. Programu ina vipaumbele vya kuzingatia pamoja na afua mbalimbali zinazolenga kutoa elimu ya mafunzo ya malezi kwa maafisa wa Serikali wa kada mbalimbali, viongozi wa dini na walezi ambao kwa namna moja au nyingine wanahusika katika makuzi na malezi ya mtoto. Aidha, programu hii pia inamlenga kijana balehe kwa kumpatia elimu ya uelewa wa masuala ya makuzi na kujikinga na athari mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, kufikia Aprili 2024, Serikali kwa kushirikiana na Wadau imejenga uelewa kuhusu Programu hiyo kwa Maafisa 3,123 wa Serikali na Wadau wengine katika Mikoa yote
26 na Halmashauri 184 ikihusisha Wakuu wa Mikoa, Wajumbe wa Kamati za Usalama za Mikoa na Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa. Aidha, mafunzo hayo yamefikia Wakurugenzi Watendaji,

Wenyeviti wa Halmashauri, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Lishe, Maafisa Elimu na Waganga Wakuu katika Halmashauri zote nchini. Kupitia mikutano ya utambulisho wa Programu hii, washiriki waliweza kuainisha vipaumbele vya MMMAM kwa ajili ya kuingizwa kwenye mipango na bajeti ya Mikoa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa nafasi kubwa waliyo nayo viongozi wa dini katika kusaidia na kuimarisha malezi na makuzi ya watoto wetu kupitia mafunzo ya dini; Wizara imeratibu na kusimamia mafunzo ya kujenga uelewa wa Programu ya MMMAM kwa Viongozi wote wa Dini wa ngazi ya Taifa kutoka muunganiko wa Taasisi za dini ambazo ni Wakatoliki (TEC), Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT), Wapentekoste (CPCT), Waadiventista Wasabato (SDA) na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA). Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa viongozi hawa kuhusu umuhimu wa kuwekeza kwenye MMMAM na hatimaye kuingiza maudhui ya MMMAM kwenye miongozo ya dini ili kuitumia katika mahubiri na mihadhara.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Viongozi wa dini imeandaa kitabu cha malezi ya watoto kwa muktadha wa dini ya kiislam na kikristo kinachoitwa “Wazazi wangu, Kesho yangu’’. Maudhui ya Kitabu hicho yanalenga kuimarisha malezi bora kwa watoto na familia kwa

muktadha wa dini za kiislamu na kikristo. Na Maudhui ya kitabu hicho yataweza kutumika kuelimisha waumini wao kote nchini.
Mheshimiwa Spika, Wizara ina jukumu la kusimamia ukuaji chanya wa watoto kupitia malezi ya familia pamoja na vituo vya kulelea Watoto wadogo na wachanga. Katika kufanikisha hili, Wizara imeendelea kuhamasisha uanzishwaji wa vituo vya kulelea Watoto wadogo na watoto wachanga ambavyo vinatoa huduma ya uchangamshi wa awali unaowasaidia watoto kukua kimwili, kiakili, kiafya, kihisia na kimaadili na hatimae kuwaandaa kujiunga na elimu ya awali. Aidha, vituo hivi ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha ulinzi wa watoto na usalama wao wakati wazazi na walezi wao wakijihusisha na shughuli za kiuchumi badala ya kuwepo mitaani. Vituo hivi vina jukumu pia la kusimamia afya na lishe bora kwa watoto, pamoja na kuimarisha malezi yenye mwitikio na nafasi ya kujifunza.
Mheshimiwa Spika, kufikia Aprili 2024, jumla ya vituo 3,862 vya kulelea watoto wadogo mchana vimesajiliwa vyenye jumla ya watoto 397,935 (Me 175,517 na Ke 222,418) na vituo vya Kijamii 206 (vikiwemo 30 vya mfano) vyenye jumla ya watoto 11,675 (Me 4,833 na Ke 6,842), ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo kulikuwa na jumla ya vituo 3,033 na vya kijamii 200 vilivyokuwa na jumla ya watoto 184,606 (Me 86,832 na Ke 97,774). Hatua hii imefanya kuwa na ongezeko la vituo 829 sawa na

21.5% na ongezeko la watoto 225,003 sawa na 55%.​
Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba, Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwanzo Afrika zilizoandaa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto mwaka 2021 baada tu ya mwongozo wa kimataifa kutoka mwaka 2018. Kutokana na utayari huo na mafanikio yaliyopatikana katika kuratibu utekelezaji wa programu hii, Tanzania ilipewa Heshima ya kuandaa mkutano wa Kimataifa wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki uliofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 14 Machi, 2024 Jijini Dar Es Salaam.
Mheshimiwa Spika, mkutano huu uliandaliwa na Wizara kwa kushirikiana na Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Afrika yaani “Africa Early Childhood Network” na ulikuwa na Kaulimbiu “Wekeza katika Malezi na Makuzi ya Watoto Wadogo; Kujenga Rasilimali Watu Yenye Tija”. Yaani “Investing in Early Childhood; Building Human Capital along the Life Course”.
Mheshimiwa Spika, mkutano huu ulihudhuriwa na jumla ya washiriki 1,300 kutoka, Nchi za Afrika Mashariki, Bara la Afrika, Amerika, Ulaya na Asia ambapo, lengo lilikuwa ni kubadilishana uzoefu, maarifa na kuvutia

uwekezaji katika afua za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto. Pamoja na kufanikiwa kutangaza Programu ya MMMAM, kupitia Mkutano huo, kama nchi kupitia ajenda hii ya maendeleo ya mtoto tumeweza kuitangaza nchi yetu katika sekta za utalii.
Mheshimiwa Spika, afua nyingine tunayotekeleza kwa kushirikiana na wadau Katika Programu ya MMMAM ni ile ya Elimu ya Malezi Jumuishi yanayohusisha wazazi, walezi na vijana wa umri wa miaka 10 - 17. Programu hiyo inalenga kutoa elimu ya malezi kuhusu masuala ya msingi yanayohusu nafasi ya vijana balehe, wazazi na walezi katika makuzi yao kwenye familia kwa kushirikishana. Majaribio ya Programu hii yamefanyika katika mikoa ya Mbeya (Mbarali) na Songwe (Ileje, Mbozi na Tunduma) ambapo, Jumla ya Wazazi/Walezi 400 na Vijana Balehe 520 wameshiriki na tathmini yake inatarajiwa kukamilika June 2024 ambapo, itasaidia Wizara kufanya maamuzi juu ya hatua stahiki za kuchukua.
Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na inaratibu utekelezaji wa Ajenda ya Taifa ya Kuwekeza kwenye Afya na Maendeleo kwa Vijana Balehe nchini yaani NAIA- AHW (2021/22 – 2024/25). Uratibu wa Ajenda hii unajumuisha Sekretarieti ya Taifa, Kamati Tendaji ya Taifa (Wakurugenzi); Kamati ya Uratibu wa Ufuatiliaji na Tathmini; Kamati Elekezi ya Taifa (Makatibu

Wakuu), na Jukwaa la Waheshimiwa Mawaziri wa Wizara za Kisekta. Lengo la autekelezaji huu ni kuongeza uwekezaji katika huduma mbalimbali kama Elimu (VVU/UKIMWI, kujikinga na Mimba za utotoni), vilevile kutoa elimu juu ya athari za utoro mashuleni pamoja na kuepuka masuala yanayopelekea mmomonyoko wa maadili ili kuwawezesha vijana kukua na kufikia ndoto zao.
Mheshimiwa Spika, kufikia Aprili, 2024 jumla ya Vijana balehe 983,487 (wavulana 261,293, wasichana 722,194) walipatiwa huduma za upimaji wa VVU na kati ya hao waliopatikana na maambukizi walikuwa 6,154 sawa na 8.5% ya vijana balehe waliopima (wavulana walikuwa 772 sawa na 12.5% na Wasichana 5,382 sawa na 87.5%. Waathirika wote waliunganishwa na huduma za matibabu (CTC). Aidha, Jumla ya Vijana 8,380,871 (wavulana 5,394,334 na Wasichana 2,986,537) walipata elimu ya Afya ya Uzazi kwa lengo la kuwakinga na mimba za utotoni na athari nyingine zinazotokana na uzazi usio salama.
Mheshimiwa Spika, suala la Lishe, ni moja ya afua katika mpango unaohusisha vijana Balehe ambapo, katika kuimarisha lishe kwa vijana hawa jumla ya shule za msingi na sekondari 921 zimehamasika na kuanzisha miradi ya kilimo cha bustani kwa lengo la kuzalisha vyakula vyenye lishe mashuleni. Aidha, wakufunzi 30 walipatiwa mafunzo ya elimu ya lishe; sambamba na kutekeleza

kampeni za elimu lishe kwa jamii. Katika kuwapa vijana ujuzi na ufundi, jumla ya vijana 11,845, walipatiwa mafunzo ya uanagenzi katika fani mbalimbali ikiwemo TEHAMA ili kukuza ujuzi na jumla ya vijana 1,888 (wavulana 1,070 na wasichana 809,) wameunganishwa na ajira mbalimbali kupitia programu ya Mafunzo kwa Vitendo (internship). Vilevile, jumla ya vijana 1,411,254 (wavulana 698,076 na wasichana 713,178) walifaidika na mradi wa kusaidia kaya maskini kupitia TASAF (cash transfer).
Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na mila na desturi zenye madhara kwa Watoto na jamii, Wizara imeendelea kuratibu utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza Ukeketaji wa mwaka 2020/21-2024/25 wenye lengo la kutokomeza vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike na wanawake nchini.
Mheshimiwa Spika, kufikia Aprili, 2024 Wizara kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imekuwa ikitoa elimu kwa njia mbalimbali ambapo watoto, viongozi wa kimila, viongozi wa dini, watu mashuhuri, mang’ariba na jamii kwa ujumla walifikiwa. Elimu iliyotolewa imesaidia kuongeza uelewa wa jamii kuhusu kuacha vitendo vya ukeketaji ambapo, takwimu za Hali ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania za mwaka 2022/2023 zinaonesha kupungua kwa vitendo vya ukeketaji nchini kutoka asilimia 10 kwa mwaka 2015/2016 hadi asilimia 8 kwa mwaka 2022/2023.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, katika baadhi ya mikoa kiwango cha ukeketaji bado ni kikubwa mfano, Arusha (43%), Manyara (43%),
Mara (28%), Singida (20%), Tanga (19%), Dodoma
(18%), Iringa (12%), Morogoro (10%), Kilimanjaro
(9%), Njombe (7%), Pwani (5%) na Mbeya (3%). Mikoa mingine, ukeketaji upo chini ya asilimia 1. Wizara inaendelea na utekelezaji wa Mkakati huo ili kufikia lengo la kupunguza vitendo vya ukeketaji hadi asilimia 5 ifikapo mwaka 2025.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika udhibiti wa ukeketaji, tarehe 9 - 11 Oktoba, 2023, Serikali ilipata Heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa Kimataifa wa Kutokomeza Ukeketaji kwa nchi za wanachama wa Umoja wa Africa uliokuwa na kaulimbiu "Mabadiliko katika Kizazi". Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kubadilishana uzoefu miongoni mwa Wadau katika kuimarisha mikakati iliyopo ya kutokomeza ukeketaji kwa watoto na wanawake miongoni mwa nchi wanachama. Aidha, Mkutano huo ulitoa fursa kwa Tanzania kuwasilisha ujumbe kwenye jumuiya ya kimataifa kuhusu juhudi na mchango wa nchi yetu katika kutokomeza vitendo vya ukeketaji nchini ikiwa pamoja na ukeketaji wa kuvuka mipaka ambao wahusika huvuka mipaka kwenda nchi jirani ili kutekeleza vitendo hivyo. Aidha, nchi ilipata mapato kupitia huduma zilizotolewa na fursa ya kutangaza uwekezaji na vivutio vya utalii

vinavyopatikana hapa nchini. Mkutano ulifanyika kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo ambapo jumla ya washiriki zaidi ya 1,000 walihudhuria.
ENEO LA 4: HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII
Mheshimiwa Spika, Wizara ina jukumu la kusimamia, kuratibu na kutoa huduma za Ustawi wa Jamii hapa nchini zikiwemo: haki, matunzo na ulinzi kwa wazee; watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi; watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani; watoto walio katika mkinzano na sheria; huduma kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia na waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu; huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii. Majukumu haya yanatekelezwa na wataalam wa Ustawi wa Jamii kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mahsusi inayoongoza utoaji wa huduma za Ustawi wa Jamii.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2023/24, Wizara imeendelea na utekelezaji wa kuratibu afua za ustawi ambazo ni pamoja na; huduma kwa makundi maalum; huduma kwa familia zisizo na uwezo; usajili na usimamizi wa makao ya watoto, nyumba salama, vituo vya kulelea watoto wadogo mchana na watoto wachanga; makazi ya wazee na wasiojiweza; huduma za malezi ya kambo na kuasili; na utatuzi wa migogoro ya familia na ndoa; na huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, Wizara imeendelea kusimamia na kuratibu utambuzi na utoaji wa huduma kwa kundi hili wakiwemo watoto waliotelekezwa, wanaoishi na kufanya kazi mitaani, wanaotoka katika kaya masikini, wanaolelewa na wazee wasio na uwezo, watoto wanaojilea wenyewe, watoto yatima, na wale wanaokinzana na sheria pamoja na watoto waliozaliwa nje ya ndoa na watoto walio katika familia zenye migogoro.
Mheshimiwa Spika, utambuzi wa makundi haya ya watoto hufanywa na Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto ngazi ya Kijiji/Mtaa zilizoundwa kupitia Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) pamoja na mfumo jumuishi wa mashauri ya watoto (National Intergrated Case Management System (NICMS).
Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2024,
jumla ya watoto 708,957 (Me 340,661, Ke 368,296) wanaoishi katika mazingira hatarishi wametambuliwa katika Halmashauri zote nchini na kupatiwa huduma kuendana na mahitaji yao ikiwemo watoto 275,058 (Me 127,667, Ke 147,391) wamesaidiwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau kupata vyeti vya kuzaliwa. Aidha, Kaya za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi 457,450 (Me 141,507, Ke 315,943) zimesaidiwa kupata Bima za afya. Vilevile, watoto wengine

wamesaidiwa kupata chakula, malazi, mavazi, elimu, matibabu, lishe, dawa za kufubaza VVU/UKIMWI, afya ya uzazi, ulinzi, msaada wa kisaikolojia na kijamii, marekebisho ya tabia, kuunganishwa na familia na mafunzo ya ufundi na stadi za maisha.
Mheshimiwa Spika, katika suala la huduma za mahabusu kwa watoto, Wizara imeendelea kusimamia utoaji wa huduma za Ustawi katika mahabusu tano (5) za watoto za Mbeya, Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Dar es Salaam. Watoto hawa ni wale walio katika mkinzano na sheria. Hadi kufikia Aprili, 2024, jumla ya watoto 381 (Me 361 na Ke 20) waliopo katika mahabusu hizi walipatiwa huduma za msingi zikiwemo chakula, malazi, mavazi, matibabu, elimu, stadi za maisha na marekebisho ya tabia. Aidha, kati ya hao, jumla ya watoto 92 (Me 89 na Ke 3) waliohukumiwa kwa makosa mbalimbali na wanaendelea kuhudumiwa katika Shule ya Maadilisho ya Irambo Mkoani Mbeya. Shule hii inatoa pia marekebisho ya tabia na elimu ya msingi na stadi za maisha kwa watoto ili wanapokamilisha hukumu zao waweze kujitegemea na kuwa raia wema.

Mheshimiwa Spika, kuhusu huduma za Mahakama kwa watoto, Wizara imeendelea kuratibu huduma za Ustawi wa Jamii katika Mahakama za Watoto 133 nchini ambapo katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, mashauri 4,462 yalipokelewa yakijumuisha mashauri 1,034 ya matunzo (maintenance), 952 ya uangalizi wa mtoto (custody), 882 ya kuona watoto (access), 680 watoto waliokinzana na sheria, 13 ya kuasili, 7 ya vinasaba (DNA order), 22 ya uthibitisho wa baba (parentage), 872 ya Huduma za afya ya akili, msaada wa kisaikolojia na kijamii (Mental Health and Pyscho-social support - MHPS). Jumla ya mashauri 3,984 kati ya yote yaliyopokelewa yalisikilizwa na kufungwa na mashauri 478 yaliyobaki bado yanaendelea kusikilizwa.
Mheshimiwa Spika, huduma za malezi ya kambo na kuasili zimeendelea kutolewa kwa watoto walio katika mazingira hatarishi kwa kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa katika ngazi ya familia kulingana na Sheria ya Mtoto, Sura ya
13. Wizara imeendelea kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari, vipeperushi na matangazo juu ya umuhimu wa malezi ya watoto ngazi ya familia kupitia huduma ya malezi ya kambo na kuasili. Kutokana na jitihada hizi, idadi ya watoto waliopata malezi mbadala imeongezeka ambapo kufikia Aprili 2024, jumla ya watoto 133 walipata malezi mbadala wakiwemo 74 malezi ya kambo, na 59 wameasiliwa, ikilinganishwa na

idadi ya Watoto 75 (41 malezi ya Kambo na 34 walioasiliwa) mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la 43.6%.
Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuharakisha maamuzi ya malezi mbadala, Wizara imefanikiwa kuwajengea uwezo watoa huduma 30 kutoka Halmashauri nane (8) za Mkoa wa Mwanza ikijumuisha Maafisa Ustawi wa Jamii, Mahakimu, Majaji, Maafisa wa Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto na Maafisa Afya ili kushughulikia maombi ya malezi ya kambo na kuasili kwa ufanisi na haraka pindi yanapowasilishwa katika Mamlaka zao.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma za msingi kwenye makao ya watoto ikiwemo usajili, malazi, chakula, malezi, matunzo, ulinzi, afya, elimu, msaada wa kisaikolojia na kijamii, mafunzo ya ufundi na stadi za maisha kwa watoto walio katika mazingira hatarishi nchini. Aidha, hadi kufikia Aprili 2024, leseni 35 za usajili wa Makao ya Watoto zimetolewa kwa watu binafsi na taasisi za dini na kufanya jumla ya makao yaliyosajiliwa kufikia 368 yenye Watoto 13,945 (Me 7,007 na Ke 6,938) ikilinganishwa na jumla ya Makao 333 mwezi Aprili 2023 ambapo jumla ya wahudumiwa ilikuwa watoto 12,077 (Me 6,050, Ke 6,027).
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa huduma kwa watoto waliopo katika Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo (Dodoma) na Kurasini

(Dar es Salaam) ambapo jumla ya watoto 215 (Me 129, Ke 86) wamehudumiwa. Kwa sasa Wizara inaendelea kuboresha huduma katika Makao ya Taifa ya Watoto ya Kikombo kwa kuanzisha miradi ya ukumbi na huduma ya chakula, kilimo biashara na bustani za mbogamboga, ushonaji, pamoja mpango wa kuanzisha kituo cha kulelea watoto wadogo mchana kitakacho hudumia watoto wa kituoni na wa nje ya kituo.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wizara nyingine za kisekta na Wadau wa Maendeleo inaendelea kutekeleza Mpango Jumuishi wa Mashauri ya Watoto (National Intergrated Case Management) ya Mwaka 2017, ambao moja ya afua ni kuwaondoa watoto mitaani kwa utaratibu wa kuwatambua na kuwapatia makazi ya muda kwenye Makao ya Watoto kwa ajili ya kupata huduma za msingi na hatimae kuwaandaa kuunganishwa na familia zao au kuwezeshwa kujitegemea katika jamii au utaratibu mwingine wa malezi mbadala ikiwemo kuasili na malezi ya kambo.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024, Wizara kwa kushirikiana na OR TAMISEMI imepanua wigo wa utambuzi wa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kwa kuyafikia maeneo mengi zaidi ambayo ni masoko, vituo vya mabasi, minada na maeneo mengine yenye mikusanyiko ya shughuli za kiuchumi. Utambuzi huu, umewezesha kupata jumla ya watoto 8,372 (Me 4,218, Ke 4,154)

kutoka katika Halmashauri za mikoa yote. Aidha, katika kipindi cha Julai 2022 hadi Aprili 2023 jumla ya watoto waliotambuliwa walikuwa 5,728 (Me 4,583 na Ke 1,145), sawa na ongezeko la Watoto 2,644. Hata hivyo, Serikali bado imeendelea kuwapatia watoto hawa huduma zikiwemo kuunganishwa na familia zao (2,457), kuwawezesha kujitegemea katika jamii (873) na 5,042 wanaendelea kupatiwa huduma kwenye Makao ya Kulelea Watoto nchini kote.
Mheshimiwa Spika, takwimu hizi zinaonesha ukubwa wa tatizo la Watoto wa mtaani kuwa linaendelea kuongezeka. Sababu kubwa zinazochangia ongezeko hilo ni pamoja na hali duni ya maisha katika baadhi ya familia wanazotoka watoto hawa, msongo rika (peer pressure), malezi duni, pamoja na kuvunjika kwa ndoa. Sababu nyingine ni pamoja na vifo vya mzazi/wazazi, au mlezi/tegemezi mkuu katika familia na kukosekana mbadala wa kuwalea watoto. Hivyo, juhudi za pamoja zinahitajika katika kukabiliana na suala hili kuanzia ngazi ya familia, Mtaa au Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa kwa kushirikisha viongozi wa ngazi zote.
Mheshimiwa Spika, mkakati mwingine ambao Wizara kwa kushirikiana na OR TAMISEMI imeweka ni uanzishaji wa madawati ya watoto katika vituo vya mabasi 21 nchini kwa ajili ya kuwatambua na kuchukua hatua stahiki kupitia Maafisa Ustawi wa Jamii ili kuwanusuru watoto

hao dhidi ya athari wanazoweza kupata iwapo wataingia mitaani. Watoto waliookolewa na maafisa ustawi katika vituo vya mabasi ni 532 (Me 215 na Ke 317)
Mheshimiwa Spika, serikali kupitia wizara hii itaratibu wadau kuongeza kasi ya kuwaondoa watoto waishio na kufanya kazi mitaani sambamba na mkakati wa kuzia waiingie kuishi na kufanya kazi mitaani kwa kuelimisha jamii na viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa kuhusu umuhimu wa kubaini watoto walio kwenye hatari ya kutoroka majumbani ili hatua stahiki zichukuliwe mapema badala ya kusubiri watoroke na kuanza kuwarejesha wakiwa tayari mitaani. Vilevile, kwa kushirikiana na OR- TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Wadau wa Elimu, Kamati za Ulinzi wa Mtoto na viongozi wa ngazi za Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji/Mtaa, tutaratibu ufuatiliaji endelevu wa mienendo ya mahudhurio ya watoto katika shule za msingi na sekondari ili kubaini wanafunzi watoro na kushirikisha wazazi na walezi kwenye kutambua changamoto zao ili kuzikabili na kuwawezesha watoto hao kudumu shuleni na kuepuka utoro wa majumbani.
Nitumie fursa hii kuwaomba Wakuu wa Mikoa na Wilaya kupitia dhamana zao kuanza kufanya tathmini ya kaya zilizo katika mazingira hatarishi na kuziwekea mkakati wa kuwasaidia ili kuzuia watoto kutorokea mitaani, kwa sababu tatizo hili linaanzia katika mamlaka zao.

Mheshimiwa Spika, kuhusu huduma ya mawasiliano na Elimu kwa Watoto, Wizara inaendelea kuratibu huduma ya msaada wa simu bila malipo Namba 116 (Child Helpline) kwa ajili ya jamii kutoa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto au kupata elimu juu ya masuala ya Watoto. Aidha, huduma nyingine ni ile ya huduma kwa mteja inayotolewa na Wizara kupitia kituo cha huduma kwa mteja kilichopo Dodoma. Mteja anapiga simu kwenye namba 0262160250, 0734986503 na pia anaweza kupiga na kutuma ujumbe na kubaki na ushahidi kwenye namba 0774112233, 0769608130 na 0766400168) kwa
ajili ya kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja wizarani na kusaidia kuwaunganisha na huduma za wataalam katika sekta mbalimbali. Natoa wito kwa mamlaka za mikoa na wilaya nao kubuni na kuanzisha vituo vya huduma za mawasiliano na wateja ili kupunguza msongamano ngazi ya wizara na kubaki na rufaa. Hii itaongeza ufanisi zaidi.
Mheshimiwa Spika, kwa ushirikiano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Wizara inatoa elimu kwa watoto na jamii kwa ujumla, na kufikia Aprili 2024, wizara imefanikiwa kurekodi vipindi viwili (2) vya malezi chanya kwa watoto vinavyoitwa Malezi na Makuzi (MAMAKUZI) na maadili kwa vijana vinavyoitwa Kijana na Maadili (KIJADILI) vyenye mada 20 ambavyo vimelenga kuelimisha jamii na vimerushwa nchini kote katika vyombo vya habari vya kijamii 150 na

inatarajiwa kufanyika tathmini ili kupata matokeo yaliyopatikana kutokana na elimu hii. Mara baada ya tathmini hiyo kukamilika awamu ya pili ya vipindi itaanza.
Mheshimiwa Spika, kupitia Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi (PJT MMAM), elimu ya malezi na makuzi kwa wazazi, walezi na jamii imeendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara katika ngazi zote kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Katika kufanikisha hili, Wizara imevitambua vyuo 63 vya mafunzo ya Malezi ya Watoto nchini pamoja na kutoa mafunzo kazini kwa walezi wa watoto wadogo na wachanga mchana. Jumla ya walezi 12,547 (Me 3,623 Ke 8,924) wameshiriki katika mafunzo ya kuongeza ufanisi wa huduma za uchangamshi wa awali na ulinzi kwa watoto.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau inaratibu na kutoa huduma ya msaada wa akili na kisaikolojia kwa makundi mbalimbali yanayokabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha katika jamii yetu kwa lengo la kuwasaidia kuwa na siha njema kiakili na kisaikolojia na kimaendeleo na majukumu yao bila changamoto. Katika kuhakikisha, huduma hii inatolewa kwa ufanisi kupitia maafisa Ustawi wa Jamii, Wizara imeendelea kuratibu utoaji wa huduma ya msaada wa kisaikolojia kwenye jamii katika Halmashauri zote nchini. Hadi kufikia Aprili 2024, Jumla ya

watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi 284,308 (Me 183,124 na Ke 101,184), wazee
wasiojiweza 245 (Ke 145 na Me 100) na waathirika wa matukio ya ukatili 2,682 (watoto 1,944 na watu wazima 738) wamepatiwa huduma hii. Aidha, katika kipindi hicho huduma hii pia imetolewa kwa wahanga wa vitendo vya ukatili 13,926 (ke 7,142 na watoto 6,784) pamoja na wahanga wa vitendo vya ukatili wa usafirishaji haramu wa binadamu 452 (Me 05, Ke 447).
Mheshimiwa Spika, vilevile, kufikia Aprili 2024, Wizara imeratibu utoaji wa huduma kwa jamii ya waathirika wa maporomoko ya matope yaliyotokea katika Wilaya ya Hanang’, Mkoani Manyara ambapo jumla ya waathirika 9,016 walipatiwa huduma ya afya ya akili na kisaikolojia ikiwa ni pamoja kuwatoa hofu na kuwapa utulivu; kufanya tathmini ya mahitaji ya waathirika kwa mtu mmoja mmoja; familia na jamii na kuwapa huduma stahiki kulingana na mahitaji. Aidha, pia uratibu ulifanyika kwenye kutoa huduma za kisekta kama vile afya na kutambua wazazi wa kuaminika (Fit Persons) kwa watoto waliofiwa na wazazi wao, kwa ajili ya kuwahakikishia usalama wao na kutoa malezi ya muda kwa watoto hao. Vilevile, waathirika wapatao 690, kutoka kaya 140 waliokuwepo katika kambi za muda na ambao walipoteza makazi yao, waliunganishwa na ndugu na jamaa zao ili kuweza kupata hifadhi ya makazi na huduma nyingine.

Mheshimiwa Spika, huduma ya akili na kisaikolojia imetolewa pia katika jamii ambazo zimeathirika kwa mambo mengine kama: Magonjwa, Ukatili, na Migogoro ya ndoa na familia. Katika maeneo haya, Wizara imeratibu utoaji wa huduma ya msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa familia za waathirika wa ugonjwa wa kipindupindu watu 79,513 (Me 38,142 na Ke 41,371) katika mikoa ya Simiyu, Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Kagera, Morogoro, Manyara, Katavi, Kigoma, Rukwa na Dodoma. Aidha, Wizara pia kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta na wadau imeendelea kutoa huduma kwa waathirika 8,920 wa mafuriko katika Wilaya za Rufiji, Kibiti, Nsimbo, Mbeya Jiji na Mlimba.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha huduma inatolewa kwa wakati, Wizara imetoa Elimu ya Mafunzo ya namna ya kutoa huduma ya afya ya Akili na Msaada wa kisaikolojia na Kijamii kwa wathirika wa majanga mbalimbali kwa wataalam 68 katika Mikoa mbalimbali, na utoaji wa elimu hii ni endelevu.
Mheshimiwa Spika, huduma ya Usuluhishi wa Migogoro ya Ndoa na Familia ni moja ya Majukumu ya Wizara hii ya jamii. Ikumbukwe kuwa, utulivu wa Ndoa na Familia ni msingi mkubwa ustawi wa familia na jamii kwa ujumla, kwani huzuia athari nyingi zikiwemo ukatili, Watoto wa mtaani na kuvunjika kwa Ndoa. Katika kuhakikisha kuna ustawi na utulivu wa familia,

Wizara kupitia maafisa Ustawi wa Jamii, imeendelea kuratibu huduma za usuluhishi wa migogoro ya ndoa na familia kupitia Baraza la Usuluhishi wa Ndoa la Kamishna wa Ustawi wa Jamii lililopo Makao Makuu ya Wizara, Mabaraza ya Kata, Mabaraza ya Jumuiya, Ofisi za Ustawi wa Jamii, wasaidizi wa msaada wa kisheria na Kampeni mbalimbali. Hadi kufikia Aprili 2024, mashauri yaliyoshughulikiwa yalikuwa 31,380 ikilinganishwa mashauri 28,773 yaliyoshughulikiwa mwaka 2022/2023 ikiwa ni ongezeko la mashauri 2,607 sawa na asilimia 8.3.
Natoa wito kwa viongozi wa dini zote kuendelea kutoa mafunzo kwa wanandoa wanaofunga ndoa na kwa vijana kupitia mikusanyiko ya vijana katika madhehebu yao, ili kuwaandaa kubeba majukumu ya ndoa na kujiandaa kwa majukumu hayo kabla ya kuingia katika ndoa.
Mheshimiwa Spika
, katika kuhakikisha huduma za Msingi zinatolewa kwa Wazee na watu wasiojiweza, Wizara imeendelea kutoa huduma za chakula, malazi, mavazi, matibabu na msaada wa kisaikolojia na kijamii katika makazi 13 ya wazee yanayomilikiwa na Serikali, pamoja na wazee wanaoishi katika jamii. Wazee hawa waasio na uwezo hutambuliwa kupitia Ofisi za Ustawi wa Jamii zilizopo kwenye Halmashauri zote nchini. Hadi kufikia Aprili 2024, wazee wasiojiweza 240 (Ke 95 na Me 145) walihudumiwa katika makazi ya wazee ya Kibirizi (26), Njoro (18), Kolandoto (18),
Bukumbi (27), Ipuli (24), Fungafunga (21),

Mwanzange (14), Misufini (18), Nunge (18),
Nyabange (14), Kilima (19), Sukamahela (16), Magugu (7). Pia, Wizara imeendelea kusimamia na kuratibu huduma za msingi zinazotolewa kwa wazee kwenye makazi ya wazee ya Taasisi Binafsi
15 yenye jumla ya wazee 268 (me 150, ke 118) katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Shinyanga, Arusha, Tanga, Dodoma na Lindi.
Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto na upungufu katika utoaji wa huduma za ustawi wa jamii, Wizara imejipanga kuimarisha mifumo ya kisheria na kitaasisi kwa kuleta mapendekezo ya kutunga sheria ya usimamizi wa watoa huduma za ustawi wa jamii katika nyanja zote za sekta ya Umma na Binafsi kwa lengo la kuwatambua, kuwasajili na kudhibiti ubora wa huduma wanazozitoa. Aidha, katika kutekeleza maagizo ya Kamati ya Mheshimiwa Rais ya kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Maboresho ya Haki Jinai, Wizara kwa kushirikiana na Wizara za kisekta na Taasisi nyingine ipo katika hatua ya kukamilisha uanzishwaji kisheria kwa Idara ya Ustawi wa Jamii kama Idara inayojitegemea, ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya imeendelea kuimarisha utaratibu wa utoaji huduma za matibabu kwa wazee wasiojiweza na ambao wanaishi katika jamii kwa kufanya utambuzi na tathmini na kisha

kuwapatia vitambulisho vya kupata huduma za Afya bure katika vituo vya Afya.​
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya wazee 574,321 (Me 214,739, Ke 359,582) ambapo kati yao wazee wasiojiweza 365,284 (Me 145,829, Ke 219,455) sawa na asilimia 63.6 ya wazee wote waliofanyiwa tathmini, wamepatiwa vitambulisho maalum kwa ajili ya msamaha wa matibabu. Vilevile, kampeni ya “MPISHE MZEE KWANZA” inaendelea kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya Taifa ili kutoa kipaumbele na kuhakikisha wazee wanapata huduma za afya kwa wakati. Kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024 kulikua jumla ya madirisha 1,066 ya huduma kwa wazee nchini kote ikilinganishwa na madirisha 629 yaliokuwepo mwaka 2022/2023 ikiwa na ongezeko la madirisha 437 sawa na asilimia 69.48.
Mheshimiwa Spika, Wizara ipo katika hatua za Mwisho za kukamilisha mabadiliko ya sera ya wazee ambapo miongoni mwa maboresho yatakayozingatiwa ni pamoja na umuhimu wa jamii kujiandaa kabla ya uzee, huduma wa afya ya akili na msaada wa kisaikolojia kwa wazee, miundombinu na mazingira wezeshi kwa wazee na uwezeshwaji wa wazee kwenye mabadiliko ya Teknolojia kama TEHAMA.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu bado inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa Maafisa Ustawi wa Jamii 17,485 ambayo ni sawa

na asilimia 94.6 ya Maafisa wanaotakiwa kuanzia ngazi ya Mkoa mpaka ngazi ya Kijiji/Mtaa kama inavyoonesha katika Jedwali Na.5
Jedwali Na. 5: Idadi ya Maafisa Ustawi wa Jamii katika Ngazi Mbalimbali
NaNgaziMaafisa Wanaohi
tajika
Maafisa
Waliopo
Upungufu
Idadi%Idadi%
1.Mkoa26361380-
2.Hospitali za Rufaa na Mikoa1574226.811573.2
3.Halmashauri1,47257539.189760.9
4.Hospitali za Wilaya55216329.538970.5
5.Kata/Vituo vya Afya3,9561904.83,76695.2
6.Mtaa/Kijiji/
Zahanati
12,3180012,318100
Jumla18,4811,0065.417,48
5
94.
6
Chanzo: WMJJWM, 2024
Mheshimiwa Spika, naomba kutaarifu Bunge lako kwamba katika kuendelea kufanyia kazi upungufu wa maafisa ustawi wa jamii, Serikali imetoa kibali cha kuajiri Maafisa 350 watakao sambazwa kulingana na mahitaji na mchakato wa ajira umeshaanza. Nichukue fursa hii kumshuruku Mheshimiwa Rais kwa kutoa kibali cha ajira hizo. Vilevile, napenda kumshukuru Waziri-OR Utumishi Mheshimiwa George Simbachawene kwa ufuatiliaji wake hadi kufanikisha suala hili. Nakiri kuwa, bado uhitaji ni mkubwa hivyo, serikali itaendelea kuongeza wataalamu hawa kadri uwezo wa ajira unavyoruhusu.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeadhimisha Wiki ya Ustawi wa Jamii ambapo kilele chake kilikuwa tarehe 18 Desemba, 2023. Katika maadhimisho hayo yafuatayo yalifanyika:
Elimu kuhusu huduma za Ustawi wa Jamii kupitia vyombo vya habari ikiwemo redio, televisheni na mitandao ya kijamii imetolewa ambapo jumla ya vipindi 24 vya redio na vipindi vitano (5) vya Luninga vimerushwa;
Huduma mbalimbali zilitolewa kwa watu 9,314 bila malipo katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Geita, Kigoma, Arusha, Dar-es-Salaam na Songwe. Huduma hizo ni pamoja na afya ya akili na msaada wa kisaikolojia na kijamii, huduma kwa manusura wa vitendo vya ukatili, huduma za usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vifo, huduma za afya, elimu ya upimaji wa vinasaba, huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi zilitolewa moja kwa moja.
Jumla ya watu 2,027 walishiriki Mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii uliofanyika Septemba 2023 mkoani Dodoma na Kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii kilichofanyika Dar-es-Salaam. Washiriki wa mikutano hiyo ni Maafisa Ustawi wa Jamii 1,025, wadau 189, wamiliki wa vituo vya kulelea wototo wachanga na wadogo vya mchana na kijamii 813.

Uzinduzi wa Kamati ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto iliyopo chini ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Mary Chatanda, Mwenyekiti wa UWT Taifa na washiriki 1,850 walihudhuria.
ENEO LA 5: MAENDELEO YA JINSIA NA
UWEZESHAJI WANAWAKE
Mheshimiwa Spika, katika eneo la maendeleo ya Jinsia na Uwezeshaji wanawake, Wizara ina jukumu la kuhakikisha kuna usawa wa jinsia kwenye maendeleo katika jamii yetu kwa kuwezesha wanawake kiuchumi ili waweze kuchangia katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya familia na nchi kwa ujumla. Katika kufanikisha hili, Wizara, inatekeleza Programu ya Kitaifa ya Kizazi Chenye Usawa 2021/22 – 2025/26 (Generation Equality Forum Commitments - GEF) ambapo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Kinara wa utekelezaji wa eneo la Haki na Usawa wa Kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, programu ya Kizazi Chenye Usawa (GEF) inahusu utekelezaji wa haki za wanawake za kiuchumi kwenye maeneo manne
(4) yakiwemo uwekezaji wenye mrengo wa kijinsia katika huduma na kazi za matunzo kwenye sekta za umma na binafsi, kazi zenye staha, upatikanaji na umilikishaji wa rasilimali za uzalishaji kiuchumi kwa wanawake, mipango ya uchumi jumla,

maboresho ya kibajeti na vichocheo vya kiuchumi kwa kaya maskini vinavyozingatia jinsia.​
Mheshimiwa Spika, Serikali imeteua Waratibu wa Programu hii na kutoa mafunzo kwao ili kuhakikisha utekelezaji wenye ufanisi. Jumla ya Waratibu 234 kutoka Wizara na Taasisi za Kisekta, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zote wamepatiwa mafunzo juu ya uratibu, usimamizi na utekelezaji wa programu hii. Aidha, Wakurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara zote ambao ni waratibu wa program hii wamepatiwa mafunzo. Wakati wa Mafunzo hayo, msisitizo uliwekwa katika kujenga uelewa juu ya umuhimu wa kuandaa bajeti yenye mrengo wa kijinsia (Gender Responsive Budgeting) na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Haki na Usawa wa Kiuchumi ambalo ni eneo namba 2 la utekelezaji wa Mpango wa Kizazi Chenye Usawa (GEF). Vilevile, uelewa juu ya Programu hii, unatolewa kwa jamii kwa kutoa taarifa zinazotekelezwa katika maeneo kuhusu fursa zilizopo kwa wanawake na wasichana katika maeneo yao.
Mheshimiwa spika, moja ya mkakati wa kumkomboa wanamke ambao unazingatiwa katika Programu ya Kizazi Chenye Usawa, ni kuhakikisha anapata muda wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kuchangia maendeleo ya familia na nchi kwa ujumla. Katika kufanikisha hili, Wizara imeweka mkazo katika utekelezaji wa afua ambazo zinalenga kumpa muda zaidi mwanamke zikiwemo, matumizi ya nishati safi,

uanzishaji wa Vituo vya Kulelea Watoto Wachanga na Wadogo na upatikanaji wa maji safi na salama.​
Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha dhamira hii, Wizara kwa kushirikiana na Wizara nyingine za kisekta imetoa elimu juu ya matumizi ya nishati safi na salama ili kuongeza idadi ya watumiaji wa nishati hiyo katika kupikia. Hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya wananchi 1,228,248 wanatumia nishati safi ya kupikia. Aidha, katika idadi hiyo, jumla ya wanawake 102,000 wasiokuwa na uwezo walipatiwa majiko ya gesi bure ikiwa ni jitihada za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwezesha wanawake kutumia nishati safi ya kupikia akiwa kinara wa utekelezaji wa Programu ya kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia Barani Afrika.
Mheshimiwa spika, nishati nyingine ambazo zinawekewa mkazo kutumika na wanawake ni umeme na nishati jadidifu ambapo, matumizi yake yatachangia kuwawezesha wanawake kuanzisha viwanda vidogo vidogo pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi ambazo wanawake wengi wamejiajiri. Hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya vijiji 11,837 sawa na asilimia 96.37 ya vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara vimeunganishwa na umeme. Aidha, kaya 5,193,148 sawa na asilimia 37 ya kaya zote 14,152,803 nchini zimeunganishwa na umeme.
Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa maji safi na salama, ni njia nyingine ya kutoa muda

kwa mwanamke kwa kumuondolea adha ya kufuata maji kutoka umbali mrefu. Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Maji na Wadau wengine imeendelea kuwekeza kwenye upatikanaji wa maji safi na salama, kuhamasisha uvunaji wa maji ya mvua na utunzaji wa vyanzo vya maji. Uhamasishaji umefanyika kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi. Hadi kufikia Aprili, 2024 jumla ya kaya 861,944 za mijini na 541,482 za vijijini zinavuna maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Aidha, kupitia uhamasishaji huu jamii imeweza kutumia mbinu mbadala za upatikanaji wa maji na utunzaji wa miundombinu ya maji kwa manufaa yao na kumsaidia mwanamke na mtoto wa kike. Vilevile, upatikanaji wa maji kwa sasa umefikia asilimia
90.1 kwa mijini na asilimia 79.6 kwa vijijini hatua ambayo imewezesha kumpunguzia muda mwanamke ili aweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. Pia, kumekuwa na ongezeko la wanawake viongozi kwenye Jumuiya za Watumia Maji ambapo asilimia 33 ya viongozi ni wanawake na sasa kuna mwanamke mmoja katika viongozi 3 wa juu.
Mheshimiwa Spika, Katika kuonesha dhamira ya Serikali katika kukuza usawa wa kijinsia, Wizara yangu imeratibu wadau wa kisekta na kukamilisha hatua za kupitishwa kwa Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya mwaka 2023 iliyozinduliwa tarehe 8 Machi, 2024 siku ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Wilayani Chamwino, Mkoa wa Dodoma.

Mheshimiwa Spika, Sera hiyo imezingatia masuala mbalimbali kama mabadiliko ya Tabia Nchi, ushirikishwaji wa wanaume katika jitihada za kuleta usawa wa kijinsia, matumizi ya teknolojia katika uzalishaji na mawasiliano, na ukatili wa kijinsia na ukatili wa mtandaoni. Masuala haya yote yamewekewa matamko na mikakati ya utekelezaji. Kwa kuwa hii ndio Sera Mama ya masuala ya jinsia nchini, utekelezaji wake utachochea jamii na wadau kuendeleza mafanikio yaliyopo katika utatuzi wa changamoto za wanawake na wanaume ili kuwa na Taifa la kizazi chenye usawa.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sera hiyo na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu aliyoyatoa katika vikao vya Bunge hili kuhusiana na kufanya mapitio ya Sheria zinazohusu ukatili wa kijinsia, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara za kisekta, itaendelea kuboresha sheria mbalimbali na kanuni zake ili kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia uliokithiri katika jamii nchini. Ninapenda kutumia nafasi hii kushukuru kwa dhati kabisa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bunge lako tukufu, Wizara za kisekta na wadau wote ambao wamechangia katika kufanikisha kukamilika kwa Sera hii.
Mheshimiwa spika,
katika kuwawezesha wanawake kiuchumi, Wizara kwa kushirikiana na Wizara nyingine za kisekta na wadau wengine wa

Maendeleo, imehamasisha upatikanaji wa masoko kidijitali (digital markets) kwa kutoa elimu ya fedha, ujasiriamali kwa kushirikiana na Taasisi za Fedha. Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024, Wizara kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (Tanzania Women Chambers of Commerce) walitengeneza mtandao wa kidigitali ujulikanao kama iSOKO App kwa lengo la kuwezesha wafanyabiashara wanawake kupata masoko ya bidhaa na huduma zao kupitia simu za mkononi. Kupitia afua hiyo, jumla ya wafanyabiashara wanawake 11,500 wakubwa na wa kati wamejisajili na kutumia App hiyo. Aidha, kumekuwa na ongezeko la wanawake katika matumizi ya simu ambapo asilimia 71 ya wanawake na asilimia 80 ya wanaume wanatumia simu. Ongezeko hili limeongeza chachu kwa wanawake kuimarika kiuchumi kwa kuweza kupata masoko ya mtandao (Digital marketing) ndani na nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake ambapo, jumla ya watu 11,336 walipatiwa elimu kupitia Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika tarehe 8 Machi 2024, na Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa iliyofanyika Arusha Machi 2024. Uhamasishaji huo umewezesha kuanzishwa na kusajiliwa kwa vikundi 6,994 na hivyo kufanya jumla ya vikundi 49,168 vilivyosajiliwa. Aidha, usajili wa vikundi hivi umeleta ufanisi wa

utoaji wa huduma kwenye sekta ndogo ya fedha ikiwemo upatikanaji wa huduma za mikopo ya vikundi yenye masharti nafuu kwa wanawake.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Benki ya NMB imezindua akaunti maalum inayoitwa Vikundi Account ambayo ilizinduliwa tarehe 3 Mei, 2024. Akaunti hii ni mahsusi kwa vikundi mbalimbali vinavyoanzishwa na itawezesha vikundi hivyo vikihusisha wanawake kutekeleza shughuli zao za kiuchumi. Akaunti hii itawezesha vikundi kufungua akaunti vyenyewe, kufanya miamala ya kibenki, kuhamisha fedha kwa wanakikundi bila makato yoyote, kuchangia michango na kukopeshana mikopo ya kikundi kupitia simu zao. Aidha, Akaunti inawezesha vikundi kupata taarifa za fedha bila kufika tawi la benki, na kwamba vikundi vikifikisha kiasi cha Shilingi 500,000 kwenye akaunti yao watapata riba ya 3% kwa mwaka. Akaunti hii ni fursa kwa vikundi kujiimarisha kiutendaji na kuongeza uwazi kwa wanachama wake. Niwaombe Watanzania wenzangu tuchangamkie fursa hii kujiunga katika vikundi na kuhakikisha kikundi kinakuwa na akaunti kwa maendeleo ya wanachama wake.
Mheshimiwa Spika,
Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kutoa mafunzo ya ujasiriamali na uendeshaji wa biashara kwa wanawake wajasiriamali. Kuanzia Julai 2023 hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya wanawake 2,222,000 wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali katika nyanja

za elimu ya fedha, matumizi ya teknolojia, masoko, mnyororo wa thamani na uongozi bora. Aidha, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024, mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 748 imetolewa kupitia Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambapo jumla ya walengwa 6,064,957 wamenufaika na mikopo hiyo; kati yao wanawake ni 3,288,186 sawa na asilimia 54 na wanaume 2,776,771, sawa na asilimia 46.
121. Mheshimiwa Spika, wanawake ni miongoni mwa wadau muhimu wanaochangia utekelezaji na uendelezaji wa Sekta ya Madini ambapo takribani asilimia 26 ya wanawake wamejiajiri kwenye sekta ya madini katika maeneo ya uchimbaji mdogo, uchenjuaji, uongezaji wa thamani na utoaji wa huduma. Katika kuhakikisha wanawake wanazidi kuwekeza katika sekta hii na kukuza ushiriki wao katika mnyororo mzima, Wizara kwa kushirikiana na Wizara mama ya Madini imewezesha vifaa kwa vikundi 10 vya wachimbaji wadogo.
Mheshimiwa Spika, kutokana na mikakati iliyowekwa na Serikali yetu kuhusu utekelezaji wa usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kiuchumi, nchi yetu imepiga hatua kubwa ambayo, imesababisha, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, UN Women, na wadau wengine kupata heshima ya kuandaa kikao kazi cha viongozi wa juu wa Afrika (African High Level Gender Financing meeting) kilichofanyika tarehe 15 hadi 17 Novemba, 2023. Kikao hiki

kilijumuisha wadau kutoka bara la Afrika na mataifa mengine. Lengo la kikao hicho ni kusisitiza umuhimu wa kutenga na kuwekeza rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa masuala ya kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake.
Mheshimiwa Spika, kupitia Mkutano huo na jitihada zinazoendelea kutekelezwa hapa nchini, Tanzania ni miongoni mwa Mataifa ya mfano yenye ushahidi katika uzingatiaji na ujumuishaji na masuala ya jinsia katika mipango ya Kitaifa na bajeti za Kisekta na Taasisi kutokana na uwepo wa Miongozo ya Bajeti ambayo hutolewa kila mwaka na Serikali. Mwongozo wa bajeti ya mwaka 2024/25 umeainisha kipengele kinachoelezea kila wizara na taasisi kujumuisha masuala ya Jinsia kwenye bajeti zao za mwaka 2024/25. Hivyo, ni matumaini yangu kuwa, Waheshimiwa Mawaziri na Wakuu wa Taasisi mtakuwa mmezingatia kipengele hiki wakati wa uandaaji wa bajeti zetu za mwaka huu. Suala la Jinsia ni mtambuka tukiungana kwa pamoja kama nchi tutaweza kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SGDs) kuhusu Jinsia kama yalivyoelekezwa.
Mheshimiwa Spika, kupitia sheria iliyopitishwa ya kuwawezesha wanawake kupata zabuni mbalimbali, asilimia 30 ya zabuni zote inatakiwa kupatiwa kwa makundi maalumu wakiwemo wanawake. Katika kutekeleza hili, Wizara kwa kushirikiana Wizara nyingine za kisekta pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeendelea kuhamasisha vikundi vya wanawake

kutumia fursa hiyo kwa zabuni zinazotangazwa na Serikali. Hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya vikundi 33 vya wanawake wamepewa zabuni zenye thamani ya Shilingi 1,372,948,845.55 ili kuwawezesha wanawake kujiajiri, kuongeza kipato na kuinua uwezo wa shughuli za vikundi vyao. Tunashukuru na kupongeza Bunge lako tukufu kwa kupitisha Sheria Mpya ya Ununuzi wa Umma, 2023 ambayo imeimarisha ushiriki wa makundi maalum ikiwemo wanawake katika fursa za ununuzi wa umma.
Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na Sekta ya mifugo na uvuvi, jumla ya wavuvi wanawake 1,023 wamekopeshwa boti za kisasa za uvuvi na wanawake 446 wamekopeshwa vizimba vya kisasa vya kufugia Samaki bila riba. Aidha, Wanawake 24 wamepatiwa mafunzo yanayohusu utotoleshaji wa vifaranga vya kuku, na wanawake
38 wamewezeshwa kuwa wazalishaji wa vitotoleshi. Katika mlengo huo wa kuwawezesha wanawake, Wizara imefanikisha upatikanaji wa mashine 250 za utotoleshaji vifaranga vya kuku na vyerehani 425 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 79 kutoka Serikali ya Watu wa China ambavyo vitasambazwa kwa wanawake nchini. Jitihada hizi zitawezesha wanawake kuongeza ari miongoni mwao na kuongeza fursa ya kujiajiri katika sekta ya uvuvi, mifugo na ushonaji.
Mheshimiwa Spika, uanzishaji wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ni fursa kwa wanawake kuweza kukutana na kujadili masuala mbalimbali wanayokabiliana nayo katika

shughuli zao za kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuweka mikakati ya ufumbuzi. Aidha, Majukwaa haya yameongeza kazi zenye staha kwa wanawake katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi kwa kufanikisha utambuzi na usajili wa vikundi vipatavyo 43,574 vya wanawake baada ya kukidhi vigezo vya kupata mikopo ya asilimia 10 inayoyotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri. Vikundi vilivyotambuliwa vina jumla ya wanachama 13,778,700 vinavyojishughulisha na ujasiliamali wa bidhaa na huduma mbalimbali. Katika kuhakikisha idadi ya majukwaa haya yanaongezeka, Wizara imeendelea kuratibu uanzishwaji na uendeshaji wa Majukwaa haya. Hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya majukwaa 3,391 yameanzishwa yakijumuisha majukwaa ngazi ya Mkoa 26, Halmashauri 152 kati ya 184, Kata 1,354 kati ya 3,957 na Mitaa/Vijiji 1,859 kati ya Vijiji 12,348. Aidha, Wizara katika kuboresha utendaji kazi wa Majukwaa inakamilisha maandalizi ya Mwongozo wa Uundaji na Uratibu wa majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ili kuyafanya yawe na ufanisi zaidi.
Mheshimiwa Spika, sambamba na uanzishaji wa majukwaa haya, Wizara imeendelea kuratibu ushiriki wa wanawake kwenye Maonyesho mbalimbali ya biashara. Maonesho haya huwapatia fursa wanawake kushiriki na kutangaza bidhaa zao ili kupata masoko ya ndani na nje ya nchi na kuchangia kuongeza wigo wa mtandao wa mawasiliano na mnyororo wa thamani wa bidhaa

zao. Hadi kufikia Aprili, 2024, Wizara iliwezesha ushiriki wa wanawake 336 katika maonesho ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na wanawake 1,880 katika maonesho ya Nanenane na Sherehe za Wakulima yaliyofanyika Kitaifa Jijini Mbeya.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (Women Development Fund - WDF) ambao una lengo la kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia mikopo ya fedha ili kujikwamua kiuchumi. Hadi kufikia Aprili, 2024, jumla ya Shilingi Milioni 77.5 zimerejeshwa kutokana na mikopo iliyotolewa kwa wanawake ikiwa ni jumla ya Shilingi 664 zilizokopeshwa kwa wajasiriamali 104 kutoka kwenye vikundi 11 na wakopaji mmoja mmoja 14. Aidha, Wizara kuanzia Julai 2024 itarejesha mikopo hii kwa utaratibu utakaotangazwa.
Mheshimiwa Spika, napenda kutoa wito kwa wanawake wote waliokopeshwa na watakao kopeshwa kuzingatia masharti ya mikopo kwa kufanya marejesho kwa mujibu wa mikataba. Aidha, ninatoa wito kwa Halmashauri zote zinazodaiwa fedha zinazotokana na mfuko huu kurejesha mikopo yao kwa makubaliano yaliowekwa ili kuuwezesha Mfuko huu kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini.
Mheshimiwa Spika
, katika kuwawezesha wanawake katika nafasi za uongozi, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya

Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Wadau wengine, imeendelea kutoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake ili kuhamasisha na kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuthubutu kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi na maamuzi, rejea Jedwali namba 6 linaloonesha hali ya nafasi za uongozi kwa wanawake kwenye baadhi ya nafasi.
Jedwali Na.6. Wanawake na nafasi za Uongozi

Na
Nafasi ya Uongozi
Asilimia (%)
1
Mawaziri
31​
2
Manaibu Waziri
19​
3
Mabalozi
25​
4
Wabunge
37​
5
Madiwani
34​
6
Makatibu Wakuu
22​
7
Naibu Katibu wakuu
28​
8
Wakuu wa Mikoa
31​
9
Makatibu Tawala
26​
10
Wakuu wa Wilaya
33​
11
Wakurugenzi wa Halmashauri
28​
Mheshimiwa Spika, kama inavyoonekana kwenye jedwali la takwimu hapo juu, ushiriki wa Wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi hapa nchini umeendelea kuongezeka katika nafasi mbalimbali. Hii inachangiwa na dhamira ya dhati ya Kiongozi wetu Mkuu wa nchi ya kuhakikisha wanawake hawaachwi nyuma kushiriki katika nafasi za maamuzi. Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwaamini na kuwateua wanawake katika nafasi mbalimbali za

Maamuzi na Uongozi. Hivyo, wanawake wenzangu tuendelee kuchapa kazi kwa weledi na uaminifu katika kila eneo tulilokabidhiwa huku tukiendelea kujiamini.
Mheshimiwa spika, umiliki wa Ardhi kwa wanawake ni moja ya nguzo muhimu katika uwezeshaji wanawake kiuchumi, kwa sababu hati miliki za ardhi zinatoa utambuzi wa kisheria na usalama kwa wanawake na kuzitumia kama dhamana ya kupata mikopo hivyo kuongeza fursa kwa wanawake kijiwezesha Kiuchumi. Katika kulifanikisha hili, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wadau mbalimbali imeendelea kuhamasisha Wanawake kumiliki Ardhi, kupitia kampeni maalum ijulikanayo kama Stand for Her Land Campaign.
Mheshimiwa Spika,
kupitia hamasa na Kampeni hii, mafunzo yalitolewa kwa jumla ya viongozi 3,063 wa Serikali za Mitaa (KE 1,234, ME 1,829) juu ya utaalam na umuhimu wa kusimamia, kulinda, na kutekeleza haki za ardhi za wanawake pamoja na kushughulikia masuala ya changamoto za umiliki wa ardhi zinazoathiri wanawake. Aidha, Wizara ilitoa mafunzo kwa wananchi 83,886 kuhusu sheria na kanuni zinazohusiana na ardhi, usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa jamii, haki za ardhi kwa wanawake na nafasi ya wanawake katika umiliki wa ardhi.

Hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya vyeti vya kimila (Certicate of Customary Right of Occupancy - CCROs) vimetolewa kwa wanawake 45,528. Wizara itaendelea kuhamasisha jamii kutambua juu ya umuhimu wa Wanawake kumiliki ardhi ili kunufaika na fursa mbalimbali za uwezeshwaji Kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wizara nyingine za kisekta pamoja na wadau wengine, ina jukumu la kuelimisha jamii kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia. Katika kufanikisha hili, shughuli mbalimbali ikiwemo kampeni ya “Zijue Fursa, Imarisha Uchumi, Kataa Ukatili, Kazi Iendelee” (ZIFIUKUKI) huratibiwa na wizara. Tarehe 25 Novemba hadi 10 Desemba, 2023 Wizara kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali (WiLDAF) imeratibu Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia katika mikoa yote nchini, ambapo kilele cha kampeni hii ilifanyika Mkoa wa Mara tarehe 10 Disemba 2023. Lengo la Kampeni hii ni kuongeza jitihada za jamii kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo Kaulimbiu ya Mwaka huu ilikuwa “Wekeza: Kuzuia Vitendo vya Ukatili”.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha ujumbe wa kampeni hii unawafikia wananchi wengi, Wizara kwa kushirikiana na wadau iliratibu Msafara wa Kijinsia ambao ulipita katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida, Tabora, Kagera, Mara, Geita na Kigoma na jumla ya wananchi 9,393 wakiwemo wanafunzi 8,503, walimu 167, waendesha bodaboda 347, wafanyabiashara sokoni 146, na waumini wa

madhehebu mbalimbali 230 walifikiwa katika nyumba zao za ibada. Msafara huo ulitoa huduma mbalimbali katika maeneo ambayo ulipita zikiwemo huduma za msaada wa kisheria, kisaikolojia, elimu ya masuala ya jinsia pamoja na uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine imeratibu Matamasha ya Maendeleo mwezi Desemba 2023 na Machi 2024, katika mikoa ya Geita na Dodoma. Matamasha haya yalilenga kutoa elimu na uelewa juu ya fursa za kiuchumi, na athari za ukatili wa kijinsia. Kupitia Matamasha haya jumla ya wananchi 45,895 (Me 21,830 na Ke 24,065) kwa mikoa hii miwili walipata huduma mbalimbali zikiwemo huduma ya msaada wa kisheria, kisaikolojia, elimu ya masuala ya jinsia, na biashara na huduma za afya.
Mheshimiwa Spika, kupitia Mwongozo wa Uanzishwaji, Uendeshaji na Ufuatiliaji wa Madawati ya Jinsia Katika Vyuo vya Elimu ya Juu na Elimu ya Kati (2021), Wizara imeendelea kuratibu uanzishwaji wa madawati ya jinsia katika Taasisi za Elimu ya Juu na Maeneo ya umma. Sambamba na uanzishwaji wa madawati haya, Wizara imeendelea kutoa mafunzo kwa Wakuu wa Vyuo pamoja na Waratibu wa Madawati haya ili kuwapa uelewa na uwezo wa kuyaratibu na hatimaye, kutokomeza ukatili katika maeneo yao. Hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya Madawati 612 yameanzishwa na kati ya hayo, 296 (48.4%) ni madawati ya jinsia.

Mheshimiwa Spika, uanzishwaji wa madawati haya umekuwa nyenzo muhimu kwa wanafunzi, walimu, watoa huduma na jamii inayozunguka Taasisi hizo na vyuo kushiriki katika kupinga ukatili wa kijinsia. Hadi kufikia Aprili 2024, jumla ya matukio 44 ya ukatili wa kijinsia yaliripotiwa katika maeneo haya ambapo matukio 39 yalipatiwa ufumbuzi na matukio 5 yalipewa rufaa kwenda kwenye Dawati la Jinsia na Watoto katika vituo mbalimbali vya Jeshi la Polisi nchini. Matukio yaliyopatiwa ufumbuzi yanajumuisha matukio (3) ya shambulio la aibu, ujumbe wa picha (6), rushwa ya ngono (5), kutelekeza familia (7), kurubuni (1), shambulio la mwili (14), na matamshi/ ishara (8). Wizara itaendelea kufuatilia na kuimarisha madawati haya ili kukabiliana na vitendo vya ukatili vyuoni.
Mheshimiwa Spika,
Wizara pia inatekeleza Mwongozo wa Uanzishwaji na Uendeshaji wa Dawati la Kutokomeza Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika Maeneo ya Umma (2023) kwa kutoa mafunzo kwa waratibu 47, wanaotoka katika masoko ya Halmashauri 46 za mikoa sita (6) ili kuwajengea uwezo wa kuanzisha madawati katika maeneo ya umma. Hadi kufikia Aprili, 2024 jumla ya waratibu 250 kutoka Halmashauri 46 za Mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam walipatiwa mafunzo ya uanzishwaji na uendeshaji wa Dawati la Jinsia katika maeneo ya umma. Aidha, baada ya mafunzo hayo, waratibu hawa walifanikiwa kuanzisha jumla ya madawati

115 katika maeneo ya masoko ya Mikoa hiyo. Madawati haya yatasaidia kuondokana na Ukatili wa Kijinsia unaofanyika kwenye maeneo ya masoko ambapo wanawake ni wahanga wakubwa wa matukio haya.
Mheshimiwa Spika,
uingizwaji wa masuala ya Jinsia ni kipaumbele ambacho Wizara imeendelea kusimamia ili kuwa na Sera, Mipango, Programu, Mikakati, Miongozo na Bajeti za Wizara za Kisekta na Sekta binafsi zenye mlengo wa kijinsia. Katika kutekeleza hilo, Ofisi ya Rais Utumishi kwa kushirikiana na Wizara imezindua Mwongozo wa Ujumuishaji wa Jinsia katika Utumishi wa Umma wa Julai 2023, ambao unaimarisha utekelezaji wa masuala ya Jinsia katika utumishi wa Umma. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza nchini imewezesha kuandaliwa kwa mkakati wa uingizwaji wa masuala ya Jinsia wa Jeshi hilo unaozingatia kundi la wafungwa wanaohudumiwa.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeratibu Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Anayeishi kijijini ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe
15 Oktoba. Kwa Mwaka 2023, Wizara kwa kushirikiana na Mkoa wa Arusha pamoja na wadau wengine ilishiriki maadhimisho haya yaliyofanyikia Kata ya Levolosi (Wilaya ya Arusha, Mkoani Arusha). Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa ni “Wezesha Wanawake wanaoishi kijijini: Kwa uhakika wa Chakula, Lishe na Uendelevu wa Familia”. Vilevile, maadhimisho hayo

yaliambatana na Kongamano la wanawake wanaoishi kijijini lililobeba ujumbe wa umiliki wa ardhi, mirathi na Maadili kwa vijana. Mwanamke anaeishi kijijini amebeba taswira pana ya uchumi wa nchi yetu ambao kwa kiasi kikubwa unategemea Kilimo na shughuli nyingine kama ufugaji, uvuvi, uchimbaji ambazo hufanyika katika maeneo ya vijijini.
Mheshimiwa Spika, jumla ya Wanawake 1,600 walifikiwa katika maadhimisho haya kwa Wilaya ya Arusha. Aidha, maadhimisho haya yalifanyika Mikoa yote hapa nchini ambapo kila Mkoa uliadhimisha siku hii kwa kushirikiana na Wadau waliopo katika Mkoa husika. Nichukue fursa hii, kuisihi jamii na wananchi wote kuthamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na wanawake wanaoishi Vijijini katika kuzalisha chakula kinachotosheleza nchini.
Mheshimiwa Spika,
Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani iliyofanyika tarehe 8 Machi 2024 katika mikoa yote nchini. Wizara ilishiriki maadhimisho haya katika wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma. Lengo likiwa ni kujenga hamasa, mshikamano na uwezo wa wanawake kushiriki katika maendeleo ili kufikia usawa wa kijinsia. Katika maadhimisho hayo, wanawake zaidi ya 10,000 wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani walishiriki na walipata huduma mbalimbali zikiwemo za kibenki na nyingine zilizolenga

kuwawezesha kiuchumi. Katika Maadhimisho hayo katika Mkoa wa Dodoma, Mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye nilimwakilisha. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa “Wekeza kwa Wanawake: Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”.
Mheshimiwa Spika,
Wizara imeshiriki Mikutano ya Kimataifa na Kikanda kwa ajili ya kutekeleza masuala ya Jinsia na Uwezeshaji Wanawake ambayo nchi yetu imeridhia. Kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024, Wizara ilishiriki Mkutano wa Women Deliver uliofanyika Nchini Rwanda Kigali Julai, 2023. Pia Tulishiriki katika Mkutano wa 13 wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya wanawake wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (JYM) – The 13th Commonwealth Women’s Affairs Ministerial Meeting (CWAMM) uliofanyika Agosti 2023, Jijini Nassau, Bahamas.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeshiriki katika Mkutano wa Mapitio kipindi cha kati cha utekelezaji wa Programu ya kizazi chenye Usawa (GEF Mid-Point Review) uliofanyika Jijini New York Marekani Septemba, 2023 ambapo nilimuwakilisha Mheshimiwa Rais, ambaye alialikwa kama Mgeni Mahsusi. Aidha kuanzia tarehe 11 mpaka 22 Machi 2024, Wizara tulishiriki Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani uliofanyika Jijini New York, Marekani, ambapo

Mhe. Spika wewe binafsi ulishiriki Pamoja nasi kwa nafasi yako ya Rais wa Mabunge ya Dunia.​
Mheshimiwa Spika, pamoja na kutekeleza matakwa ya ushiriki wa nchi katika mikutano hii, ushiriki wetu umekuwa na manufaa mengi ikiwemo kujifunza kutoka kwa nchi wanachama masuala yanayohusu wanawake na uwezeshaji kijinsia na hatimaye kuongeza uzoefu wa nchi katika masuala haya.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu na kumuendeleza kielimu ili kuweza kujikomboa kiuchumi na kimaisha, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na wadau wa maendeleo imeendelea kutekeleza mikakati ya kumuendeleza mtoto wa kike kupitia programu mbalimbali, zikiwemo integrated training for entrepreneurship promotion (INTEP), ambapo jumla ya wanufaika 2,101 (KE 1483, ME 618) walinufaika. Aidha, uhamasishaji wa wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali wakiwemo wasichana waliokatisha masomo ya Sekondari ulifanyika ambapo wasichana 3,022 waliandikishwa kuendelea Shule ya Sekondari kwa njia mbadala.
Mheshimiwa Spika, kupitia ufadhili wa masomo ya sayansi na hisabati kwa wasichana (STEM), wasichana 21,991 kati ya 46,455 walichaguliwa kusoma tahasusi za sayansi na hisabati. vilevile, kupitia Programu ya Samia Scholarship jumla wasichana 417 kati ya 1,025

wamepewa ufadhili kusoma masomo ya sayansi katika vyuo mbalimbali. Aidha, Uwekezaji mkubwa wa Serikali katika sekta ya Elimu hususan mikakati inayogusa kumuendeleza mtoto wa kike imewezesha uwepo wa uwiano wa 1:1 katika uandikishaji wa watoto wa kike na kiume katika Elimu ya Msingi. Hii ni hatua kubwa katika safari ya kumkomboa mtoto wa kike. Kwa kuzingatia umuhimu huo, Wizara ya Elimu kwa kushirikiana Wizara za Kisekta ilifanikisha maadhimisho ya kitaifa ya wanawake na wasichana katika sayansi yenye lengo la kuimarisha na kuhamasisha ushiriki wa wanawake na wasichana katika masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu. Jumla ya wanawake na wasichana 1,500 walishiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika Februari, 2024.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa michezo na utamaduni katika kuchangamsha mwili, kuleta furaha, kuimarisha Afya, kutoa fursa za Ajira, na hali kadhalika kuitangaza nchi kimichezo na kitamaduni, Wizara kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya Michezo na Utamaduni Pamoja Wizara nyingine za Kisekta na wadau wengine wa michezo imeendelea kuhamasisha ushiriki wa wanawake na wasichana katika michezo.
Mheshimiwa Spika, kupitia jitihada za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza ushiriki wa michezo kwa makundi mbalimbali nchini, yakiwemo ya wanawake na wasichana, hivi

karibuni tumeshuhudia Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa miguu “Twiga Stars” kufuzu kucheza mashindano ya WAFCON yanayotarajiwa kufanyika Juni, 2024 nchini Morocco. Vilevile, Timu ya Wavu ya KOROSHO Queens ya Mkoani Mtwara inayodhaminiwa na Bodi ya Korosho Tanzania walitwaa ubingwa wa Mashindano ya Wavu ya ukanda wa Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Rwanda mwezi Agosti, 2023. Wizara itaendelea kuhamasisha ushiriki wa Wanawake kwenye michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa shule za michezo mahsusi kwa wasichana ili kuzalisha vipaji na ajira nchini.
Mheshimiwa Spika, wakati ninapohitimisha katika eneo hili la usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi, napenda kulitaarifu Bunge lako tukufu kwamba, jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameiweka Nchi yetu katika nafasi nzuri Kimataifa katika utekelezaji wa usawa wa jinsia kwa vitendo katika nyanja zote. Hivyo, Bunge lako tukufu, watumishi wote, Wadau wa Maendeleo, jamii kwa ujumla, na kwa upekee WANAWAKE WOTE hatuna budi kumpongeza na kumuunga mkono katika jitihada hizi kwa kuendelea kujenga uelewa na fursa kwa mafanikio zaidi hapa nchini.

ENEO LA 6: URATIBU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI.
Mheshimiwa Spika, usajili, uratibu na ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali unalenga kuweka mazingira wezeshi kwa mashirika hayo kuendelea kutoa michango yao katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla kupitia miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Kilimo, Afya, Mazingira, Maji, Elimu, Jinsia na Utawala Bora. Aidha, Usajili na uratibu huu unafanywa kwa kuzingatia Sheria ya Mashiriki Yasio ya serikali, Sura ya 56. Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024 Wizara imesajili jumla ya Mashirika 1,028 na kufanya jumla ya mashirika yote yaliyosajiliwa kufikia 10,538. Kati ya Mashirika yaliyosajiliwa katika kipindi hiki, Mashirika ya Kimataifa ni 43, Kitaifa ni 937, Kimkoa ni 29 na Kiwilaya Mashirika 19.
Mheshimiwa Spika, kuhusu ufuatiliaji, Wizara kwa kushirikiana na Wasajili Wasaidizi wa Mikoa na Halmashauri imeendelea kufanya ufuatiliaji wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kubaini kama wanatekeleza kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na pia matumizi sahihi ya fedha kwa kuzingatia malengo ya kusajiliwa. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili 2024, jumla ya Mashirika 1,124 yamefuatiliwa kati ya mashirika yote (10,538). Aidha, uchaguzi wa mashirika haya yanayofuatiliwa hufanyika kulingana na afua ambazo ni kipaumbele cha mwaka huo.

Mheshimiwa Spika, katika ufuatiliaji huo Mashirika mengi yalibainika kutekeleza kazi zao kwa kuzingatia sheria. Vilevile, miradi ya kisekta iliyotekelezwa imeinufaisha jamii mathalani ujenzi wa vyoo, kusaidia watu wenye ulemavu (kuimarisha utengamavu), kuwajengea uwezo walimu wa shule namna ya kuwahudumia watoto wenye ulemavu, kuwezesha makundi mbalimbali kiuchumi (kutoa elimu ya ufundi wa cherehani, kuwapatia wananchi mifugo kama ngo’mbe wa maziwa), kuchimba visima virefu vya maji; kuwezesha uundwaji wa mabaraza ya watoto na kuwezesha watoto kushiriki Baraza la Watoto Taifa. Vilevile, umefanyika uwezeshaji wa mtoto mmoja kushiriki kwenye Mkutano wa Dunia wa Watoto uliofanyika nchini Marekani.
Mheshimiwa Spika, aidha, Mashirika 775 kati ya 1,124 yalibainika kuwa na mapungufu yakiwemo, kutowasilisha kwa wakati ripoti za mwaka kuhusu kazi zao na kutokulipa ada za usajili za mwaka. Wizara kupitia Ofisi ya Msajili, ilitoa onyo kwao na kuwataka kuzingatia matakwa ya kisheria.
Mheshimiwa Spika, Katika suala la Uratibu, Wizara inaratibu shughuli mbalimbali zikiwemo za mikataba ya ufadhili kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mujibu wa kanuni namba 609 ya Mwaka 2018 inayoweka misingi ya uwazi na uwajibikaji wa fedha za wafadhili. Katika mwaka 2023/24, Wizara imetoa vibali vya mikataba 316

yenye thamani ya Shilingi Bilioni 377 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kisekta ikiwemo afya, elimu, mazingira, kilimo, maji, haki za binadamu na utawala bora. Nyingine ni uboreshaji wa miundo mbinu, uwezeshaji wa jamii na ulinzi wa jamii. Kabla ya kutoa vibali vya mikataba kusainiwa, ofisi ya usajili inalazimika kujiridhisha juu ya mfadhili anayetoa fedha na pia mpango wa matumizi ya fedha hizo kwa mashirika.
Mheshimiwa Spika, katika kufanya ufuatiliaji na uratibu kuwa rahisi pamoja na kuongeza uwazi wa kazi za mashirika yasiyo ya kiserikali, Wizara imeboresha Mfumo wa Kielektroniki wa Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuongeza sehemu ya Ramani ya Utambuzi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Ramani ya utambuzi imelenga kuwezesha wadau, Taasisi za Serikali na Jamii kwa ujumla kupata taarifa za Mashirika haya kwa urahisi mahali popote walipo.
Mheshimiwa Spika, mfumo huu ulizinduliwa na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wakati wa Mkutano wa Jukwaa la mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali lililofanyika jijini Dodoma tarehe 05 Oktoba, 2023. Hadi kufikia Aprili 2024 jumla ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 10,538 yameshatambuliwa kwenye ramani na tayari yamewekewa taarifa kuanzia ngazi ya kata.

Mheshimiwa Spika, katika hali ya kuufahamisha umma na Wadau wa Maendeleo juu ya mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali; Kila Mwaka Wizara inaandaa taarifa ya mchango wa Mashirika hayo katika Maendeleo ya Taifa. Kwa mwaka 2022 Wizara ilikamilisha taarifa hii na tarehe 03 – 05 Oktoba 2023, Wakati wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali taarifa hii ilisambazwa kwa wadau mbalimbali yakiwemo Mashirika yenyewe, Wadau wa Maendeleo na Taasisi binafsi.
Mheshimiwa Spika, aidha, taarifa hiyo imebainisha kuwa, katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2022, jumla ya Mashirika 1,257 yaliyowasilisha taarifa zao yalipokea kiasi shilingi 2,249,244,846,280/= kutoka vyanzo mbalimbali vya fedha. Kati ya fedha hizo Shilingi 1,959,334,118,380/= zilitumika katika utekelezaji wa miradi kwenye afua za mazingira, afya, uwezeshaji jamii, ulinzi wa jamii, kilimo, elimu, utawala bora, maji, haki za binadamu na jinsia na kiasi cha shilingi 289,910,727,900/= zilitumika katika kulipa posho na mishahara, kodi za ujuzi, kodi za mishahara, michango katika Hifadhi ya Jamii na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Mheshimiwa Spika, pamoja na manufaa ya ujumla kwa jamii katika Nyanja tofauti ambazo nimeelezea hapo juu, vilevile kazi na huduma za mashirika haya zimeweza kutoa ajira kwa jumla ya watu 9,974 ambapo, kati ya hao Watanzania ni

9,818 na Wageni 156. Manufaa Mengine ni kuchangia katika pato la Taifa kwa kulipa Kodi na michango mbalimbali kwa mujibu wa sheria.
Mheshimiwa Spika, pamoja na taarifa ya jumla ya mchango wa mashirika yasiyo ya Serikali ambayo hutolewa kila Mwaka, katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2023, Wizara kwa Kushirikiana na Mtandao wa TAWASANET chini ya Wizara ya Maji, imeandaa Taarifa ya Mwaka ya Mapitio ya Utekelezaji Katika Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira kwa kuangalia mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Sekta ya Maji. Taarifa hiyo ambayo iliwasilishwa kwa Wadau wa Maendeleo ya Sekta ya Maji wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji tarehe 16 - 22 Machi 2024, imeainisha mchango wa asasi za kiraia katika sekta hii kwa mwaka 2022 na 2023 ambapo, mchango umekuwa jumla shilingi 63,311,771,943, ambazo zilitumika katika kutekeleza wa miradi ya maji.
Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) inaratibu Majukwaa ya Mashirika Yasio Ya serikali kila Mwaka katika Ngazi zote (Wilaya, Mikoa, Taifa). Lengo la Majukwaa haya ni kuwezesha majadiliano kati ya mashirika, Serikali na wadau wa maendeleo kuhusu ukuaji na maendeleo ya sekta. Aidha, wakati wa Majukwaa hayo, shughuli mbalimbali za kijamii hufanyika kama sehemu ya maadhimisho zikiwemo mfano; uchangiaji wa damu na upandaji

wa miti. Katika kipindi cha mwaka 2023/24, majukwaa katika ngazi zote yalifanyika likiwemo lile la Ngazi ya Taifa lililofanyika tarehe 03 – 05 Oktoba 2023 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, jumla ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2,427 yalishiriki katika Jukwaa la Taifa na Kupitia jukwaa hilo; jumla ya chupa 165 za Damu zilitolewa na washiriki kama mchango kwa wahitaji, vilevile upandaji wa miti 300 katika shule ya sekondari ya Ilazo na kutoa mahitaji mbalimbali kwa Watoto 80 wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima cha Matumaini kilichopo Mihuji Dodoma.
Mhe Spika Nichukue fursa hii, kuipongeza Mikoa na Halmashauri zote zilizojitokeza kuratibu majukwaa katika ngazi zao kwani majukwaa hayo yanaimarisha uratibu wa pamoja na ushirikiano na Mashirika hayo kuanzia ngazi za msingi hadi Taifa. Aidha, natoa rai kwa Mikoa kuendelea kuratibu mikutano hiyo muhimu kwa maendeleo ya sekta kwa mwaka 2024.
Mheshimiwa Spika
, Wizara inaratibu uendeshaji wa Bodi inayosimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Sura ya 56 kwa kufanya vikao kila robo. Lengo la vikao hivi ni kujadili, kushauri na kutoa maamuzi kuhusu uendeshaji wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya

Kiserikali. Katika mwaka 2023/24 Vikao vya robo mbili za kwanza vilifanyika tarehe 25 Oktoba 2023 na tarehe 14 Machi, 2024 ambapo, kupitia vikao hivyo, wajumbe wa Bodi walitoa ushauri na kuelekeza Wizara na Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) kufanya uchaguzi wa wajumbe wa NaCoNGO ifikapo Juni, 2024. Aidha, vikao hivyo viliyafutia usajili Mashirika 15 kutokana na kushindwa kujiendesha.
Naipongeza Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kusimamia utekelezaji wa Sheria na Kanuni zinazosimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini. Aidha, natoa rai kwa Mikoa na Halmashauri kutoa ushirikiano katika kufanya Uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa maendeleo ya sekta.
Mheshimiwa Spika
, kwa vile shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hufanyika katika sehemu zote mbili za Muungano, kwa maana ya kwamba baadhi ya Mashirika yanayosajiliwa Bara hufanya kazi Zanzibar na pia yaliyosajiliwa Zanzibar hufanya kazi pia Bara. Wizara yangu inafanya kazi kwa karibu na kwa ushirikiano mkubwa na Wizara ya Maendeleo Zanzibar katika mambo mbalimbali ya Maendeleo na Ustawi wa Jamii, lakini pia na Ofisi ya Rais- TAMISEMI Zanzibar katika suala la usimamizi wa usajili, uratibu na ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kupitia ofisi ya Msajili Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, ushirikiano huu hufanyika kwa kubadilishana taarifa, uzoefu na utaalam baina ya watendaji wa Wizara hizi, na hasa katika uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Ushirikiano huu pia unalenga kuendeleza na kuimarisha Muungano wetu. Aidha, tarehe 17 Februari, 2024 Idara ya Msajili kutoka Wizarani kwangu na Ofisi ya Msajili Zanzibar zimefanya kikao cha mashirikiano ambapo pamoja na masuala mengine kiliazimia kuboresha uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ikiwa ni pamoja na kuainisha Mashirika yatakayoshiriki katika utoaji wa elimu ya mpiga kura na usimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 pamoja na kuanza maandalizi ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, 2024 linalotarajiwa kufanyika mwezi Septemba, 2024, Tanzania Bara.
ENEO LA 7: URATIBU WA MPANGO KAZI WA TAIFA WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO (MTAKUWWA).
Mheshimiwa Spika,
Wizara yangu imeendelea na jukumu la kuratibu utekelezaji wa Mpango wa kupunguza/kuondoa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA-I) wa Mwaka 2017/18 – 2021/22). Mpango huu, ulilenga kuimarisha uchumi wa kaya pamoja na kuimarisha huduma za msaada wa waathirika wa vitendo vya ukatili.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mapambano dhidi ya Ukatili ni Suala Mtambuka na endelevu, Mpango huu wa kwanza (MTAKUWWA-I) uliandaliwa kwa kushirikiana na Wizara nyingine za Kisekta, pamoja na wadau wa Maendeleo. Utekelezaji wa MTAKUWWA katika kupunguza au kumaliza ukatili ulizingatia takwimu za ukatili za ujumla zilizowasilishwa na Tanzania Demographic Health and Malaria Indicator Survey ya mwaka 2022, ambayo ilionesha kiasi cha ukatili wa kimwili kwa wanawake kuwa ni asilimia 40, na ukatili wa kingono kuwa ni asilimia 27, na ule unaotokana na ukeketaji kuwa ni asilimia 10.
Mheshimiwa Spika, wakati utekelezaji wa MTAKUWWA-I umeanza, hapakuwa na takwimu sahihi za ukatili dhidi ya watoto katika maeneo yote matatu. Aidha, napenda kutoa taarifa kwamba, sasa hivi Wizara kwa kushirikiana na wadau wa kisekta tunafanya utafiti katika mikoa yote ya Tanzania bara na pia Zanzibar kupitia Wizara husika ili kubaini takwimu halisi za ukatili dhidi ya Watoto. Utafiti huu umefikia hatua nzuri na upo karibu kukamilika hivyo, itasadia kupata takwimu halisi za ukatili dhidi ya Watoto ambazo tutaziwasilisha kwa Umma na Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Takwimu za ukatili zlizowasilishwa katika taarifa ya TDHMIS ya mwaka 2022 kama kipimo cha utekelezaji wa MTAKUWWA-I, Tathmini iliyofanyika Oktoba 2022 imeonesha kupungua kwa ukatili wa kimwili kwa wanawake kutoka asilimia 40 mwaka 2015 hadi asilimia 27 mwaka 2022, na ukatili wa kingono umepungua kutoka asilimia 17 mwaka 2015 hadi asilimia 12 mwaka 2022. Aidha, vitendo vya ukeketaji vimepungua kutoka asilimia 10 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 8 mwaka 2022.
Mheshimiwa Spika, matokeo haya ya kupungua kwa ukatili, yanatokana na juhudi za ushirikiano zilizofanyika kati ya Wizara yangu na Wizara nyingine pamoja na vikundi vya kijamii vinavyopambana na ukatili na wadau wa maendeleo kupitia MTAKUWWA-I. Ili kuendeleza juhudi dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa Kisekta, imeandaa Mpango Kazi wa Taifa Awamu ya Pili wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA-II) kwa kipindi cha Mwaka 2024/25 – 2028/29) ambao umezinduliwa tarehe 15 Mei, 2024.
Mheshimiwa Spika, mpango huu umeboreshwa kwa kuzingatia kuimarisha maeneo yenye upungufu ambayo yamebainika katika utekelezaji wa MTAKUWWA-I. Hivyo, MTAKUWWA-II imepanua wigo wa washiriki katika utekelezaji ikiwemo Jamii yenyewe kwa Ujumla. Aidha,

umeweka malengo ya kupunguza ukatili wa kimwili kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia 14, na ukatili wa kingono kutoka asilimia 12 hadi kufikia asilimia 6 na hali kadhalika kupunguza vitendo vya ukeketaji kutoka asilimia 8 hadi kufikia asilimia 2 itakapofika mwaka 2028/29.
Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha Malengo haya yanafikiwa na ikiwezekana kabla ya muda uliowekwa au kumaliza kabisa, Serikali kwa kushirikiana na wadau itatekeleza afua zinazolenga kumaliza changamoto zinazosabisha ukatili zikiwemo; kuimarisha uchumi wa kaya ikiwemo kuendelea kutoa mikopo yenye masharti nafuu na kuweka mazingira Rafiki ya kiuchumi, kutoa elimu kuhusiana na mila na desturi zenye madhara na kuimarisha mila zenye matokeo chanya, kuimarisha ulinzi wa mwanamke na mtoto katika maeneo ya umma na katika mitandao na pia kuongeza vituo vya kutolea huduma kwa wahanga wa ukatili kama vile nyumba salama na vituo vya mkono kwa mkono.
Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha Mpango huu, na hatimaye kumaliza suala la ukatili, ni muhimu kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kila mmoja kutambua wajibu wake. Hivyo, nitumie nafasi hii, kutoa Rai kwa makundi mbalimbali kushiriki utekelezaji wa mpango huu kama ilivyoainishwa kwa kila kundi. Aidha, niwaombe Waheshimiwa Mawaziri kuubeba mpango huu na kuujumuisha katika Mipango na Bajeti ya Wizara zenu. Vilevile, nawaomba

Waheshimiwa Wabunge kufuatilia utekelezaji wake katika majimbo yenu kupitia vikao vya halmashauri ambavyo nyie ni wajumbe au viongozi kuelekea mabaraza ya waheshimiwa madiwani.
  • UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapo awali, Wizara inaendelea kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zilizo chini yake ambazo ni Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Arusha na Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Kijitonyama Dar es Salaam.
Mheshimiwa Spika, Taasisi hizi zina jukumu kubwa la kutoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kwa ngazi za Cheti, Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili. Aidha, majukumu mengine ya Taasisi hizi ni pamoja na kufanya utafiti na kutoa huduma ya ushauri elekezi katika nyanja zinazo shabihiana na taaluma wanazotoa.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa mafunzo 2023/24, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru imeongeza idadi ya udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 2,918 (Me 983 na Ke 1,935) waliodahiliwa mwaka wa masomo 2022/23 hadi kufikia wanafunzi 3,019 (Me 1,052 na Ke 1,967) katika mwaka 2023/24 sawa na ongezeko la 3.5%. Aidha, kwa mwaka 2023/24, jumla ya wanafunzi 1,651 (Me 575 na Ke 1,076) walihitimu katika fani

na ngazi mbalimbali ikilinganishwa na wanafunzi 1,619 (Me 498 na Ke 1,121) waliohitimu 2022/23 kama inavyoonekana katika Jedwali Na.7. Taasisi inaendelea kuboresha mafunzo na kutoa wahitimu wenye uwezo. Ili kufikia lengo hili, Taasisi katika mwaka wa masomo 2023/2024 imeanzisha jumla ya mitaala mipya 12.
Jedwali Na.7 Taarifa za udahili na wahitimu kwa kipindi cha 2022/23 na 2023/24 katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru.
2022/23
Udahili
Wahitimu
Me​
Ke​
Me
Ke
983​
1,935​
498
1,121​
Jumla​
2,918
1,619
2023/24
1,052​
1,967​
575
1,076​
Jumla​
3,019
1,651
Ongezeko
3.4%
3.5%
Mheshimiwa Spika, katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii, udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2023/24, umeongezeka kufikia 3,039 (Me 904 na Ke 2,135) ikilinganishwa na wanafunzi 2,966 (Me 1,102 na Ke 1,864) mwaka 2022/23
ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 73 sawa na 2.5%. Aidha, Katika mwaka wa masomo 2023/24 jumla ya wanafunzi 2,829 (Me 1,016 na Ke 1,813) walihitimu ikilinganishwa na wanafunzi 3,075 (Me 880 na Ke 2,195) waliohitimu mwaka 2022/23 ikiwa ni upungufu wa wanafunzi 246 sawa na 8% kama inavyooneshwa katika jedwali Na.8 hapo chini.

Jedwali Na.8: Taasisi ya Ustawi wa Jamii, udahili na Wahitimu kwa Kipindi cha 2022/23 na 2023/24
2022/23
Udahili
Wahitimu
Me​
Ke​
Me​
Ke​
1,1021,864
880​
2,195​
Jumla​
2,966
3,075
2023/24
904​
2,1351,016
1,813​
Jumla​
3,039
2,829
Ongezeko
(Upungufu)
2.5%
(8 %)
Mheshimiwa Spika, Aidha, katika hali ya kuimarisha mifumo ya utoaji wa mafunzo, Taasisi hizi zimeendelea kuboresha mitaala ya kufundishia pamoja na kuanzisha programu mpya zinazoendana na mahitaji ya soko la ajira. Baadhi ya mitaala mipya iliyoandaliwa na kuboreshwa na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru inahusu kazi za jamii, watoto na vijana katika ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada ambazo ni; Taaluma ya Saikolojia; Ukuzaji Ujasiriamali, Utatuzi Mbadala wa Migogoro Mahali pa Kazi. Mitaala hii imeshawasilishwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa ajili ya kupata ithibati. Taasisi inatarajia kudahili wanafunzi katika programu hizi kwa mwaka wa masomo 2024/25.
Mheshimiwa Spika, Taasisi hizi pia hutoa mafunzo ya muda mrefu, kutoa mchango na kushiriki katika masuala mbalimbali ya jamii. Katika eneo hili, Taasisi ya Tengeru ilitoa mafunzo ya elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa maafisa wa

polisi na maafisa wa dawati la jinsia 954 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Pia, ilitoa mafunzo ya uongozi wa kimkakati kwa watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Viwanda Zanzibar. Mafunzo mengine yalihusu uongozi na utawala bora kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Aidha, kwa upande wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, mafunzo ya muda mfupi yaliyotolewa ni pamoja na; mafunzo ya msaada wa kisaikolojia kwa wanafunzi na Jamii, mafunzo kwa wanafunzi yaliyohusu ukatili wa kijinsia, mahusiano, mawasiliano na stadi za maisha.
Mheshimiwa Spika, kama ilivyo katika vyuo vyote vya Maendeleo ya Jamii, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, pia inatekeleza programu ya kuchochea na kuendeleza ubunifu (innovation) miongoni mwa wanafunzi kupitia Kituo cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidijitali (Jamii Outreach Digital Innovation Center – JODIC). Kituo hiki kinatumika kuratibu utekelezaji wa programu za ubunifu wa kidijitali, ushirikishwaji jamii na uanagenzi. Kupitia Programu hii, Taasisi imetekeleza kazi zifuatazo:-

Kushiriki katika kuhamasisha na kuelimisha jamii ya wakazi wanaoishi ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuhama kwa hiari kwenda katika maeneo yaliyotengwa na Serikali (Msomera, Saunyi na Kitwai) pamoja na maeneo

mengine watakayoamua wenyewe. Katika zoezi hili, jumla ya kaya 807 zilifikiwa na kaya zipatazo 306 zilijiandikisha tayari kwa kuhama kwa hiari;
Kushiriki katika zoezi la kuwabainisha wahanga wa maporomoko ya matope yaliyosababishwa na mvua yaliyotokea Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara tarehe 03 -12 Desemba, 2023 ambapo jumla ya wahanga 1,291 katika Kaya 491 walibainishwa. Kati ya kaya hizo, wahanga 89 makazi yao yalikuwa yameharibiwa na mafuriko ambapo wahanga wote waliweza kupatiwa huduma ya ushauri kuhusu mpango wa makazi ya muda mfupi na muda mrefu. Vilevile, wahanga walipatiwa huduma ya hali na mali pamoja na msaada kisaikolojia.
Mheshimiwa Spika, Kama zilivyo Wizara nyingine, Wizara yangu na Taasisi zake inao wajibu wa kushiriki katika masuala ya jamii na majanga mbalimbali kupitia wataalamu wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii. Wizara na Taasisi zake hizi mbili (2) pamoja na vyuo vingine vya kati ilishiriki kutoa huduma kwa wahanga wa majanga yaliyotokea katika maeneo mbalimbali. Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii walitoa huduma ya kuhamasisha na kuelimisha jamii ya wakazi wanaoishi ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuhama kwa hiari kwenda katika maeneo yaliyotengwa na Serikali (Msomera, Saunyi na Kitwai) pamoja na maeneo mengine watakayoamua wenyewe. Aidha, Wataalamu wa

Ustawi wa Jamii walitoa huduma ya elimu, ushauri, msaada wa kisaikolojia, afya ya akili na namna bora ya kukabiliana na mazingira mapya.
Mheshimiwa Spika, vilevile, wataalamu hawa walishiriki katika zoezi la kuwabainisha wahanga wa mafuriko ya matope yaliyotokea Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara Pamoja na kuwashauri na kuwaunganisha na ndugu/jamaa zao ili kupata makazi ya muda mfupi na baadae makazi ya muda mrefu. Aidha, wahanga hawa walipatiwa pia huduma ya ushauri nasaha, saikolojia na afya ya akili. Huduma kama hizi, tulizitoa pia katika kama maeneo mengine ambayo yalitokea majanga mbalimbali ikiwemo Mikoa ya Pwani, Morogoro, Mbeya, Dodoma na Tanga. Wizara yangu itaendelea kushiriki na kutoa huduma pale majanga yatakapo tokea.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Jamii ina elimu juu ya majanga, ikiwa ni pamoja kujikinga na athari zake na kuchukua tahadhari, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru inaandaa mtaala unaolenga kutoa taaluma juu ya mabadiliko ya tabianchi, madhara yake na jinsi ya kukabiliana nayo. Aidha, elimu hiyo imejumuishwa na itaendelea kutolewa wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na Kusimamia Maendeleo Ngazi ya Msingi wa mwaka 2022/23 - 2025/26 (Bottom Up).

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha wana Taaluma wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii wanapata nafasi ya kubadilishana uzoefu pamoja na kufanya tathmini ya utendaji wa kazi zao, Taasisi zote mbili (2) kwa kushirikiana na Vyama vya Taaluma hizi, huandaa makongamano kila mwaka ambayo idadi kubwa ya wataalamu hushiriki. Kwa Mwaka wa 2023/2024 Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru iliandaa kongamano la mwaka ambalo liliambatana na maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo mwaka 1963. Kongamano hilo pamoja na maadhimisho hayo, yalihudhuriwa na Mhe. Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu ambae pia alikuwa Mgeni Maalum. Kupitia maadhimisho hayo, Taasisi ilifanya shughuli mbalimbali zikiwemo; uzinduzi wa kitabu cha maendeleo ya jamii (Community Development Handbook) kitakachotumika kama rejeo kwa wadau, wakufunzi, wahadhiri na wataalamu wa maendeleo ya jamii nchini; uzinduzi wa Mfuko wa Udhamini wa Masomo (Maendeleo Scholarship Fund) kwa wanafunzi ambao watapata changamoto ya kujilipia masomo baada ya kupata usajili na kuanza masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kufiwa na wazazi/wategemezi; na shughuli nyingine ni pamoja na upandaji wa miti 500 katika vyanzo vya maji na maeneo ya Taasisi.
Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Ustawi wa Jamii nayo, iliadhimisha kumbukumbu ya

miaka 50 tangu kuanzishwa kwake ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maadhimisho hayo yalitanguliwa na shughuli za utoaji wa huduma za ustawi wa jamii katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Geita, Songwe, Kagera na Dar es Salaam ambapo jumla ya watu 3,066 walipatiwa huduma hizo. Maadhimisho hayo yalihitimishwa na kongamano lililohudhuriwa na washiriki zaidi ya mia nane (800) ambapo mada kuu iliyojadiliwa ilihusu “Malezi na makuzi bora ya watoto na vijana ni tija kwa Taifa”.
Mheshimiwa Spika, sambamba na makongamano na maadhimisho hayo, Taasisi pia ziliandaa na kuratibu mabonanza ya michezo, makala maalum (Documentary) ya miaka 60 ya Taasisi ya Tengeru na Ustawi wa Jamii ambapo viongozi wakuu wa Kitaifa walihojiwa. Makala hii imerushwa katika kituo cha luninga cha TBC na nakala 250 za toleo la miaka 60 ya Taasisi ya Tengeru zimechapishwa na kusambazwa kwa wadau mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, Taasisi kupitia Kituo cha Kitaifa cha Utafiti na Uhifadhi wa Machapisho ya Wanawake kiliandaa Kongamano la Kitaifa la Wanawake kwa kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT). Kongamano hilo lilifanyika jijini Dodoma tarehe 07 Machi, 2024 na kufanikiwa kuwafikia wadau
300. Kauli mbiu ya kongamano kwa mwaka 2024

ilihusu “Usawa wa kiuchumi: Kuwawezesha wanawake kuifikia jamii yaani “Economic Equality: Empowering Women, Enriching Societies". Katika kongamano hilo kituo kilifanikiwa kukusanya tafiti 12 na mawazo bunifu manne (4) yaliyohusu masuala ya kuchochea na kukuza usawa wa kiuchumi kwa kuwawezesha wanawake kuimarika kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, katika eneo la utafiti, ushauri elekezi na maandiko, Taasisi zote mbili (2) zimeendelea kutekeleza majukumu haya, kama ifuatavyo:
Kutoa ushauri elekezi juu ya kuandaa Mpango Mkakati wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Mkuranga na Shirika la Christian Social Services Commission (CSSC) Tanzania;
Kutoa ushauri elekezi juu ya kuboresha upatikanaji wa haki katika masuala yanayohusiana na familia kupitia njia mbadala za utatuzi wa migogoro katika shirika la Kilimanjaro Women Information Exchange and Community Organization (KWIECO) mkoani Kilimanjaro; na
Kuchapisha makala mbili (2) za kitaaluma pamoja na kutoa matokeo ya tafiti mbili (2) ambazo ni kuchunguza kanuni, maadili na mbinu zinazowalinda wanawake dhidi ya unyanyasaji nchini.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi, Serikali kupitia Wizara imepeleka fedha katika Taasisi na vyuo kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na hosteli. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili 2024, Taasisi ya Maendeleo Tengeru imepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa kumbi mbili pacha za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,008 pamoja na hosteli ya wasichana yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi
568. Aidha, kiasi cha Shilingi Milioni 500 zilipokelewa katika Chuo cha Maendeleo Monduli kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hosteli ya wasichana ambayo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 576 kwa wakati mmoja.
Mheshimiwa Spika, kwa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, jumla ya shilingi 259,116,083.80 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Hosteli katika kampasi ya Dar es salaam. Aidha, Taasisi imepokea kiasi cha shilingi 28,116,083.80 kwa ya ujenzi wa ofisi ya Muangalizi wa hosteli (warden), stoo, na chumba cha kufulia katika chuo cha Ustawi Kisangara.
Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kusimamia Taasisi hizi pamoja na vyuo vya kati ili kuhakikisha malengo na matarajio ya serikali yanafikiwa. Nichukue nafasi hii kuwapongeza Wenyeviti wa Bodi za Taasisi hizi pamoja na

wajumbe wote wa Bodi kwa kazi yao kubwa na nzuri ya kusimamia vyuo hivi.
  • UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi, Wizara imeendelea kutekeleza afua mbalimbali za miradi ya maendeleo ikiwemo; utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa, kuimarisha afua za haki na ulinzi wa mtoto pamoja na miradi ya ujenzi na ukarabati wa majengo na miundombinu katika Taasisi na Vyuo vilivyo chini yake. Kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili 2024, Wizara imepokea fedha za ndani za maendeleo kiasi cha Shilingi Bilioni 4.88, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (Shilingi Bilioni 2), utekelezaji wa shughuli za programu ya kizazi chenye usawa (Shilingi Bilioni 2.48) na Mradi wa Huduma za Ustawi wa Jamii (Shilingi Milioni 400).
Mheshimiwa Spika, kati ya fedha za ndani zilizopokelewa Shilingi Bilioni 2 zilitolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru zimepokelewa Shilingi Bilioni 1.5, Chuo cha Maendeleo ya jamii Monduli zimepokelewa Shilingi Milioni 500.
Mheshimiwa Spika, kazi zilizotekelezwa kutokana na fedha hizo ni: Kuanza kazi za awali za ujenzi wa Jengo la Utawala katika Taasisi ya

Maendeleo ya Jamii Tengeru na ujenzi huo unaendelea. Kwa upande wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli, fedha zilizopokelewa zimetumika kuendelea na ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 576 kwa wakati mmoja na ujenzi huo bado unaendelea.
Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kusimamia utoaji wa huduma katika Mahabusu 5 za watoto zilizopo mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Dar es Salaam. Aidha, katika kuboresha huduma katika eneo hili kati ya fedha za ndani zilizopokelewa kiasi cha Shilingi Milioni
400
zimeelekezwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Mahabusu ya watoto Mwanza.
Mheshimiwa spika, kati ya fedha za ndani zilizopokelewa, kiasi cha Shilingi Bilioni
2.48
zimetolewa kwa ajili ya kuratibu na kufanya ufuatiliaji wa uanzishwaji na uendeshwaji wa Madawati ya Jinsia kwenye maeneo ya soko na Taasisi za Elimu ya Juu na ya Kati; kufanya mapitio ya Mwongozo wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi; Kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake; kutoa mafunzo kwa waratibu wa programu yenye Kizazi chenye Usawa katika ngazi za Mikoa na Halmashauri pamoja na mafunzo kwa Wakuu wa Idara ya Sera na Mipango; Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) na kuwezesha ushiriki wa nchi kwenye Mkutano wa mapitio ya

kipindi cha kati cha Utekelezaji wa GEF uliofanyika Septemba 2023 jijini New York 2023.​
Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha afua za kutoa elimu ya malezi chanya kwa watoto katika ngazi zote nchini na kuzuia aina zote za ukatili dhidi ya watoto ikiwemo ukeketaji na ukatili mitandaoni, Wizara imepokea fedha za nje kiasi cha Shilingi Milioni 66 kwa ajili ya kufanya kampeni ya ulinzi na usalama wa mtoto mtandaoni.
VIPAUMBELE VYA WIZARA NA BAJETI YA MAPATO, MATUMIZI YA KAWAIDA NA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2024/25.
Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2024/25, Wizara kupitia Idara na Taasisi zilizo chini yake itatekeleza vipaumbele sita (6) ili kuboresha utoaji wa huduma za maendeleo na ustawi wa jamii. Vipaumbele hivyo ni kama vifuatavyo: -
Kukuza ari ya jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa Ngazi ya Msingi;
Kuratibu afua za kukuza usawa wa kijinsia na kutokomeza vitendo vya ukatili, uwezeshaji wanawake kiuchumi, upatikanaji wa haki, ulinzi na malezi chanya ya watoto;

Kuratibu na kuimarisha utoaji wa huduma za msingi za ustawi wa jamii;
Kutambua, kuratibu na kuendeleza Makundi Maalum wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo;
Kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia katika Taasisi na Vyuo vya Ustawi na Maendeleo ya Jamii; na
Kuimarisha ushiriki na mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa, Wizara kwa mwaka 2024/25 imekadiria kutumia kiasi cha Shilingi 67,905,259,000. Kati ya fedha hizo, Shilingi 47,487,079,000 ni fedha za matumizi ya kawaida ambapo Shilingi 21,650,426,000 ni Fedha za Mishahara na Shillingi 25,836,653,000 ni fedha za uendeshaji wa ofisi. Aidha, Shilingi. 20,418,180,000 ni fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shillingi 18,025,673,000 ni fedha za ndani na Shillingi 2,392.507,000 ni fedha za nje. Baadhi ya maeneo yaliyotengewa fedha kwa mwaka 2024/25 ni pamoja na: -
Katika eneo la kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi (Generation Equality Forum - GEF), kiasi cha shilingi Bilioni 3.2 zimetengwa.

Katika eneo la kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kiasi cha Shilingi Bilioni 3.15 kimetengwa;
Katika eneo la kutambua na kuratibu shughuli za kiuchumi za Makundi Maalum hususan wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo machinga, mama/baba lishe, waendesha bodaboda na bajaji na ma makundi mengine yenye biashara ndogo halali zilizosajiliwa, kiasi cha Shilingi Bilioni 10.5 kimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo yenye masharti nafuu ili kuongeza mitaji na kuboresha shughuli zao za kiuchumi;
Kwenye eneo la huduma za ustawi wa jamii na watoto, kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2 kimetengwa kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa huduma za marekebisho ya tabia kwa watoto waliokinzana na sheria; kufuatilia utoaji wa huduma katika Makao ya Watoto, Vituo vya Kulelea Watoto wadogo Mchana na Watoto Wachanga; Kukarabati Shule ya Maadilisho ya Upanga na Mtwara; na Kuendeleza ujenzi wa Mahabusu ya Watoto Mwanza;
Katika eneo la ustawi wa Wazee wasiojiweza, Shilingi Bilioni 1.06 zimetengwa kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa huduma katika Makazi ya Wazee 13;

Kwenye eneo la Taasisi na Vyuo, kiasi cha Shilingi Bilioni 2 kimetengwa. Fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo na miundombinu katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, na Vyuo vitatu (3) vya Maendeleo ya Jamii vya Uyole, Rungemba na Buhare;
Eneo la Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali limetengewa kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5 kwa ajili ya kusajili na kufanya ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kuandaa Taarifa ya Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mwaka 2024, kuratibu utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (2022/2023 - 2025/2026), na kuratibu vikao vya Bodi na Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali;
Eneo la maendeleo ya jamii limetengewa kiasi cha Shilingi Milioni 826.1 kwa ajili ya kutekeleza Kampeni ya Kitaifa ya Kuamsha Ari ya Jamii kuhusu ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu kwa kutumia teknolojia rahisi na kutekeleza Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na Kusimamia Maendeleo Ngazi ya Msingi wa mwaka 2022/23 - 2025/26 (Bottom Up) katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara; na

Katika eneo la ufuatiliaji na tathmini, kiasi cha Shilingi Milioni 150 kimetengwa. Fedha hizo ni kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa mipango, programu na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Taasisi, Vyuo na Vituo vya Ustawi wa Jamii vilivyo chini ya Wizara.
  • SHUKRANI
Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa ikipata ushirikiano mkubwa kutoka nchi rafiki, Mashirika ya Kimataifa na Sekta mbalimbali zinazosaidia na kuchangia katika huduma za maendeleo na ustawi wa jamii. Aidha, Naomba nitumie fursa hii kuzishukuru Serikali za nchi rafiki zikiwemo; Marekani, Japan, Ufalme wa Uingereza, Ufalme wa Sweden, Jamhuri ya Watu wa China, Ufalme wa Norway, Falme za Nchi za Kiarabu, Italia, Ujerumani, Ubelgiji, Ufaransa, Canada, Ufalme wa Denmark, Ireland, Jamhuri ya Uswisi, Bangladesh na nchi nyingine ambazo zimeendelea kuisaidia Wizara kwa njia mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, ninayashukuru Mashirika na Taasisi za Kimataifa kwa ushirikiano wao waliotoa kwa Wizara ikiwa ni pamoja na: - Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo UNICEF, UNFPA, UN-Women, WHO, UNDP, ILO, IOM, WFP, FAO, UNESCO na UNHCR. Vilevile,
ninashukuru Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), na Jumuiya za Umoja wa Nchi za Ulaya (EU). Pia nayashukuru Mashirika ya

Kimataifa ambayo ni:-Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Mfuko wa Abbott Fund, Global Fund na Hilton Condrad Foundation. Aidha, nazishukuru Taasisi za Kifedha za hapa nchini zinazoshirikiana na Wizara ambapo ni pamoja na Benki za CRDB, NMB, Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Stanbic, Azania, NBC, Equity, Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Akiba Commercial Bank (ACB) na Benki ya Mkombozi na Benki ya Biashara Tanzania.
Mheshimiwa Spika, nayashukuru Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya ndani ya nchi na Mashirika ya Dini kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia uimarishaji wa huduma za maendeleo na ustawi wa jamii. Mashirika hayo ni pamoja na; World Vision, PACT Tanzania, The Aga Khan Foundation, Foundation for Civil Society, HelpAge International, Compassion International, Responsible Organization Tanzania, Both Ends Believing (BEB), Safe Society Platform Tanzania, Children in Crossfire, Care International Tanzania, Railway Children Tanzania, WiLDAF, ICS, TAWLA, TAYOA, LSF, SOS Children’s Village Tanzania, BRAC Maendeleo Tanzania, Plan International - Tanzania, Kivulini, Uongozi wa Mgodi wa Geita, FSDT, WFT, TANLAP,Save the Children, Equality for Growth (EfG), Landesa, CAMFED, CSEMA; REPPSI, Amani Girls Home, Pelum Tanzania, LHRC, Haki Elimu, TWCC, TECDEN, EGPAF,FAGDI, na MEWATA.

Mheshimiwa Spika, nitoe pia shukrani zangu kwa Jumuiya za makundi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanya kazi na Wizara. Jumuiya hizo ni pamoja na: - Baraza la Wazee Tanzania, Chama cha Wazee Wanaume Tanzania, Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Tanzania (CHAMWAPITA), Machifu na Viongozi wa Kimila Tanzania, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Chama Cha Wanawake Wajane Tanzania (CCWWT), Jukwaa la ULINGO, Jumuiya ya Wazazi CCM, Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, TAWIA, Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) na Umoja wa Mama na Baba Lishe Tanzania. Pia naomba nizishukuru Klabu za Mpira wa Miguu Tanzania hususan Yanga, Simba, AZAM na vikundi/kampeni za Kijamii kama (Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii (SMAUJATA), Foundation for Ambassadors of Gender Development Initiatives (FAGDI), Sauti ya Watoto Tanzania (SAWATA) NA MALEZI BORA NETWORK pamoja na vyombo vyote vya habari.
Mheshimiwa Spika, nitoe shukrani zangu pia kwa viongozi na taasisi zetu za dini zikiwemo Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA).

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha utekelezaji wa majukumu yangu nikiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, nimepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi na wafanyakazi wa Wizara. Naomba kumshukuru Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe, Katibu Mkuu na Bw. Amon A. Mpanju, Naibu Katibu Mkuu kwa mchango na ushirikiano wao katika kuwezesha utekelezaji wa majukumu yangu. Aidha, nawashukuru Makamishna, Wasajili, Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wataalam wote wa Wizara kwa utendaji wao mahiri uliowezesha kukamilisha maandalizi ya Hotuba yangu kwa wakati.
Mheshimiwa Spika, kipekee naomba kuwashukuru Bodi na Menejimenti za Taasisi ya Ustawi wa Jamii na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru. Pia, nawashukuru Wakuu wa Vyuo nane
(8) vya Maendeleo ya Jamii kwa ushirikiano wao mzuri unaonirahisishia utekelezaji wa majukumu yangu. Natoa shukrani kwa sekta zote ambazo tunashirikiana nazo katika kutoa huduma za maendeleo na ustawi wa jamii pamoja na wananchi wote kwa ushirikiano wao.
Mheshimiwa Spika, vilevile, kupitia OR – TAMISEMI nawashukuru sana Wakuu wa Mikoa yote, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote na Wataalam wote chini ya Ofisi zao na Wadau wote wa sekta mbalimbali wanao hudumia katika maeneo yao

pamoja na wananchi mmoja mmoja na mitandao yote ya habari za kijamii ambao wamekuwa wakifuatilia na kutoa ushirikiano mkubwa kwenye utekelezaji wa majukumu ya wizara yangu hasa kupambana kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii pia kuishukuru familia yangu, hususan mume wangu mpendwa Wakili Msomi Methusela Gwajima na watoto wetu pamoja na wote ambao wamekuwa sehemu ya familia yetu kwa uvumilivu wao wa kipekee kwa kunitia moyo katika kutekeleza majukumu yangu ya Kitaifa. Aidha, nawashukuru wananchi wote wa Tanzania kwa kuipatia ushirikiano Wizara ninayoisimamia wakati wote wa kutekeleza majukumu yangu na pia kwa wao binafsi kuendelea kupambana kuhakikisha maendeleo na ustawi wa jamii kwa usawa wa jinsia huku wakitumia mawasiliano kupitia simu nilizozisema awali.
  • MAOMBI YA FEDHA KWA KAZI ZILIZOPANGWA KUTEKELEZWA KATIKA MWAKA 2024/25
Makadirio ya Makusanyo ya Maduhuli kwa Mwaka 2024/25
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/25, Wizara imekadiria kukusanya kiasi cha Shilingi 7,040,129,000 kutoka katika vyanzo mbalimbali. Vyanzo hivyo ni pamoja na: Ada za Vyuo vya Maendeleo ya Jamii; Mitaala ya vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii; Ada ya

malazi kwa wanafunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Usajili na Ada za mwaka za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
Matumizi ya Kawaida
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/25, Wizara inakadiria kutumia kiasi cha Shilingi 47,487,079,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi 25,836,653,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Shilingi 21,650,426,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi.
Miradi ya Maendeleo
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa shughuli za maendeleo, Wizara inakadiria kutumia Shilingi 20,418,180,000.00 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 18,025,673,000.00 ni Fedha za Ndani na Shilingi. 2,392,507,000.00 ni Fedha za Nje.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2024/25, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum (Fungu 53) inaomba jumla ya Shilingi 67,905,259,000.00 ili kutekeleza majukumu yake kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Mheshimiwa Spika, Hotuba hii inapatikana pia katika tovuti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum www.jamii.go.tz

Mheshimiwa Spika, Naomba Kutoa Hoja.
 
Back
Top Bottom