Walikua wanaweka uchafu tu
Kule Arusha nilipita juzi.Wala hawajui kinachoendelea.Bado wamejazana kila mahali.Mtaa wa Congo (Majengo) ndo kumekucha.Nadhani kwa vile mji wa kitalii, hawahusiki.Ila likiisha hili lifuate la bodaboda.Nao wajipange.Vinginevyo waanze kusoma PGO.
 
Wanabomoa vibanda vyenu wanaweka vibanda vyao. Mtetezi wenu ndio kashaondoka pambaneni na Hali zenu. Wajanja wameangalia wamejua mnapiga hela maeneo fulani fulani. Wametafuta njia ya kuingia hapo na ndio hio kwamba vibanda vyenu vichafu havifai kuwa hapo ILA vibanda vyao visafi ndio vinastahili! Wewe mlalahoi kibanda chako peleka kijijini kwenu huku tunataka vibanda vya akini tipisi, fishifishi na wajanja wengine wa mjini

Muhimu sana serikali kuhakikisha matajiri, wenye maduka makubwa hawaweki meza zao au kujenga vibanda vyao safi.

Sheria ile ile iliyowatoa wamachinga itumike kwa watu wote bila kujali status zao, upendeleo, rushwa.

Njia za wanaotembea zibaki wazi kwa wanaotembea kwa miguu.
 
Muhimu sana serikali kuhakikisha matajiri, wenye maduka makubwa hawaweki meza zao au kujenga vibanda vyao safi.

Sheria ile ile iliyowatoa wamachinga itumike kwa watu wote bila kujali status zao, upendeleo, rushwa.

Njia za wanaotembea zibaki wazi kwa wanaotembea kwa miguu.
Mnaotembea kwa miguu mnasababisha foleni road
 
Wenzetu walizingatia mazingira ya miji ila pia walizingatia na mazingira ya vipato vya hao wananchi!

Machinga wengi ni graduates kwa sasa, unapomfurumusha eneo analopatia chochote kitu na kumuajiri huwezi unategemea familia yake ya mama na katoto kake pekee wakale wapi?

Wenzetu wanaweka mazingira ila bongo mazingira ni kutupwa Vikindu huko! Ukiangalia wanunuzi wenye access na kariakoo hawawezi kufuata vitu vikindu huko eti kisa bei ya nafuu!

Mazingira ya biashara, kilimo, exports, kodi, tozo muhimu yawe rafiki kwa wafanyabiashara na wakulima wote wakubwa na wadogo.

Hizi sera zinabidi ziwe strategic pia kuwe na join-up thinking.

Wakati wamachinga wanaondolewa barabarani, lazima kuwe na sera za uhakika, endelevu kuhakikisha taifa halizalishi wamachinga wengine wengi.

Kuongeza tozo kunapunguza ajira/kipato kwa wakala wa miamala, bei za mbolea inaongeza vikwazo kwa wakulima.

Hizi sera inabidi ziende kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom