Lutandagula
JF-Expert Member
- Apr 8, 2018
- 1,762
- 2,157
Bao la mkono
Ni Rasmi Sasa!
Tundu Antipass Lissu mwana wa Afrika na mwanademokrasia wa kweli wa Tanzania amepitishwa rasmi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiitangazia Dunia Mwenyekiti wa NEC Jaji Kaijage amesema Lissu ametimiza vigezo vyote na Masharti ya kuwa mgombea Urais kupitia Chadema.
Kulikuwa na hofu kubwa katika nchi kuanzia asubuhi baada ya Mgombea wa Chadema Kuwasili katika ofisi za Tume tangu asubuhi saa 5 Kama Ratiba ilivyoelekeza lakini Time haikumteua kwa wakati kwa kile walichodai bado fomu zake kuhakikiwa
Kwa kadiri muda ulivyokuwa unasogea ndivyo Watanzania walivyokuwa na hofu kwa kile walichodhani Kuna hujuma dhidi ya chaguo Lao .
Taarifa kutoka mikoa kadhaa inasema Mara baada ya kuteuliwa Shangwe za watu zimesikika kutoka sehemu kadhaa zikiwemo za starehe, masokoni na mashuleni huku kwa jiji la DSM watu kadhaa wamesikia wakipiga honi za magari barabarani Kama ishara ya kufurahia kuteuliwa Tundu Lissu ambaye anaonekana ndiye mwenye uwezekano mkubwa wa kushinda nafasi hiyo ya Urais kutokana na kuungwa mkono na Wananchi walio wengi.
[/QUOTe
hii ndo habari ilikuwa inangojewa na wengi, kazi imeanza
Ccm kimekuwa chama cha mashetani.Ipo sehemu ya kumchinjia, hapa peupe sana. Tulieni
Mbona unaandika kwa unyonge kiasi hiki?Hongera Tundu Lissu
Lissu hawezi kutangazwa mshindi wa urais.