Labda mtu atujuze, mwenge ni Nini?na nikwanini unakimbizwa kila mwaka?na unafaida gani kwa taifa?mean kwa Pato la taifa na mwananchi wa kawaida?je usipokimbizwa nchi mzima Nini kitatokea?na je wakifanya kuwasha kwenye siku ya Uhuru tu sehemu ambayo itaadhimishwa ki taifa kutakuwa na dhara lolote?
 
Toka nimeanza kuufahamu huu mwenge na kufatilia umuhimu wake kwakweli sijaona manufaa yake.
Hayo mambi ya kuzindua miradi, wanasiasa wanaizindua wenyewe. Zaidi zaidi kuongeza matendo mauvu tu pale unapolala.
 
Asalaam alaykum,

Wito Sina Nia ya kuchafua serekali. Hivi kwa kipindi hichi cha janga la wimbi la tatu la Covid, Kuna umuhimu gani wa kukimbiza mwenge? Maana naona unaleta mikusanyiko isiyo na ulazima na kuchochea ongezeko la ugonjwa huu. Mfano mzuri niliona Jana mwanza,bmwenge ulilala wilaya ya nyamagana (buhongwa shuleni) kikweli nilisikitika ...
MWENGE Ni shetani linalo ongoza Taifa hili. Mwendazake hakukimbiza MWENGE akafa.
 
Asalaam alaykum,

Wito Sina Nia ya kuchafua serekali. Hivi kwa kipindi hichi cha janga la wimbi la tatu la Covid, Kuna umuhimu gani wa kukimbiza mwenge? Maana naona unaleta mikusanyiko isiyo na ulazima na kuchochea ongezeko la ugonjwa huu. Mfano mzuri niliona Jana mwanza,bmwenge ulilala wilaya ya nyamagana (buhongwa shuleni) kikweli nilisikitika Sana watu walikuwa wengi hakunaa social distance ya mtu na mtu, mask zilikuwa zinatolewa Ila asilimia kubwa walikuwa hawana cause Ni wananchi wa chini, pili kulikuwa na show za wasanii watu walikuwa wanajazana wakiwa wamezunguka kuwashangaa.

Tatu usiku walikesha na disco vumbi usiku kuchaa. Mbaya zaidi kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi na watoto wengine hambao hawajui tahadhari au Kinga kifasaha kuhusu covid. Ni aibu kwa serekali kuu ambayo inajifanya inajali kuhusu wimbi la tatu la covid huku wakiruhusu mwenge uzunguke nchi mzimaa. Shame on you!

Kuna ulazima gani wa kukimbiza mwenge? Na ksma Kuna ulazima kwani wasiuzungushe na magari tu na ukifika wilaya au mkoa unapotakiwa ukalale, ulalee ofisi ya mkuu wa mkoa au wilaya na kuwe na limit ya watu.

Alafu najiuliza, huo mwenge kwa Karne hi unamanufaaa gani kwa taifa?maana naona unahamashisha ulevi, uzizii, ugovi wa familia na watoto kupotea kila utapo lala mahali.mtanisamehe sio muandishi mzuri Ila naomba kuwakilisha.

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
hakuna umuhimu
 
Mwaka jana hakukuwa na Mwenge barabara zisizo za lami huko vijijini hazikufanyiwa hata marekebisho kidogo.
Mwaka huu mwezi wa tano nimepita sehemu huko nikaomba poo.

Kama mwenge tu unafanya tufanye vitu fulani, basi uendelee. Nahisi kuna vingi viliathirika
 
sio mwenge tu hambacho hakina faida je lile chuma ninalewekwa mezani ndani ya bunge mara linatolewa na kuwekwa kabatini mara linatolewa kuwekwa juu ndio bunge lianze lina faida gani?
 
Tulishaongea sana kuhusu hili swala la mwenge, nadhani kuna watu wana maslahi nalo labda walozi, washirikina na waabudu mizimu.......maana imani ya kikristo hairuhusu ibada za moto, hiyo inakuwa ni ibada kwa ibilisi....
 
Ebanaaeee..nilikuwa nasikia mwenge mwenge..juzi nikasema ngoja nikauone!!!

Nilitegemea nitakuta ni limoto likubwaaaaaaa linawaka eneo lote linakuwa na mwanga.

Picha linaanza tumefika eneo la tukio saa 4 usiku sion hata mwanga wa moto naona tu balbu za umeme. Nikauliza "Oya mwenge umeshasepa? Akinionesha ule pale!!

Wakuu Nilishangaa mnooooo!!! Kamoto kadogo af jamaa wamekazunguka!! Af nilicheka kwa chini chini hadi machozi!!!
 
Na hauna replacement, mwenge huu unaojulikana wa UHURU umeisha nguvu na umeshindwa kuwamulika CCM wezi wa kura walioliteka jeshi la polisi na kulitumikisha kama punda, hapa tulipo Jeshi la polisi limekuwa mtumwa wa CCM. Polisi wanashindwa kuwakemea CCM,inaonekana wazi CCM wanafanya mikutano kila pembe lakini wengine ni hapana na inakuwa ni kosa kubwa sana ,la jinai .

Mwenge umeshindwa kuiona hali hii na hauna tena zile nguvu zake eti umulike kila kona,hamna kitu tena na nina wasiwasi karibu CCM watafanikiwa kuuzima hata hako kajimuangaza kalichobakia,ili wainyonyoe Tanzania na kuacha mashimo matupu.

Mwenge umeshindwa kuimulika CCM na matendo yake.
 
Magufuli alisitisha mbio za huo Mwenge mkamtukana weeee!
Kwamba kasitisha kidikteta na kibabe bila kushirikisha wengine, na pia kasitisha sababu kaharibu uchumi na hivyo hana hela za kufadhili mbio za huo Mwenge!

Sasa ni hivi, mimi binafsi siasa za tangu Jk, Magu na sasa Samia zimenifundisha mambo mengi sana juu ya watz.

Kwahiyo Samia wewe ongoza nchi uonavyo tena ikiwezekana apore hata hela akafiche ughaibuni huko!

Na mtumishi yeyote mwenye nafasi asipofisadi kwa kigezo eti anafanya uzalendo atakuwa mpumbavu sana!
 
Mataga na UVCCM hawana akili, hawajui tofauti ya kukosoa na kutukana.

Katiba mpya yazidi kurindima, Dr. Hosea anena

Serikali iache matumizi ya anasa, Serikali ina matumizi ya hovyo, luxury na anasa

Viongozi wanafanya ubadhirifu, na Ufisadi, .. Wananchi wanashindwa kuwawajibisha. KATIBA MPYA inatakiwa

Mwenge ni mojawapo ya matumizi ya hovyo
 
Na hauna replacement ,mwenge huu unaojulikana wa UHURU umeisha nguvu na umeshindwa kuwamulika CCM wezi wa kura walioliteka jeshi la polisi na kulitumikisha kama punda,hapa tulipo jeshi la polisi limekuwa mtumwa wa CCM. Polisi wanashindwa kuwakemea CCM,inaonekana wazi CCM wanafanya mikutano kila pembe lakini wengine ni hapana na inakuwa ni kosa kubwa sana ,la jinai .

Mwenge umeshindwa kuiona hali hii na hauna tena zile nguvu zake eti umulike kila kona,hamna kitu tena na nina wasiwasi karibu CCM watafanikiwa kuuzima hata hako kajimuangaza kalichobakia,ili wainyonyoe Tanzania na kuacha mashimo matupu.

Mwenge umeshindwa kuimulika CCM na matendo yake.
UMEBAKIA KUENEZA UKIMWI....TU😃😃🤣👆😁😁
 
Mimi binafsi hadi leo sielewi kwa kina nini maana ya mbio za mwenge,unasaidia nini ktk taifa letu ukikimbizwa na usipokimbizwa.Kuna mambo nikiulizwa mf nini faida ya majeshi yetu najuwa na kazi zao naona.Tafadhali wanajf
 
Mimi binafsi hadi leo sielewi kwa kina nini maana ya mbio za mwenge,unasaidia nini ktk taifa letu ukikimbizwa na usipokimbizwa.Kuna mambo nikiulizwa mf nini faida ya majeshi yetu najuwa na kazi zao naona.Tafadhali wanajf
Hakuna faida ya mwenge lakini unadumaza akili za watanzania yaani hakuna kuhoji,lakini pia kama unawatoto waambie kabisa wasikaribie huo Moto ni hatari Kwa maisha yake
 
Back
Top Bottom