Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Wametakiwa wafike ofisni kwa ajili ya 'utaratibu mwingine'

Bila shaka ni kujaza fomu za kuchangia ile 1 million kwa kila mbunge wa viti maalum kwa Chama utaratibu ambao ulilalamikiwa sana na Wabunge wa viti maalum wa bunge lililopita
Ahahahahahahahahahah!!!
 
Mojawapo ya tatizo kubwa la cdm ni kufanya vitu kwa hisia na jaziba,hakuna deep thinking yaani,,
 
Maswali yafuatayo yanapaswa kujibiwa na Mbowe/Mnyika:

1. Nani amepeleka Orodha ya Majina ya Wabunge wa Viti Maalum NEC?
2. Orodha hiyo imepelekwa kwa njia gani?
3. Kama msimamo wa chama na wa Katibu Mkuu ni kuwa Orodha haikupelekwa, walioapishwa jana walipatikanaje?
4. Hatua gani zinachukuliwa na CHADEMA ikiwa usaliti umetokea?
5. Ilikuwaje Nusrat Hanje aachiwe tu kutoka mahabusu na asubuhi yake aapishwe kuwa Mbunge wa Viti Maalum?
6. Nani yuko nyuma ya suitafahamu hii nzima ndani ya CHADEMA na anashughulikiwaje?
Wazee wa KUIBADILI GIA angani wana jambo lao bana.....

Eti mtu aujue "uvungu" wa kitanda chako bila ya yeye kukifahamu "chumba"?!!mmmh CHADEMA "nguli" wana mambo mengi YASIYOJULIKANA na wanachama wao wa kawaida....


MAENDELEO HAYANA VYAMA
 
Hii ni Harufu ya mgogoro Mkubwa.

Ndani ya Chama hicho hicho wapo wanaounga mkono viti maalumu na wapo wanaopinga.

Makundi yote mawili yana viongozi wakubwa nyuma yake. Lile lenye nguvu ndilo litashinda na maisha yataendelea.
 
Ijumaa sio mbali mbona anajiuma uma kuhusu hatua za kuchukua.

Walau tumejua sio msimamo wa viongozi wote huko juu kususia bunge wamegawanyika Mnyika mwenyewe amekiri. Si ajabu watu wakaona waende na mtindo wao bila ya ku implicate uongozi (ila kwa baraka za nyuma ya pazia).

Either way kama kuna mgawanyiko jinsi ya kwenda mbele baadhi ya viongozi wa juu ndani ya CDM harakati za Lissu zishawachosha.

Funika kombe mwanaharamu apite.
 
Mimi sipendelei upande wowote lakini kwa ujumla hao walioapishwa wana makosa. Kikanuni Chama ndicho kinatakiwa kipeleke majina yao NEC baada ya kila mmoja kujaza fomu inayotakiwa. Katibu Mkuu amekiri kuwa hayo yote hayakufanyika. Sasa kulikoni?.
 
Back
Top Bottom