Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
797
1,000

Leo Novemba 25, 2020 katibu mkuu wa CHADEMA amezungumza na vyombo vya habari makao makuu ya chama hicho eneo la Ufipa, Kinondoni mada kuu ikiwa uteuzi wa wabunge wa viti maalum ambapo uapisho wao ulifanyika jana bungeni jijini Dodoma jana.

Yafuatayo ni maelezo kwenye mkutano huo kuanzia mwanzo hadi mwisho pamoja na maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

PIA, SOMA: Hatimaye Wabunge wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

=> Ester Matiko: Kama chama kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari

============​

JOHN MREMA: Mbele yetu katibu mkuu wa chama, John John Mnyika akiwa na mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi na mahusiano ya mambo ya nje na msemaji mkuu kwa siku ya leo atakuwa katibu mkuu wa chama.

JOHN MNYIKA: Tarehe 28 Oktoba kulifanyika uchafuzi ulioitwa uchaguzi mkuu ambapo mtakumbuka kati ya mambo yaliyofanyika ni hujuma za wazi za mfumo wa kiserikali ukihusisha tume ya Taifa ya uchaguzi kupika matokeo ya uchaguzi.

Chama cha demokrasia na maendeleo hakijateua wabunge wa viti maalum au wagombe ubunge viti maalum wala hakijawasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum.

Kwa katiba ya CHADEMA, mamlaka ya uteuzi wa wabunge yapo kwa kamati kuu ya chama. Kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha kuteua majina ya wabunge wa viti maalum wakati wowote.

Pili katibu mkuu wa chama ambae ndie mwenye mamlaka ya kimawasiliano ya kuwasiliana na tume ya Taifa ya uchaguzi, katibu mkuu wa chama sijawahi kuwasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya wanaoitwa waliopendekezwa wabunge wa viti maalum.

Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu.

Mimi kama katibu mkuu, hakuna fomu yoyote ya mtu yoyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yoyote.

Mchakato huo wote haukufatwa, kwa hiyo kwa tafsiri nyepesi, kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi ambayo imehusisha mfumo wa kiserikali, tume ya Taifa ya uchaguzi na kwakweli niseme vilevile imehusisha hao waliokwenda kuapa bila ridhaa ya chama na bila baraka za chama na bila kupishwa kwa mamlaka halali za chama.

Chama inabidi kichukue hatua, katiba yetu inasema hatua zozote zisichukuliwe bila ya wahusika kuitwa, kujieleza. Sasa kwa kuwa hili jambo ni la dharula, chama kitatumia utaratibu wa dharula katika kushughulika na jambo hili na tutaongozwa na kanuni za chama.

Kwa kuwa mamlaka ya jambo hili ni kamati kuu ya chama, naomba kuwatangazi kwamba tumeitisha kikao cha kamati kuu ya chama maalum, kitafanyika siku ya Ijumaa tarehe 27 hapa jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwa tutawaandikia wahusika, ili kusitokee kisingizio kwa yeyote kwamba hakuitwa, hakupata taarifa ya kuitwa naomba kutangaza 'Public notice' kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kwenda kula kiapo jana tarehe 24 kufika makao makuu ya chama bila kukosa.

Kuna tukio la mwanachama wetu ambae ni kiongozi wa baraza la baraza la vijana la CHADEMA, Nusrat Hanje ambae amesota ndani kwa kesi ya kubambikiziwa kwa siku 133 akiwa mahabusu na leo tarehe 25 mahakama kuu ndio ilikuwa inakutana kutoa uamuzi juu ya rufaa ambayo amekata baada ya kusota ndani kwa muda mrefu.

Kituko kinachoashiria mfumo kuhusika katika huu mchezo, tarehe 23 usiku alikwenda kutolewa gerezani ili kesho yake apelekwe kuapa na alitolewa na mfumo bila hata kuzingatia masharti ya kisheria. Tunashkuru kwamba mwanachama wetu na kiongozi wetu ametoka baada ya kusota ndani kwa muda mrefu lakini mfumo ulimtoa ili kutekeleza malengo yao.

Sasa Ndugai amesema alipelekewa majina tarehe 20 Novemba na tume, Nusrat Hanje alietolewa gerezani tarehe 23 Novemba, uteuzi wa tume unasema umefanyika tarehe 20, fomu yake aliijaza lini, hakimu aliemuapisha alikuwa wapi kabla ya tarehe 20 tume ilipomteua mambo ambayo yanadhihirisha wazi kwamba hili jambo ni kazi ya mfumo.

Lengo la wazi la mfumo ni kutaka kufifisha ajenda ya kwamba Tanzania ilifanya uchaguzi haramu tarehe 28 Oktoba ulioitwa uchafuzi wakati umma ukishinikiza, jamii ya kimataifa ikishinikiza, bunge likionekana la chama kimoja ili kujaribu kulipa uhalali serikali ya illegitimate president Magufuli ikaamua kushiriki huu mchezo haramu wa kuhusisha tume, spika wa bunge na hatimaye tumefika hapa tulipofika.

Nitoe rai kwa watanzania, jambo hili lisitutoe watanzania kwenye mjadala mkubwa na muhimu zaidi kwamba tarehe 28 Oktoba kulifanyika uchafuzi na kwamba sisi tunataka uchaguzi ufanyika upya chini ya tume huru ya uchaguzi.

Sisi tunaotaka hilo tunatengenezewa mazingira ya mjadala kuhama, umma wa watanzania usikubali kuingizwa kwenye mtego wa dola wa kuhamisha mjadala na kufifisha hasira za wananchi.

Kauli iliyotolewa jana wakati wa kuapishwa iliyotaka kujenga ishara kama mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe alihalalisha hili linaloendelea, hii kauli sio ya kweli na mwenyekiti wa chama ndie atakaeongoza kikao cha kamati kuu ya chama kitakachofanyika tarehe 27.

MASWALI NA MAJIBU

MWANDISHI (Halifa-Mwandishi wa kujitegemea):
Swali la kwanza kwa Mnyika, unadhani hili suala litaiacha vipi CHADEMA kama chama kwa sababu kuna hofu, ukizingatia watu walioenda bungeni kuapishwa, kina Mdee, Ester Matiko ni watu wakubwa kwenye chama, unadhani litakiacha chama salama?

Swali la pili, umesema hili suala limetengenezwa na mfumo kwamba kuna hujuma flani unadhani CHADEMA kinafanyiwa, katika mazingira kama hayo unadhani CHADEMA kinapaswa kuchukua hatua gani? Mnakabiliana nalo vipi suala la mfumo kujaribu kuhujumu chama chenu ili kuepusha matukio kama hayo kujirudia siku za mbeleni.

JOHN-Dar Mpya: Swali la kwanza, katibu mkuu umesema sakata zima hili la kuwaapisha kina Halima limekuwa 'engineered' na dola lakini kuna taarifa ambazo mimi binafsi nnazo kwamba majina haya, mchakato mzima huu wa maandalizi ulifanyika ndani ya ofisi ya katibu mkuu aidha ni wewe au wasaidizi wako. Kama kiongozi nilitegemea utaweka pia 'doubt' kwamba dola haiwezi kulikamilisha jambo hili bila kushirikiana na viongozi ndani ya chama maana yake wewe kwenye uongozi mzima wa chama haujaonyesha hata mashaka yoyote yale kwamba inawezekana dola imesaidiwa na either watu ndani ya ofisi yako au ndani ya CHADEMA kwa sababu wewe umejaribu kutuonyesha fomu hapo kwamba fomu za tume umekadhibiwa katibu mkuu lakini what If mtu anajenga hoja kwamba ya msaidizi wako alipitia mlango wa nyuma alienda akazichukua hizo fomu ofisi ya tume akaja akazisaini kwa niaba ya katibu mkuu kwa sababu unavyosema saini ni ya katibu mkuu inatakiwa, what if kuna barua ambazo chama kimekuwa kikifanya mawasiliano na tume kupitia naibu katibu mkuu

Swali la pili, uasi na usaliti ndani ya CHADEMA, hawa watu walioenda kuapa ni viongozi wakubwa ndani ya CHADEMA, mimi naona jambo hili hawa watu hawawezi kuwa wamekwenda bila 'top management' kuwa nyuma yao. Hii 'courage' na 'doubt' yangu inaweza kuwa inasapotiwa na kauli ya Halima jana kwamba alimtaja mwenyekiti, unazungumziaje level ya uasi huu?

REGINA-Mwanahalisi: Kilichofanywa na kina Halima Mdee ndio hichi hicho kilichofanywa na mbunge Aida Khenan lakini hapo katibu mkuu amesema wanaopaswa kuja siku ya Ijumaa ni hao wabunge 19 walioapa jana, vipi kuhusu Aida?

MAJIBU
JOHN MNYIKA:
Nianze na la Aida, nilisema leo nimekuja kuzungumzia walioapa jana, hizi ni kesi mbili zinashahabiana lakini ni case mbili tofauti kwa sababu case ya walioapa 19 kimsingi inahusisha cilevile kughushi orodha ya majina ya chama na mchakato mzima wa fomu.

Suala la Aida linahusisha kukiuka tamko lililotolewa na viongozi wakuu wa chama, haya yote mawili tutayashughulikia na kila moja tutashughulikia kwa namna yake.

Maswali ya Halifa, kwamba chama kitabaki salama, naomba niwahakikishie watanzania chama hiki kitaendelea na kitabaki kuwa salama, kitapita katika mchakato huu kikiwa na nguvu zaidi ya kuendelea kujipanga kushika dola na historia ya CHADEMA inadhihirisha hivyo.

Umenukuu jambo hili limehusisha mfumo, sasa tutachukua hatua gani. Naomba nisizungumze hatua kwa sasa kwasababu kama nilivyosema tunakwenda kufanya kikao cha kamati kuu tarehe 27 na nitoe wito kwa wanachama na viongozi popote pale, milango iko wazi na wadau wa demokrasia kutoa maoni kwa chama juu ya ni hatua gani zikachukuliwe na kamati kuu tarehe 27 kwahiyo sitaki kutoa hukumu.

John, Dar Mpya mpaka ninavyozungumza na nyinyi sijaletewa ushahisi na yoyote juu ya uhusika wa mtu yoyote ndani ya ofisi ya katibu mkuu kushirikiana na mfumo kufanya jambo hili. Jambo ambalo nina hakika nalo moja kwa moja, hao 19 walioenda kuapa walishiriki kwenye huu ubatili na wanaufahamu huu ubatili.

Narudia kusisitiza halina baraka zozote za mwenyekiti Mbowe kwa hiyo ndugu John ulieuliza swali ni vyema ukafatilia na ukaandikana pia ukapata 'quotation' kati ya viongozi wakubwa unaosema wamebariki au wameunga mkono jambo hili, ni kiongozi gani?

Jambo la kuzingatia, kiongozi mmoja mmoja anaweza akawa na mawazo yake binafsi, wapo waliokuwa na maoni kwamba tupeleke majina haraka, wengine wanasema tusipeleke, wapo wanaosema tuendelee na msimamo wetu uleule wa kutopeleka majina, hiki ni chama cha demokrasia na maendeleo, watu wanaweza kuwa na maoni lakini ajitokeze mtu mmoja aseme ni kikao gani kimekaa kikafanya uteuzi wa majina, hakuna mtu atakaekwambia.

Kwa ufupi hawa waliokwenda kuapa, kimsingi walijiteua na wakashirikiana na dola kwenda kuhalalisha huo ubatili, usaliti, uasi na uharamu wa kushiriki kiapo, sasa chama kitachukua hatua gani? Hio sio kazi ya katibu mkuu. Kazi ya katibu mkuu ni kuhakikisha kamati kuu imeitishwa, itafanyika Ijumaa na chama kitaeleza hatua ambazo itachukua, tunawashukuru sana.
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,013
2,000
Chama sio biashara binafsi. Huwezi kufukuza watu kwenye chama kwa kigezo cha hisia tu.

CHADEMA haina hoja ya kupinga matokeo ya Uchaguzi na kuzuia Wabunge kufanya kazi yao.

Kisheria huwezi kumfukuza mtu kwenye Chama kama anatimiza wajibu wake wa kikatiba.

Wakifanya hivyo, basi litaamuliwa Mahakamani. Mahakama huangalia maslahi mapana ya taifa.
 

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,523
2,000
Maswali yafuatayo yanapaswa kujibiwa na Mbowe/ Mnyika:

1. Nani amepeleka Orodha ya Majina ya Wabunge wa Viti Maalum NEC?
2. Orodha hiyo imepelekwa kwa njia gani?
3. Kama msimamo wa chama na wa Katibu Mkuu ni kuwa Orodha haikupelekwa, walioapishwa jana walipatikanaje?
4. Hatua gani zinachukuliwa na CHADEMA ikiwa usaliti umetokea?
5. Ilikuwaje Nusrat Hanje aachiwe tu kutoka mahabusu na asubuhi yake aapishwe kuwa Mbunge wa Viti Maalum?
6. Nani yuko nyuma ya suitafahamu hii nzima ndani ya CHADEMA na anashughulikiwaje?
 

El Maestro

Senior Member
Apr 12, 2020
167
250
Katibu Mkuu wa CHADEMA anazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchakato wa wabunge wa Viti Maalum ambao wameapisha siku ya jana tarehe Novemba 24, 2020.

Katibu Mkuu, John Mnyika amewataka wabunge wote walioapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum kufika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama siku ya Novemba 27, saa mbili asubuhi bila kukosa kwa ajili ya utaratibu mwingine.
Acha masihara bhana, yani ndo kaita watu kusema hivyo... utaratibu upi wa kuchangia pesa za ubunge au
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom