covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 4,902
- 10,675
Safi sana kama WHATSUP call ilivyorahisisha mawasiliano kote duniani.Mwakani Elon Musk atazindua huduma ya internet kupitia kampuni yake ya Starlink. Elon Musk alisema kwenye tweet yake kuwa mwakani atazindua huduma ya internet ambayo itakuwa inapatikana dunia nzima bila kujali eneo gani upo.
Ikumbukwe kuwa internet ya Elon Musk itakuwa inarushwa na satellite zake yeye mwenyewe alizoweka angani huko. Naona kama mpango wa Elon Musk utaweza kuumiza biashara ya Internet inayotumika na mitandao ya simu inayotumia minara. Hivyo itaweza kuleta ushindani wa kibiashara.
Lakini na wasiwasi kama mitandao ya simu ya hapa Tanzania itaweza kushindana na Elon Musk kulingana na Teknolojia anayotumia?
Natamani Elon Musk angeanzisha hata mwaka huu ili tupumue gharama za vifurushi. Mitandao ya simu pigeni faida kwa mara ya mwisho. Kuanzia mwaka ujao bilionea atawanyanyasa sana. Je mtaweza kushindana naye?
Wanajukwaa mna mtazamo gani juu ya hili?