BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
Kitendo cha Waziri Nape Nnauye kusema bado Serikali haijafikia muafaka wa kumruhusu Mwekezaji na Tajiri namba 2 duniani, Elon Musk kuwekeza nchini ili kutoa huduma ya Intaneti yenye kasi kupitia Satelite hadi atakapoweka ofisi zake nchini Tanzania, inaonesha wazi bado tumekumbatia Sera za kikoloni zisizoangalia fursa kwanza.
Kampuni ya Starlink imeshafanya uwezekaji kwenye Nchi nyingi duniani ikiwemo za Afrika ambako sidhani kama kote amepewa masharti ya kuweka ofisi kwanza. Mfano mzuri ni jirani yetu Rwanda ambaye tayari ameshatoa vibali kwa Elon kuwekeza huduma hiyo.
Ni kama vile sera zetu zinaangalia zaidi kubana uwekezaji kuliko kuangalia faida itakayopatikana baada ya uwekezaji kuanza. Kwanini hatujifunzi kwa Nchi nyingine zinafanya nini kwanza? Kitendo cha Elon kusema anasubiri Serikali impe kibali kimetuma picha mbaya kwa wawekezaji wengine na kuona Tanzania ina sera ngumu za uwekezaji.