Shule za Rwanda kutumia internet ya Starlink

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Taasisi ya TonyBlair imetangaza kufanya kazi na serikali ya Rwanda kwa ajili ya kuunganisha huduma ya Internet kutoka katika kampuni ya SpaceX ''StarLink'' iliyopo chini ya Elon Musk.

Mapema mwezi March mwaka huu, Wizara ya Elimu kutokea nchini Rwanda ilianza kwa kuunganisha huduma hiyo kwa shule takribani 50, huku shahuku na nia ya serikali ya nchini Rwanda ni kuzifikia shule 500 ili kuhakikisha kila shule inapata huduma ya Internet.

Kufanikiwa kwa mchakato huu wa ufungaji wa vifaa vya internet kutokea StarLink unategemewa kuleta matokeo chanya kwa uzalishaji wa wabunifu na wavumbuzi alisema waziri wa mawasiliano, teknolojia na uvumbuzi Paulo Ingabire wa nchini Rwanda.

Sasa unaweza kuwa na maswali hii STARLINK ni nini? Kwa ufupi ni huu ni ni mkusanyiko wa mtandao wa setilaiti unaoendeshwa na SpaceX

Faida ambazo zinatofautisha upatikanaji wa Internet wa kawaida ukilinganisha na StarLink

-Inakasi mara tatu zaidi ya mfumo wa kawaida wa Internet, mfumo wa kawaida ni Mbps 100 Lakini StarLink inazidi mpaka kufikia Mbps 300 na hii Mbps ni kifupi cha ''Megabits per second'' ambapo kipimo kidogo zaidi cha kasi ya data ni bits lakini ikiwa kwenye kiwango cha kuhamisha bit Milioni moja ndio huitwa Megabit.

-Urahisi wa gharama ukilinganisha na watoa huduma wengine, kwenye StarLink mtu hulipa kiasi cha Dollar 60 ambayo ni 144,000 kwa pesa ya Tanzania kwa kasi ya MB's 100/10 na kwa mujibu wa wisevoter.com speed ya Internet kwa nchi ya Tanzania ni 22.05 Mbps na kuifanya kuwa nchi ya 150 Duniani kwa kasi ya Internet.

-Upatikanaji wake, Huduma ya StarLink haijalishi wewe unaishi wapi inapatikana popote duniani bila ya uwepo wa changamoto ya upatikanaji wake.

Changamoto za StarLink
-Kasi ya Internet kuwa ya kiwango cha chini kwenye miji kwa sababu ya idadi kubwa ya watu kutumia ''bandwidth'' moja kwa pamoja, na kuhusu bandwidth hiki ni Kiwango cha juu zaidi cha data inayotumwa kwenye muunganisho wa internet kwa muda fulani.

-Matawi kwa ajili ya usambazaji wa Bidhaa/Vifaa, Mfano waya wa kisimbuzi ukiharibika ni rahisi kwenda kununua kwa wauzaji madukani lakini StarLink hawana maduka kwa baadhi ya maeneo ikiwa kifaa kimeharibika.

-Changamoto nyinginezo kwenye ukubwa wa kifaa ambao unaleta ulazima wa mtu kuwa sehemu husika ili awezeshwe na huduma tofauti na Internet ya SImu ambayo unakuwa nayo mahali popote.

Credit: EATV

Pia soma: Serikali iachane na Sera zinazobana Wawekezaji, mfano kumtaka Elon Musk kuweka ofisi za Starlink Tanzania
 
Mean while hapa Tanzania tuna mtu anayejinasibu kuwa ni waziri wa mawasiliano ambaye hajitambui kwa sera zake kazi kuvuruga sekta ya mawasiliano na hakuna analofanya katika kucontain situation.
 
Back
Top Bottom