Status
Not open for further replies.
Kwanza mpaka kuja kumeguka na kuwa bara lingine wewe wala wajukuu zako hawatakuwepo, labda kama bado UHAI utakuwepo basi vitukuu wa vilembwe wako nk...
duh tukiwekwa na hawa al shabaab mi ntahama!
 
Ndugu wana JF.

Nchi imetafunwa mno hii na hawa mchwa. Sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Mzalendo Dr. JPM kuendelea kufyeka haya matango pori.

Weka taarifa yako hapa ili isaidie kutumbua. As far as Magufuli ni mfuatiliaji atanusa hapa tuuu.

Karibuni sana.

MWONGOZO:

Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

* Taarifa zote zitafanyiwa kazi kwa kupelekwa kwa mamlaka husika
 
Mashirika ya hifadhi ya jamii ubadhirifu wa fedha za wanachama; nasikia LAPF mwaka 2014 watendaji walitumia fedha za Mfuko kujinunulia viwanja manispaa ya kinondoni takriban milion 800 zilitumika; ajira za kindugu na kiswahiba mwaka 2014 kuna watumishi 3 waliajiriwa bila kufanyiwa usaili; mwenyekiti wa bodi kwenda kutibiwa london kwa fedha za mfuko na kulipiwa gharama za zote yeye pamoja na mke wake; licha ya posho zote kupigwa marufuku juzi wamefanya baraza la wafanyakazi na wamelipana laki 3 kwa kila kikao je huu uongozi uko juu ya sheria?
 
WanaJamii,

Hii ni rai yangu kwa raisi wa Jamuhuri ya Tanzania.Maoni yangu ni yangu binafsi na sio ya mtu yeyote.Kwanza,nampongeza sana Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya katika kuleta tija kwa taifa na sio mtu mmoja mmoja.Kuna kasoro katika kufanya na kutekeleza haya maazimio "hapa kazi tu",lakini kwa hali tuliyokuwa nayo nahisi Mungu alipenda tuanze upya kusuka nchi yetu maana ilikuwa imeisha,ikibaki kwa kipande kipande.

Kwa ufupi naweza kusema,nathani tumeona uwozo mwingi sana kwenye kila sekta.Nathani,hata wew msomaji kwa namna moja au nyingine nawewe unahusika katika kuhujumu uchumi,au kushiriki na wale wanofanya hii biashara haramu;sisi watanzania wote tu majipu na tunahitaji kutumbuana kwakweli.Hali ilifika pabaya.

kama nilivyosema,Magufuli anafanya kazi pamoja na mapungufu yake,ila kwangu naona ni sawa na kujenga nyumba juu mchanga.Kufukuza,kusimamisha,kufungana,nk hakuta leta tija kwa nchi kwa muda mrefu maana hii imekuwa sehemu ya maisha au niseme culture kwetu sisi watanzania wote.Ujanja ujanja ni mwingi sana hata katika sekta binafsi na sio tu serikalini.

Na hapa ndio namshauri Magufuli,aanze harakati za kuleta katiba ya wananchi.Katiba ya wananchi ndio itaenda na wakati huu,na kuweza kulinda maslahi ya nchi na sio chama kama ilivyo sasa.
Napenda kuona katika katiba mpya,kuna kuwa na mfumo mpya,structure mpya ya uongozi na ngazi zake ambao pia utapunguza matumizi kutokana na ukubwa wa serikali,na pia kuondoa urasimu kwenye mambo mengi.

Napendekeza,wabunge wasiwe na uongozi mwinigine;hii leo mbunge yuko kwenye bodi,waziri wa wizara fulani,na mamb mengi ambayo sioni umuhimu wao.Pia,napendekeza,maraisi wastaafu washtakiwe kwa makosa waliofanya na pia wapunguziwe nguvu waliyonayo sasa ambayo inawafanya wasiguswe.

Kuna mambo mengi sana ambayo ni ya lazima kuwepo kwenye katiba mpya maana kwa kazi anayofanya sasa,hata akifa leo,au kuondoka madarakani,nchi itarudi kwenye matatizo lukuki tuliyonayo sasa.Napendekeza "CHECK AND BALANCE SYSTEM" ndio system bora itakayofanya kazi kwa haki,ufasaha na kwa tija ya nchi tu.
 
Ndugu wana JF.

Nchi imetafunwa mno hii na hawa mchwa. Sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Mzalendo Dr. JPM kuendelea kufyeka haya matango pori.

Weka taarifa yako hapa ili isaidie kutumbua. As far as Magufuli ni mfuatiliaji atanusa hapa tuuu.

Karibuni sana.

MWONGOZO:

Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

* Taarifa zote zitafanyiwa kazi kwa kupelekwa kwa mamlaka husika


Jana nilikuwa Morogoro, kuna wafanyakazi wa Chuo cha Ualimu Morogoro walikuwa wanajadili kuwa kuna sehemu ya eneo la Chuo liliuzwa na watumishi wa ardhi Manispaa ya Morogoro kwa mwarabu/singasinga, Mkuu wa chuo hicho aligombana nao lakini wakamtishia na sasa mwarabu huyo amejenga nyumba yake na amehamia anaishi ndani ya eneo la chuo hicho, nashauri vyombo vya habari vimulike swala hili ni kashfa kubwa kwa mtu binafsi kuishi ndani ya eneo la taasisi ya serikali
 
Serikali chini ya dakt. Magufuli inaendesha tiba ya utumbuaji majipu. Ni ugonjwa wa kujitakia, lakini kiapo cha daktari ni kuponya kama ulivo wajibu wa mzazi kufundisha na kurekebisha. Tiba hii inaumiza. Miili ya wagonjwa wengi imeoza, majipu yana miaka. Majipu mengi yapo ndani ya miili. Hata yanayotumbuliwa, mengine huota pembeni kabla dakt hajamfunga bandaji. Ushauri kwa daktari ni kubadirisha tiba. Hana haja ya kuingia maabara kufanya c&s. Antibiotic kali tena kwenye drip itakupa tiba bora. Itasambaa haraka mwili mzima na kuyakausha yote. Itaondoa hatari ya dakt kurukiwa na usaha na kupata maambukizi ya majipu. Sio wote watapona. Watakaopona watamshukuru daktari na kazi itaendelea, kwa mwanzo mpya.
 
Thread kama hizi huwa najiuliza mnapata muda wapi kuziandikA
Naona kila mtu anataka nchi iongozwe anavojiskia yeye. Ni makosa kuamin kwamba Hakuna hatua nzuri tumepiga Baada ya kutumbuliwa majipu. Tuwape muda viongozi wetu
 
Wakuu napenda kumpongeza Rais wetu kwa kuwa mbele ya wapigaji labla hawajapiga mzigo, mfano juzi kati aliibukia BOT na kuzuia malipo ya bilioni 900 mpaka wizara ya fedha wapite upya, tofauti na miaka mingine ambayo tulisubiri repoti ya CAG huku pesa zimeshaliwa na hatuwezi kuzirudisha hata km tumegundua wizi. Pia mawapongeza usalama wa taifa ambao sasa wapo kazini wakifanya kazi yao ya unyetishaji wa taarifa kwa mkuu wetu wa nchi. Kwaani iwapo tutaokoa hata biliona 50 kati ya hizo ni pesa nyingi sana.

Labda tu niombe Rais azibe sehemu chache ambazo bado watu wanakula pesa watakavyo mfano kwenye vituo vya mabasi kama Kibaha, msamvu, Dom, Arusha na nk. watumie mashine za EFD.
 
Siku akiingia TANAPA na kwenye gesi akatindua tindua na kule, hii nchi itanyooka sana.

Utalii na bandari na bandari pekee vinaweza kuifanya hii nchi ikapaa sana kiuchumi
 
Mh Magufuli mimi ni mwananchi wa kawaida ila kupia hapa nadhani ujumbe utakufikia baba rais. Tumbua majipu mpaka vipele vyote wizara ya fedha, Hazina na wahasibu wote,kuna watu waliokufa mpaka leo wapo kwenye payroll, mishahara hewa kibao.

Pia yale mafungu ya stahili za wakurugenzi pitia na malipo yote ya kwenye mawizara nina uhakika utatumbua majipu mpaka utalia mwenyewe kuna watu walioshindikana huko maserikalini wanakula pesa zako kama haupo kabisa mh rais wanacheza na system tu wanajipatia pesa kiulani baba wakati huku wananchi tunahenyeka na maisha magumu.
 
Dk fanya hayo hapo juu heshima ya nyerere ofisini zinarudi nasema

Ondoa wote wenye vyeti feki

Ondoa mishahara hewa

Ondoa marehemu wote wanaoendelea kulipwa tangu enzi za Jk

Hii na laana kula pesa za marehemu sawa na kudhulumu mirathi ya marehemu
 
Jamani suala la vyeti ni issue. Maana hapa wengi tuna vyeti feki a.k.a kufoji. Na hawa wasio na vyeti ndo wametufikisha hapa tulipo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom