Status
Not open for further replies.
Ushauri wng acheke na kila mmoja ila asimuamini kila ane cheka nae.naunga mkono utendaji wk kazi,yy binaadamu hawezi kamilika ktk kila idara,hivyo tusiogope kumpa ushauri au kumkosoa kwa busara nae kwa hekma aliyopewa na MWENYEEZI MUNGU.ninaamini atakua pamoja na wanao muunga mkono wa dhati si wakumdhihaki.piga kazi mwanawane.call spade a spade.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitapasahahu Muhimbili, ukiandikiwa rufaa ya kupeleka mgonjwa wako pale ni bora ukae nae nyumbani maana hali ni mbaya mno wako kimasilahi zaidi sana tu kuliko huduma aipatayo mgonjwa.
Ukweli Muhimbili ya wakati wa Mwalim Nyerere sio ya leo hata kidogo, ebanae kuna watu pale wanajiita social worker hawa ni watu wa ajabu sana sijapata kuona wao badala ya kutatua tatizo huongeza tatizo na kitengo hiki hakina manufaa yoyote yale tofauti na kuwafanya Watanzania kuwa fukara maradufu.
 
Yeye anafikili kuongoza watu ni kuwatisha na kuwafanya waishi maisha ya taabu ili wamnyenyekee. Nimeamini uongozi ni kujiandaa sasa yeye ametoka from no where
 
Yeye anafikili kuongoza watu ni kuwatisha na kuwafanya waishi maisha ya taabu ili wamnyenyekee. Nimeamini uongozi ni kujiandaa sasa yeye ametoka from no where
Yeye anafikili kuongoza watu ni kuwatisha na kuwafanya waishi maisha ya taabu ili wamnyenyekee. Nimeamini uongozi ni kujiandaa sasa yeye ametoka from no where

Pamoja na kwamba nacomment kwenye hii post, lakini nakushauri utafakari kwanini watu hawachangii post yako.
 
Mimi nachangia post yako na nakushauri uwe makini na ujitambue vinginevyo utaishia pabaya kwa kukosa maarifa. Mwacheni rais afanye kazi. Maslahi binafsi yameifikisha nchi hapa tulipo. Rais wetu hafanyi haya mnayoyachukia wachache kwa manufaa yake binafsi na familia yake kama mnavyotaka nyie sisi tuwaamini kuwa magufuli mbaya. Anayafanya haya kwa maslahi mapana ya taifa letu.

Mwacheni afanye kazi.

Yeye anafikili kuongoza watu ni kuwatisha na kuwafanya waishi maisha ya taabu ili wamnyenyekee. Nimeamini uongozi ni kujiandaa sasa yeye ametoka from no where
 
Mimi nachangia post yako na nakushauri uwe makini na ujitambue vinginevyo utaishia pabaya kwa kukosa maarifa. Mwacheni rais afanye kazi. Maslahi binafsi yameifikisha nchi hapa tulipo. Rais wetu hafanyi haya mnayoyachukia wachache kwa manufaa yake binafsi na familia yake kama mnavyotaka nyie sisi tuwaamini kuwa magufuli mbaya. Anayafanya haya kwa maslahi mapana ya taifa letu.

Mwacheni afanye kazi.
Usitupangie mkuu huwezi kutulazimisha tumpende huyo jiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefikiri sana hizi sintofahamu na kauli tata za Rais Magufuli na kuona zinazidi kumtenga sana na jamii ya Wa kizazi cha kuhoji.
Ili twende kwa pamoja ni vema Rais, watendaji wa serikali na wananchi watende kwa falsafa moja ili tufanikiwe.
Kwa vile Mara nyingi hatuelewani sababu yeye ndiye muongeaji pekee, sasa umefika wakati apatikane Mwandishi mahiri afanye naye mahojiano huru kuhusu mipango yake
 
Mhe. Rais John Magufuli,

Pole sana na majukumu ya kazi ngumu ya kuliongoza taifa hili.

Nia ya uzi huu ni kukupa tu mambo ambayo nafsi yangu ingependa sana kuona vinatokea na kufanyika. Naona kama vile nikiviona vimetendeka kikamilifu, nafsi yangu itakuwa na furaha iliyoje kiasi kwamba naona kabisa uwezekano wa kusahau makosa kadhaa ya msingi kabisa niliyoyaona yametendeka katika serikali yako.

Bila kupoteza muda naomba niiache nafsi yangu iorodheshe mambo hayo:
  • Kujenga mji mpya kule Bagamoyo wa tafiti, sanaa na biashara. Napendekeza mji huo uwe mahususi kwa waafrika wote na uitwe John Magufuli African Renaissance. Mji huu uwe wa kukutanisha vijana na wafanyabiashara wa kiafrika katika kubuni na kujenga mawazo na biashara mpya za kiafrika zitakazokuwa na lengo la kusambaa zaidi ya nchi moja. Lengo hasa liwe kwenye sekta za sayansi na teknolojia, sanaa na viwanda vya ubunifu mpya. Ni kama uiunganishe Silicon Valley na Hollywood. VETA, BASATA, SIDO na vyuo kama cha Kilimo Sokoine na kile cha sayansi cha Arusha cha Mandela watakuwa ndiyo wadau wakubwa katika hili. Sababu moja muhimu ya kujumuisha sanaa kwenye hili ni kwa sababu ikifanyika sawasawa, sanaa inaweza kutumika vizuri kusambaza mawazo mapya mazuri pamoja na huduma na bidhaa zitakatokuwa zinatoka. Pia, mawazo hayatakuwa tu yanaishia kwenye tafiti ila viwanda na mfumo thabiti wa mtandao wa wadau wenye biashara zao Afrika nzima utakuwepo kuchukua mawazo bora na kutengeneza bidhaa, huduma na biashara mpya kabisa. Hili ni muhimu sana. Tulikuwa chachu ya ukombozi wa kisiasa wa Mwafrika, nadhani Afrika inatusubiri tuwe tena chachu ya ukombozi wetu wa kiuchumi na kifikra.
  • Kujenga City Park ya kisasa na kuvutia sana itakayosambaa katika bonde la msimbazi, kuanzia huko Kigogo (au popote linapoanzia) hadi kule Jangwani, Magomeni, Kinondoni. Kama kuna mradi naweza kuunga mkono hata tukichukua mkopo kwa wachina huko ni huu hapa. Mji huu bado una changamoto, hauvutii kabisa. Kuna uzi niliwahi kuuandika humu kuhusu wazo hili, nikiupata nitauambatanisha.
  • Kujenga kiwanda cha Kiswahili. Hapa namaanisha kufanya utafiti (kama bado haujafanyika) na kutoa misaada kwa makampuni na biashara za kitanzania zitakazotangaza matumizi ya kiswahili kwa njia mbalimbali. Kuna ajira lukuki na mapato yasiyo na kipimo kwenye kiwanda hiki.
  • Kutambua sehemu zote zilizotengwa kwa ajili ya jamii na kujenga bustani safi, za kisasa na zitakazokuwa zina watu maalumu wa kuzisafisha muda wote.
  • Kufufua na kupanua mpango wa wakati ule wa kujenga shule maalumu za michezo, kama Makongo. Njia pekee ya kupata wanamichezo bora watakaofanya hatimaye na sisi tujivunie mafanikio yao na timu zetu ni kama watatokea katika misingi bora ya elimu ya michezo na hata elimu dunia. Vilevile, tusing'ang'anie sana mpira wa miguu pekee. Kuna michezo mingi, hasa ya mtu mmoja mmoja ambayo inaweza kututangaza sana. Ukifanya hili, ndani ya miaka 15-20 tutakuwa moja ya mataifa bora Afrika katika michezo.
  • Kuyaangalia masoko yetu yote ya vyakula na kuyajenga na kuyaboresha. Nadhani ungeanzisha kitengo maalumu kitakachojumuisha watu wa wizara ya kilimo, serikali za mitaa na biashara kuliangalia hili. Masoko yetu inabidi yawe siyo tu masafi na ya kisasa, ila yawe na taa za kutosha na yanafanya kazi masaa 24. Nadhani tujiongeze kidogo kwenye hili, itaboresha sana maisha ya mtanzania.
Kwa haraka haraka, nafsi yangu imeongea hayo. Ni matumaini yangu mawazo yangu yatakufikia na utayafanyia kazi yale utakayoona yana manufaa na yanatekelezeka.

Nakutakia kila la kheri.
 
hitaji lako la kwanza umechemka kwa kutaka mji uitwe magufuli ( anti-birth control movement)
sh!thole countries zinahuzunisha,badala mipango ya mendeleo ipitishwe na bunge,huku inapitishwa kwa hisani ya mtu mmoja!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom