....anaefuga wezi nae anaitwaje!Kwa Mhe Rais wetu, Rais Mtukufu na wa wanyonge wote Tanzania.
Salaam.
Jana nilikuangalia na kukusikiliza kwa makini ulipokuwa wanatoa neno baada ya kuwaapisha Majaji uliowateua wiki hii. Niliona pia ulipomsimamisha CAG na kumuuliza kama kuna pesa trillioni 1.5 alizogundua kwamba zimeibiwa na akakujibu hakuna.
Pia nilikusikia ukisema umeisoma taarifa ya CAG mwanzo hadi mwisho.
Haraka nilikimbilia kitabu changu ambacho nami nimekisoma mwanzo mpaka mwisho.
Nilipofungua ukurasa wa 34 niligundua haya:-
1. CAG Anasema, kwa mwaka wa fedha 2016/17 Serikali ilipanga kukusanya mapato yenye dhamani ya Shilingi Trillioni 29.5
2. Mapato halisi yaliyokusanywa ni Shilingi Trillioni 25.3
3. Serikali ilitumia shilingi Trillion 23.8
4. Trillioni 25.3 ukitoa Trillion 23.8 ni Trillion 1.5 ambazo ndizo anazotaka apewe maelezo.
Mtukufu Rais CAG hajasema pesa zimeibiwa. Wala ktk hatua hii hawezi kusema hivyo. Anachosema fedha hizo, matumizi yake hayaonekani na hazipo popote. Inawezekana kweli zimeibiwa, zimetumika kwa uzembe bila kufuata sheria au zipo mahali fulani.
Kwa taratibu za kibunge Maafisa Masuuli(accounting officers) wanatakiwa wampelekee ushahidi wa matumizi yake au ziliko ktk Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali yaani PAC mbele ya CAG ili hoja hii ifungwe. Kama wakishindwa kuifunga PAC na CAG sasa wanaweza kuomba msaada wa Polisi na au Takukuru kutafuta wezi au wabadhirifu.
Mhe Rais bila shaka umesoma pia ktk ripoti kwamba Serikali ktk ujumla wake imepata HATI CHAFU.
Wakati ukipokea taarifa hii Ikulu uliagiza Mkurugenzi wa Mji wa Kigoma Ujiji na wa Pangani watumbuliwe kutokana na maeneo yao kupata hati chafu.
Mhe unasubiri nini kumtumbua Katibu Mkuu hazina kwa kuisababishia Serikali yako kupata Hati chafu? Mbona kila mara unaapa kuwa mtu wa haki na jana uliwaagiza Majaji wakatende haki kwa Watanzania hasa wanyonge?
Mheshimiwa Serikali yako imepata doa kubwa. Vyombo vya dola haviwezi kulizuia kwa kuwatisha wanaoandika. Hizi ni fedha za maskini wote unaowatetea wauza maandazi, mitumba, mchicha na wengine wakubwa.
Ninakushauri baadala ya kuwatisha wanaohoji, waagize watendaji wa Serikali yako, wapeleke maelezo ya kutosha yenye ushahidi kwa CAG. Vinginevyo hatutaacha kukuuliza kila mara ZIKO WAPI PESA ZETU SHILINGI TRILLION 1.5
Jana Naibu waziri wa fedha alisema uongo Bungeni akidai sehemu ya fedha hizo Billioni 200 Serikali ya Muungano iliisaidia Serikali ya Zanzibar kukusanya mapato yake huku Bara.
Wote tunajiuliza vyanzo vya mapato ya ZNZ huku bara ni vipi? Hebu atutajie tuvijue na je! utaratibu huo ulikuwa wa 2016/17 peke yake tangu uhuru au ulikuwepo Taifa lisijue?
Mheshimiwa naona nakuchosha lakini nataka kusema neno la mwisho.
Inawezekana unadanganywa sana na waliokuzunguka na kwamba hawakuambii mambo mengi kwa faida yao. Wanapenda tu kukuambia yale wanayogundua unapenda kuyasikia na wanaogipa kukukosoa kutokana na ukali wako. Panua wigo wasikilize hata wale ambao hupendi kuwasikia hutakosa jambo lenye faida. Asante.
Kaondoa wezi wa awamu ya nne. Sasa kaweka wa kwake. Ndiyo mfumo wa serikali za Afrika. Hakuna jipya.Kwa Mhe Rais wetu, Rais Mtukufu na wa wanyonge wote Tanzania.

Unajua accrual accounting concept inayotumiwa na serikali as against cash basis accounting concepts? Ukijua dhana hizi na tofauti zake kwenye uhasibu utagundua kuwa Ripoti ya CAG iko sahihi na wala hakuna pesa iliyoibiwa. Usipojitahidi kuelewa mwenyewe utaendelea kuwa mtumwa wa wapotoshaji milele.
Wacha kutema makohozi weweKwa hiyo huna uzalendo ndani ya chama Na nchi unabwata humu ili uteuliwe? Uzalendo ni zaidi ya maslahi binafsi unatakiwa kuweka chama Na nchi Na serikali ya chama chako mbele jua liwake mvua inyeshe uwe mtu wa kawaida au Na cheo uwe Na ajira au la uwe unajulikana au hujulikani
Itakufa na njaaKwako mh Rais ,tumehama chama na kujiunga na ccm kukuunga Mkono kwa juhudi zako za kuwaletea wananchi maendeleo
Tunakusifia kila siku mh kwenye midahalo nje na ndani kwenye vyombo vya habari
Mbona wale waliokuwa madiwani na wabunge,mnawapa nafasi ya kugombea na wanashinda wanarudi tena?,sisi ambao hatukuwa na nafasi mh tupeni angalau ukuu wa wilaya
Tupo wengi mheshimiwa ,Akina Kafulila,Machali,Katambi na wengine wengi,tuonee huruma mkuu
Tupo wengine tunaandika makala za kukutukuza mkuu,Tupo akina Muro na Le mutuz
Na wengine kila siku tunakuandika front page ya magazeti yetu mh
Kama Tanzanite na Jamvi la habari mbona tunakusifia kila kukicha mkuu
Mkuu tunaomba uteuzi wako ,tumechoka kusakamwa
Rais amteua Anamringi Macha kuwa mkuu wa wilaya Kahama
Kafulira na musibaUsiseme sisi!! izungumzie nafsi yako bana...
KILAZA KTK UBORA WAKOLeo nimekubali Tanzania ina bahati ya kumpata Raisi anayependa kuiona ikibadilika na kuwa bustani yenye amani na furaha.
Nimemfuatilia kipindi chote anapofanya teuzi mbalimbali na kugundua yeye MH. JPM anamtazamo chanya Ila watendaji Ndio wanaomwangusha. Hongera Sana Uncle HON. JPM kwa juhudi zako za dhati.
Upande wa majeshi umezungumza jambo lenye hekima Sana la usawa na sisi raia tumekuelewa Vizuri Sana. Kabla Hujamaliza mda wako yafanye yafanane kimasilahi na katika swala la mavazi ili kuepuka ufisadi na uchakachuaji ukichagizwa na ongezeko la mavazi feki yanayoaibisha majeshi yafanye yatumie Hata vazi Moja watofautiane kofia tuu. Mfano jeshi la magereza hadi huruma maana hadi Leo huwa sielewi Rangi halisi ya vazi Lao. Ni aibu Sana kwa Kweli.
Nakupongeza tena Endelea na kasi hiyo hiyo mtukufu Toka kwa Mungu mheshimiwa raisi Dr. John P Magufuli.... Hongera Sana.