Status
Not open for further replies.
Magufuli huyu anayeongea sana kuliko kusikiliza na kutenda, kana kwamba ana midomo miwili na sikio moja, hawezi kufanya lolote katika miaka yake mitano ya Urais... huyu hakika Urais kakutana nao tu barabarani na anaushangaa na ataendelea kushangaa mpaka 2020 - si ajabu anazidisha vituko kila kukicha kiasi cha kufikia kucheza gwaride siku ya Uhuru badala ya kukagua gwaride!

Angalia mambo makubwa aliyoyafanya Mkapa kipindi cha Urais wake:
1. Kujenga barabara za lami kuunganisha mikoa yote nchini,
2. Kuanzisha taasisi mbalimbali imara ili kuboresha utendaji wa serikali - Mfano TRA, TIC, TIB na TANROADS,ambazo kwa hakika zimeleta tija katika shughuli za serikali.
3. Kuanzisha programu mbalimbali kubwa ambazo hadi leo akina Magufuli wanapandia juu yake na hawajaweza kuongeza ubunifu wowote, mfano TASAF. MMEM. Anachokifanya Magufuli kuhusu TASAF ni kuwa watu 'wanapiga dili' lakini TASAF wamekuwa wakitenda kazi yao vema tu miaka mingi
4. Kufanya nchi iheshimike kimataifa na kusamehewa madeni makubwa yaliyokuwa yakiikabili nchi

Sasa mimi najiuliza, Magufuli huyu anayevuvuzelika tuuuuuuuuuuuu mchana kutwa ata-achieve nini kipindi cha Urais wake???? Hivi haongei na Mkapa apewe akili?
 
Mkuu wangu nadhani wapiga dili wamekuwa wengi kuliko mafisadi pia wamepora fedha nyingi sana. Nakuomba mkuu futa mahakama ya mafisadi anzisha ya wapiga dili.
 
Hahaha eti kama anamidomo mawili NA sikio moja nimecheka mpaka bas hata mambo ya dangote aliyajua akayapuuzia mpaka jamaa akaenda kutusemea huko duniani ndo akashtuka

Nadhani kazi aliyopewa ni kubwa hauwezi
 
Mhe Rais magufuli nakuomba sekretarieti ya ajira uifute maana haina majukumu sasa hivi lengo la sekretarieti ya ajira ni kutangaza kazi na kufanyia usaili waajiriwa wapya kwenye idara mbalimbali serikalini tangu rais magufuli aingie madarakani idara hii haijatangaza nafasi za kazi ,watumishi wa idara hii ni hewa hawana kazi kutokana na kusitishwa kwa ajira kwenye idara na taasisi zote serikalini hivyo kuwafanya hawa watumishi kukoswa kazi za kufanya na kupokea mishahara ya bure ili kubana matumizi tunaomba serikali ifute hii idara maana kwa sasa haina kazi yeyote.

Miezi sita sasa tangu ajira serikalini zimesimamishwa idara hii hajawahi kuita watu kwenye usaili wala kutangaza nafasi za kazi hivyo watumishi wake wamekaa tu bila kazi yoyote .

Ili kubana matumizi mabovu ya kodi za watanzania tunaomba uwahamishe watumishi wa idara hiyo ili wasichukue mishahara bure .
 
Mhe Rais magufuli nakuomba sekretarieti ya ajira uifute maana gains majukumu sasa hivi lengo la sekretarieti ya ajira ni kutangaza kazi na kufanyia usaili waajiriwa wapya kwenye idara mbalimbali serikalini sasa hivi ni miezi sita watumishi wa idara hii hawana kazi kutokana na kusitishwa kwa ajira kwenye idara na taasisi zote serikalini hivyo kuwafanya hawa watumishi kukoswa kazi za kufanya na kupokea mishahara ya bure ili kubana matumizi tunaomba serikali ifute hii idara maana kwa sasa haina kazi yeyote.

Miezi sita sasa tangu ajira serikalini zimesimamishwa idara hii hajawahi kuita watu kwenye usaili wala kutangaza nafasi za kazi hivyo watumishi wake wamekaa tu bila kazi yoyote .

Ili kubana matumizi mabovu ya kodi za watanzania tunaomba uwahamishe watumishi wa idara hiyo ili wasichukue mishahara bure .
Hoja nzuri Sana kuwahi kutokea hapa jf.

Sahihisho...

Zaidi ya mwaka mmoja Sasa hii mamlaka watumishi wake wanakula mishahara ya bure. Ni watumishi hewa
 
Mhe Rais magufuli nakuomba sekretarieti ya ajira uifute maana haina majukumu sasa hivi lengo la sekretarieti ya ajira ni kutangaza kazi na kufanyia usaili waajiriwa wapya kwenye idara mbalimbali serikalini sasa hivi ni miezi sita watumishi wa idara hii hawana kazi kutokana na kusitishwa kwa ajira kwenye idara na taasisi zote serikalini hivyo kuwafanya hawa watumishi kukoswa kazi za kufanya na kupokea mishahara ya bure ili kubana matumizi tunaomba serikali ifute hii idara maana kwa sasa haina kazi yeyote.

Miezi sita sasa tangu ajira serikalini zimesimamishwa idara hii hajawahi kuita watu kwenye usaili wala kutangaza nafasi za kazi hivyo watumishi wake wamekaa tu bila kazi yoyote .

Ili kubana matumizi mabovu ya kodi za watanzania tunaomba uwahamishe watumishi wa idara hiyo ili wasichukue mishahara bure .
Sema tangu aingie madarakani hajatangaza ajira, sio miezi 6. Fanya nyeupe iwe nyeupe, sio nyeupe mpauko!!
 
Mhe Rais magufuli nakuomba sekretarieti ya ajira uifute maana haina majukumu sasa hivi lengo la sekretarieti ya ajira ni kutangaza kazi na kufanyia usaili waajiriwa wapya kwenye idara mbalimbali serikalini sasa hivi ni miezi sita watumishi wa idara hii hawana kazi kutokana na kusitishwa kwa ajira kwenye idara na taasisi zote serikalini hivyo kuwafanya hawa watumishi kukoswa kazi za kufanya na kupokea mishahara ya bure ili kubana matumizi tunaomba serikali ifute hii idara maana kwa sasa haina kazi yeyote.

Miezi sita sasa tangu ajira serikalini zimesimamishwa idara hii hajawahi kuita watu kwenye usaili wala kutangaza nafasi za kazi hivyo watumishi wake wamekaa tu bila kazi yoyote .

Ili kubana matumizi mabovu ya kodi za watanzania tunaomba uwahamishe watumishi wa idara hiyo ili wasichukue mishahara bure .
Kwani watu wasipoumwa tunafukuza kazi madaktari?
 
Sahihi kabsa, naona leo wametoa majibu yao ya kuzungumzia hili! Wanasema wana kaz nyingne tofauti na kutangaza ajira tu!
 
Wamekalia matamko na MAKANUSHO tu, hovyo kabsa, uhakiki miez 7 hafu ikiwa mambo yote yamesimama, unafanya zoezi 1 muda wote huo hafu mambo mengme yamesimama je kazi yao ni IPI? Bora kweli kuwatoa ili wengne wachukue nafasi zao!
 
Mh. Raisi Wa jamuhuri ya muungano Wa Tanzania, ama waziri mkuu Wa Tanzania, tumeona jinsi vijana wengi walomaliza chuo jinsi mlivo wapa matumaini ya ajira 70,000 na vijana wengi wakashindwa kutafuta fulsa binafsi za kufanya lakin hatimaye mmewachinjia baharini.

Si kwamba vijana hawawezi kujiajiri, no! wanaweza Ila mliwapa matumaini na ndo maana wakakaa kusubiri huku wakiwa hawana vibarua vya kuwajenga kiuchumi.

Walijaribu kwenda private institute wakanyimwa mikataba kwa hofu kwamba serikali itawaajiri. Mh. Raisi / waziri mkuu ona jinsi vijana walivopoteza mdaa wao kwa sababu ya matamshi Wa wateule (mawaziri) wako. Huoni kwamba wao wamechangia kiasi kikubwa kudhoofisha nguvu kazi ya taifa.

Mh. raisi, sasa hivi kuna ahadi ya ajira kwa vijana Wa sayansi na hisabati, tangu vijana tuambiwe kutuma soft copy za vyeti no muda sasa umepita. Mimi in mmoja wapo Wa kundi hili LA sayansi na nimetuma vyeti( softcopy) lakini nakosa imani na ahadi za wateule wako, kwani mpaka sasa no kimya tu hakuna majina yalowrkwa wazi.

Hii inatia hofu kwani endapo watachelewa kutoa majina na kicha kutoa majina machache watatuathiri sisi ambao GPA zetu ziko chini.

Nakuomba mh. raisi ama waziri mkuu uamuru wateule wako watoe majira ya watakao waajiri mapema sana ya mwezi huu hats kama hawawaajiri sasa ili tufahamu ambao hawatapewa fulsa ya ajira ktk sayansi na hisabati ilikusudi waweze ama tuweze kubuni namna nyingine ya kufanya mapema ya mwaka huu.Pia tuweze kutafuta sehemu nyingine binafsi za kufanya kazi. Mh. raisi/ waziri mkuu, please usipuuze maneno haya. Ahsanteni na Mungu awajaze hekima ktk kuongoza.
 
Mimi miongoni mwa watanzania zaidi ya milioni hamsini natumia fursa hii kutuma hoja tano kwend kwa JPM kama sehemu yangu ya kumshauri kiongozi wangu wa nchi tuweze kufikia kile wengi tunachokitamani.

1. Nguvu kazi iliyopo utumiwe ipasavyo na kuwa na mkakati kfanikisha wazalishaji mali (producers) wazidi walaji(consumers). Hapa serikali ufungue kilimo na shughuli zingine asilia ambazo ndiyo zinabeba idadi kubwa ya watu. Serikali na secta binafsi nunueni tractors na kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo cha mazao mbalimbali na vijina wawekwe ktk mashamba hayo kwa ajili ya kuzalisha. Irrigation schemes ziwepo kwa wingi na serikali iweke utaratibu wa upatikanaji masoko.

2. Tuwe na viwanda vinavyoa aksi malighafi yetu tunayoizalisha sisi ili tukuze hizo shughuli zinazotoa malighafi. Si lazima kuwa na viwanda vikubwa sasa hivi bali tuanze na viwanda vyetu vidogovidogo vinavyoaksi uchumi wetu badala ya kupokea viwanda toka nje hii hataisaidia kwa mda mrefu kwani badae tutajikuta hatumiliki uchumi sisi.

3. Fedha inayopatikana asilimia kubwa yake ifanye maendeleo ya jamii kkt huduma za jamii km afya na miradi ya maendeleo kuliko kuendesha serikali kwani ni wazi kuna bilioni nyingi zinatumika kuendesha serikali pasipo na ulazima . Mfano idadi kubwa ya magari ya kifahari kutokana na vyeo vvyingi km vile idadi kubwa ya wabunge,wakuuu wa mikoa na wilaya,RPCs,wakurugenzi,mawaziri na utitili mwingi ambao wote wanatumia pesa nyingi.

4. Mabadiliko na utungaji wa sheria mpya na hata katiba mpya ili kuiweka Tanzania ktk nafasi salama zaidi yenye maslahi mapana ya nchi.

5. Yapo mambo makubwa yanalitafuna taifa na bado hayajaguswa wala kuzungumziwa mfano mikataba mibovu ya madini. Rais sasa ahame toka kwenye kupapasa ili akajikite na mambo hayo mazito ambayo ni shida kwa taifa.

Asante
By GGM.
 
Namshauri Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM arejeshe viwanja vyote vya michezo serikalini kama alivyofanya kwa shule huko mkoani Kagera.

Najua kwa namna ya uongozi wake haitaji kikao chochote cha chama kulitekeleza hili kwani hata kwa ile shule aliamua mwenyewe na akafanya.

Tutamkumbuka milele akifanya hivyo. Kwani viwanja ni Mali ya watanzania wote maskini lakini CCM kwa kutumia nafasi yao wakajimilikisha wachache!
 
Ni Mwaka moja na miezi michache tu imepita tangu JOHN POMBE MAGUFULI atangazwe kuwa ndiye Rais wa JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA.

Ukisikiliza Wananchi mtaani waliopiga Kura na ambao hawakupiga kura, Malalamiko ni mengi sana dhidi ya Rais aliyeko Madarakani kuliko lugha za Kumpongeza.

Ukiangalia na kuchunguza kwa Makini Malalamiko mengi yanazalishwa na yeye mwenyewe MKUU WA KAYA.
Kila wakati Kiongozi huyu anaposhika Microphone ili kuhutubia Wananchi popote pale alipo huzalisha jambo gumu jipya lenye kuleta maswali mengi katika jamii yetu.

Kauli alizozitoa Rais Magufuli juu ya walioathirika na Tetemeko huko Bukoba na juu ya Njaa hazifai hata kidogo kutolewa na Kiongozi mwenye dhamana ya juu kama yake yakuliongoza Taifa hili.

Tangu Zama za AGANO LA KALE kwenye BIBLIA Kiongozi alipopewa Mamlaka ya kuongoza watu wake, Nafasi hio ilimhusisha Kuwajibika Kuwahudumia WANANCHI kwenye Maeneo makuu Matatu:-

1. VITA
2. NJAA
3. TAUNI/MAGONJWA.

Mfalme ama Mtawala ndiye aliyetoa mwelekeo Jeshi na Raia wanafanye nini mara Vita inapotokea.
Ilimlazimu kuhakikisha watu wake wako salama dhidi ya Maadui wowote wale.

Tanzania kuna njaa, hata kama sio njaa nzito yakufikia watu kula mavi ya njiwa lakini ukweli kuna njaa.

RAIS MAGUFULI nakushauri uje na suluhisho mahali penye tatizo si vema kukuza ama kuongeza tatizo wakati tayari Raia wamelewa na shida zao.

YUSUFU MWANA WA YAKOBO/ISRAEL MJUKUU WA ISAKA NA KITUKUU WA IBRAHIMU kwa ajili ya Ndoto zake Mungu alimwinua akawa WAZIRI MKUU katika Nchi ya Kigeni ya Misri.
Mungu alimtumia kutafasiri ndoto za watu wawili kisha Hatimaye akatafasiri ndoto ya FARAO na kutolewa Gerezani na kuwa WAZIRI MKUU WA MISRI.
Moja ya kazi kubwa aliyoifanya Yusufu ni kuhakiki watu Wameshiba.
Wakati washibe aliweka Akaiba ya Kutosha kwa ajili ya Taifa la Misri na Mataifa Jirani.

Kabla ya kuweka Misimamo migumu kwa kila Raia wa Taifa letu lazima Kiongozi wa Taifa husika uhakiki umejenga Mfumo imara wa kuifanya kila Kaya au Boma ama Familia inajitosheleza kwa kuwa na Uchumi Imara na huko ndiko kulifanya Taifa liwe na Nguvu ya Kiuchumi.
Ukishawajenga watu wawe na uchumi Imara utakuwa na Uhalali wa kuwakemea kama utakavyo maana ulitanguliza FUNDISHO LA KUTIKA KWENYE NJAA KWANZA.

Pia kwa habari za MATIBABU ili kuondoa maradhi kwa Wananchi ni Kiongozi wa Taifa husika ndiye atakayesimamia kwa kuhakikisha Kila Hospitali ina MADAWA YA KUTOSHA KWA AJILI YA WANANCHI KUTIBIWA.

RAIS MAGUFULI Unao Wajibu wa Kuwalisha na Kuwajengea watu walioathirika na Tetemeko huko Bukoba.
Ni kazi yako na Uongozi wooote uliochini yako Mnapaswa kuhakiki kila BOMA/KAYA katika Vijiji vyote kwa kila Mkoa wana CHAKULA chakutosha.

NI HESHIMA NA FAHARI KIONGOZI WA TAIFA LOLOTE LILE AKIONGOZA WATU WALIOSHIBA, WENYE AFYA NJEMA NA WAKO SALAMA BILA VITA YOYOTE.

Rais Magufuli utatenda vema ukiyasimamia masula haya kwa Moyo wa Upendo na Huruma maana Wapiga Kura wako wakifa kwa Njaa ni nani ATAKAYEKUPA KURA 2020? Kauli ngumu zisizojali UMMA ni hatari kwa Mstakabali wako wa Kurudi Ikulu 2020 labda uwe huna mpango wa kugombea tena Uchaguzi ujao.

MUNGU IBARIKI AFRIKA!
MUNGU IBARIKI. TANZANIA.
 
Serikali imeshasema chakula kipo cha kutosha na hakuna njaa jamani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom