Kwanza nampongeza Rais wetu kwa kufanya ziara yenye mafanikio makubwa nchini Kenya, namuomba asiishie tu kenya sasa ni wakati wa kuonana na mataifa makubwa na kuwavutia wawekezaji.
 
Kwanini mnamwita mama Samia badala ya Rais Samia Suluhu? Au ana mtoto anaitwa Samia? Mbona Magufuli hamkuwa mnamwita baba John Magufuli? Mwiteni Rais kwa cheo chake hilo la mama ni nyumbani huko kwa mumewe na watoto.

Mtapata taabu saana maana Mama Samia is the 'iron lady'! Ukiingia anga zake tu kuvuruga serikali iliyoyaanzisha chini ya JPM, ambayo yy naye alikuwa sehemu ya serikali hiyo lazima apite na weye!

Hamtaamini huyu mama atakavyokuwa zaidi ya Magufuli kwa kutokucheka na nyani! Mama Samia atapandisha viwango vya uongozi kiasi kwamba tutatamani aendelee kutawala kwa muda mrefu!

Nafasi ya mwanamke kuchukua madaraka makubwa inaenda kuhakikishwa kwa utendani bora wa Mama Samia! Wezi mmeula wa chuya! Hamna chenu hapa!
 
NINAVYOMTAZAMA MHE SAMIA SULUHU HASSAN RAIS WA JMT.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kama Mama, Ifahamike kuwa Mama akiwa na Watoto ndani basi KAZI yake ni kuhakikisha anawalea Watoto wake kwa viwango vinavyofanana. Hata kama Mama atakuwa anampenda mtoto mmoja zaidi ya wengine bado hawezi kuonyesha upendo huo hadharani. Mama Samia ni Mama kwa kuwa toka ameapishwa kuwa Rais anatulea Watanzania wote mazingira sawa. Amezingatia zaidi Utanzania na si ukada. Amevaa vizuri uhusika wa Mama.

Ametenganisha muda wa siasa na muda wakazi. Ni dhahiri kuwa Mama Samia kwa sasa anafanya KAZI na hafanyi Siasa. Anatambua kuwa kuna muda wa kazi na kuna muda wa siasa. Ukisikia hotuba zake hazungumzii kabisa juu ya Chama cha siasa, bali anazungumza zaidi juu ya mambo yanayowagusa watu wote bila kujali itikadi. Kutokana na mfumo wake huo wa kuendesha nchi amejipatia wafuasi wengi ndani ya Chama chake na kwenye vyama vingine. Hotuba zake zinaonyesha kutibu majeraha ya baadhi ya Watu ambao walikuwa na vidonda. Toka ameingia madarakani hotuba zake zimepokelewa vizuri na viongozi wakuu wa vyama vya siasa .

Ninamuona kama Mwanadipolomasia aliyebibea. Dunia ya sasa imejipambanua katika diplomasia ya kiuchumi. Yaani mahusiano ya nchi yamejikita zaidi kwenye mahusiano ya kiuchumi na si mahusiano tu ya urafiki. Mhe Samia alipoapishwa baada ya kumteua Mhe Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema Tanzania haiwezi kujifungia na kutekeleza miradi mikubwa hii pekee yake. Alisema watu wana njaa ya mifukoni. Lakini Jana akiwa nchini Kenya amerudia kauli hiyo kwa lugha tofauti huku akisema anarudi Tanzania "ninaenda kufungua nchi, hakuna nchi ina develop pekee yake". Tafsiri yake ni kuwa Mhe SAMIA anaamini katika Uchumi wa kisasa ambao unajengwa katika misingi ya Mahusiano ya kiuchumi. Ameenda Kenya kutatua Mgogoro ambao ulikuwa unajengeka na kujaribu kuua Biashara ya muda mrefu ya Tanzania na Kenya.

Anaamini katika Umoja wa Kitaifa, Rais Samia alionyesha nia ya kutaka kuonana na viongozi wa vyama vya siasa nchini. Bila shaka nia yake hiyo ilikuwa ni kuendelea kutibu makovu na kujaribu kuwaambia nia yake ya kusahau yaliyopita na kuanza kujenga Taifa upya. Lakini hata wiki iliyopita akihutubia wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma alisema kuwa Chama kitaanza kutoa Elimu kwa viongozi wake ili waweze kuendana na siasa za sasa. Wadadisi wa mambo ya siasa wanasema inawezekana kwenye utawala wake ushindi wa CCM ukawa unajitenga na dola kubaki mahakamani. Anataka haki itakayo tokana na nguvu ya Chama na si nguvu ya dola kala alivyowahi kunukuliwa Katibu Mstaafu Bashiru.

Ni muumini wa Utawala wa Sheria ambao msingi wake mkubwa ni Demokrasia. Demokrasia inajengwa na misingi ya haki na wajibu. Hakuna haki bila wajibu, na kwenye utawala wa sheria ndiko unakoweza kuona tunda la haki na wajibu. Mhe SAMIA SULUHU alishatoa maelekezo kwa watu ambao wako magereza na Kesi zao hazina miguu wala kichwa waachiwe. Alishatoa maagizo pia kwa TRA ambayo imekuwa inachangia sana kuua Biashara za watu kwa sababu ya SHERIA kandamizi. Lakini Jana amepigilia msumari wa Mwisho kwa kusema hatuwezi kuwa watumwa kwenye sheria zetu wenyewe. Hivyo ninamuona SAMIA kama Rais anaye kuja kuhakikisha utawala wake mtu yeyote halii kwa kuonewa.

Zipo sifa nyingi ambazo ninaweza kumpa Mhe Samia. Duniani kote huwa viongozi wakubwa hupimwa baada ya siku mia Moja. Lakini kwa muda mfupi ambao Mama SAMIA ameliongoza Taifa inaweza kutoa taswira kuwa atatuongoza vizuri.

Ninaamini Mama huenda akaua kabisa sera ya Chama Cha CUF ambayo walikuwa wakitubagaza kuwa Watanzania kwa mjibu wa tafiti hawana furaha. Leo utafiti ungefanyika ninadhani watu wanafuraha.

Mimi si muumini wa msemo wa unapofika wakati wa kupokezana Madaraka yoyote kuwa hivi huyu kiatu cha mtangulizi kitamtosha? Mimi si muumini wa hili kwa kuwa ninajua wanaopokezana madaraka huwa si mapacha na hivyo miguu haifanani. Kila mtu ana mguu wake. Ninaamini kitu alichovaa Mama SAMIA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinamtosha.
 
Nilipofungua huu Uzi tu na kukutana na namba ya simu.

Nikahitimisha tu hapa hamna kitu maono yako lazima yatakuwa biased tu - kwa kuwa kwa kuweka namba ya simu hapo maana yake unajioendekez.
 
Rais yeyote yule ajaye iwe ni kwa ghafla tu au kwa Mfumo wa Kisiasa ( Kupigiwa ) Kura akitawala kwa Kutoyarudia yale mabaya ( mapungufu ) ya Mtangulizi wake ( yaliyowachukiza Wananchi wengi ) ni 'obvious' tu atakubalika na hata kuanza Kupendwa na Watu wa nchi husika.
 
Hongera sana, lakini mbona Ndugai anakuangusha sana???Wewe una hekima na busara ya kiulimwengu/kidunia iweje ulifumbie macho swala la COVID 19 wa chadema?
 
Rais wetu kipenzi mama Samia umekuwa kwenye harakati za hapa na pale tangu uchukue nafasi ya mtangulizi wako baada ya M/Mungu kumpenda zaidi. Tangu kipindi hicho umekuwa safarini muda mwingi kuanzia Dar-Dom-Chato kumuaga hayati, Kampala/Entebbe kusaini bomba la Hoima-Tanga, Dodoma kuhutubia bunge, Nairobi kuhutubia bunge/wafanya biashara na leo Dar kuongea na watanzania kupitia wakaaji wa Dar. Ni jambo jema, ila wasiwasi wangu isije kufikia ukaonekana motivational speaker zaidi kuliko Rais wa Tanzania.

Please, hata kama hutaiona hii thread mlio karibu naye mfikishieni ujumbe huu, ni muda sasa wa kukaa ofisini Magogoni/Chamwino kushughulika na mambo mbalimbali yanayohitaji uwepo wako ofisini na uonekane pale tu itakapohitaji uwepo wako. Hayati na watangulizi wake walishawahi kusema walikuwa wanalala na mafaili kitandani-msiniulize wake zao walikuwa wanalala wapi.

Note; Usisahau pia, hao wanaokusifia leo siku chache zijazo wengi wao ndo watakuwa wakosoaji wakubwa wako, kwa sababu mbali2 ikiwa ni pamoja na kukosa yale wanayoyatarajia kutoka kwako kama vyeo na mteremko kwenye biashara zao n.k
 
Kwanini mnamwita mama Samia badala ya Rais Samia Suluhu? Au ana mtoto anaitwa Samia? Mbona Magufuli hamkuwa mnamwita baba John Magufuli? Mwiteni Rais kwa cheo chake hilo la mama ni nyumbani huko kwa mumewe na watoto.
Kwa sbb siyo mgumba 😂!
 
Kwanini mnamwita mama Samia badala ya Rais Samia Suluhu? Au ana mtoto anaitwa Samia? Mbona Magufuli hamkuwa mnamwita baba John Magufuli? Mwiteni Rais kwa cheo chake hilo la mama ni nyumbani huko kwa mumewe na watoto.
Kwa sbb siyo mgumba 😂!
 
Rais wetu mpendwa hebu simamia wastaafu wa ATCL walipwe madai yao. Mahakama ilisha amuru walipwe, ofisi ya Katibu mkuu kiongozi ilikwisha elekeza na kuionya wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuhusu ucheleweshaji malipo haya lakini hadi leo hakuna kilichofanyika. Wizara ya Fedha imefanya uhakiki wa wastaafu wa ATCL ili kulipa lakini hakuna kinacho lipwa lugha kuu ni vuteni subra. Miaka inazidi kwenda wastaafu wanaendelea kufariki na kupoteza haki zao. Chonde mheshimiwa rais wasaidi hawa wazee wastaafu wa ATCL walipwe madai yao.
 
Mhe. Rais ajitahidi kuwa mkali, hata kama sio hulka yake lkn ajifunze kuwa mkali wa kukemea maaana yeye ndiye kiongozi wetu wa mwisho, kama kuna ubadhirifu umetokea akemee kwa sauti ya ukali haswa, kama kuna uonevu umetokea, ukiukwaji wa maadili, madawa ya kulevya, rushwa, n.k, kuna mambo lazima atoe sauti kali ya kukemea.
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naiandika Makala fupi yenye mighani mifupi inayotafakarika na kubayanishika.

Baada ya uchaguzi wa 2020 vyama vya upinzani viliibuka na malalamiko na matamko kadha wa kadha wakilalamikia mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi mkuu 2020.

Walidai kwamba wakurugenzi ambao ni wateule wa Rais hawakutenda haki katika zoezi Hilo na kwamba walipokea maelekezo ya kuiba na kupora kura za wapinzani, na waliwatangaza wagombea wa ccm kwa nguvu ya mamlaka zilizo juu.

Kwa hali hiyo walidai kwamba hawatajihusisha na Jambo lolote la serikali iliyopatikana kwa Kura za wizi na walidai serikali na bunge vyote havina uhalali kabisa.

Mtakumbuka moja ya chama cha upinzani kilidai hakitawaruhusu wabunge wa viti maalum kuhudhuria wala kutambuliwa na bunge batili.

Kwa mkitadha huo walimaanisha kwamba wabunge wote wa CCM walio bungeni ni batili kwa sababu walitangazwa kwa kura za wizi.

Baada ya siku kadhaa tume ya uchaguzi ilitoa orodha ya majina ya wabunge 19 wa viti maalumu, lakini katibu wa chadema Bwn JJ Mnyika alitoa taarifa kwa umma ya kwamba chama chake hakitambui orodha hiyo na kilishatoa msimamo wa kutoshiriki bunge la wabunge waliopatikana kwa Kura za wizi, yaani wabunge wote wa Chama cha Mapinduzi.

Licha ya mvutano wote huo bado wabunge hao 19 waliapishwa na hata sasa ni wabunge wa Chadema ambayo inapokea ruzuku kutokana na kuwepo kwao bungeni.

Hivi Sasa ninapoandika makala haya
Nimeona mivutano baina ya viongozi wa chadema na spika wa bunge Mh. J Ndugai yakizuka na hii ni baada ya kifo Cha aliyekuwa Rais wa JMT, Hayati JP Magufuli.

Hii Ina maana gani?
Kwamba Sasa wapinzani wanadhani Mh. Rais Samia ni dhaifu sana asiyeweza kupambanua hoja zao za siri, na kwamba watamfanya usigundue kwamba atakuwa anakubaliana na hoja yao ya kwamba uchaguzi mkuu 2020 CCM iliiba kura na kwamba serikali yake na bunge havina uhalali na Ni batili.

Haya tutayaona mara tu Mh. Rais atakapokubaliana na maombi yao kivuli yaliyo na agenda ya kutaka kumdhalilisha baadae, endapo ataamuua kumshauri spika wa bunge na kupokea hoja za chadema za kuwavua ubunge, ndipo tutakapowaona wakiibuka na ajenda yao halisi ya kwamba Hilo bunge Sio halali maana hata Rais mwenyewe kakubaliana hoja ya kwamba wabunge wa ccm walitangazwa kwa Kura za wizi.

Hata wale wabunge wa CCM wanaosisitiza kwamba maamuzi ya Chadema yaheshimiwe wanakosea bila wao wenyewe kujua kwamba wanaunga mkono hoja ya Chadema juu ya kutangazwa kwa Kura za wizi.

Chadema wafanye nini?
1. Wanapaswa kumeza kauli zao za awali kwamba kura ziliibiwa na wakili hadharani kwamba uchaguzi huo 2020 walipoteza kihalali.
2. Waibuke na hoja yao Sasa ya kwamba wabunge wanaoketi bungeni kwa tiketi ya chadema na mahakama Sio wabunge halali kwa sababu majina yao hayakuwasilishwa na chama kwenye ofsi ya tume.

Lakini wafute kabisa hoja ya kutoshiriki bungeni kwa kisingizio cha kuibiwa kura, maana watakuwa wakimtukana Rais huku wakiomba msaada wake.

Naitwa Mtemi Nyakarungu
0754459572
 
Back
Top Bottom