Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

COLOMBOZI AJAY

New Member
Feb 19, 2024
3
2
BUKOBA MANISPAA
KAGERA ,TANZANIA


Nakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. : Kwanza Hongera na kazi katika harakati za kulipambania Taifa hasa kwenye secta ya AFYA hapa nchini.

Sisi ni wahudumu wa afya ngazi ya jamii, kutoka MKOA KAGERA wilaya ya BUKOBA MANISPAA tulifanya uhamasishaji wa Jamii kuhusu jinsi ya kujikinga na mripuko wa ugonjwa wa MARBURG ambapo ofisi ya HALMASHAURI ilituahidi kuwa tutalipwa kiasi cha shilingi lakini moja ( 100,000/) kwa kila moja kila mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu yaani kuanzia mwezi March 2023 mpaka mwezi June 2023 kutokana na uhamasishaji huo. Tulisainishwa fomu na kuambiwa tufungue Account kila mmoja kwa ajili ya kupata malipo hayo.

Tulianza kazi hiyo tangu 17/03/2023 mpaka 30/06/2023 kulingana na maelekezo tuliyopewa na mratibu wa C H Ws BUKOBA MANISPAA.

Tumehangaika Kwa mda mrefu tukitaka kujua ni lini tutalipwa POSHO hiyo. Hatukupata MAJIBU sahihi. Kwa ngazi ya wilaya mpaka mkoa

Mh: Malalamiko hayo yanatoka Kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii (C H Ws) zaidi ya 120 Kwa KATA zote 14 na mitaa yake. Mh: mpaka Sasa ni muda mrefu umepita bila majibu.

Tunaomba msaada ili tuweza kupa utatuzi wa kero hii

Tutashukuru sana endapo suala Letu lipatatiwa ufumbuzi, wako katika ujenzi wa Taifa.

Mwakilishi wa (C H Ws). KUTOKA BUKOBA MANISPAA MKOA KAGERA.

Asante.

IMG_20240103_134001_244 - Copy.jpg
 
Wakati makonda anafika huko hamkupeleka kilio chenu?anyway fikeni ofisi aa chama mkajieleze mana serikali imepewa nguvu na chama.
 
Nakusalim kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh kwanza ongera na kazi katika harakati za kulipambania taifa, hasa kwenye suala la afya. Mh sisi ni wahudumu wa afya ngazi ya jamii, kutoka Mkoa wa Kagera, Wilaya ya Bukoba Manispaa, tulifanya uhamasishaji wa jamii kuhusu jinsi ya kujikinga na mripuko wa ugonjwa wa Marburg.

Ambapo Ofisi ya Halmashauri ilituahidi kuwa tutalipwa kiasi cha shilingi lakin moja (100,000/) kila mwezi, yaani kuanzia mwezi Machi 2023 mpaka mwezi Juni 2023, kutokana na uhamasishaji huo. Tulisainiwa fomu na kuambiwa tufungue akaunti kila mmoja kwa ajili ya kupata malipo hayo.

Tulianza kazi hiyo tangu 17/3/2023 mpaka 30/6/2023 kulingana na maelekezo tuliyopewa na mratibu wa CHWs Bukoba Manispaa. Mh tumehangaika kwa muda mrefu tukitaka kujua ni lini tutalipwa posho hiyo. Hatukupata majibu sahihi kwa ngazi ya wilaya mpaka mkoa. Mh malalamiko hayo yanatoka kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii CHWs zaidi ya 120.
Screenshot_20240306-151518.jpg
 
Hili swala la madai ya wahudumu ni janga karibu kila mkoa, kiukweli wahudumu wanadhulumiwa haki zao sana. Serikali kupitia viongozi wake waliangalie sana hili swala
 
CHWs BUKOBA !!

Kwanza nashukuru management NZIMA ya jamiiforums Kwa KAZI kubwa mnayoifanya. Kutoka KAGERA, BUKOBA MANISPAA kuhusu SUALA letu la wahudumu wa afya ngazi ya jamii C H Ws. Kuhusu malalamiko ya POSHO zetu. Baadae ya kurusha taarifa yao ya madai 18/3/2024 . Waliweza kuona ufuatiliaji Kwa upande wa MKOA pamoja na wilaya. Japo baada ya siku chache waliitwa C H Ws BUKOBA MANISPAA ili kupewa maelezo kuhusu ulipwaji wa POSHO hiyo . Ambapo mratibu aliitisha kikao cha C H Ws 26/3/2024 ambapo aliwahaidi kuwa watalipwa baada ya sikukuu ya Pasaka . Sasa sikukuu imepita bado wanaona ukimya umeendelea kutanda. Tangu wanadai POSHO hiyo Mwaka mmoja umepita Sasa .ASANTE.

NAMBA YA SIMU YA MULATIBU CHWs wilaya

0784487205
THEONESTINA KASHERO
 
Back
Top Bottom