Wizara ya Afya: Mtumishi mmoja wa Afya alifariki kwa Ugonjwa wa Marburg Virus

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,383
8,132

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma ambapo ametoa pole na pongezi kwa Watumishi waliokuwa wakihudumia walioathirika na Ugonjwa huo mkoani Kagera.

Machi 16, 2023 Serikali iliripoti uwepo wa Wagonjwa 7 na waliopoteza maisha 5 kutokana na Ugonjwa ambao haukufahamika na baadaye Machi 21, 2023, Wizara ya Afya ilithibitisha kuwa Ugonjwa ulisababishwa na Marburg Virus.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa kipindi cha mwaka 2023 hadi kufikia Aprili 23, Ugonjwa wa Marburg ulikuwa umeambukiza watu 23 na kusababisha Vifo 17 barani Afrika.
 
Back
Top Bottom