Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Rais Samia Hassan Suluhu amemteua Jacob Simon Nkwera kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba.
Kabla ya uteuzi huu, Nkwera alikuwa Afisa Mwandamizi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
Kutokana na uteuzi huo inamaanisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Hamid Njovu ameondolewa katika nafasi yake.
Mkeka wote wa Uteuzi na uhamisho uko hapa - Uteuzi na Uhamisho: Rais Samia amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali
Uamuzi huo umefanyika ikiwa ni siku chache tangu Member wa Jamii Forums aripoti kuhusu kutolipwa kwa posho za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) Wilaya ya Bukoba ambao waliingia makubaliano na Ofisi ya Makurugenzi wa Manispaa kusaidia Jamii wakati wa mlipuko wa Ugonjwa wa Marburg.
Wahudumu hao ambao walidai kuwa walishiriki uhamasishaji kwa Jamii jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Marburg kwa kuzunguka kata mbalimbali kw muwa wa miezi mitatu (Machi – Juni 2023) hawajalipwa posho zao ambazo waliahidiwa, walidai kuwa waliandika barua kwa Mkurugenzi huyo Januari 2024 wakikumbushia malipo lakini hawakujibiwa.
Andiko la Member hili hapa: Malalamiko ya posho ya CHWs ya uhamasishaji wa kujikinga na ugonjwa wa mlipuko wa Marburg Bukoba