figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri.

1641807451474.png

Rais Samia kasema watu Wasimpake matope Lukuvi. Wala Wasimsingizie kwamba anaenda kugombea Uspika bali Wamuache amsaidie kazi Ikulu ya Kusimamia hawa Mawaziri Vijana aliowateua.

"Wengine wameanza kumletea [William Lukuvi] meseji za ajabu ajabu wakijua atagombea Uspika, hatogombea. Ana kazi na mimi. Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.kasema Rais Samia

Rais Samia amesema Kabudi atakuwa na Kazi moja tu Ikulu, Kusimamia kupitia na Kushughulikia Mikataba yote ambayo Serikali inaingia.

"Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki...Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba." amesema Rais Samia Suluhu

Amesema hizi kazi hazipo kwenye Muundo wa Serikali lakini anaona ni Msaada Mkubwa Kwake.

MY TAKE:

Je, Kassim Majaliwa na Mkuchika Wameshindwa kumsaidia rais? Kwanini Lukuvi na Kabudi wawe juu yao?

Kapteni George Huruma Mkuchika yeye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) na Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anawakilisha serikali katika bunge la taifa. Yuko chini ya mamlaka ya rais.

 
Kwahio hii ni kazi Mpya au?

Wanajitolea au ni Matumizi mengine ya fedha zetu?

Kwahio kama amewatoa sababu ya umri na wanafaa sana kwa ushauri, wale aliowatoa ili waende wakafanye matayarisho 2025 / hawaendani na kasi yake ni kina nani?
 
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri.
Hebu nyoosha maelezo ya hiyo habari uliyoileta hapa jamvini; ili wakuu waelewe vizuri nini unamaanisha.
 
Salaam Wakuu,

William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia Rais Samia kuwasimamia Mawaziri.
Tatizo la mama Samia anataka kumfuraahisha kila mtu! Hayuko tayari kufanya maamzi! Ndo tabia za watu wa pwani za unafiki! Amewatoa wa nini? Ikulu wanaenda kufanya nini?

Ameongeza baraza la mawaziri la nini? Mzigo wa serkali ni mkubwa maana mawaziri na washauri ni wengi! Mama fanya maamzi bila kuwa accountable utapata taabu sana! Nakukumbusha huwezi kupendwa na kila mtu!
 
Back
Top Bottom