Ikulu-Dar es Salaam: Rais Samia awaapisha Majaji. Asema suala la kutoa haki ni la Mungu peke yake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi Wateule Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 14 Septemba, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi kwa wateule walioapishwa leo na amewakaribisha katika kuwatumikia wananchi na watanzania kwa ujumla.

Suala la kutoa haki ni la Mungu peke yake, kama Mungu amekujalia umeteuliwa kusimamia haki za wanadamu wenzio, unafanya kazi inayofanana na hiyo. Nendeni kasimamieni haki, amesema Rais Samia.

Amewaasa majaji hao kufuata falsafa ya R4 ambayo amezichagua kama falsafa inayoongoza utendaji wa Serikali yake.
 
Kila siku anaapisha tu akitoka hapo anaenda kugawa mamilion kwa wachezaji wa ndondo huku Moshi Hai Kuna mama kafia ndani kwa kukosa nauli ya kumpeleka hospital.
 
Hivi kuapisha ni moja ya kazi kwenye job description yake? Maana naona ndiyo kazi inayomkeep busy kuliko zote
 
Kila siku anateua anaapisha na kutengua sasa huo muda wa wateule wake kushughulika na kero za wananchi utapatikana wapi?

Hujasikia katoa mamilion kwenye ndondo cup.
 
Nikijaribu kuvaa viatu vya Mheshimiwa naona ni ngumu sana.

Everyone everywhere complains
 
Rais wa JMT mh Dr Samia Suluhu Hassan amesema Suala la Kutoa Haki ni la Mungu Peke yake

Rais Samia amewaambia Majaji " kama Mungu amekujalia umeteuliwa kusimamia Haki kafanye Kazi inayofanana na hapo, kasimamieni Haki sababu mmeapa na mmeshika Vitabu mnavyoviamini"

Source: East Africa TV
 
Back
Top Bottom