Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Nawasalimu Waungwana wa JF,

Mwanzo mwanzoni nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai na afya anazotujalia hata kuendelea kupashana habari za hapa na pale kupitia mtandao wetu huu pendwa wa JamiiForums.

Hivi punde, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri kwa kuteua Mawaziri wapya; kuwahamisha wengine; kuteua Manaibu Mawaziri na kuwahamisha wengine na kuwateua Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu na kuwahamisha wengine.

Kingine na kikubwa zaidi ni uteuzi alioufanya Mhe. Rais Samia kumteua Dkt. Doto Biteko kuwa Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Hili ni kubwa kwakuwa limeanzisha mjadala kwa wadau, wakiwemo watumiaji wa JF, kudai kuwa uteuzi huo (wa Naibu Waziri Mkuu) umekiuka Katiba.

Kikatiba, Mhe. Rais yuko sahihi. Ibara ya 36, Ibara Ndogo ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais, pamoja na mambo mengine, kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inasomeka:

36.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria nyingine yoyote, Rais atakuwa na mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, nafasi ambazo zimetajwa katika Katiba hii au katika sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuziunaofanywa na Rais.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2), masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria yoyoteinayohusika, mamlaka ya kuwateua watu wengine wotewasiokuwa viongozi wala watendaji wakuu, kushika nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na pia mamalaka ya kuwapandisha vyeo watu hao, kuwaondoa katika madaraka, kuwafukuza kazi na mamlaka ya kudhibitinidhamu ya watu waliokabidhiwa madaraka, yatakuwa mikononi mwa Tume za Utumishi na mamlaka mengineyo yaliyotajwa na kupewa madaraka kuhusu nafasi za madaraka kwa mujibu wa Katiba hii au kwa mujibu wa sheria yoyote inayohusika.

(4) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya (3) hayatahesabiwa kuwa yanamzuia Rais kuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya watumishi na utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.


Ni wazi kuwa kabla ya leo ( achilia mbali wakati wa uongozi wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi), hakukuwa na nafasi ya Naibu Waziri Mkuu. Leo, akitumia mamlaka yake kikatiba, Mhe. Rais ameanzisha nafasi hiyo ya Naibu Waziri Mkuu. Ili nafasi hiyo ifanye kazi, akamteua Dkt. Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Kwa mamlaka hayo hayo, leo hii hii, Mhe. Rais amefuta iliyokuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na kuanzisha Wizara mbili: Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi. Na uteuzi wa Mawaziri; Manaibu Mawaziri na Makatibu Wakuu ukafanyika. Yote haya yamefanyika kikatiba.

Kimsingi, Katiba yetu ya sasa inaruhusu kuanzishwa na/au kufutwa kwa nafasi yoyote ile ya kimadaraka. Wengi wetu tunajua, kwa kutumia Katiba hii hii, Rais Mstaafu Mwinyi aliwahi kumteua Hayati Augustine Lyatonga Mrema kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Ilitumika Katiba hii hii na Ibara hii hii iliyorekebishwa mwaka 1984 na mwaka 2000.
 
Na kwa kuruhusu huko ndio mwanya wa kuanzisha hata vyeo na kujaza watu wasio na tija.

Suluhisho ni kipatikane kitabu kipya kitakachomshikisha adabu yoyote asiyekiheshimu sasa kama mtu anapewa nafasi ya kuunda chochote na kumuweka yoyote halafu muda huo anayepewa mamlaka haya hawezi kushtakiwa akiwa madarakani au baada ya kutoka haijalishi kwa madhila gani atakayoliletea taifa , tjhis must come to and end.
 
Kimsingi, Katiba yetu ya sasa inaruhusu kuanzishwa na/au kufutwa kwa nafasi yoyote ile ya kimamlaka. Wengi wetu tunajua, kwa kutumia Katiba hii hii, Rais Mstaafu Mwinyi aliwahi kumteua Hayati Augustine Lyatonga Mrema kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Ilitumika Katiba hii hii na Ibara hii hii iliyorekebishwa mwaka 1984 na mwaka 2000.
Nadhani na Salim aliwahi kuwa Naibu waziri mkuu katika awamu ya kwanza ya Mzee Mwinyi.
 
Na kwa kuruhusu huko ndio mwanya wa kuanzisha hata vyeo na kujaza watu wasio na tija.

Suluhisho ni kipatikane kitabu kipya kitakachomshikisha adabu yoyote asiyekiheshimu sasa kama mtu anapewa nafasi ya kuunda chochote na kumuweka yoyote halafu muda huo anayepewa mamlaka haya hawezi kushtakiwa akiwa madarakani au baada ya kutoka haijalishi kwa madhila gani atakayoliletea taifa , tjhis must come to and end.
Kumbe anaweza kufuta hata cheo cha Waziri Mkuu na kuanzisha kingine hakuna hata wa kuhoji? hii katiba ni mbovu sn na ya hovyo
 
Kwenye katiba kinafahamika cheo cha WAZIRI MKUU tu na kimetajwa kabisa.Kungekua na uhitaji wa naibu kingetajwa ni sawa na Cheo cha speaker na Naibu Speaker vyote viko kwenye katiba. Swala la Rais kuanzisha wizara au vyeo mbalimbali haliwezi fika hadi kwa PM kufanya anavyojisikia.

Upande wa PM ni nyeti na ndio maana akimpiga chini serikali nzima inakua imevunjwa na inatakiwa aunde upya. Swala ukimfukuza PM unakua umevunja serikali, ukimfukuza Naibu inakuaje?PM anathibitishwa na Bunge,Huyu Naibu wake vipi?
 
Kwenye katiba kinafahamika cheo cha WAZIRI MKUU tu na kimetajwa kabisa.Kungekua na uhitaji wa naibu kingetajwa ni sawa na Cheo cha speaker na Naibu Speaker vyote viko kwenye katiba. Swala la Rais kuanzisha wizara au vyeo mbalimbali haliwezi fika hadi kwa PM kufanya anavyojisikia. Upande wa PM ni nyeti na ndio maana akimpiga chini serikali nzima inakua imevunjwa na inatakiwa aunde upya. Swala ukimfukuza PM unakua umevunja serikali, ukimfukuza Naibu inakuaje?PM anathibitishwa na Bunge,Huyu Naibu wake vipi?
Nakazia
 
Elezea na waziri mkuu anavyopatikana
51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii naambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge.

(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzianayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge waliowengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge walio wengi.

(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi-(a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake; au(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au(c) siku atakapojiuzulu; au(d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwaWaziri Mkuu; au(e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu wa masharti mengineyo ya Katiba hii.
 
Wakuu kwa mtazamo wangu hiki cheo kipya kimewekwa kwa wakati huu ili kupoozesha hali ya kisiasa iliyopo kwa sasa maana hali imekuwa mbaya hasa upande wa serikali maana mashambulizi yamekuwa makali sana

Ili kupunguza joto la kisiasa tumeletewa mabadiliko ya baraza la mawaziri na kwa hilo tu isingekuwa na lolote la kushtua maana watu ni walewale ikabidi liwekwe hili la Naibu Waziri Mkuu ili ndiyo liwe mjadala hawa waulizane hili lipo kikatiba, hawa majukumu yake ni nini, wale hatujawahi kukisikia hiki cheo mwisho mjadala wa bandari na waraka wa TEC vife natural death

Hili lisitutoe kwenye mjadala muhimu wa rasilimali zetu ni jambo lisilo na umuhimu
 
51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii naambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge...
Haya rudi kwa naibu waziri mkuu,kama hakuna hiyo ibara uteuzi huu ni null and void
 
Back
Top Bottom