Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Kasim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kuwa Makamu wa Rais Dkt Isdory Mpango ni mzima wa afya na yupo nje ya nchi kimajukumu.

Waziri Mkuu amesema kuwa watanzaia waachane na ule mtandao unaosema maneno ya ajabuajabu na wasiwe wasiwasi wowote Kwa kuwa Makamu wa Rais Dk. Mpango ni mzima na yupo nje ya nchi kimajukumu. Hata hivyo hajataja nchi ambako Makamu wa kaenda, na jukumu hilo linahisu nini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa Dodoma akiongea na wadau waliohudhuria kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya watu wenye Ulemavu Duniani.

"Vilevile Makamu wa Rais Dk. Isdory Mpango ambaye pia naye yuko nje kimajuku, achana na ule mtandao unaosemasema mambo ya ajabu ajabu, yupo nje kimajukumu, anawatakiwa kila la kheri watu wote ambao mmeshiriki hapa leo kwenye haya maadhimisho ya kitaifa anawaombea sana, anawatakia kila la kheri".

Kasim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kuwa Makamu wa Rais Dkt Isdory Mpango ni mzima wa afya na yupo nje ya nchi kimajukumu.

Waziri Mkuu amesema kuwa watanzaia waachane na ule mtandao unaosema maneno ya ajabuajabu na wasiwe wasiwasi wowote Kwa kuwa Makamu wa Rais Dk. Mpango ni mzima na yupo nje ya nchi kimajukumu. Hata hivyo hajataja nchi ambako Makamu wa kaenda, na jukumu hilo linahisu nini.

"Vilevile Makamu wa Rais Dk. Isdory Mpango ambaye pia naye yuko nje kimajuku, achana na ule mtandao unaosemasema mambo ya ajabu ajabu, yupo nje kimajukumu, anawatakiwa kila la kheri watu wote ambao mmeshiriki hapa leo kwenye haya maadhimisho ya kitaifa anawaombea sana, anawatakia kila la kheri".

Waziri Mkuu ( Premier ) Kassim Majaliwa nadhani GENTAMYCINE nilishakushauri hapa hapa JamiiForums kuwa kukiwa na Taharuki yoyote au Tukio lolote lile la Kihisia usipende kuwa na Kiherehere cha Kulisemea kwani Kirekodi una Gundu kwani kila ukijitokeza Kutetea Jambo fulani kwa dhana ya Kulificha huwa linakuumbua na hatimaye Kudharaulika, Kuchekwa na Kutoaminiwa tena.

Premier Kassim Majaliwa jana Umesikika na Kunukuliwa mahala ukisema kuwa Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isidori Mpango yuko mzima na nje ya nchi anafanya Shughuli zake za Kiutendaji na Kiuwajibikaji.

Premier Kassim Majaliwa Mimi GENTAMYCINE sina tatizo na hii Taarifa yako ila Kinachonishtua zaidi ni kwamba hata kwa Hayati Dk. Magufuli Uvumi wa Kifo chake ulipoanza na Kuenea kwa Kasi ndani na nje ya Tanzania kama kawaida yako ya kuwa na Kiherehere ulijitokeza na Kutuambia kuwa yuko ni mzima wa Afya, ulizungumza nae, anakunywa Chai Ofisini huku akipitia Mafaili yake wakati kumbe tayari na zamani sana alishakuwa amelazwa katika Mochwari ya Hospitali mbili tofauti kabla ya kupelekwa katika Mochwari ya Wanamedani wa kati ya Kawe na Mwenge.

Binafsi sikuamini tena Premier KMK.
 
Back
Top Bottom