Serikali iache ushamba kwani ingetangaza makamu wa Rais Mpango yuko nje nini kingetokea?

Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
2,155
3,798
Huu ni ushamba kwa serikali inayojinasibu kuwa ni ya watu kufichaficha vitu ambavyo havistahili kufichwa! Kwani serikali ingetangaza kuwa Makamu wa Rais Dr. Mpango amesafiri kwenda nje ya nchi kutibiwa, au kupima afya au kusoma ingepungukiwa nini? Badala yake Kigogo amepata ujiko kwa kusambaza uvumi kuwa Mpango amekata moto na hivyo kuleta taharuki nchi nzima!

Rais Kikwete alikwenda kutibiwa tezi dume Marekani ambako alikaa mwezi mzima Taifa lilipewa taarifa, na wakati wote akiwa anapata matibabu watu walimutumia salamu za kumuombea kwa Mungu apone haraka. Mbona hali ilikuwa shwari na hukukuwa na minong'ono ya kijinga kama iliyotokea sasa!

Kumbukeni mlificha maradhi ya Magufuli na kifo kikawaumbua, hadi leo kuna taharuki ya tarehe rasmi aliyofariki kwa kuwa wananchi wanaamini serikali imeficha. Mbaya zaidi wananchi wanaamini kuwa Magufuli aliuawa na siyo kifo cha kawaida! Imani hii kuwa Magufuli aliuawa kamwe serikali haitaweza kuifuta katika fikra za wananchi!

Sasa serikali inadai Mpango alikwenda nje kwa kazi maalumu, je ni kazi gani hiyo ambayo sisi wananchi hatupaswi kuifahamu au hatutanufaishwa nayo? Au alitumwa kwenda kukamilisha mipango ya kuuzwa kwa rasilimali zetu?

Nyie chawa wa serikali acheni ushamba, wauaji wakubwa!
 
Ni matokeo ya serikali kukosa uwajikaji na wawajibishaji,wananchi ni vilaza ndo maana serikali inafanya inachokitaka.
 
NCHI INA VIONGOZI WA AJABU SANA

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom