Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson, amesema kuwa Bunge limewapa Tanesco muda kufikia mwezi wa sita mgao wa umeme uwe umeisha.
"Wacha tuipe serikali muda, kwa maana ipi wao walijipanga mwezi wa sita (shida ya umeme kuisha) wakarejesha nyuma mwezi wa pili, tunawapongeza sana na mmerejesha mpaka mwezi wa tatu kwa hizo mashine zote kukamilika, Bunge linawapa mpaka mwezi wa sita ili bunge linapokuwa hapa mgao uwe umeisha, tunawapongeza sana kwa kazi nzuri," - Spika wa Bunge
Pia soma:
- Naibu Waziri wa Nishati: Mgawo wa umeme nchini utaisha mwezi wa tatu