Ahadi za Serikali juu ya tatizo la Mgawo wa Umeme Nchini kuanzia mwaka 2010 hadi 2024

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1708342936788.png
Desemba 24, 2010: Aliyekuwa Meneja Uhusiano wa TANESCO, Badra Masoud, alitangaza kuanza kwa Mgawo Mkali wa Siku 30 nchi nzima na kuahidi utaisha Januari 2011

Machi 2011: Aliyekuwa Meneja Uhusiano wa TANESCO, Badra Masoud, alisema Mgawo utaisha mwaka 2013

Juni 2014: Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alisema Matatizo yote ya Umeme yataisha mwaka 2025

December 2014: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Jenerali Mstaafu Robert Mboma, alisema Mgawo utaisha Machi 2015

Desemba 2015: Aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, aliiagiza TANESCO kuondoa upungufu wa Umeme ifikapo Februari 2016

Desemba 4, 2017: Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard, alisema Mgawo wa Umeme utaisha Desemba 15, 2017

Machi 2020: Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, aliagiza TANESCO kusitisha Mgawo wa Umeme nchi nzima

Machi 2021: Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, alitoa siku 5 kwa TANESCO na Songas kuondoa tatizo la Mgawo wa Umeme

Novemba 2021: Aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande, alisema Mgawo wa Umeme utaisha Machi 2022

May 2022: Aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande alisema matatizo ya Mgawo yataisha Novemba 2022

Julai 2023: Aliyekuwa Waziri wa Nishati, January Makamba alisema kuwashwa kwa Mitambo ya Bwawa la Nyerere (JNHPP) kutamaliza Mgawo wa Umeme

Septemba 2023: Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi Gisima Nyamo-Hangahilo, alisema Mgawo utaisha Machi 2024

Septemba 2024: Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa muda wa miezi 6 kwa TANESCO kumaliza Mgawo, muda ambao unaisha Machi 25

Februari 1, 2024: Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, alisema Mgawo utaisha Februari 16, 2024

Februari 6, 2024, Bunge lilipitisha azimio la kuitaka Serikali ihakikishe mradi wa Bwala la Umeme la JNHPP unaanza uzalishaji Februari 2024

Februari 16, 2024: Naibu Waziri Kapinga, alisogeza mbele ahadi ya kumalizika Mgawo hadi Machi 2024

Februari 16, 2024: Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, aliipa Serikali muda wa Miezi 4 hadi Juni 2024 kumaliza Mgawo wa Umeme.

==============For English Audience Only==============

Government Commitments on Tanzania's Power Outages from 2010 to 2024​

Over the past decade, Tanzania has grappled with persistent power outages, prompting successive governments to make commitments to address the issue. A review of these commitments reveals a recurring pattern of setting deadlines for resolving the problem. Here is a timeline of government promises and actions related to power outages in the country from 2010 to 2024.

2010-2015: Periodic Commitments and Extended Deadlines
The timeline began in 2010 when TANESCO's then-Relations Manager, Badra Masoud, announced a 30-day nationwide power rationing with the assurance that it would end in January 2011. However, over the following years, different officials, including Secretary-General Eliakim Maswi and Board Chairman Robert Mboma, made promises that extended the resolution deadline to 2025.

2017-2021: Continued Pledges and Ministerial Orders
In December 2017, former Minister of Energy and Minerals Dr. Medard pledged the end of power rationing by December 15, 2017. Subsequent years witnessed orders from Minister Kalemani to TANESCO to eliminate power shortages by February 2016 and, later, the suspension of nationwide power rationing in March 2020. Despite these announcements, the problem persisted.

2022-2024: Evolving Promises and Legislative Resolution
The timeline progressed with former TANESCO Director Maharage Chande setting a deadline of March 2022 for the end of power rationing. However, this was later extended to November 2022. In July 2023, former Energy Minister January Makamba indicated that powering the Nyerere Hydroelectric Power Plant (JNHPP) would resolve the issue. The most recent commitment came in September 2024 when President Samia Suluhu Hassan gave TANESCO six months to end the power rationing, with a deadline set for March 25, 2025.

As Tanzania navigates through these commitments and deadlines, the government faces the challenge of fulfilling promises made over the years. The recent resolution by the Parliament, giving the government until June 2024 to address the power outages, highlights the ongoing efforts and pressures to find a sustainable solution to this long-standing issue.
 
Tuna vyanzo mbadala vingi sana vya umeme hapa nchini ,ila hatuna utashi wa kisiasa unaoweza kupanga mkakati na kusimamia utekelezaji wake. Tunachoshuhudia ni porojo tu siku ziende mbele basi.
 
Mi nimefurahishwa na hiyo ahadi ya raisi tu aliyoitoa Septemba 2024. Kweli Mama anaupiga mwingi, hadi muda!!!!!!!


Weka pia ile ahadi ya Muhongo ya kuuza umeme ifikapo lini sijui....
 
....ahadi ya JK kuhusu umeme!,haya jamaa ni waongo na ndio maana familia zao nazo zimejaa waongo, nani mmliki wa UDA?
 
Tatizo ni serikali,tanesco mnaionea,magufuri alifanyeje kwenye hili,miaka3 hakuna mgao,mzee baba yule mungu umsamehe madhambi yake
 
Back
Top Bottom