MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 34
- 30
Mgao mkali wa umeme uliopo unatokana na upungufu uliopo katika uzalishaji dhidi ya mahitaji. Kuwashwa kwa Mtambo namba 9 katika Mradi wa Bwawa la uzalishaji umeme la Julius Nyerere ambao unazalisha megawati 235 kuingia katika gridi ya Taifa kunakwenda kuleta nafuu kubwa kwa takribani asilimia 85.
Mwezi Machi, 2024 tutashuhudia mtambo namba 8 nao ukiwashwa ambao nao utazalisha megawati 235 kwenye Gridi ya Taifa. Hivyo kufanya katika kipindi cha miezi miwili kupata ongezeko la megawati 470.
Aidha mwezi Aprili, 2024 kupitia mradi wa uzalishaji umeme wa Rusumo unaotekelezwa na nchi tatu za Tanzania, Burundi na Rwanda chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) utakaozalisha Megawati 80 ambazo Kila Nchi mshirika itapata mgao wa megawati 26.66 katika Gridi yake ya Taifa. Hivyo mpaka mwezi Mei, 2024 Gridi yetu ya Taifa itakuwa imepokea Megawati 496.66
Nakisi ya umeme nchini kwa sasa ni kati ya Megawati 300 - 400 hivyo ni dhahiri tatizo la mgao wa umeme linakwenda kumalizika kabisa na kuwa na ziada ya Megawati 96.66
Mpaka mitambo yote iwashwe JNHPP tutakuwa na umeme wa kutosha. Kama Nchi ili kuondokana na kadhia hii na kutoa uhakika wa nishati ya umeme kwa wawekezaji, wafanyabiashara na wajasiriamali ni lazima kuendelea kutekeleza mpango mkakati wa uzalishaji zaidi wa umeme kwa manufaa ya miaka mingi ijayo kazi ambayo serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan wanaendelea nayo.
Pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani wakati anaingia madarakani mwaka 2021 aliupokea mradi ukiwa asilimia 33 za utekelezaji huku ukiwa umeshalipwa kiasi cha shilingi trilioni 1.45 kati ya shilingi trilioni 6.5 gharama za utekelezaji wake. Leo mradi upo asilimia 98 na mkandarasi akiwa ameshalipwa asilimia 90 ya fedha zote za mradi.
Tuendelee kuziamini hatua ambazo serikali yetu inachukua ili kuondokana na tatizo hili la umeme nchini kwetu.
Mtoto wa Mama Kizimkazi
#HakunaKilichosimama #2025TunaendeleaNaSamia
#KaziIendelee