tweenty4seven
JF-Expert Member
- Sep 21, 2013
- 15,672
- 19,187
Daah chama kina gundu mwenezi ni chapati ya maji,yani anatafunwa kama mwanamkeTunaitaka Chadema kubadilika na kuanza kufanya siasa za hoja, zenye kutoa kipaumbele maendeleo ya wananchi na Taifa badala ya siasa hizi za kuhimiza ghasia, vurugu na kueneza uongo na chuki nchini.
Kadhalika Mnyika aache upotoshaji na kumlisha maneno Rais Samia ambayo hakuyasema au kuingilia mwenendo wa kesi ya Mbowe mahakamani kama anavyotumia nguvu kubwa kutaka kuaminisha umma.
Rais Samia katika maelezo yake alisema hakuna mahali nchini Demokrasia imeminywa na ndio maana vikao vya kikatiba vya vyama mbalimbali vya siasa nchini vinaendelea. alisisitiza siasa zenye mrengo wa vurugu na ghasia hazina nafasi na wala hazitavumiliwa kwani hiyo sio demokrasia.
Kuhusu sakata la kesi ya mwenyekiti wa chama hicho inayoendelea mahakama ya kisutu hakuna pahala katika maelezo yake Rais Samia wakati wote wa mahojiano aliingilia uhuru wa mahakama kama Mnyika alivyopotosha zaidi alitaka watu kuwa watulivu waipe nafasi mahakama kutekeleza wajibu wake.
CDM waache vioja vya kudai demokrasia imeminywa na hawaruhusiwi kufanya mikutano wala vikao wakati wameendesha operesheni haki, chadema kidigitali na vikao mbalimbali vya ndani bila bugudha yoyote. Lakini cha ajabu (leo) Mnyika ameendelea kuingilia uhuru wa mahakama jambo ambalo linaoonyesha jinsi alivyo na papara na jazba na kudhihirisha juu ya uchanga wake kisiasa.
Muhimu wakafahamu ikiwa maandalizi yao ya mikutano au vikao na operesheni zozote za kisiasa yatakuwa na viashiria au dhamira ya kupanga, kuratibu, kuasisi au kutekeleza vurugu na ghasia nchini vyombo vya dola havitakaa kimya sio kwao tu bali kwa yeyote yule.
Bahati mbaya ni kwamba hawana desturi ya kufanya mikutano, vikao au operesheni zao za kisiasa kwa amani na kwa kufuata taratibu na sheria hivyo wabadilike ili kuepuka kusigana na vyombo vya dola. Wao kukiuka taratibu na sheria ili kupata matukio ya kukabiliana na vyombo vya dola kwao umekuwa mradi wa kutafuta fedha kwa wafadhili wao nje ya nchi ndio maana hawataki kubadilika.
Rais Samia ameapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Tanzania, ikiwemo kuhakikisha ustawi wa amani na utulivu nchini. Hivyo haitatokea hata mara moja akakubali watu wachache kwa maslahi yao wakavuruga nchi.
Jambo jingine watanzania wanapaswa kujua Chadema sio chama kikuu cha upinzani wakati huu kwani kina mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa hivyo hawana sifa hiyo.
Tunashangazwa na dhamira ya Chadema kutaka kuonana na Rais Samia wao kama wao ilihali wao sio chama pekee cha upinzani nchini. Rais Samia alitoa msimamo wa kuonana na vyama vyote vya upinzani kwa umoja ambapo atatoa tarehe na muda wakukutana nao.
Hili la Chadema kutaka kukutana na Rais Samia wakiwa pekee yao ni muendelezo wa siasa za ubinafsi na ubaguzi ambao umekuwa utamaduni wao jambo ambalo Serikali ya CCM inayongozwa na Rais Samia haitazipa nafasi.
Nitoe rai kwa watanzania na wadau wote wa maendeleo ndani na Nje ya Nchi kuiunga mkono serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kwa pamoja tuifikishe Tanzania katika maendeleo endelevu.
End